Bao La Asubui-Muda wako wa KUINULIWA unapofika, huwa kuna DALILI utaziona.

Radio Fortune Africa-Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Muda wako wa KUINULIWA unapofika, huwa kuna DALILI utaziona.

Mara nyingi, dalili hizi ni UTANGULIZI wa kile ambacho MUNGU anataka kufanya kwenye maisha yako…

…ukiziona UJUE kuna kitu kikubwa KINATAKA KUZALIWA.

Cha kwanza, Mungu atainua watu wa kuanza KUKUSEMEA.

Yaani, wataanza kubeba habari zako Njema na kuzizungumza kwenye MAENEO ambayo wewe HAUWEZI KUFIKA.

Yaani kuna watu wataanza kupeleka SIFA zinazohusu KIPAJI chako, ELIMU yako au UZOEFU wako.

Wakati mwingine hata kukumbushia mambo MAZURI ya NYUMA…

…ambayo ULIYAFANYA uliyodhani YAMESAHAULIKA.

Na hili linapotokea, Mungu atahakikisha UNAJUA kuwa linafanyika hata kwa sehemu ndogo.

Cha Pili, utaanza kuona UPENDELEO (Favor), Yaani kilekile ulichokuwa unafanya ZAMANI…

…kwa sababu kitapewa NGUVU KUBWA SANA.

Ni kama, kuna kitu kilikufunika sasa unakuwa UMEFUNULIWA ili UONEKANE…

…na kila mtu atakuwa ANASHANGAA ulikuwa wapi siku zote.

Ukiona mambo haya MAWILI, Jipange ni MAJIRA YAKO.

Endelea kufanya kwa BIDII na USIACHE KUMUOMBA MUNGU.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment