
Urusi inasema imechukua vijiji viwili zaidi mashariki mwa Ukraine haswa katika maeneo ya Donetsk na Lugansk ambapo wanajeshi wake wameendelea kuripotiwa kupiga hatua katika uwanja wa mapambano.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imeeleza kwamba maofisa wake wamechukua kijiji cha Mykolaivka, karibia kilomita 15 kutoka katika mji wa Pokrovsk katika jimbo la Donetsk, sawa na eneo lenye makazi ya watu ya Stelmakhivka, jirani na Lugansk.
Wanajeshi wa Urusi wamekuwa wakipiga hatua kuelekea katika mji wa kimkakati wa Pokrovsk, ambapo karibia watu Elfu 60 wamekuwa wakiishi katika miezi ya hivi karibuni.

Wanajeshi wa Ukraine wameonekana kukabiliwa na upungufu wa silaha haswa wakati huu wanapoendelea kusubiria silaha kutoka katika nchi washirika wake.
Mapema mwezi huu, Kyiv ilianzisha mashambulio ya ardhini katika eneo la Kursk kwenye mpaka na Urusi ikiwa na matumaini ya kuwaondoa wanajeshi wa Urusi kutoka katika eneo la Donetsk.
Licha ya mashambulio ya Ukraine katika mji wa Kursk, Urusi katika upande mwengine imeonekana kuendelea kupiga hatua katika mji wa viwanda wa Donetsk.
Haya yanajiri wakati huu shambulio la Urusi katika mji wa Nikopol kusini mwa Ukraine likiripotiwa kusababisha kifo cha mtu mmoja, wengine watano wakiwa wamejeruhiwa kwa mujibu wa mamlaka.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC ||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.