Ukingo wa Magharibi: Jeshi la Israeli linaendelea na oparesheni za kijeshi
Idadi ya watu waliouawa katika oparesheni ya siku ya pili ya jeshi la Israeli kwenye Ukingo wa Magharibi imeendelea kuongezeka, hatua inayokuja w

Jeshi la Israeli lilianzisha oparesheni hii wakati huu pia hali katika Ukanda wa Gaza ikiripotiwa kuendelea kuwa mbaya tangu shambulio la Hamas la tarehe 7 ya mwezi Oktoba.
Oparesheni za Israeli zilianza siku ya Jumatano katika miji ya Jenin, Tubas na Tulkarem kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi katika kile ambacho jeshi linasema ni oparesheni dhidi ya ugaidi.

Soma piaOparesheni za #israel katika Ukingo wa Magharibi
Magari ya kivita na ndege za kijeshi za Israeli yameonekana katika kambi za wakimbizi za Tubas na Tulkarem, pamoja na Jenin, makabaliano yakiripotiwa kati ya Israeli na wapiganaji wa Palestina.
Katika upande mwengine, jeshi la Israeli limesema limewaua wapiganaji watano wa Palestina katika mji wa Tulkarem katika oparesheni ya hivi karibuni katika Ukingo wa Magharibi na kufikisha idadi ya watu waliouawa kuwa 14.

Wapiganaji wa Islamic Jihad kutoka Palestine wamethibitisha kifo cha Muhammad Jabber, maarufu kama Abu Shujaa ambaye ni kamanda wake kwenye kambi ya wakimbizi ya Nur Shams katika eneo la Tulkarem.
Makabiliano hayo yamesababisha uharibifu mkubwa haswa katika eneo la Tulkarem, gavana wa eneo hilo akiitaja hatua hiyo kama ishara hatari.
Wizara ya afya ya Palestine ilisema kwamba Wapalestina 12 waliuuawa katika siku ya kwanza ya oparesheni hiyo ya Israeli.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.