Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Natumai unaendelea vyema, karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara ya leo, ikiwa ni tarehe 22.08.2024.
WIZARA ya Fedha imetoa kima cha Sh40 bilioni kwa idara mbalimbali za serikali, ili kufanikisha utendakazi wa serikali.
Bw John Mbadi ndiye Waziri wa Fedha na Hazina ya Kitaifa.
Fedha hizo zimesambazwa kama ifuatavyo:
Idara ya Elimu ya Msingi imepokea Sh1.6 bilioni kufadhili elimu ya bure katika shule za msingi, ilhali Sh 14.1 bilioni zingine zitatumika kwa masomo ya sekondari ya bure katika shule za kutwa.
Kitita kingine cha Sh6.1 bilioni, kimetengewa Idara ya Elimu ya Sekondari Msingi.
Bodi ya Kufadhili Elimu ya Juu (Helb) na Bodi ya Hazina ya Vyuo Vikuu, zimetengema Sh5.1 bilioni na Sh2.8 bilioni, mtawalia.
Idara ya Barabara imepewa Sh2 bilioni huku ile ya Unyunyiziaji imekabidhiwa Sh2.6 bilioni.
Katika kilimo, Bodi ya Mazao na Nafaka (NCPB) itapokea Sh2 bilioni kulipa madeni ya mbolea nafuu katika Mwaka wa Kifedha 2023|2024 kulipokuwa na mvua chache na kubwa.

Shirika la Maziwa (KCC), limepokezwa Sh800 milioni katika Idara ya Mashirika.
Hazina inayolenga kuwainua wafanyabiashara wadogo wadogo, ambayo ilibuniwa na Rais William Ruto alipotwaa uongozi 2022 maarufu kama Hustler Fund, imeongezewa kima cha Sh500 milioni kupiga jeki operesheni zake.
Sh1 bilioni zimetengewa Wizara ya Viwanda ili zitumike katika ujenzi wa Viwanda vya Uzalishaji Mazao ya Kilimo, maarufu kama County Aggregation and Industrial Parks (CAIPS).
Idara ya Uwekezaji, imetengewa Sh600 milioni ili kufaidi shughuli za usindikaji wa bidhaa za kusafirisha nje ya nchi.

ALIYEKUWA Waziri Mkuu, Bw Raila Odinga, Jumatano, Agosti 21, 2024 alitangaza kwamba amejiondoa kutoka siasa za Kenya na kuingia katika siasa za Bara la Afrika katika juhudi zake za kuwania uenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika (AUC).
Bw Odinga alisemna kuwa hatajishughulisha sana na siasa za Kenya kuanzia sasa ili kuangazia kampeni zake za wadhifa wa Bara.
Akizungumza wakati wa kikao cha pili na wanahabari pamoja na Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi jijini Nairobi, Bw Odinga alisema atawekeza juhudi zote katika kampeni zake baada ya kuwasilisha rasmi ombi la kuwania uenyekiti wa AUC.
“Nitaanza kufanya kazi barani mara tu nitakapochaguliwa na hiyo itakuwa Februari mwaka ujao, 2025.

“Kwa sasa ninahusika katika kampeni lakini hiyo haimaanishi kuwa Kenya itakoma kuwepo,” Bw Odinga alisema.
Aliendelea: “Sitashiriki sana katika siasa za Kenya kuanzia sasa ninapoendelea kuelekeza mawazo yangu katika kampeni ya bara. Lakini ni kipindi cha mpito kutoka kushiriki kikamilifu siasa za Kenya hadi siasa za bara la Afrika,” alisema.
Jumanne, Agosti 27, 2024 Rais William Ruto atamtambulisha rasmi waziri mkuu huyo wa zamani kama mgombeaji wa kiti cha uenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika (AUC) na kuzindua rasmi kampeni zake kote barani.
Bw Mudavadi, ambaye pia ni Waziri wa Masuala ya Kigeni na Wakenya walio ng’ambo mnamo Jumatano Agosti 21, 2024 alitangaza kwamba Dkt Ruto atatoa ratiba rasmi ya kampeni ya Raila.
Bw Mudavadi alisema azma ya Bw Odinga kuwania wadhifa wa juu wa bara ni “shughuli ya kitaifa.”
“Hii ni zaidi ya ugombeaji tu; ni shughuli ya kitaifa. Mheshimiwa Raila Odinga anawakilisha sauti, maadili na matarajio ya Kenya katika bara hili. Anaposonga mbele, tusimame naye, si tu kama serikali bali kama watu walioungana,” Bw Mudavadi alisema.
Aliwataka Wakenya kumuunga mkono kiongozi huyo wa ODM.
“Kwa Wakenya wenzangu, kama taifa, kila mara tunaungana ili kusimama nyuma ya mmoja wetu, iwe kwenye nyimbo, uwanjani, au kwenye jukwaa la kimataifa. Kama tulivyoshangilia wanamichezo wetu katika michezo ya Olimpiki ya hivi karibuni, tumuunge mkono kikamilifu Mheshimiwa Raila akibeba bendera ya Kenya juu katika kinyang’anyiro cha Uenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika.”
Bw Mudavadi alisema kuwa Rais Ruto atazindua rasmi timu ya kampeni ya Bw Odinga, na kuongeza kuwa sekretarieti hiyo itatayarisha kampeni kali kote barani.
Baadhi ya wapanga mikakati wa Bw Odinga ni pamoja na; aliyekuwa balozi wa Kenya nchini Amerika Elkanah Odembo, aliyekuwa katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) Mahboub Maalim, Balozi Anthony Okara, Prof Makau Mutua na aliyekuwa Naibu Gavana wa Nyeri Dkt Caroline Karugu.
Bw Mudavadi alisema kuwa katika ombi lake la kutaka kuwa mwenyekiti wa AUC, Bw Odinga alieleza maono yake kwa muungano huo wa kanda ambayo alibainisha kuwa yanaegemea nyanja mbalimbali zikiwemo ushirikiano wa Afrika na maendeleo ya miundombinu, mabadiliko ya kiuchumi Barani Afrika, kuimarisha biashara Afrika, uhuru wa kifedha, mabadiliko ya kilimo, hatua za hali ya hewa, amani na usalama, uwezeshaji wa vijana, na usawa wa kijinsia.
Bw Odinga alisema anafurahi kwamba serikali ya Kenya imemfanya kuwa mgombea wake rasmi.

WAZIRI wa Madini, Uchumi wa Majini na Masuala ya Bahari, Bw Ali Hassan Joho, amelaumu mashirika mengine ya serikali kwa kutatiza ujenzi wa Kituo cha Huduma na Mafunzo ya Kilimo cha Uvuvi cha Kabonyo kwa gharama ya Sh2.5 bilioni eneo la Nyando, Kaunti ya Kisumu.
Licha ya fedha kupatikana kwa mradi huo wa mabilioni, Waziri huyo alishtumu maafisa wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (Nema) na Mamlaka ya Kitaifa ya Ujenzi (NCA) kwa kuhujumu mradi huo uliozinduliwa na Rais William Ruto Oktoba 6, 2023.
“Tayari tumepata mwanakandarasi na kutia saini, tumekamilisha miundo na fedha zilitolewa na serikali ya Hungary. Kwa bahati mbaya, hatukuweza kuanzisha mradi huu kutokana na vizingiti vilivyowekwa na maafisa wa Nema na NCA,” alisema Jumanne, Agosti 20, 2024 wakati wa ziara rasmi mjini Kisumu.
Katika juhudi za kupata idhini kutoka kwa Nema na NCA, Bw Joho alisema mwanakandarasi huyo mpya alizungushwa kutoka afisi moja hadi nyingine na kuchelewesha ujenzi wa mradi huo unaolenga kuimarisha uvuvi katika eneo hilo.
Waziri huyo aliagiza afisi hizo mbili kuwezesha mwanakandarasi huyo kuanza mradi huo wiki hii kabla ya ziara ya Rais Ruto katika eneo la Nyanza wiki mbili zijazo.

ZIARA ya Ikulu na madai ya kuingiliwa kisiasa yamehusishwa na hatua ya Seneti kumtimua Gavana wa Meru Kawira Mwangaza, huku jaribio la dakika za mwisho la magavana wa kike za kumuokoa mwenzao zikigonga mwamba.
Waliopanga kumtimua waliwashawishi maseneta kwa misingi ya kisiasa wakilenga kura nyingi zaidi za wale wa muungano tawala wa Kenya Kwanza.
Kulingana na duru zinazofahamu njama za kisiasa zilizosababisha kutimuliwa kwa Bi Mwangaza, timu ya viongozi wa kisiasa kutoka Meru ilienda Ikulu Jumatatu ambapo waliripotiwa kumsihi Rais William Ruto kutoingilia suala hilo.
Wakiwa na ujasiri, timu hiyo ilienda kwa Seneta wa Kenya Kwanza, anayeshikilia wadhifa mkubwa wa uongozi na kumpa jukumu la kuwashawishi maseneta 28 kutoka muungano huo, idadi iliyotosha kumpeleka nyumbani Bi Mwangaza, mwenye umri wa miaka miaka 50.
Mkakati huu ulikuwa wa kuhakikisha wamevuka hitaji la kisheria la maseneta 24 wanaohitajika kuunga mkono kuondolewa mamlakani kwa Gavana Kawira.
Bi Mwangaza alipata agizo la Mahakama kusitisha kwa muda kutimuliwa kwake.
“Viongozi walioenda Ikulu walitajwa wakati wa kusikilizwa kwa mashtaka mbele ya seneti. Walimsihi Rais asichukue msimamo kuhusu suala hilo. Hii iliwapa nguvu za kufanikisha ushawishi kwa misingi ya chama,” alisema mdokezi anayejua yaliyoendelea..
Mdokezi huyo alisema magavana wa kike walijaribu kuingilia kati kwa kuwasiliana na Rais lakini inasemekana hakuchukua msimamo wowote.
Muungano wa Kenya Kwanza una maseneta 30 baada ya maseneta sita wa United Democratic Movement na Jubilee Party kujitenga na upinzani na kushirikiana na muungano tawala, na kuongeza maseneta 24 wa United Democratic Alliance (22) na mmoja kutoka Ford Kenya na Democratic Party (DP).
Azimio kwa sasa ina maseneta 17, 13 kutoka ODM, watatu kutoka Wiper ya Kalonzo Musyoka na Seneta wa Busia Okiya Omtatah wa chama cha National Reconstruction Alliance.
Upigaji kura ulipoitishwa na Spika wa Seneti Amason Kingi, maseneta 26 walipiga kura kuunga mkono shtaka la kwanza la ukiukaji mkubwa wa Katiba na sheria zingine huku maseneta wanne wakipiga kura dhidi ya shtaka hilo na 14 wakisusia.
Maseneta hao 26 walipiga kura tena kuunga mkono shtaka la pili la utovu wa nidhamu, huku wawili pekee wakipiga kura kupinga.
Waliosusia walikuwa 14.
Katika shtaka la tatu la matumizi mabaya ya afisi, maseneta 27 walipiga kura kuunga mkono, mmoja akipinga huku 14 wakikataa kushiriki.
Hata hivyo, upigaji kura haukuendelea bila mtafaruku kwani kizaazaa kilizuka katika Seneti huku maseneta wakipiga kelele huku Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna akifikia hatua ya kumwita Spika Kingi “aibu”.
Seneta mteule Gloria Orwoba alitupwa nje ya Bunge na Spika Kingi, alipolalamikia ukosefu wa mjadala kabla ya kupiga kura.
Maseneta wa Azimio walikataa kushiriki upigaji kura na wakaungana na Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, anayetoka Kenya Kwanza.

UKOSEFU wa dawa muhimu ni changamoto kuu kwa wagonjwa wa Saratani katika eneo la Nyanza licha ya magavana wa eneo hilo kujizatiti kujenga vituo vya kutibu ugonjwa huo hatari.
Changamoto hiyo ilijitokeza waziwazi Jumatano, Agosti 21, 2024 Gavana wa Kisii Simba Arati alipofungua rasmi kitengo cha kutibu Saratani katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kisii (KTRH).
Wagonjwa wa kansa, watunzaji wao na waliopona baada ya kupata tiba walimwarifu Bw Arati kwamba juhudi zake za kupambana na ugonjwa huo zisiishie katika uzinduzi wa kitengo hicho pekee bali ahakikishe zipo dawa za kutosha.
Walielezea mateso wanayopitia kwa kukosa dawa za kudhibiti makali ya ugonjwa huo katika hospitali za umma na wakamtaka Bw Arati kununua dawa hizo.
Kwa mfano, walitaja dawa ya Tomoxifen inayotumiwa kutibu Kansa ya matiti kwa wanaume na wanawake, wakisema ni nadra kupatikana au haipatikani kabisa.
“Dawa hii ya Tomoxifen haipatikani hapa Kisii na hata katika hospitali nyingine za kaunti za eneo zima la Nyanza. Mara nyingi huwa tunaagizwa kusaka dawa hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Moi (MTRH) Eldoret,” akasema mgonjwa mmoja ambaye alimshukuru Gavana Arati kwa kujenga Kitengo cha kutibu kansa katika hospitali ya KTRH.
Mgonjwa huyo vilevile, alieleza kuwa kadi ya Bima ya Kitaifa ya Afya (NHIF) haiwezi kuwasaidia kupata Tomoxifen katika hospitali za kibinafsi.
Sasa wagonjwa hao wanalazimika kusaka dawa sehemu za mbali, hali ambayo inawabebesha gharama kubwa.
“Ugonjwa huu umetufyonza rasilimali. Tumesalia maskini hohehahe,” akasema mgonjwa huyo, aliyeomba tubane jina lake.
Dkt Bahati Riogi, mtaalamu wa Kansa na msimamizi wa kitengo cha kushughulikia ugonjwa huo hospitalini KTRH, alithibitisha uwepo wa tatizo la uhaba wa dawa.
“Dawa ya Tomoxifen, ambayo mgonjwa anafaa kumeza kila siku kwa kati ya miaka mitano na 10, huimarisha afya ya mgonjwa anayeugua Kansa ya matiti. Dawa hiyo inagharimu Sh300 katika maduka ya dawa kwa muda wa mwezi mmoja. Bei hiyo inaonekana nafuu. Lakini ukipiga hesabu Sh300 kwa miezi 12 na miaka 10 ni pesa nyingi zaidi kwani wagonjwa hao pia wanakumbwa na gharama nyingine maishani,” akasema.
Dkt Barasa alieleza kuwa kuletwa kwa dawa hiyo karibu na watu katika vituo vya kiafya kutawafaa zaidi wagonjwa wa Saratani.
Kwa upande wake, Gavana Arati aliahidi kununua dawa hizo na kuzisambaza katika vituo vya afya katika kaunti hiyo.
HABARI MSETO KUTOKA KWINGINEKO
- zilizopitzilizopitaMpango wa kusitisha mapigano Gaza ni wa dharura – Biden.Chanzo cha picha,Getty ImagesRais wa Marekani Joe Biden “amesisitiza dharura” ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza na kuachiliwa kwa walioshilikiliwa mateka, Ikulu ya Marekani imesema.Katika mazungumzo ya simu siku ya Jumatano, ambayo pia Makamu wa Rais Kamala Harris alijiunga nayo, Bw Biden alizungumzia umuhimu wa kuondoa “vikwazo vyovyote vilivyosalia” vinavyozuia makubaliano na Hamas.Pia alisisitiza dhamira ya Washington ya kusaidia kuilinda Israel dhidi ya kile Ikulu ya White House ilichokiita “vitisho vyote kutoka Iran, vikiwemo vikundi vya kigaidi vyenye uhusiano wa karibu vya Hamas, Hezbollah na Houthi”.Hayo yamejiri baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani kumaliza ziara ya kidiplomasia katika eneo la Mashariki ya Kati, akishinikiza kupatikana kwa makubaliano ambayo yanaweza kumaliza vita.Soma zaidi:Israel na Gaza: Je, kwanini mpango wa kusitsha mapigano wa Marekani ni mgumu kutekeleza?Kifahamu kikosi cha Jeshi la Israel katika milima ya GolanMshirikishe mwenzako, Mpango wa kusitisha mapigano Gaza ni wa dharura – BidenDakika 29 zilizopitaMvulana, 6, apatikana katika msitu wa Vietnam baada ya siku tano.Chanzo cha picha,chombo cha habari cha serikali ya VietnamMvulana mwenye umri wa miaka sita ambaye alitoweka kwa siku tano sasa amepatikana ndani kabisa ya msitu nchini Vietnam.Dang Tien Lam, ambaye anaishi katika mkoa wa kaskazini-magharibi wa Yen Bai, alikuwa akicheza kwenye mkondo wa maji na ndugu zake tisa mnamo Agosti 17 wakati alipoingia kwenye vilima na kupotea, ripoti za ndani zilisema.Alipatikana Jumatano na wakulima wa eneo hilo ambao walisikia sauti ya mtoto akilia walipokuwa wakisafisha shamba la mdalasini karibu na msitu huo.Lam, ambaye alikutwa amekaa kwenye vichaka vya mihogo takriban kilomita 6 (3.7mi), kutoka alikopotea, alikuwa amedhoofika sana na kushindwa kusimama.”Nimechoka sana, siwezi kusimama, tafadhali nibebeni”, Lam alisema, kulingana na mkulima mwenye umri wa miaka 52 Ly Van Nang, ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliompata mvulana huyo.Lam aliishi kwa kula majani na matunda ya mwituni, na pia kunywa maji ya mto, ripoti zilisema.Picha mtandaoni zinaonyesha wenyeji wakimhudumia na kumpa keki baada ya kufikishwa nje ya msitu.Alikuwa amevalia fulana nyekundu na kaptula ambayo imechafuka kweli kweli.Mshirikishe mwenzako, Mvulana, 6, apatikana katika msitu wa Vietnam baada ya siku tanoSaa 1 iliyopitaRaia wa Nigeria wakasirishwa na ndege mpya ya raisgChanzo cha picha,Nigeria PresidencyMaelezo ya picha,Rais Tinubu alisafiri hadi Ufaransa kwa ndege hiyo mpyaaMpango wa kusitisha mapigano Gaza ni wa dharura – Biden
Chanzo cha picha,Getty ImagesRais wa Marekani Joe Biden “amesisitiza dharura” ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza na kuachiliwa kwa walioshilikiliwa mateka, Ikulu ya Marekani imesema.Katika mazungumzo ya simu siku ya Jumatano, ambayo pia Makamu wa Rais Kamala Harris alijiunga nayo, Bw Biden alizungumzia umuhimu wa kuondoa “vikwazo vyovyote vilivyosalia” vinavyozuia makubaliano na Hamas.Pia alisisitiza dhamira ya Washington ya kusaidia kuilinda Israel dhidi ya kile Ikulu ya White House ilichokiita “vitisho vyote kutoka Iran, vikiwemo vikundi vya kigaidi vyenye uhusiano wa karibu vya Hamas, Hezbollah na Houthi”.Hayo yamejiri baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani kumaliza ziara ya kidiplomasia katika eneo la Mashariki ya Kati, akishinikiza kupatikana kwa makubaliano ambayo yanaweza kumaliza vita.Soma zaidi:Israel na Gaza: Je, kwanini mpango wa kusitsha mapigano wa Marekani ni mgumu kutekeleza?Kifahamu kikosi cha Jeshi la Israel katika milima ya GolanMshirikishe mwenzako, Mpango wa kusitisha mapigano Gaza ni wa dharura – Biden - Dakika 29 zilizopitaMvulana, 6, apatikana katika msitu wa Vietnam baada ya siku tano
Chanzo cha picha,chombo cha habari cha serikali ya VietnamMvulana mwenye umri wa miaka sita ambaye alitoweka kwa siku tano sasa amepatikana ndani kabisa ya msitu nchini Vietnam.Dang Tien Lam, ambaye anaishi katika mkoa wa kaskazini-magharibi wa Yen Bai, alikuwa akicheza kwenye mkondo wa maji na ndugu zake tisa mnamo Agosti 17 wakati alipoingia kwenye vilima na kupotea, ripoti za ndani zilisema.Alipatikana Jumatano na wakulima wa eneo hilo ambao walisikia sauti ya mtoto akilia walipokuwa wakisafisha shamba la mdalasini karibu na msitu huo.Lam, ambaye alikutwa amekaa kwenye vichaka vya mihogo takriban kilomita 6 (3.7mi), kutoka alikopotea, alikuwa amedhoofika sana na kushindwa kusimama.”Nimechoka sana, siwezi kusimama, tafadhali nibebeni”, Lam alisema, kulingana na mkulima mwenye umri wa miaka 52 Ly Van Nang, ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliompata mvulana huyo.Lam aliishi kwa kula majani na matunda ya mwituni, na pia kunywa maji ya mto, ripoti zilisema.Picha mtandaoni zinaonyesha wenyeji wakimhudumia na kumpa keki baada ya kufikishwa nje ya msitu.Alikuwa amevalia fulana nyekundu na kaptula ambayo imechafuka kweli kweli.Mshirikishe mwenzako, Mvulana, 6, apatikana katika msitu wa Vietnam baada ya siku tano - Saa 1 iliyopitaRaia wa Nigeria wakasirishwa na ndege mpya ya rais
Chanzo cha picha,Nigeria PresidencyMaelezo ya picha,Rais Tinubu alisafiri hadi Ufaransa kwa ndege hiyo mpya
- iliyopitaRaia wa Nigeria wakasirishwa na ndege mpya ya rais
Chanzo cha picha,Nigeria PresidencyMaelezo ya picha,Rais Tinubu alisafiri hadi Ufaransa kwa ndege hiyo mpyaRaia wengi wa Nigeria wameghadhabika baada ya ndege mpya kununuliwa kwa ajili ya Rais Bola Tinubu wakati ambapo uchumi unakumbwa na mzozo mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kizazi.Ndege hiyo imenunuliwa wiki mbili baada ya maelfu ya watu kumiminika barabarani kote nchini kulalamikia njaa inayoongezeka na kupanda kwa gharama ya maisha.Bw Tinubu ambaye alichaguliwa mwaka jana kuongoza nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika, ameanzisha mageuzi kadhaa ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta, ambayo imechangia mfumuko mkubwa wa bei, ambao kwa sasa ni zaidi ya 30%.Rais Tinubu alisema mageuzi hayo ni muhimu ili kupunguza matumizi ya serikali na kuchochea ukuaji wa muda mrefu.Mnamo Januari, rais wa Nigeria alitangaza kupunguza kwa asilimia 60 ya idadi ya maafisa wa serikali wanaosafiri nje ya nchi , ikiwa ni pamoja na wasaidizi wake mwenyewe.Hata hivyo Jumatatu, rais aliondoka kuelekea Ufaransa kwa kutumia ndege mpya aina ya Airbus A330, ambayo imekuwa nyongeza ya hivi punde zaidi ya ndege zaidi ya tano za rais.Gharama ya ndege hiyo haijawekwa wazi, na wala sababu ya safari yake hhaijaelezwa wazi.Mtumiaji wa X @Fdmlearn alisema haikuwa sawa kwamba Wanigeria waliambiwa wapate maumivu ya kiuchumi wakati serikali inamnunulia rais ndege mpya.Mtumiaji mwingine wa X @RealOlaudah alikasirika zaidi.“Tuambizane ukweli. Ununuzi mpya wa ndege ya rais wa Airbus ya Tinubu kwa fedha za Nigeria bilioni 150 wakati wa njaa, na mahitaji ya kitaifa unaonyesha jinsi alivyo muovu, mbinafsi, mwenye kujifurahisha, na asiyejali masaibu ya Mnigeria wa kawaida.Hata hivyo, @Timi_The_Law anasema anaunga mkono uamuzi wa rais kwani ndege hiyo si ya kibinafsi bali ni ya ofisi ya rais.Mshirikishe mwenzako, Raia wa Nigeria wakasirishwa na ndege mpya ya rais - Saa 2 zilizopitaKenya: Maafisa wa jiji la Nairobi wawakamata watu kwa kujisaidia katikati ya jiji
Chanzo cha picha,Publicis PixelparkWakaazi 30 wa Nairobi wameripotiwa kukamatwa kwa kujisaidia haja ndogona kutupa uchafu katika Wilaya yenye shughuli nyingi kibiashara jijini Nairobi (CBD) kama sehemu ya hatua ya serikali ya kaunti ya Nairobi ya kukabiliana na makosa madogo.Wakiongozwa na afisa mkuu wa mazingira wa jiji la Nairobi Geoffrey Mosiria, timu za watekelezaji sheria za kaunti hiyo zwalishika doria katika mitaa iliyochaguliwa ya CBD ili kuwakamata Wakenya waliokiuka sheria hiyo.Sheria ya kero ya Umma ya Nairobi 2021 inasema kwamba mtu yeyote atakayepatikana akijisaidia haja ndogo au haja kubwa katika eneo la umma atawajibika kulipa faini ya Ksh.10,000, kifungo cha miezi sita jela au kupewa adhabu zote mbili.Zaidi ya hayo, viongozi wa kaunti hiyo waliwaamuru wafanyabiashara wa barabarani kusafisha lundo lao la takataka na kuzitupa ipasavyo.Wahalifu 30 walikamatwa Jumatatu usiku na kufikishwa katika mahakama ya jiji siku ya Jumanne ambayo iliwapatia adhabu ya kufanya kazi kwa manufaa ya umma katika vituo vya umma.Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na kusafisha chumba cha kuhifadhia maiti cha jiji na uwanja wa Uhuru Park.Mshirikishe mwenzako, Kenya: Maafisa wa jiji la Nairobi wawakamata watu kwa kujisaidia katikati ya jiji - Saa 3 zilizopitaDRC: Takriban watu 24 wafa maji baada ya boti yao kupinduka
Chanzo cha picha,Getty ImagesMaelezo ya picha,Boti zinazobeba abiria kwenye Mito ya Kongo mara nyingi hazitunzwa vizuri na zinajaa kupindukiaTakriban watu 24 wamefariki katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo baada ya mashua iliyokuwa imejaza mizigo kupinduka kwenye mto katika jimbo la Mai-Ndombe nchini Kongo, na idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka huku abiria wengi wakitoweka, afisa mmoja wa eneo hilo alisema Jumatano.Boti iliyobeba takriban abiria 250 hadi 300 ilipinduka Jumapili usiku baada ya kugonga vizingiti chini ya maji, msimamizi wa eneo la Kutu Jacques Nzenza aliliambia shirika la habarila Reuters.Kupakia watu na miziko kupita kiasi ndio chanzo kikuu cha ajali hiyo, alisema. “Kulikuwa na wasi wasi katika boti na watu waliojawa na hofu walienda kwenye sehemu moja kuweka uzito upande mmoja, na kusababisha mashua kupinduka.”Kiongozi wa jumuiya ya kiraia katika eneo hilo, Fidele Lizoringo, amesema watu 43 walinusurika lakini wanakijiji waliokuwa na hasira walimpiga meneja wa boti hiyo kwa sababu baadhi ya ndugu zao walikufa katika ajali hiyo.Usafiri wa kwenye mito na ajali mbaya za boti ni jambo la kawaida katika nchi hiyo ya Afrika ya kati, ambayo ina barabara chache za lami katika eneo lake kubwa lenye misitu na vyombo vya usafiri mara nyingi hupakiwa kupita uwezo wake.Mshirikishe mwenzako, DRC: Takriban watu 24 wafa maji baada ya boti yao kupinduka - Saa 4 zilizopitaPostikadi yafika ilipokusudiwa miaka 121 baada ya kutumwa
Chanzo cha picha,Swansea Building SocietyPostikadi ambayo haijawasilishwa hatimaye imefika mahali ilipokusudiwa takriban miaka 121 baada ya kuchapishwa kwa mara ya kwanza kwenye chapisho.Kadi hiyo yenye mada ya Krismasi iliwasilishwa kwa Swansea Building Society’s tawi la Cradock Street nchini Uingereza, wiki iliyopita ingawa ilitumwa hapo awali mnamo 1903 – kwa hivyo ni zaidi ya karne moja tu.Wafanyakazi wanasema wanatumai kupata jamaa za Bibi Lydia Davies, ambaye hapo awali aliishi kwenye anwani hiyoambaye alikuwa ametumiwa kadi hiyo ili kuwakabidhi.Royal Mail ilisema kuna uwezekano postikadi hiyo “iliwekwa tena” kwenye mfumo wao, badala ya “kupotea kwenye chapisho kwa zaidi ya karne”.Mshirikishe mwenzako, Postikadi yafika ilipokusudiwa miaka 121 baada ya kutumwa - Saa 5 zilizopitaMiili 5 ilipatikana ndani ya boti ya kifahari iliyozama nchini Italia
Chanzo cha picha,EPAMaelezo ya picha,Yacht ya kifahari ya BayesianWafanyakazi wa uokoaji wamepata miili 5 Jumatano ndani ya boti ya kifahari ya Bayesian, ambayo ilizama Jumatatu kwenye pwani ya Sicily, kusini mwa Italia.Boti hiyo ya kifahari yenye urefu wa mita 56 iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Uingereza ilikuwa imebeba watu 22 (abiria 12 na wafanyakazi 10), akiwemo bilionea wa Uingereza na mtendaji mkuu wa benki ya Morgan Stanley.Boti hiyo, Bayesian ilizama katika dhoruba kali mapema Jumatatu asubuhi.Watu 15 waliokuwa ndani yake waliokolewa wakiwa hai na mtu mmoja akapatikana amekufa: mpishi wa boti, Recaldo Thomas.Bado mwili mmoja wa mwisho haujapatikana kati ya jumla ya sita waliopotea katika ajali hiyo.Watu ambao bado hawajapatikana wametajwa kuwa ni: tajiri wa teknolojia wa Uingereza Mike Lynch na binti yake mwenye umri wa miaka 18 Hannah; Mwenyekiti wa Kimataifa wa kampuni ya Morgan Stanley Jonathan Bloomer na mkewe Judy Bloomer; Chris Morvillo, wakili wa Marekani wa Lynch, na mkewe Neda Morvillo.Mshirikishe mwenzako, Miili 5 ilipatikana ndani ya boti ya kifahari iliyozama nchini Italia - Saa 6 zilizopitaJeshi latofautiana na vyombo vya habari kuhusu ajali ya ndege ya rais wa Iran
Chanzo cha picha,IRNA/ReutersMaelezo ya picha,Maelfu ya Wairani walijitokeza kumwona Raisi katika safari yake ya mwisho.Sababu ya ajali ya helikopta ya Iran, aliyosababisha kifo chaaliyekuwa rais wan chi hiyo Rais Ibrahim, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir Abdollahian na maafisa ni kutokana na kwamba ilikuwa imejazwa watu wengi zaidi wkupita kiasi.Shirika la Habari la Iran, Fars liliripoti hii Jumatano, likinukuu vyanzo vyake katika huduma za kijasusi. Jenerali wa Jeshi la Iran baadaye alisema kuwa huo ulikuwa uwongo.Shirika la Fars liliandika kwamba uchunguzi rasmi kuhusu ajali hiyo ulifikia hitimisho kwamba kulikuwa na watu wa ziada kwenye ndege hiyo.Ibrahim Raisi, aliyetajwa kuwa mrithi wa kiongozi mkuu zaidi wa nchi hiyo Ayatollah Ali Khamenei, alianguka Mei 20 katika eneo la milimani karibu na mpaka na Azerbaijan.”Helikopta iliyombeba Rais ilikuwa imebeba watu wawili zaidi ya inavyotakiwa na itifaki za usalama. Kwa hivyo, rubani alipoona ukungu na kujaribu kuruka helikopta hadi urefu alioutaka, hakuwa na nguvu za kutosha kufanya hivyo.Na katika hali ya kutoonekana vizuri (kutokana na ukungu), kulikuwa na mgongano na mlima,” shirika la habari la Urusi, TASS linanukuu taarifa hiyo, kutoka kwa shirika la Iran.Mkuu wa wafanyakazi wa Irani alisema kwamba toleo la vyanzo vya shirika la habari la Fars sio wakweli.Unaweza pia kusoma:Ebrahim Raisi: Kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali aliyekuwa rais wa IranNini kinachofuata nchini Iran baada ya kifo cha Rais Ebrahim Raisi?Mshirikishe mwenzako, Jeshi latofautiana na vyombo vya habari kuhusu ajali ya ndege ya rais wa Iran - Saa 6 zilizopitaRoketi za Hezbollah zapiga Milima ya Golan baada ya Israel kushambulia ndani kabisa ya Lebanon
Chanzo cha picha,ReutersMaelezo ya picha,Jenerali wa Israel aliishutumu Hezbollah kwa kuwalenga raia moja kwa moja huko KatzrinHezbollah imerusha makumi ya roketi katika eneo la Milima ya Golan linalokaliwa kwa mabavu baada ya ndege za Israel kushambulia ndani kabisa ya Lebanon, huku hofu ya kutokea kwa vita vikali ikiongezeka.Jeshi la Israel lilisema kuwa lilipiga vituo vya kuhifadhia silaha vya Hezbollah katika Bonde la Bekaa usiku kucha. Wizara ya afya ya Lebanon imesema mtu mmoja aliuawa na wengine 30 kujeruhiwa.Kujibu shambulio hilo, Hezbollah, ambayo inaungwa mkono na Iran, ilisema shambulio lake lililenga maeneo ya kijeshi ya Israeli katika Milima ya Golan kwa msururu wa roketi. Mamlaka ya Israel imesema nyumba mbili zilipigwa na roketi na mtu mmoja kujeruhiwa.Wakati huo huo, vuguvugu la Fatah la Palestina liliishutumu Israel kwa kumuua mwanachama wa ngazi ya juu wa mrengo wake wenye silaha nchini Lebanon katika juhudi za kuzusha mzozo wa kieneo.Jeshi la Israel limesema limemuua Khalil al-Makdah katika shambulio lililofanyika katika mji wa bandari wa kusini wa Sidon kwa sababu alikuwa akifanya kazi kwa niaba ya Walinzi wa Mapinduzi ya Iran na alihusika katika kuelekeza mashambulizi na kusafirisha silaha kwa njia ya magendo hadi Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.Lilikuwa ni shambulio la kwanza kwa mwanachama wa Fatah tangu kuanza kwa vita vya Gaza, ambalo limesababisha kuongezeka kwa uhasama wa mpaka kati ya Israel na Hezbollah.Mvutano umeongezeka katika wiki za hivi karibuni baada ya Israel kumuua kamanda mkuu wa Hezbollah huko Beirut, ambaye ililaumu mauaji ya watoto 12 katika shambulio la roketi.Unaweza pia kusoma:Je, nguvu ya mashambulizi ya Iran inalinganishwaje na ya Israel?Hezbollah imebadilika vipi tangu vita na Israel mwaka 2006?Je Iran itajiunga na Hezbollah katika vita na Israel?Mshirikishe mwenzako, Roketi za Hezbollah zapiga Milima ya Golan baada ya Israel kushambulia ndani
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.