Afrika Leo Mchana -Habari Kamili.

Radio Fortune Africa-Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa.

RAIS William Ruto sasa anaonekana kuwa adui wa kisiasa wa wakazi wa Mlima Kenya kutokana na ukuruba wake na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Katika chaguzi nne zilizopita Bw Odinga amekuwa akinadiwa kama ‘adui’ wa eneo hilo na wanasiasa wengi wamejijengea sifa kwa kumpiga vita kisiasa.

Hatua ya Rais Ruto kuridhiana kisiasa na Bw Odinga imewashangaza viongozi wa Mlima Kenya akiwemo Naibu Rais Rigathi Gachagua, kiasi cha wadadisi kubashiri kuwa huenda eneo hilo likamuunga mkono mpinzani wa Dkt Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2027.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT), Bw Charles Mwangi , anasema itakuwa vigumu kwa Rais Ruto kugeuza dhana ya wakazi wa Mlima Kenya kuwa amewasaliti na sasa ni ‘adui’ wao alivyokuwa Bw Odinga katika chaguzi zilizopita.

“Ukisikiza sauti za raia maeneo ya mashinani katika Mlima Kenya, wengi wamehamisha hasira na chuki zao kutoka kwa Bw Odinga hadi kwa Rais Ruto. Hii ni kutokana na masuala ya uongozi yaliyochochea maandamano ya Gen Z yaliyoshudiwa hata katika miji kadhaa ya Mlima Kenya ambako fujo kama hizo hazijawahi kuonekana miaka ya nyuma,” Bw Mwangi anasema.

Anaongeza kuwa kuundwa kwa baraza jipya la mawaziri, lililoshirikisha wandani wa Bw Odinga, kulionekana kama dharau kwa eneo hilo lililompa Rais asilimia 42 za kura katika uchaguzi uliopita wa urais.

Kwa upande wake, mchanganuzi wa masuala ya kisiasa, Bw Gasper Odhiambo, ameiambia Taifa Leo kuwa huenda wakazi wa eneo la Mlima Kenya wakasusia uchaguzi mkuu kama njia ya kumwadhibu Rais Ruto.

“Wengine huenda wakampigia kura Bw Odinga akiwania tena endapo atakosa kiti cha mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC). Sababu ni kwamba baada ya wao kumwangusha, hurejea mezani na kumegewa minofu serikalini,” anaeleza.

“Ikiwa kuna hasira ambazo zitawafanya wakazi wa Mlima Kenya kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa urais 2027, basi zitakuwa ni za kumwangusha Rais Ruto kulipiza kisasi usaliti wa 2022,” Bw Odhiambo anaongeza.

Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee, Bw Jeremiah Kioni, anasisitiza kuwa mnamo 2027, “wakazi wa Mlima Kenya wataungana dhidi ya uongo wa kisiasa na uongozi mbaya unaoendelezwa na serikali hii”.

Mbunge huyo wa zamani wa eneo la Ndaragua, anabashiri kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba mwaniaji mkuu wa urais atakayempinga Rais Ruto na serikali yake mnamo 2027, atashinda.

“Upigaji kura hautaongozwa tena na chuki dhidi ya Bw Odinga bali chuki na hasira dhidi ya Dkt Ruto na utawala wake,” Bw Kioni anaeleza.

Kulingana naye, wakazi wa Mlima Kenya sasa wameeruvuka; hawatakubali tena kudanganywa kwani wameamua kwa kauli moja kupinga serikali hii.

Lakini msimamo huu unapingwa na Katibu Mkuu wa chama cha United Democratic Alliance (UDA), Bw Hassan Omar, akisema hauna mashiko.

“Hamna kiongozi atakayekuwa na uwezo wa kutumia kadi ya ukabila kushawishi mkondo wa siasa katika eneo lolote nchini,” Bw Omar akaambia Radio Fortune Africa.

“Siasa ni telezi. Wale ambao wanadhani wanaweza kutumia kelele kupata uungwaji mkono na kupanda mbegu za migawanyiko watagundua kuwa mbinu kama hizo hazitadumu,” akaongeza.

SERIKALI ya Kenya imeimarisha doria katika mpaka wake na Uganda ili kuzuia maambukizi zaidi ya ugonjwa wa homa ya nyani (Monkeypox).

Idara ya Afya katika Kaunti ya Trans Nzoia imechukua tahadhari kuhusu mlipuko wa ugonjwa huo kutoka nchi jirani ya Uganda, huku wahudumu wa afya wakishika doria kwenye mpaka wa Suam.

Afisa anayedhibiti mlipuko wa magonjwa katika Kaunti hiyo, Bw Brian Ateka, alibainisha kuwa wizara ya afya imeanzisha kituo cha uchunguzi wa mashirika mbalimbali kwenye mpaka wa Suam ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo nchini.

“Timu mbalimbali ziko humo tayari kushughulikia dharura yoyote. Maafisa wetu wa uchunguzi wa magonjwa pia wako katika hali ya tahadhari hasa kuangalia watu wanaoingia ndani ya nchi na wanaotoka,” Bw Ateka aliambia Taifa Dijitali.

Watu wote wanaoingia au kutoka nchini, wanachunguzwa kama itifaki ya kimsingi ya afya ili kuzuia maambukizi yoyote ya ugonjwa huo.

“Wale wote wanaopita mpakani wanapaswa kuchunguzwa kabla ya kuingia Kenya. Hii ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha kwamba kaunti na eneo letu liko salama,” aliongeza.

Kamati ya Kukabiliana na Dharura katika Kaunti hiyo iliyoanzishwa wakati wa janga la corona, imenaza kutekeleza jukumu lake kama sehemu ya hatua za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo nchini.

HUENDA mpango wa elimu bila malipo ukatekelezwa katika kiwango cha chuo kikuu endapo serikali itazingatia ushauri wa wabunge na kuunda sera ya kuunganisha hazina zote za kufadhili masomo katika ngazi hiyo.

Wakiongozwa na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula, wabunge walisema uwepo wa hazina nyingi za kutoa basari hauna faida yoyote na hutoa mwanya wa kuingizwa ufisadi katika mpango huo.

Bw Wetang’ula Jumanne, Agosti 20, 2024 alisema hamna mantiki yoyote kwa Madiwani (MCA), Wabunge, Wabunge Wawakilishi, Serikali za Kaunti, Hazina ya Kufadhili Masomo ya Vyuo Vikuu (UF), Bodi ya Kufadhili Elimu ya Juu (HELB), Wizara ya Elimu na mashirika ya kibinafsi kuendesha mipango sambamba ya utoaji basari ya masomo.

“Ikiwa mwaweza kuunda sera ya kuweka pamoja hazina hizi, Bunge hili litakuwa tayari zaidi kuigeuza kuwa sheria ili tuwe na mpango wa elimu bila malipo katika kiwango cha Chuo Kikuu,” Bw Wetang’ula akasema.

“Shida yetu itasuluhishwa mara moja,” Bw Wetang’ula akaongeza, akitoa ushauri kwa Katibu katika Idara ya Elimu ya Juu Beatrice Inyangala.

Spika huyo alisema hayo wakati wa kikao kisicho rasmi cha wabunge (Kamukunji), kufuatia pendekezo la Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi kwamba hazina zote za serikali za kutoa basari za masomo ziwekwe pamoja.

Bi Inyangala alikuwa amealikwa katika kikao hicho, katika majengo ya bunge, kufafanulia wabunge kuhusu mpango mpya wa kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka familia maskini.

Hii ni baada ya wabunge kukosoa mfumo unaotumiwa kubaini wanafunzi wenye uhitaji mkubwa kufuatia kukithiri kwa visa ambapo wanafunzi kutoka jamii maskini walipata ufadhili mdogo kinyume na hitaji lao.

Wabunge pia waliilaumu Idara ya Elimu ya Juu inayoongozwa na Bi Inyangala kwa kutotoa ufafanuzi kamili kuhusu mfumo mpya wa ufadhili wa masomo waliosema unabagua wanafunzi kutoka familia maskini.

Walimlaumu afisa huyo kwa kumwachia Rais William Ruto wajibu wa kufafanua utendakazi na umuhimu wa mfumo huo mpya wa ufadhili wa masomo katika vyuo vikuu.

Wazo la wabunge la kuundwa kwa hazina moja ya kufadhili masomo katika vyuo vikuu linajiri baada ya Wizara ya Elimu kuandaa mswada wa kufanikisha lengo hilo.

Mswada huo unaojulikana kwa kimombo kama “Basic Scholarships and Bursaries Bill, 2024” unalenga kuunganisha ufadhili unaotolewa na serikali na basari na kuziweka chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu.

Hatua hii itaondoa usimamizi wa hazina hizo mikononi mwa wanasiasa, kama vile madiwani, wabunge na magavana.

Vile vile, wiki jana, Mbunge Mwakilishi wa Nairobi Esther Passaris alitoa notisi ya hoja kuhusu mageuzi katika utoaji basari nchini.

Bi Passaris pia anapendekeza kuwekwa pamoja kwa misaada ya masomo inayotolewa na serikali na basari na kuziweka chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu.

Jopo kazi la Rais kuhusu Mageuzi katika Elimu pia lilipendekeza kuvunjwa kwa bodi ya HELB, hazina ya UF na Asasi ya Kuteua Wanafunzi wanaojiunga na Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kadri (KUCCPS) ili kuundwe asasi moja ya kutoa ufadhili kwa masomo ya juu.

MWANAFUNZI bora kutoka Kaunti ya Kwale amekumbwa na wasiwasi baada ya kuorodheshwa katika kundi la wanafunzi ambao familia zao zinajiweza katika mfumo mpya wa kufadhili elimu.

Licha ya Suheil Mumba kutafuta wafadhili wa kumsaidia kufikia ndoto yake ya kuwa daktari mwezi uliopita, hajafanikiwa kupata ufadhili kutoka kwa serikali kuu vile alivyodhania.

Suheil amewekwa katika daraja la tano (Band 5), ambalo kulingana na Wizara ya Elimu, ni la familia zinazopata kipato cha zaidi ya Sh120,000 kila mwMwanafunzi bora wa KCSE Kwale akosa karo ya kusomea Udaktari

Kilichomshangaza ni kuwa wazazi wake wote hawajaajiriwa, na hufanya vibarua vidogo ili kujikimu kimaisha.

“Niliposikia kuwa barua mpya ya shue ilikuwa imetoka, nilifurahi nikitarajia kuwa serikali itagharamia karo yangu ya shule. Lakini sijaelewa kwa nini nimewekwa katika Band 5,” Suheil alisema katika mahojiano na Taifa Leo.

Alieleza kuwa ombi lake la awali la kutafua wafadhili halikufaulu, kwani watu wengi ambao wangemfadhili walisema serikali ina mpango wa kusaidia na kugharamia karo ya wanafunzi hasa waliotoka kwenye familia maskini kama yeye.

Hata hivyo, alipata usaidizi wa kugharamia chumba cha kulala katika Chuo kikuu cha Egerton, Kaunti ya Nakuru.

Suheil alikuwa mwanafunzi bora wa KCPE katika shule yake ya msingi baada ya kupata alama 389.

Chuo kikuu cha Egerton
New University Funding Model
ruto
Suheil Mumba

WANDANI wa Naibu Rais Rigathi Gachagua sasa wanataka hitaji la mshindi wa urais kupata asilimia 50 na kura moja zaidi liondolewe kupitia kura ya maamuzi ya kubadilisha katiba.

Uhusiano kati ya Bw Gachagua na Rais William Ruto umeendelea kudorora hasa baada ya mawaziri wanne kutoka ODM kuteuliwa serikalini.

Matakwa haya yamefasiriwa kama yanayolenga uongozi wa nchi baada ya uchaguzi wa 2027. Viongozi wanaoegemea mrengo wa Bw Gachagua waliandaa mkutano usiku wa Jumapili katika hoteli moja mjini Thika ambapo waliazimia kuwa eneo hilo sasa lazima liamue mkondo litakaouchukua mwaka wa 2027.

Wanasiasa hao walisema kuwa wamechoshwa na tabia ya wandani wa Bw Raila Odinga kuingizwa serikalini na marais wanaotumia kura za eneo hilo kuingia mamlakani.

Mbali na Rais Ruto, mtangulizi wake Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta pia alishirikiana na Bw Raila katika muhula wa pili wa utawala wake.

Aidha, wanataka chama chochote ambacho kitabuni serikali kiwe na asilimia 60 za kura na kikishindwa basi kisheria kiruhusiwe kuunda serikali ya muungano.

Bw Odinga alikuwa katika serikali ya ‘nusu-mkate’ na Rais Mwai Kibaki kati ya 2008-2013 baada ya uchaguzi wa 2007/08 kugubikwa na ghasia.

Masharti mengine ambayo wanasiasa wa Mlima Kenya sasa wanataka yatimizwe kupitia mabadiliko ya katiba ni Afisi ya Kiongozi wa Upinzani kutengewa bajeti na pia rasilimali za nchi zigawanywe kwa kuzingatia idadi ya watu na siyo ukubwa wa maeneo.

Aliyekuwa Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu ambaye sasa ni msaidizi wa kibinafsi wa Bw Gachagua anasema licha ya kuwa bosi wake hakuhudhuria mkutano huo, anaunga mkono yaliyojadiliwa na kuafikiwa.

“Kama mkutano haujaandaliwa kumpiga vita mtu yeyote basi hana tatizo. Mkutano unaolenga kuunganisha watu na kutafuta mwongozo wa kulisaidia eneo letu hauna chochote kibaya,” akasema Bw Wambugu.

Wakili wa Mahakama Kuu Mwangi Kariuki ambaye alinakili yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo alisema kuwa kutakuwa na mikutano mingine ya kushauriana kuhusu mustakabali wa kisiasa wa Mlima Kenya.

“Kwa sasa wanaoshindwa kura wanatumia fujo serikalini lakini tunataka mabadiliko ya kisheria ili hilo liwe rahisi. Kura za Mlima Kenya zimekuwa zikitumika kuwasaidia watu kutwaa uongozi lakini wanapigwa kumbo baada ya baadhi ya watu kutumia fujo kuingia serikalini na hilo husababisha mauti ya raia,” akasema Bw Kariuki.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Naivasha Jayne Kihara ambaye alihudhuria mkutano huo, wanalenga kuwashirikisha Gen-Z ili wawe na ushawishi wa kuamua nani ataunda serikali mwaka wa 2027.

Bi Kihara alisema ni mikutano kama hiyo ndiyo ilimsaidia Rais Ruto kupenya ukanda wa Mlima Kenya, Bw Kenyatta alipokuwa mamlakani, huku wanasiasa wa eneo hilo wakimuunga Bw Raila.

Mbunge wa zamani wa Gatanga Nduati Ngugi aliyesema anawakilisha Bw Kenyatta katika mkutano huo, alisema kuwa eneo hilo lazima liungane la sivyo hesabu za kisiasa zitawachenga 2027 na 2032.

Wanasiasa wa Mlima Kenya waaminifu kwa Bw Gachagua wamekuwa wakisema kuwa kuna mipango inayoendelezwa kichinichini na mrengo wa Raia/ Ruto ili kubadilisha katiba na kufungia eneo lao kutawala siasa za nchi.

GAVANA wa Meru Kawira Mwangaza amepoteza kiti chake baada ya maseneta kupitisha hoja ya kumtimua afisini iliyopitishwa na madiwani wa kaunti hiyo majuzi.

Jumla ya maseneta 26 walipiga kura ya NDIO, kuunga mkono shtaka la kwanza dhidi ya Bi Mwangaza – la ukiukaji wa Katiba na sheria nyinginezo.

Maseneta 4 walipiga kura ya LA kwa shtaka hilo, huku wengine 14 wakisusia upigaji kura.

Katika shtaka la pili la mienendo mibaya, maseneta 26 walipiga kura ya NDIO na kukubaliana na msimamo wa madiwani wa Kaunti ya Meru, 2 wakakatalia mbali shtaka hili huku 14 wakisusia kupiga kura.

Jumla ya maseneta 27 walikubaliana na hoja iliyopitishwa na Bunge la Kaunti ya Meru kwamba Bi Mwangaza alitumia vibaya mamlaka ya afisi yake, huku mmoja akipiga kura ya kumwondolea Mwangaza lawama.

Maseneta 14 walisusia upigaji kura kuhusu shtaka hilo.

Idadi kubwa ya maseneta waliosusia upigaji kura kuhusu mashtaka hayo matatu walikuwa ni wale wa mrengo wa Azimio la Umoja-One Kenya.

“Kwa mujibu wa Kipengele 181 cha Katiba na Sehemu ya 33 ya Sheria ya Serikali za Kaunti na Sheria za Seneti nambari 86, Seneti imeamua kumwondoa afisini Gavana wa Meru Kawira Mwangaza,” Spika wa Seneta Amason Kingi akasema kwenye uamuzi wa mwisho aliosoma mwendo wa saa tano za usiku, Jumanne, Agosti 20, 2024.

Awali, Bi Mwangaza alipinga mashtaka yote dhidi yake akishikilia kuwa hayakuwa na msingi wowote na yalichochewa na mahasidi wake wa kisiasa.

Bi Mwangaza sasa anashikilia rekodi kama Gavana wa Kwanza kuondolewa afisini baada ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Hii ilikuwa mara ya tatu kwa madiwani wa Kaunti ya Meru kumtimua Bi Mwangaza.

MAHAKAMA kuu imepiga teke na kusambaratisha hatua ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Ingonga kumshtaki kiongozi wa Chama cha Safina Jimi Wanjigi kumiliki silaha hatari kinyume cha sheria na kusitisha mchezo wa paka na panya kati ya Serikali na mwanasiasa huyo mtajika.

Jaji Bahati Mwamuye alisitisha kufunguliwa mashtaka 11 dhidi ya Wanjigi na DPP.

Kusitishwa kushtakiwa kwa Wanjigi kulizima msururu wa majimbizano makali kati ya mwanasiasa huyo na asasi ya usalama “aliyosema inatumiwa vibaya na maafisa wakuu serikalini kumnyamazisha.”

Jaji Mwamuye alisitisha kushtakiwa kwa Wanjigi aliyekamatwa Agosti 19, 2024 na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kamkunji pamoja na msaidizi wake David Kibe Wakonyo.

Wote wawili wamefunguliwa mashtaka 14. Wanjigi ameshtakiwa kwa makosa 13 peke yake.

Jaji Mwamuye aliombwa atumie mamlaka ya mahakama kuu na kuzima hatua ya DPP kumshtaki Wanjigi ilhali korti ilizima kushtakiwa kwake mnamo Agosti 9, 2024.

“Hii serikali inadharau maagizo ya mahakama na yapasa kuzimwa,” Jaji Mwamuye.

Awali, mawakili wenye tajriba ya juu Kalonzo Musyoka, Martha Karua, Paul Muite, Dkt John Khaminwa na Willis Otieno walikuwa wamemuomba hakimu mkuu Susan Shitubi asimame kidete na “kuzuia nchi hii ikirudishwa katika enzi za utawala wa kimla wa hayati Daniel arap Moi”.

“Kesi hii inatazamwa na kufuatwa katika pembe zote. Ni wakati wako usimame na haki na kuzima hatua ya serikali ya kukandamiza haki za Wanjigi. Simama kidete na useme haki kwa Wanjigi,” Kalonzo alieleza hakimu.

Bi Karua naye hakusita kueleza hali ilivyo akisema “ni wazi serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake na sasa imegeukia watu inaowaona kama wapinzani sugu.”

Bi Karua alisema wakati ni sasa haki itendeke na kila Mkenya apate haki yake.

Jaji huyo alielezwa na Dkt Owiso masaibu ya Wanjigi aliyefikishwa mbele ya Bi Shitubi yanatokana na tuhuma kwamba alikuwa anaunga mkono maandamano ya kupinga sera mbaya za serikali ya Rais Ruto yaliyoandaliwa na Gen Z.

Katika uamuzi wake, Jaji Mwamuye alizima hatua ya kumfungulia mashtaka Wanjigi na Wakonyo.

Jaji Bahati Mwamuye, alisema haki za Wanjigi zimekandamizwa ikitiliwa maanani alikuwa amepewa leseni za kumiliki bunduki na bastola.

Jaji Mwamuye alisema ni jambo la kusikitisha polisi wamekaidi agizo la mahakama kuu la Agosti 9, 2024 kwamba “wasimkamate na kumfungulia mashtaka Wanjigi kuhusiana na umiliki wa silaha.”

Wanjigi, kupitia mawakili wenye tajriba ya juu Kalonzo Musyoka, Eugene Wamalwa, Paul Muite, Dkt John Khaminwa, Jackson Kala, Willis Otieno na Dkt Owiso Owiso walimweleza Jaji Mwamuye kwamba “serikali imekaidi maagizo ya mahakama kuu ya kutomfungulia mashtaka Wanjigi.”

Mawakili hao walimweleza Jaji Mwamuye, mnamo Jumanne (agosti 20) alasiri “iwapo hii mahakama haitazima hatua hii ya kumshtaki Wanjigi itachekelewa na kuonekana haitekelezi majukumu yake kwa mujibu wa sheria.”

Wakili Dkt Owiso Owiso aliyewasilisha ombi hilo la kusitisha kushtakiwa kwa Wanjigi alieleza mahakama wakati umewadia wakati nchi hii itetewe na mahakama.

Kabla ya Jaji Mwamuye kusitisha kesi dhidi ya Wanjigi, hakimu mkuu Bi Susan Shitubi alikuwa amemwachilia kwa dhamana ya Sh10 milioni.

Baada ya kutoka kizuizini, Wanjigi alimtaka Rais Ruto apambane naye kuhusu masuala ya kiuchumi na jinsi ya kuwasaidia vijana waliohitimu vyuo kupata ajira.

Bi Shitubi aliagiza kesi hiyo itajwe Septemba 12, 2024 kwa maagizo zaidi.

MASWALI yameibuka baada ya mshukiwa mkuu wa mauaji ya wanawake 42, ambao miili yao ilipatikana imetupwa kwenye timbo mtaani Kware, Embakasi, kutoroka katika Kituo cha Polisi cha Gigiri, Nairobi.

Collins Jumaisi Khalusha, ambaye ilidaiwa alikiri kuhusika na mauaji hayo ambayo baadaye yalipunguzwa kuwa ya wanawake sita, alikuwa miongoni mwa washukiwa 13 waliotoroka kutoka seli za kituo hicho cha polisi, saa tisa alfajiri Jumanne.

Kaimu Inspekta Jenerali wa polisi, Gilbert Masengeli alisema maafisa wanane waliokuwa kazini walisimamishwa kazi na kukamatwa kwa kusaidia mahabusu hao kutoroka.

Maafisa ambao walikamatwa mara moja ni pamoja na Kamanda wa polisi wa Kaunti ndogo ya Gigiri, afisa mkuu wa kituo hicho na wengine sita miongoni mwao waliokuwa katika afisi ya kupokea ripoti na mlinzi wa seli.

Bw Masengeli alisema maafisa hao walilengwa baada ya uchunguzi wa awali kuonyesha kutoroka kwa mahubusu hao kulikuwa “kazi ya ndani” ya maafisa waliokuwa zamu na wengine.

“Tunachunguza tukio hilo na uchunguzi wetu wa awali unaonyesha kuwa, walisaidiwa kutoroka na watu wa ndani ya kituo, ikizingatiwa kuwa maafisa walikuwa wamewekwa ipasavyo kulinda kituo,” Bw Masengeli alisema.

“Kwa hivyo, nimewasimamisha kazi maafisa wanane waliokuwa zamu jana usiku.” Kituo hicho kiko katika eneo la kimkakati ambayo inafanya vigumu kwa mahabusu kutoroka.

Kutoroka kwa Jumaisi kunaibua maswali hasa ikizingatiwa kuwa alihepa siku chache kabla ya kurudishwa kortini alikotarajiwa kufunguliwa mashtaka ya mauaji.Polisi walitarajiwa kumfikisha kortini Ijumaa Agosti 23 baada ya kukamilisha uchunguzi.

Vile vile, kutoroka kwake na washukiwa wengine kumeibua maswali hasa ikizingatiwa ulinzi mkali unaopaswa kupatiwa washukiwa wa mauaji na siku chache kabla ya kufunguliwa mashtaka. Bw Masengeli alisema kulikuwa na mahabusu 17 katika seli na ni wanne waliobaki.

Alisema kwamba, waliotoroka pamoja na Jumaisi ni raia wa Eritrea 12 waliozuiliwa katika kituo hicho kwa kuwa nchini kinyume cha sheria.

Kamanda wa polisi Nairobi Adamson Bungei ambaye awali alithibitisha kisa hicho, alisema msako umeanzishwa ili kuwakamata tena mahabusu waliotoroka.

“Tunafuatilia suala hilo kwa lengo la kuchukua hatua,” alisema.

Ripoti ya polisi iliyonakiliwa katika kituo hicho, OB 05/20/08/2024, ilionyesha kuwa kisa hicho kiliripotiwa na maafisa wa polisi Evans Kipkirui na Gerald Mutuku waliokuwa wakisimamia seli hizo.

Maafisa hao walisema walifanya ziara yao ya kawaida katika seli wakiwa na meneja wa hoteli ya polisi ili kuwapa mahabusu kiamsha kinywa walipogundua washukiwa walikuwa wametoroka.

Walisema walipofungua mlango wa seli, walishtuka baada ya kubaini kuwa watuhumiwa 13 walikuwa wametoroka kwa kukata waya kwenye eneo la kuotea jua.

Jumaisi alikuwa seli, akisubiri kufikishwa mahakamani Ijumaa, Agosti 23, 2024.

Ingawa polisi walisema alikuwa amekiri kuua wanawake 42 na kutupa miili yao katika timbo huko Kware, walidai wangemshtaki kwa mauaji ya wanawake sita pekee ambayo walikuwa wamethibitisha.

Kwa mujibu wa duru zilizozungumza na Radio Fortune Africa,Jumaisi, 33, ambaye awali polisi walisema alikiri kuwaua wanawake 42 akiwemo mkewe alipata kifungua kinywa katika kituo cha polisi.

Kiamsha kinywa katika seli za polisi kwa kawaida hutolewa baada ya mahabusu kuhesabiwa kunakofanyika kati ya saa kumi na moja na saa kumi na mbili alfajiri.

Hii inamaanisha kuwa, mfungwa huyo alikuwa ndani ya seli baada ya 12 kutoweka. Kutokana na maelezo haya, maswali ya kutatanisha ni: Jumaisi alitoroka saa ngapi? Na katika hali gani?

Duru ziliiambia  Radio Fortune Africa kwamba, Jumaisi alisaidiwa kutoroka baada ya wengine kwa sababu ya mzozo kuhusu mpango wa kusaidia mahabusu wengine kuhepa.

Radio Fortune Africa ilibaini kuhusu madai ya ugomvi kati ya maafisa fisadi kuhusu pesa ambazo Waeritrea walidaiwa kulipa ili kununua uhuru wao.

Kulingana na mdokezi wetu, wale waliohisi kutengwa walipopata Waeritrea 12 hawakuwepo, walichagua kupaka matope wenzao kwa kumwachilia Jumaisi ambaye angevutia hasira kali zaidi za umma.

HABARI KWINGINEKO DUNIANI

  1. Meya wa zamani anayeshutumiwa kwa kuwa jasusi wa China na kuwa na uhusiano na makundi ya wahalifu ametoroka kutoka Ufilipino, na kusababisha ghadhabu nchini humo.Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr alisema Jumatano kwamba “watu watafutwa kazi ” baada ya maafisa kukiri Alice Guo aliondoka nchini bila kutambuliwa mwezi mmoja uliopita na kusafiri hadi Malaysia, Singapore na Indonesia.Bw Marcos alisema kuondoka kwake “kumeweka wazi ufisadi unaodhoofisha mfumo wetu wa haki na kuondoa imani ya watu”.Bi Guo hajaonekana tena hadharani tangu mwezi Julai wakati jopo la Seneti lililochunguza madai yake ya kuhusishwa na vituo vya ulaghai na kamali za mtandaoni lilipoamuru akamatwe kwa kukataa kutoa ushahidi wake katika uchunguzi wake.Anashutumiwa kwa kuruhusu mashirika ya biashara haramu ya binadamu na vituo vya ulaghai kufanya kazi katika mji wake kwa kujifanya kuwa kamali za mtandaoni.Maseneta pia wamemshutumu kwa kuwa mhudumu au jasusi wa Uchina, wakitaja majibu yake “ya wazi” ya maswali kuhusu asili ya wazazi wake ya Uchina.Polisi wamewasilisha malalamishi ya uhalifu dhidi yake, huku shirika la kupambana na ufisadi nchini Ufilipino hivi majuzi lilimfukuza kazi kwa madai ya “upotovu mkubwa”.Amekanusha madai yote.Mshirikishe mwenzako, Hasira yatanda Ufilipino baada ya anayeshukiwa kuwa jasusi wa China kutoroka
  2. Saa 2 zilizopita Operesheni ya Kursk: Vikosi vya Ukraine vyatishia kuteka eneo lingine la UrusifChanzo cha picha,EPAMaelezo ya picha,Kifaru cha kijeshi cha Ukraine katika kilichoharibiwa wakati wa uvamizi wa UrusiWiki mbili baada ya uvamizi wa kikosi cha wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Kursk, jeshi la Urusi bado halijaweza kuzuia kabisa mafanikio hayo.Vikosi vya Ukraine sio tu vimepanuaukubwa wa eneo lililoteka, kuongeza wanajeshi wa akiba, lakini pia, muhimu zaidi, huenda linajiandaa kwa mashambulizi ya eneo jipya ndani ya Urusi, kwa ajili ya kukata mifumo ya usambazaji ya Urusi katika wilaya ya Glushkovsky iliyopo katika jimbo la Kursk.Moja ya hasara kwa Urusi kuhusiana na eneo ambalo vikosi vya Ukraine vilifanikiwa kuliteka katika mkoa wa Kursk ni kwamba, kwa asili, lilikuwa eneo dogo lililozungukwa pande tatu na ukanda unaodhibitiwa na Urusi.Katika wiki mbili za mapigano, vikosi vya Ukraine havikuongeza mafanikio, lakini vilipanua wigo wa maeneo, na kushambulia maeneo ya kando katika jimbo hilo.Unaweza pia kusoma:Ukraine iko ‘huru kutumia’ silaha za Uingereza kwenye ardhi ya Urusi – Wizara ya UlinziUkraine yaendelea kusonga mbele ndani ya eneo la UrusiUrusi: Hali katika eneo la Belgorod ‘ni tete’, – GavanaUrusi lazima ilazimishwe kuleta amani – ZelenskyPutin: ‘Lazima tumfukuze adui nje ya eneo letuWanajeshi wa Ukraine wapo kilomita 30 ndani ya eneo la UrusiKwa nini Ukraine imeanzisha mashambulizi ya mpakani dhidi ya Urusi?Steve Rosenberg: Uvamizi wa Ukraine unaonyesha vita vya Urusi haviendi kama ilivyopangwaUrusi yaongeza mashambulizi dhidi ya wakosoaji wake nje ya njeMshirikishe mwenzako, Operesheni ya Kursk: Vikosi vya Ukraine vyatishia kuteka eneo lingine la Urusi
  3. Saa 3 zilizopita Obama na Michelle Obama watoa wito kwa Wamarekani kuunga mkono ‘ukurasa mpya‘ na HarrisgChanzo cha picha,Getty ImagesObama amewaahidi Wanademocrat kwamba Harris “atazingatia matatizo yako” na “hatashughulikia tu wapiga kura wake na kuwaadhibu wale wanaokataa kupiga goti.”Wawili hao walikuwa wakizungumza kwenye kongamano la Democrat ambapo wamemuunga mkono Kamala Harris kama mgombea wa urais wa chama hicho.Obama pia anasema anampenda Tim Walz, ambaye amesema ni “aina ya mtu anayepaswa kuwa katika siasa – mtu ambaye alizaliwa katika mji mdogo, aliitumikia nchi yake, alifundisha watoto, alifundisha soka, na kuwajali majirani zake.””Anajua yeye ni nani na ni nini muhimu.”Obama aliendelea kusema kuwa kuwachagua Harris na Walz “haitakuwa rahisi”.”Kazi yetu ni kuwashawishi watu kwamba demokrasia inaweza kuleta mafanikio,” amesema.”Kamala anaelewa hili,” anasema.Wakati huo huo Michelle Obama amesema kwamba Harris ni “mmoja wa watu wenye uwezo kuwahi kugombea wadhifa wa urais”.”Na yeye ni mmoja wa watu wenye hadhi kubwa, heshima kwa mama yake, kwa mama yangu, na pengine kwa mama yako pia,” Obama anaongeza. “Mfano wa hadithi tunazojieleza kuhusu nchi hii.”Obama anasema kwamba “hadithi yake ni hadithi yako. Ni hadithi yangu. Ni hadithi ambazo Wamarekani wengi wanaojaribu kujenga maisha bora”.Mshirikishe mwenzako, Obama na Michelle Obama watoa wito kwa Wamarekani kuunga mkono ‘ukurasa mpya‘ na Ha Jennifer Lopez awasilisha kesi ya talaka dhidi ya Ben AffleckGetty ImagesChanzo cha picha,Getty ImagesMaelezo ya picha,Lopez aliandika tarehe ya kutengana kwao kuwa Aprili 26 katika hati za mahakamaWaigizaji nyota wa Hollywood Jennifer Lopez na Ben Affleck wanatalikiana baada ya miaka miwili ya ndoa.Lopez aliwasilisha kesi ya talaka Jumanne katika Mahakama ya Juu ya Kaunti ya Los Angeles, kulingana na hati za mahakama ambazo BBC ilizishuhudia.Wawili hao – waliopewa jina la Bennifer na magazeti ya udaku – walifunga ndoa rasmi Las Vegas Julai 2022 na kufanya sherehe kubwa zaidi ya harusi huko Georgia mwezi uliofuata.Mapenzi yao yalianza baada ya kukutana wakati wakifanya kazi kwenye filamu ya uhalifu ya mapenzi – 2003 crime caper Gigli.Hapo awali walikuwa wamepanga kuoana mwaka huo, lakini walikatisha uhusiano wao mapema mwaka wa 2004.Karibu miongo miwili baadaye walirejesha uhusiano wao.”Upendo ni mzuri. Upendo ni wema. Na iligeuka kuwa upendo ni subira. Subira ya miaka ishirini,” Lopez alisema mnamo 2022 baada ya kutangaza harusi ya Las Vegas.Mshirikishe mwenzako, Jennifer Lopez awasilisha kesi ya talaka dhidi ya B Hamas: Kauli za Biden ni za “kupotosha na hazionyeshi msimamo wetu”fChanzo cha picha,ReutersMaelezo ya picha,Wapalestina wakiwa wamebeba moja ya mwili wa mtu aliyefariki baada ya uvamizi wa Israel katika mji wa GazaHamas imesema Jumanne kwamba “taarifa za Rais wa Marekani Joe Biden kwamba vuguvugu hilo linaunga mkono makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza na Israel ni za kupotosha.””Israel inasema inaweza kufikia makubaliano, na iko tayari kufikia makubaliano,” Biden alisema wakati akijibu maswali kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano. “Lakini ninaambiwa kuwa Hamas sasa inaunga mkono.””Bado tunasubiri, tutaendelea na shinikizo,” aliongeza wakati akipanda ndege yake baada ya kuzungumza katika mkutano wa kitaifa wa chama cha Democratic mjini Chicago siku ya Jumatatu.Hamas imesema, “Kauli za Biden hazionyeshi msimamo wa kweli wa vuguvugu hilo, ambalo lina nia ya kukomesha uchokozi.”Vuguvugu hilo liliongeza kuwa “kile kilichowasilishwa hivi karibuni kwa vuguvugu hilo ni mapinduzi dhidi ya kile ambacho vyama vilifikia Julai 2, ambacho kilitokana na tamko la Biden mwenyewe la mnamo tarehe 31 Mei na Azimio la Baraza la Usalama 2735 mnamo Juni 11.”Unaweza pia kusoma:Wapalestina wasimulia unyanyasaji katika jela za IsraelHospitali ya chini ya ardhi ya Israel inayojiandaa kwa mashambulizi
  1. 6 zilizopitaMarekani yakosoa msimamo wa Netanyahu wa kusitisha vita mara mojagChanzo cha picha,PA-EFE/REX/Shutterstock Maelezo ya picha,Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken (kushoto) alikuwa na mkutano wa saa tatu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumatatu.Afisa mkuu wa utawala wa Marekani amepuuza maoni yaliyoripotiwa na Benjamin Netanyahu, akimshutumu waziri mkuu wa Israel kwa kutoa msimamo wa “mara moja na papo hapo” ambao “haufai katika kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano katika mstari wa mwisho”.Hii inakuja wakati mazungungumzo ya awamu kubwa ya diplomasia ya kikanda yakifanywa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, huku Marekani ikijaribu kuendeleza maendeleo yaliyofikiwa katika makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka.Siku ya Jumatatu, Bw Blinken alikuwa na mazungumzo yaliyodumu kwa saa tatu na kiongozi huyo wa Israel mjini Jerusalem.Baadaye alisema Bw Netanyahu amekubali pendekezo la Washington lililoitwa “kuweka madaraja” kwa lengo la kujaribu kutatua masuala ya tata ili kuiwezesha Israeli na Hamas kufikia makubaliano.Unaweza pia kusoma:Wapalestina wasimulia unyanyasaji katika jela za IsraelHospitali ya chini ya ardhi ya Israel inayojiandaa kwa mashambuliziJe ‘vita kati ya Israel na Iran vitakuwaje?’ – Sunday Times.
  2. Mshirikishe mwenzako, Marekani yakosoa msimamo wa Netanyahu wa kusitisha vita mara moja
  3. Saa 6 zilizopitaVikosi vya Urusi vyadai kuuteka mji mwingine mashariki mwa UkrainefChanzo cha picha,Getty ImagesMaelezo ya picha,Polisi wa Ukraine wanajaribu kuwashawishi wakaazi kutoroka uvamizi wa Urusi huko ToretskJeshi la Urusi linasema kuwa limeuteka mji mdogo mashariki mwa Ukraine unaoitwa Niu-York, kama sehemu ya harakati zake kuelekea maeneo makubwa ya watu katika eneo la Donetsk.Jeshi la Ukraine halijathibitisha kutekwa kwa mji waq Niu-York, likisema tu kwamba vikosi vya Urusi vinashambulia karibu na mji huo na maeneo mengine. Jeshi linafanya kashambulizi hayo “kwa makabiliano yanayostahili … na mapigano yanaendelea”, lilisema.Ingawa ni makazi madogo tu, kuudhibiti mji wa Niu-York kunaweza kuonyesha hatua nyingine kuelekea maeneo ya kati yajimbo la Donetsk Toretsk na Pokrovsk.Inadhaniwa kuwa moja ya malengo ya Ukraine kuteka eneo katika eneo la Kursk nchini Urusi ni kuilazimisha Urusi kuhamisha baadhi ya vikosi vyake mbali na eneo la mapigano la mashariki.Hakuna dalili hadi sasa ya hilo kutokea, licha ya kamanda mkuu wa Ukraine Oleksandr Syrskyi kudai udhibiti wa vijiji na miji 93 ya Urusi.Rais Volodymyr Zelensky alielezea hali ya vita vya mashariki kuwa ngumu, lakini akasema wanajeshi wa Ukraine wanafanya kila wawezalo kuangamiza vikosi vya Urusi.Unaweza pia kusoma:Ukraine iko ‘huru kutumia’ silaha za Uingereza kwenye ardhi ya Urusi – Wizara ya UlinziUkraine yaendelea kusonga mbele ndani ya eneo la UrusiUrusi: Hali katika eneo la Belgorod ‘ni tete’, – GavanaUrusi lazima ilazimishwe kuleta amani – ZelenskyPutin: ‘Lazima tumfukuze adui nje ya eneo letuWanajeshi wa Ukraine wapo kilomita 30 ndani ya eneo la UrusiKwa nini Ukraine imeanzisha mashambulizi ya mpakani dhidi ya Urusi?Steve Rosenberg: Uvamizi wa Ukraine unaonyesha vita vya Urusi haviendi kama ilivyopangwaUrusi yaongeza mashambulizi dhidi ya wakosoaji wake nje ya njeMshirikishe mwenzako, Vikosi vya Urusi vyadai kuuteka mji mwingine mashariki mwa Ukraine

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment