Afrika Leo Jioni

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

YAJAYO KATIKA AFRIKA LEO JIONI…

Rais wa Ufaransa Emmanuel anakabiliwa na kibarua kigumu kuitisha mazungumzo mapya kuhusu uundwaji wa serikali, baada ya vyama vya siasa za mrengo wa kushoto kukataa kushiriki tena kufuatia hatua yake ya kumkataa mgombea wao wa nafasi ya waziri mkuu.

  1. Rais wa Kenya William Ruto ameandaa hafla maalum katika ikulu ya Nairobi ambapo amezindua rasmi ugombea wa kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga, wa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika. Marais kadhaa wamehudhuria hafla hiyo akiwemo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Salva Kiir wa Sudan Kusini na Yoweri Museveni wa Uganda. Je, Odinga atafanikiwa katika azma ya kuwa mwenyekiti wa AU?

3.Umoja wa Mataifa umetoa taarifa iliyosema una wasiwasi mkubwa kuhusiana na hali inavyozidi kuwa mbaya nchini Libya, kutokana na maamuzi yaliyofanywa hivi majuzi kuhusiana na mzozo uliopo katika Benki Kuu ya taifa hilo. Kuna hofu kwamba huenda kukawa na ubadhirifu wa fedha za taifa hilo.

  1. Waziri mmoja anayeegemea siasa kali za mrengo wa kulia nchini Israel amezua ghadhabu miongoni mwa Wapalestina kwa kudai kwamba, angekua na uwezo angejenga sinagogi katika eneo lililo na msikiti wa Al-Aqsa. Eneo hilo ni eneo la tatu takatifu kwa Waislamu na ni utambulisho wa kitaifa wa Palestina.

5.Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya Atomiki – IAEA Rafael Grossi ameanza leo ziara ya kufanya uchunguzi huru wa hali ilivyo katika kinu cha nyuklia cha Kursk nchini Urusi. Hii ni kufuatia mashambulizi yasiyo ya kawaida ya Ukraine ndani ya mpaka wa mkoa huo wa Urusi.

TheHeartBeatofAfrica

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inamuuunga mkono Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).

Rais Samia ametoa kauli hiyo aliposhiriki uzinduzi wa kampeni ya kumnadi mgombea huyo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Nairobi.

Hafla hiyo
imehudhuriwa pia na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Salva Kiir wa Sudan Kusini na Waziri Mkuu wa Burundi, Gervais Ndirakobuca.

Rais Samia amempongeza Odinga kwa kudumisha uhusiano na viongozi wa Afrika na wabia wake, huku akimuelezea kama kiongozi mwenye busara na
mwenye uwezo wa kujenga Umoja wa Afrika.

TheHeartBeatofAfrica

AMRI ya Rais William Ruto kuwa vijana kwenye mafunzo ya Huduma za Kitaifa kwa Vijana (NYS) wafundishwe kutumia bunduki inaendelea kuzua maoni tofauti miongoni mwa Wakenya.

Rais William Ruto mnamo Jumatatu, Agosti 26, 2024 aliamrisha Waziri wa Utumishi wa Umma, Justin Muturi akimtaka ashauriane na Wizara za Ulinzi na Usalama wa Ndani ili waibuke na mwongozo wa kuwafunza vijana wa NYS jinsi ya kutumia bunduki.

Akitoa amri hiyo wakati wa kufuzu kwa makurutu Gilgil, Kaunti ya Nakuru, Rais alisema mafunzo ya kutumia bunduki yatawezesha vijana hao kushiriki oparesheni za kijeshi katika maeneo mbalimbali nchini kukiwa na haja.

Hata hivyo, amri hiyo imepingwa na mawakili ambao wanasema Rais Ruto anastahili kukosolewa kwa kuwa matamshi yake hayazingatii sheria kwa msingi wa jinsi ambavyo idara za usalama huendesha shughuli zake.

Wakili Evans Ogada, anasema kuwapa vijana hao mafunzo ya kutumia bunduki kunaweza kusababisha kuchipuka kwa makundi ya wapiganaji nchini.

“Vijana 20,000 huchukuliwa na NYS kila mwaka na hata wakifunzwa matumizi ya bunduki si wote wataingizwa jeshi au katika idara ya polisi. Swali ni kipi kitafanyika na wale ambao wataachiliwa na hawana kazi?” akauliza Bw Ogada.

Kuhusiana na Katiba, Bw Ogada alisema jinsi ambavyo amri hiyo ilitolewa ni ishara tosha tu kuwa haina mashiko.

Anasema amri hiyo haina mashiko kwa kuwa lazima iandikwe rasmi lakini, hata hivyo, bado itakabiliwa na changamoto za kisheria.

Sheria inamhitaji rais apate idhini kutoka kwa Baraza la Kitaifa la Usalama kabla ya kutoa matamshi kama hayo yanayohusiana na suala la usalama wa nchi.

Wakili Waikwa Wanyoike naye alisema kuwa Rais hana mamlaka ya kuamua kinachostahili kusheheni kwenye mafunzo ya NYS kwa kuwa jukumu hilo ni la mkurugenzi wa asasi hiyo.

Mafunzo ya bunduki
mawakili
nys
Rais Ruto

WABUNGE wametaka maelezo kuhusu ni kwa nini Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inadaiwa jumla ya Sh4.9 bilioni na baadhi ya kampuni za mawakili walioiwakilisha katika kesi kadhaa za uchaguzi.

Pesa hizo pia zinajumuisha pesa ambazo IEBC ilitarajiwa kulipa baada ya kupoteza kesi mbalimbali dhidi yake mahakamani.

Hata hivyo, Afisa Mkuu Mtendaji wa tume hiyo Marjan Hussein Marjan, aliwaambia wabunge wanachama wa Kamati ya Bunge kuhusu Uhasibu (PAC) kwamba viwango vya ada zinazolipwa mawakili “ni vile vilivyokubaliwa.”

Wabunge waliambiwa kuwa Sh163 milioni kati ya kiasi chote cha fedha zinazodaiwa IEBC, ni pesa ambazo tume hiyo ilipaswa kulipa kutokana na maamuzi yaliyotolewa dhidi yake mahakamani.

Wanachama wa PAC Nabii Nabwera (mbunge wa Lugari) na mwenzake wa Mathioya Edwin Mugo walitaja kiasi hicho cha pesa (Sh4.9 bilioni) kama cha juu zaidi.

Walipendekeza kuwa kamati ya kuthibitisha madeni ambayo hayajalipwa inapasawa kuchambua madeni kabla ya IEBC kuyalipa.

“Kama ningekuwa Waziri wa Fedha na niambiwe nitoe kiasi hiki cha pesa kuwalipa mawakili, ningejivuta kufanya hivyo,” Bw Nabwera akasema.

“Je, tunajipata kuhitajika kulipa fedha nyingi kama ada za mawakili kwa sababu ya utepetevu au kukosa mawakili wa serikali? Mbona IEBC ilipe kiasi kikubwa kama hiki?” Bw Nabwera akauliza.

Naye Dkt Mugo akasema: “Tunahitaji ripoti ya kamati ya kuthibitisha madeni kabla ya fedha kama hizo kutolewa kwa kampuni za mawakili waliokodiwa na IEBC.”

Hata hivyo, Bw Marjan alitaja kiasi hicho cha fedha kama halali akisema ukodishaji wa mawakili kutoka nje uliidhinishwa na Afisi ya Mwanasheria Mkuu.

“Mawakili wetu hawangeweza kushughulikia idadi kubwa ya kesi za kupinga matokeo ya chaguzi mbalimbali zilizowasilishwa dhidi ya IEBC mahakamani,” Afisa huyo Mkuu Mtendaji akaiambia PAC Jumatatu, Agosti 26, 2024.

“IEBC ilitafuta ushauri kutoka kwa Mwanasheria Mkuu na akasema kuwa IEBC haiwezi kutumia mawakili walioko katika afisi yake. Alisema IEBC hutunga kanuni zake mahsusi kuhusu ukodishaji mawakili kutoka nje,” Bw Marjan akaambia kamati hiyo chini ya uongozi wa Mbunge wa Butere Tindi Mwale.

Bw Marjan alifichua kuwa tume hiyo ina mawakili wanne wanaoongozwa na Bw Chrispinus Owiye, mkurugenzi wa masuala ya kisheria.

Baada ya uchaguzi mkuu wa 2017, jumla ya kesi 301 za kupinga matokeo ya chaguzi za viti mbalimbali ziliwasilishwa mahakamani.

Kesi hizo zilijumuisha ile ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais na ambapo matokeo hayo yalibatilishwa.

Katika uchaguzi mkuu wa 2022, IEBC ilikumbwa na kesi 124 za kupinga matokeo ya chaguzi, ikiwemo ile ya kupinga matokeo ya urais na iliyofeli.

Baadhi ya kampuni za mawakili zinazoidai IEBC mamilioni ya fedha ni pamoja na Cootow and Associates (Sh20.52 milioni), Mukele Moni and Advocates (Sh17.2 million) kuhusu kesi tano za chaguzi zilizowasilishwa Nairobi, Garane and Somane Advocates (Sh55.6 million) na kampuni ya Kimani Muhoro and Advocates inayodai jumla ya Sh12.8 million.

chaguzi
DENI
iebc
wabunge

MBUNGE wa Kimilili Didmus Barasa amekanusha madai kwamba amewahi kula rushwa kutoka kwa mtu yeyote.

Alisema haya alipoagizwa kufika mbele ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuhusu madai ya kuitisha hongo ya Sh2 milioni kutoka kwa mwanamke mfanyabiashara mwaka uliopita, 2023.

Alisema Jumapili, Agosti 25, 2024 kuwa pesa hizo zilikuwa mkopo kutoka kwa mwanasiasa huyo.

Bw Barasa alisema mwanasiasa huyo aliyewahi kugombea ugavana ndiye chanzo cha masaibu yake ambapo baada ya kutofautiana naye kuhusu malipo ya deni hilo, alizua madai hayo ya rushwa ili kumpaka tope.

“Ningependa kukufahamisha kuwa Sh2, 000, 000 zilizotumwa kwenye akaunti yangu ya benki zilikuwa mkopo kutoka kwa mwanasiasa huyo aliyewania bila kufua dafu ugavana katika kaunti moja nchini, Desemba 13, 2023. Nakala hizo zinafanana kabisa na zinazotumika katika mchakato wa kutuma pesa katika akaunti ya benki, zinaashiria ni mkopo, unaweza kuzidurusu. Suala kuhusu ni kwa nini sijalipa, ikiwemo mvutano kuhusu masharti ya kandarasi si tatizo lenu,” alisema Bw Barasa.

Alisema suala hilo liliripotiwa kwa Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI) Karen na likapuuziliwa mbali.

“Hii ni kuwafahamisha kuwa sitatimiza maagizo hayo kwa sababu ni ukiukaji wa majukumu ya tume. Hamuwezi mkanialika nitawatafsirie sababu ni kwa nini hela hizo zilitumwa ilhali mmesoma nakala zinazothibitisha mchakato huo kwa sababu, hata kama kiasi kilichotumwa ni Sh100, unahitaji nakala za kuthibitisha,” alisema.

“Kama sijazingatia wajibu wa kifedha, ni kwa sababu ya mzozo kati yangu na mhusika. Ni sharti nieleze EACC kuwa mna jukumu muhimu kwa Katiba yetu. Hamna wajibu wa kusaidia mhusika kulipwa hela alizonikopesha. Mna stakabadhi zinazoonyesha ni kwa nini fedha hizo zilitumwa kwenye akaunti yangu. Acha mhusika aende kortini tukutane huko.”

Jumapili, EACC ilimwagiza Bw Barasa kujibu kuhusu madai hayo ya ulaji rushwa.

Kupitia barua iliyoandikwa Agosti 21, 2024 EACC ilisema “pesa hizo zilitumwa Desemba 13, 2023.”

Kulingana na tume, hii ni mara ya pili inamwagiza Bw Barasa kujiwasilisha kwake baada ya kukaidi kujitokeza Agosti 14, 2024 jinsi alivyoagizwa.

Baada ya kukaa rumande kwa siku 15, mlinzi Spencer Kipkorir alipata afueni alipoachiliwa na hakimu mwandamizi Kennedy Cheruiyot Jumatano.

Wakili Ham Kiplagat aliyemwakilisha Spencer alieleza mahakama kwamba mkurugenzi wa mashtaka ya umma hajafikia uamuzi ikiwa atamfungulia mashtaka mshukiwa huyo au la.

“Afisa anayechunguza kesi dhidi ya mshukiwa hajakamilisha zoezi hilo kwa vile chuo kikuu cha Nairobi kinefungwa na mashahidi,” kiplagat aliambia hakimu.

Aliomba mshukiwa aachiliwe kwa dhamana akiongeza” siku ile uchunguzi utakamilika DPP ataamua ikiwa atamfungulia mashtaka.”

Wakili Ham Langat (kushoto) akiwa na Kipkorir nje ya mahakama ya Milimani. Picha/ Richard Munguti
Akitoa uamuzi Bw Cheruiyot alisema mashahidi hawajapatikana na mshukiwa hawezi zuiliwa hadi wakati ule mashahidi watakapopatikana.

Hakimu alimwachilia kwa dhamana ya Sh1milioni moja pesa tasilimu.

Bw Cheruiyot alimwamuru mshhkiwa huyo aripoti kila siku kwa afisa anayexhunguza kesi hiyo katika kituo cha polisi cha Kilimani hadi uamuzi wa kumfungulia mashtaka utakapochukuliwa na DPP.

Bw Cheruiyot alisema madai yanayomkabili mshukiwa huyu ni makali kwa vile mwanafunzi wa chuo kikuu alipoteza maisha.

rumande

Baada ya kukaa rumande kwa siku 15, mlinzi Spencer Kipkorir alipata afueni alipoachiliwa na hakimu mwandamizi Kennedy Cheruiyot Jumatano.

Wakili Ham Kiplagat aliyemwakilisha Spencer alieleza mahakama kwamba mkurugenzi wa mashtaka ya umma hajafikia uamuzi ikiwa atamfungulia mashtaka mshukiwa huyo au la.

“Afisa anayechunguza kesi dhidi ya mshukiwa hajakamilisha zoezi hilo kwa vile chuo kikuu cha Nairobi kinefungwa na mashahidi,” kiplagat aliambia hakimu.

Aliomba mshukiwa aachiliwe kwa dhamana akiongeza” siku ile uchunguzi utakamilika DPP ataamua ikiwa atamfungulia mashtaka.”

Wakili Ham Langat (kushoto) akiwa na Kipkorir nje ya mahakama ya Milimani. Picha/ Richard Munguti

Akitoa uamuzi Bw Cheruiyot alisema mashahidi hawajapatikana na mshukiwa hawezi zuiliwa hadi wakati ule mashahidi watakapopatikana.

Hakimu alimwachilia kwa dhamana ya Sh1milioni moja pesa tasilimu.

Bw Cheruiyot alimwamuru mshhkiwa huyo aripoti kila siku kwa afisa anayexhunguza kesi hiyo katika kituo cha polisi cha Kilimani hadi uamuzi wa kumfungulia mashtaka utakapochukuliwa na DPP.

Bw Cheruiyot alisema madai yanayomkabili mshukiwa huyu ni makali kwa vile mwanafunzi wa chuo kikuu alipoteza maisha.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment