Bao La Asubui-Awamu 4 utakumbana nazo baada ya Kustaafu.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Awamu 4 Kubwa Utakazopitia BAADA Ya KUSTAAFU.

Mara baada ya kutoka kazini, kuna vipindi ambavyo kila mstaafu lazima avipitie.

Uimara wako katika kuvipitia vipindi hivi kwa mafanikio ndio itajulisha pia utafanikiwa kwa kiwango gani baada ya kustaafu.

a. Vacation Phase (Awamu Ya Kuwa Likizo)

b. Loss And Lost Phase (Awamu Ya Kupoteza Na Kupotea)

c. Awamu Ya Tatu: Trial And Error (Kujaribu Vitu Vipya)

d. Awamu Ya Nne: Reinvent & Rewire (Kutengeneza Mwanzo Mpya).

Leo tutaangalia awamu ya kwanza:

a. Vacation Phase (Awamu Ya Kuwa Likizo)

Mara baada ya kutoka kazini, mstaafu hukutana na kipindi hiki cha kwanza…

…ambacho mara nyingi hudumu kwa muda kama wa mwaka mmoja hivi.

Katika kipindi hiki, mstaafu mara nyingi huwa na furaha kwa sababu anakuwa hana misukosuko.

Na watu wengi wanakuwa wana mthamini kwa sababu walimmisi kwa muda mrefu sana.

Kwa sababu kwa miaka mingi alikuwa bize mno.

Baadhi ya vitu ambavyo vinatokea ni pamoja na:

i. Ideal Retirement (Kufurahia Hali Ya Kustaafu).

ii. Relaxation (Kujiachia)

iii. Freedom (Uhuru Wa Kufanya Mambo Yako)

iv. Boredom Starts (Unaanza Kuboreka).

Tunaanza kwa kuangalia Ideal Retirement.

Katika kipindi hiki, mstaafu ndio anaona haswa amestaafu.

Kwa sababu anakuwa hana kitu cha kufanya.

Yaani hakuna tena kukimbizana asubuhi kuamka mapema.

Wala kupigiwa simu na kuuliziwa kuhusu jambo fulani au kuambiwa akafuatilie jambo fulani.

Mara nyingi kwenye kipindi hiki, mstaafu atakuwa anaonesha kufurahia maisha mapya.

Maisha ambayo hakuwahi kuwa nayo kwa muda mrefu sana.

Kwenye kipindi hiki, utatembelewa na watu wengi sana.

Na kila utakakoenda kutembelea watakupokea kwa furaha sana.

Unakuwa mtu muhimu kwenye jamii yako.

Ila usisahau, huwa hakidumu, utaona kinachotokea kwenye awamu ya pili.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment