DRC: Wanawake wafungwa zaidi ya 260-walibakwa katika gereza la Makala: UN

Wanawake wafungwa zaidi ya 260 walibakwa katika jela ya Makala nchini DRC, mapema mwezi huu wakati wa jaribio la wafungwa kutoroka jela, imesema ripoti ya umoja wa mataifa.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ripoti hiyo aidha imeongeza kuwa wanawake hao walilazimika kutafuta mbinu za kuzuia magonjwa baada ya kutendewa vitendo hivyo vya kikatili.
Ripoti hiyo aidha imeongeza kuwa wanawake hao walilazimika kutafuta mbinu za kuzuia magonjwa baada ya kutendewa vitendo hivyo vya kikatili. AP

Ripoti hiyo imebaini kwamba kati ya wafungwa 348 katika gereza hilo la Makala, wafungwa 268, walitendewa vitendo vya unyanyasaji wa kingono ikiwemo ubakaji, wanawake 17 kati ya waliobakwa wakiwa chini ya umri wa miaka 19.

Ripoti hiyo aidha imeongeza kuwa wanawake hao walilazimika kutafuta mbinu za kuzuia magonjwa baada ya kutendewa vitendo hivyo vya kikatili.

Awali serikali ya DRC ilikuwa imekiri kubakwa kwa wanawake hao ila haikotoa idadi ya wanawake waliobakwa.

Gari la maofisa wa polisi likiondoka katika gereza la Makala jijini Kinshasa, Septemba 3, 2024
Gari la maofisa wa polisi likiondoka katika gereza la Makala jijini Kinshasa, Septemba 3, 2024 AFP – HARDY BOPE

Kadhalika ripoti hiyo pia imesema wafungwa 129 waliojaribu kutoroka jela waliuawa kwa kupingwa risasi, katika gereza hilo la Makala ambao linastahili kutoa huduma kwa wafungwa 1500, ila lina zaidi ya wafungwa alfu 15.

Rais Felix Tshisekedi ameagiza kufanyika kwa uchuguzi kuhusiana na jaribio hilo la wafungwa kutoka, na mikakati ya kupunguza idadi ya wafungwa katika gereza hilo la jiji Kinshasa.

Wanawake wafungwa zaidi ya 260 walibakwa katika jela ya Makala nchini DRC, mapema mwezi huu wakati wa jaribio la wafungwa kutoroka jela, imesema ripoti ya umoja wa mataifa.

atika gereza hilo la jiji Kinshasa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024

Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment