Afrika Leo Mchana -Habari Kamili Agosti 16,2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

WAANZILISHI wa United Democratic Alliance (UDA), wamepuuza kauli iliyotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Cleophas Malala kwamba alifurushwa kwa kutetea Naibu Rais Rigathi Gachagua asitimuliwe mamlakani, wakiitaja kama uongo na kuapa kumtimua kama mwanachama wa chama hicho.

Wakiongozwa na Joe Khalende, waanzilishi hao walisema katika taarifa kwamba madai ya Bw Malala kwamba angali katibu mkuu wa chama ni ya uongo.

“Waanzilishi wa UDA wanasisitiza kwamba wanaunga mkono kwa dhati mabadiliko yaliyofanywa katika chama kwa kumteua Hassan Omar kama Kaimu Katibu Mkuu na kumshauri Malala akomeshe mawazo potovu kuhusu yaliyopita,” Bw Khalende alisema katika taarifa.

Haya yalijiri saa chache baada ya Bw Malala kudai kuwa kuondolewa kwake hakukuwa halali na kunahusishwa na mipango ya kumuondoa ofisini Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Chama hicho kimesema kuwa taarifa ya Bw Malala imethibitisha hofu yao kuu kwamba amekuwa akifanya kazi na watu wasio na nia njema ili kuhujumu chama kutoka ndani.

Huku Bw Malala akipinga kuondolewa kwake, chama hicho kimewaonya maafisa wa chama dhidi ya kujihusisha naye.

“Pia tunamuonya dhidi ya kutumia nembo ya chama kutuma taarifa kwa vyombo vya habari. Tunachukua fursa hii mapema kutahadharisha wafanyakazi dhidi ya kujihusisha au kufanya shughuli yoyote na Bw Malala.”

Bw Khalende alidai kuwa wakati wa uongozi wa Bw Malala, chama hicho kilikumbwa na uhuni wa kisiasa, na usimamizi mbaya wa raslimali za chama.

Chama hicho kiliendelea kusema kwa kufichua uhusiano wake na Bw Gachagua, Bw Malala alianika juhudi zake za siri za kuhujumu ajenda ya kiongozi wa chama hicho, Rais William Ruto.

Viongozi hao walipuuza madai ya Malala dhidi ya mwenyekiti wa chama Cecil Mbarire na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wa kwamba wawili hao walikuwa wakipanga njama ya kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua.

“Waasisi na mamilioni ya wanachama wa chama hawataruhusu amani na utulivu unaopatikana kwenye chama kuvurugwa na wanasiasa walioshindwa uchaguzini wanaojitafuta maslahi yao ya kibinafsi. Waanzilishi wa UDA wamekuwa wakitilia shaka tabia ya Malala, mienendo ya uongozi, maamuzi na uaminifu wake.”

Waliapa kushinikiza kufukuzwa kwa Bw Malala kutoka chama hicho miongoni mwa hatua zingine kupitia Kamati ya Kusuluhisha Mizozo ya Ndani ya chama.

Bw Malala aliahidi kutoa ripoti ambayo itafichua kwa kina jinsi baadhi ya maafisa wa chama hicho walikuwa wakipanga kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua.

gachagua
malala
uda

RAIS Mstaafu, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuitisha mkutano na vyama tanzu vya Muungano wa Azimio la Umoja – One Kenya, kufuatia hali ya wasiwasi inayoendelea katika muungano huo wa upinzani, kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amesema.

Akiwa mwenyekiti wa muungano huo, Bw Kenyatta anatarajiwa kuita vinara wenza kutoa mwelekeo na kudhibiti hali ya wasiwasi katika muungano huo kufuatia kubuniwa kwa Serikali Jumuishi.

“Tunatarajia Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ambaye ni mwenyekiti wa Baraza Kuu la Azimio la Umoja aitishe mkutano ili tuweze kujadili kwa uwazi masuala yanayotikisa muungano,” Bw Musyoka alisema.

Muungano huo umeonekana kuporomoka baada ya chama ODM cha Bw Raila Odinga kuamua kushirikiana na Rais William Ruto na baadhi ya viongozi wa chama chake kuwa mawaziri.

Mkutano huo unatarajiwa kujiri huku vinara wenza wakionekana kutofurahishwa na hatua ya Bw Odinga ya kuunga mkono serikali ya Kenya Kwanza.

Kwa hivyo, mkutano na Bw Uhuru unapaniwa kuokoa Azimio au kilichosalia kuhusu muungano huo.

Tayari, kiongozi wa Chama cha Narc-Kenya Martha Karua ametoa notisi ya kujiondoa Azimio.

Hatua hiyo ilijiri huku mvutano ukiongezeka kati ya baadhi ya viongozi wa Azimio baada ya Rais Ruto kuteua viongozi wa chama cha ODM kuwa mawaziri.

Kiongozi wa Chama cha Wiper alisema kuwa misukosuko ni ya “kawaida” katika muungano wowote wa vyama vya kisiasa na kwamba Azimio la Umoja bado ni imara.

“Si rahisi kamwe kusimamia miungano. Azimio la Umoja haiwezi kuepuka hali kama hiyo. Lakini inapotokea, inatupatia fursa ya kujadiliana zaidi,” akasema Bw Musyoka, na kueleza kuwa ni katika hali kama hiyo ambapo wahusika huelewana vyema.

Hata hivyo, alisema, “Chochote kinawezekana. Na kuanzia sasa na kwenda mbele, hatupuuzi uwezekano wowote. Tuko tayari pia kwa changamoto yoyote,” kauli ambayo inaonekana kuashiria uwezekano wa Azimio la Umoja kuvunjika iwapo hakutakuwa na muafaka.

Bw Kalonzo alikuwa akizungumza Alhamisi, Agosti 15, 2024 wakati wa Kongamano la Vijana la Oslo Centre Africa ambapo alizungumza kuhusu maandamano ya kupinga serikali yaliyoongozwa na vijana, Gen Z, akisema yalifanikiwa na kuhimiza vijana wajumuishwe katika mazungumzo ya kitaifa.

Pia, alitoa wito wa haki kwa wahasiriwa wa maandamano wakati wa mkutano ulioleta pamoja watetezi wa vijana, viongozi wa serikali, wataalamu kutoka bara zima kushughulikia maswala yanayowakabili vijana Afrika, kubadilishana maarifa na kutafuta suluhu za kiubunifu kwa maendeleo endelevu.

INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IG) Mteule Douglas Kanja ameahidi kutekeleza mageuzi makubwa katika Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) iwapo uteuzi wake utaidhinishwa na Bunge.

Kwanza, Bw Kanja, 60, Alhamisi, Agosti 15, 2024 aliwaahidi wabunge na maseneta waliokuwa wakimhoji kubaini ufaafu wake kwa wajibu huo, kwamba atapambana vikali na zimwi la ufisadi kwenye polisi.

Alisema atafanya hivyo kwa kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika udumishaji usalama kwa kuamuru maafisa wote wavalie beji zenye majina yao wakiwa kazini.

“Aidha, nitapambana na polisi wanaoshirika mgongano wa kimasilahi wakiwa kazini. Polisi watalazimika kuamua kufuata mkondo mmoja,” akasema Bw Kanja ambaye amehitimu kwa shahada ya digrii katika Biashara.

“Nilipohudumu kama Naibu Inspekta Jenerali, niligundua kuwa baadhi ya maafisa wa polisi ndio wamiliki wa matatu zinazovunja sheria au mabaa yanauza pombe haramu. Niliwaambia kufuata mkondo mmoja, kuacha kazi ya polisi na kuendesha biashara ya matatu au kuacha biashara ya matatu na kujishughulisha na kazi katika NPS,” Bw Kanja, ambaye amehudumu kama afisa wa polisi kwa miaka 39, akaambia Kamati ya Pamoja ya Bunge la Kitaifa na Seneti iliyokuwa ikimpiga msasa Alhamisi katika majengo ya bunge.

Endapo, kamati hiyo na mabunge yote mawili yataidhinisha uteuzi wake, Bw Kanja atachukua nafasi ya Japhet Koome aliyejiuzulu Julai 12, 2024.

ALIYEKUWA Waziri wa Barabara Franklin Bett alipata majeraha baada ya kuhusika kwenye ajali katika barabara kuu ya Kericho-Kisumu Alhamisi usiku, Agosti 15, 2024.

Kulingana na ripoti ya polisi gari ambalo Waziri huyo wa zamani alikuwa akisafiria, liligonga trekta iliyokuwa ikisafirisha miwa.

Ajali hiyo ilitokea karibu na Karange katika eneo la Awasi-Kericho mwendo wa saa moja usiku.

“Kutokana na ajali hiyo, Bw Bett alipata jeraha sehemu ya mbele ya kichwa huku wanawake wengine wawili watu wazima na dereva wakipata majeraha madogo,” ripoti ya polisi inasema.

Bw Bett na abiria wengine waliokuwa kwenye gari hilo walikimbizwa katika hospitali ya Awasi Catholic wakiwa katika hali nzuri na baadaye wakapelekwa hospitali ya Aga Khan kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, duru katika familia yake zilisema Ijumaa asubuhi, Agosti 16, 2024 kwamba mwanasiasa huyo wa zamani alipelekwa katika hospitali ya Siloam katika mji wa Kericho.

“Waziri huyo wa zamani yuko katika hali nzuri na ataruhusiwa kuondoka leo kwa vile alilazwa usiku kucha kwa uchunguzi,” mtu wa familia ambaye hakutaka kutajwa jina aliambia Taifa Dijitali kwa njia ya simu.

Aliongeza, “Nimetoka kumuona hospitalini asubuhi ya leo na yuko sawa. Hakuna sababu ya kutisha.”

Gari ambalo mwanasiasa huyo alikuwa akisafiria baadaye lilivutwa hadi kituo cha polisi cha Awasi.

Polisi walieleza kuwa trekta lililohusika katika ajali hiyo halikusimama na linaendelea kutafutwa.

Kulikuwa na mvua kubwa wakati wa ajali hiyo kulingana na polisi.

KUNA mambo unayofaa kufahamu na kutekeleza ili wanaume wavutiwe nawe na uolewe katika umri wa kufurahia maisha ya ndoa.

Kwanza kabisa, wanaume huwa wanapenda vipusa wanaotabasamu.

Hili ni tabasamu linaloanzia kwa macho na kuangaza uso na mashavu yako.

Tabasamu la uhakika la mwanamke ni ndumba kali inayopagawisha wanaume, linamfanya avutie machali.

Dada, jifunze kutabasamu, kukunja uso kunakuharibia raha na kufanya sura yako nzuri ikose mvuto.

Na usiwe mkali, kuwa mnyenyekevu iwapo unataka kupata na kudumisha mwanamume katika uhusiano.

Hii haimaanishi ujiachilie, elewa unacholenga. Usiwe mtu wa kujishaua na mwenye majitapo na uchunge ulimi wako.

Usiwe mtu wa kujishasha mbele ya machali. Tabaka sio kitu hapa. Wanaume wa tabaka lako wanaweza kukuambaa kwa sababu ya kudharau wale wa matabaka ya chini.

Jifunze kuheshimu watu wa kila tabaka dada na maisha yatakuwa shwari kwako. Kila mwanamume, awe wa tabaka la juu au la chini anapenda kuheshimiwa.

Unyenyekevu wako haumaanishi ukose kujiamini. Kwa hakika, wanaume huwa wanatiwa kichaa na wanawake wanaojiamini.

Wanaojitambua, wanaojua wanachotaka katika maisha, wenye maono, ari na malengo.

Kujua unachohitaji katika ulimwengu huu dada, kunakufanya upange ndoa yako. Kujiamini, dada, kunakufungulia milango ya mahaba.

Usijifunge, wanaume na wanawake hutafutana. Changamka, toka uende kwa hafla za kanisa, semina. Furahia maisha na kukutana na watu.

Unapofanya hivyo, jikwatue, pendeza na utapendwa.

Kuwa mkarimu na vitu vyote isipokuwa mwili wako.

Usifungue mzinga wako kwa kila anayeonyesha nia ya kukuchangamkia. Usibane maoni na msaada wako kwa mwanamume.

Ukarimu wa mwanamke usio wa mwili wake unavutia wanaume. Dada, usiwe mtu wa kulipiza kisasi.

Mahusiano huja na kwenda kabla ya kupata mume wa ndoto yako. Wasamehe waliokutema, msamehe chali aliyekutusi na yule aliyekuvunja moyo ulipoweka matumaini kwake na kumpa moyo wako.

Angalau ulipata funzo. Wasamehe na usonge mbele na maisha.

Ukiendelea kuanika hasira na kisasi chako kwa wanaume waliokucheza shere, wanaume watakuhepa na utakuwa singo maisha yako yote.

Haya yote yanahitaji demu kuwa na akili.

Wanaume hupenda wanawake wenye akili. Elewa kinachotendeka katika mazingira unayoishi, jipende kwanza ikiwa unataka kupendwa.

Ukijipenda hautajiachilia, jikubali ulivyo. Wanaume hupenda wanawake wanaojipenda kwanza na usilaze damu. Wanaume wa kisasa hawapendi mwanamke mzembe

mchumba
mpenzi
raha
Tabasamu

MITIHANI ya Kitaifa itakayofanyika muhula wa tatu huenda ikavurugika baada ya walimu na wahadhiri kutishia kuandaa mgomo wakitaka nyongeza ya mshahara.

Shule na vyuo vikuu nchini vimeratibiwa kufungiliwa mwishoni mwa mwezi huu na mapema mwezi ujao mtawalia. Wanafunzi wanaofanya Mtihani wa Kidato cha Nne Nchini (KCSE) wataanza mtihani wao Oktoba na huenda ndio wataathirika zaidi na mgomo huo iwapo utafanyika.

Masomo na muda wa kudurusu kwa watahiniwa hao utavurugwa iwapo walimu watakuwa wakishiriki mgomo. Muungano wa Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu Nchini (UASU) ndio wa hivi punde kutoa notisi ya kushiriki mgomo wakilalamikia kucheleweshewa mishahara yao.

Baadhi ya vyuo vikuu navyo havijalipa mishahara kwa wafanyakazi wao na masomo huenda yakavurugika vyuo vikuu vikifunguliwa mnamo Septemba.UASU ilitoa notisi hiyo mnamo Jumatano baada ya kuandaa mkutano wa baraza lake kuu.

Katibu Mkuu Dkt Constantine Wasonga amesema kuwa vyuo vikuu vimeendelea kuchelewesha mishahara ya wahadhiri na hata vikilipa, havilipi hela zote.

Dkt Wasonga alisema kuwa vyuo vikuu navyo pia havijakuwa vikiwasilisha makato ya mikopo, pensheni na makato mengine licha ya kuyaondoa kwenye mshahara wao.

Tishio la UASU la kuandaa mgomo linakuja wiki moja baada ya Chama cha Walimu Nchini (KNUT) na Muungano wa Walimu wa Shule za Upili na Vyuo Anuwai (KUPPET) kutangaza kuwa mgomo wa walimu nchini utaanza Agosti 26.

Hii ndiyo tarehe ambapo shule zitakuwa zikifunguliwa kwa muhula wa tatu. Kuppet mnamo Jumatatu iliwasilisha malalamishi yake kwa Waziri wa Leba, Dkt Alfred Mutua, ikisema kuwa haiwezi kuyasuluhisha kwa Tume ya Kuwaajiri Walimu Nchini (TSC).

Knut pia iliwasilisha malalamishi yake kwa Dkt Mutua mnamo Jumatano baada ya kuandaa mkutano na waziri huyo Jumanne.

Miungano ya walimu imekuwa ikitaka malipo ya awamu ya pili ya makubaliano ambayo walikuwa nayo na serikali maarufu kama CBA (2021-2025).

Makubaliano hayo yalisheheni matakwa yao ambapo walimu wakufunzi 46,000 waliokuwa wameajiriwa kupitia kandarasi, wangepewa ajira ya kudumu. Pia walimu 130,000 wangepandishwa vyeo.

Mgomo huo ni makaribisho mabaya kwa waziri mpya wa elimu Julius Ogamba. Ukifanyika basi maandalizi ya mtihani na kufanyika kwake kutavurugika zaidi.Vyuo vikuu navyo havijasazwa vikiendelea kuandamwa na madeni mengi ambayo sasa yamefikia Sh84 bilioni.

Mgao ambao walikuwa wakiupata kutoka kwa serikali nao ulipunguzwa baada ya serikali kukumbatia mfumo mpya wa ufadhili.

“Si jambo la haki kwa serikali kuendelea kuchelewesha mishahara ya wafanyakazi kwenye vyuo vikuu vya umma kila mwezi. Hii imesababisha ukosefu wa heshima na aibu kwa wanachama wetu,” akasema Dkt Wasonga.

Alitaja Chuo Kikuu cha Kiufundi Kenya (TUK) aliyodai iliwalipa wahadhiri asilimia 65 ya mshahara wao mnamo Julai.

“TUK wamevuka mpaka na natoa wito kwa wanachama wetu chuoni humo waandae mgomo. Kuanzia Septemba hakutakuwa na masomo ya chuo kikuu nchini kwa sababu serikali inaona kama tunafanya mzaha,” akaongeza.

Dkt Wasonga aliwakashifu Manaibu Chansela kwa kutomwambia Rais William Ruto kuwa mfumo wa kutoa mgao kwa vyuo vikuu mwaka ujao haufanyi kazi na unalemeza vyuo kifedha.

MAAFISA wa usalama walikuwa na nafasi ya kuepusha maafa ya watu zaidi ya 400 Shakahola iwapo wangefuatilia kwa undani ripoti za uvamizi wa eneo hilo mwaka wa 2021.

Imebainika mahakamani kuwa, salili za mapema zilizoonyesha kuwa shughuli haramu zilikuwa zikiendelea ndani ya Msitu wa Shakahola mapema mwaka wa 2021, zilipuuzwa na kupelekea watu zaidi ya 429 kupoteza maisha yao katika eneo hilo hilo miaka miwili baadaye.

Aliyekuwa afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Lango Baya (OCS), Inspekta Hamara Hassan, alikiri mbele ya Mahakama ya Mombasa kwamba ripoti ya uvamizi, ugavi na uuzaji wa ardhi kiharamu iliripotiwa katika kituo chao mnamo Agosti 4, 2021, lakini kesi hiyo haikufuatiliwa zaidi kubaini waliohusika.

Bw Hassan alikuwa afisini siku hiyo wakati Bw Alfred Mwazeze kutoka Watamu na Bw Daniel Kitsao walipotembelea kituo hicho kuwasilisha malalamishi.

Wawili hao walijitambulisha kama wanachama wa kampuni inayosimamia shamba kubwa la Chakama Ranch.

“Bw Mwazeze, ambaye alikuwa katibu alilalamika kwamba ardhi ya kampuni hiyo ilikuwa inauzwa. Walitambua kipande cha ardhi ambacho walishuku kilikuwa kimeuzwa kilomita tatu kutoka Makutano ya Shakahola kuelekea Sala Gate a,” akasema Bw Hassan.

Kulingana na afisa huyo, aliwashauri wawili hao warekodi taarifa na Konstebo wa Polisi Ibrahim Ali ili suala hilo lifuatiliwe zaidi.

“Lakini waliniambia kuwa watanipigia simu baada ya kufanya kikao na kamati nzima. Waliondoka lakini hawakupiga simu kama walivyoahidi,” afisa huyo alisema wakati wa kuhojiwa na kiongozi wa mashtaka  Mohamed Yassir.

Bw Hassan alisema aliwapigia simu watu hao lakini wakamweleza kwamba suala hilo sasa lilikuwa likishughulikiwa na Naibu Kamishna  wa Kaunti Ndogo ya Lango Baya (ACC).

Shahidi huyo alisema wawili hao walimwambia kuwa wamewahi kuwasilisha malalamishi hayo kwa chifu wa eneo hilo bila mafanikio.

Afisa huyo alisema hakufuatilia suala hili tena baada ya kufahamishwa kuwa ACC ya Lango Baya alikuwa ikiishughulikia.

“Hatukujua kilichokuwa kikiendelea msituni. Si kweli kwamba tulijua lakini hatukuweza kuthubutu kumkamata Paul Mackenzie,” akasema.

Huku akiongozwa na timu ya upande wa mashtaka inayojumuisha Jami Yamina, Alex Gituma, Victor Simbi, Victor Owiti, Betty Rubia, na Hillary Isiaho, afisa huyo alisema alifanya uchunguzi na kubaini kuwa ardhi inayomilikiwa na Mackenzie haikuwa yake.

“Ardhi inayojulikana kama Kwa Mackenzie ni mali ya Chakama Ranch. Mackenzie hana hatimiliki yoyote ya ardhi hii,” alisema.

OCS huyo wa zamani, hata hivyo, alibainisha kuwa hawakuweza kumshtaki Mackenzie kwa kosa lolote kwa sababu walioripoti hawakufichua majina ya wale walioukuwa wakiuza na kuuziwa ardhi yao.

Bw Hassan pia alikiri kwamba mshukiwa mkuu, Paul Mackenzie, aliripoti katika kituo hicho cha polisi mnamo Novemba 2022, chini ya OB NO 15/8/11/2022 saa kumi jioni, kuhusu mwanamke aliyedai kwenye mtandao wa kijamii kwamba alikuwa akisafirisha watu ndani ya msituni na kuwaua.

Hata hivyo, afisa huyo alisema hakuwa kazini siku hiyo, na kwa hivyo, suala hilo lilishughulikiwa na naibu wake.

“Ningependa kufafanua kuwa sikuwa katuoni wakati huo. Sikuwa kazini kuanzia Novemba 4 hadi 13, 2022. Niliporejea, sikujua kuliendaje hadi makaburi yaligunduliwa  ilipogunduliwa Aprili 1, 2023,” aliambia Hakimu Mkuu Alex Ithuku.

Alifichua kwamba naibu wake, Inspekta Stanley Bet, ambaye alikuwa kazini wakati huo, alikabidhi ripoti ya Mackenzie kwa Konstebo wa Polisi Elizabeth Muchai.

“Baada ya kuuliza, nilibaini kuwa baada ya Mackenzie kuwasilisha taarifa hiyo, alielekezwa kwa askari mwingine ambapo alikutana na Konstebo wa Polisi Simiyu ambaye alimshauri andikishe taarifa kwa SCCIO Malindi ambako alihudumiwa na Sajenti Yator. Hakuna faili ya kesi iliyofunguliwa katika kituo cha polisi cha Lango Baya kuhusu suala hili,” akasema.

Bw Hassan, ambaye sasa anahudumu katika makao makuu ya polisi ya kaunti ndogo ya Kinango huko Kwale, alisema kuwa kituo cha polisi cha Lango Baya haikuwa na vifaa vya kutosha kushughulikia kesi ya Mackenzie kwa sababu ilihitaji utaalam wa mtandaoni ili kubaini chanzo cha chapisho hilo.

Shahidi huyo alikana kufahamu lolote kuhusu Mackenzie kabla ya kukamatwa kwake Aprili 2023, wakati makaburi ya halaiki yalipogunduliwa katika msitu huo ambapo walikuwa wamefahamishwa hapo awali kuwa watu wasiojulikana walikuwa wakigawa na kuuzia watu ardhi.

“Kwa mara ya kwanza nilimfahamu Mackenzie wakati ripoti ya mtoto aliyetelekezwa na wazazi ilipoandikishwa na nilikutana naye kwa mara ya kwanza tulipoenda kumkamata,” afisa huyo alisema.

Shahidi aliyetoa ushahidi wake siku ya Jumatatu na Jumanne, alifahamisha mahakama kuwa uongozi wa eneo hilo ulikuwa na taarifa kuhusu matukio katika msitu huo lakini haukufanya lolote kuzuia watu kufa kwa njaa.

Mackenzie na wenzake 93 wamekanusha mashtaka 238 ya kuua bila kukusudia, wakidai kuwa vifo vya Shakahola havihusiani na uhuru wa kuabudu na kukusanyika waliyokuwa wakiendesha msituni.

Wameshikilia kwamba mafundisho na imani yao yanatokana na Biblia.

  • KWINGINEKO DUNIANI

zilizopitaMaandamano ya India yazidi kuongezeka kufuatia ubakaji na mauaji ya daktari

h
Maelezo ya picha,Vyama kadhaa vya madaktari vinatazamiwa kufanya maandamano mwishoni mwa juma

Maandamano yameongezeka nchini India baada ya umati wa watu kuharibu hospitali ambapo daktari mwanafunzi wa kike alibakwa na kuuawa katika jimbo la West Bengal.

Hospitali hiyo ilishambuliwa siku ya Jumatano wakati wa maandamano makubwa yaliyotajwa kama Reclaim the Night yaliyofanyika katika mji wa Kolkata kupinga uhalifu huo wa kikatili.

Maandamano madogo pia yalifanyika katika miji mingine mingi ya India kama Delhi, Hyderabad, Mumbai na Pune.

Chama cha Madaktari wa India (IMA) ambacho ni kikubwa zaidi cha madaktari nchini humo kimetangaza kuanza kwa mgomo wa kitaifa wa huduma zisizo za dharura siku ya Jumamosi.

  1. Wanajeshi wa Ukraine wamechapisha picha za video za shambulio lao kwenye kizuizi cha mpaka cha Urusi karibu na Sudzha, katika eneo la Kursk, mnamo tarehe 6 Agosti, siku ya kwanza ya uvamizi wao nchini Urusi.Video inaonyesha majengo kwenye kituo cha ukaguzi yakichomwa moto, na mengine kuharibiwa. Video inapoishia unaweza kuona kifaru chenye lenye nembo ya Ukraine kikielekea eneo la kaskazini, kuelekea Sudzha.Tulithibitisha eneo kwa kulinganisha mpangilio wa barabara na majengo kwenye kituo cha ukaguzi na picha za setilaiti zinazopatikana kwenye Google, Bing na nyinginezo.Tunaweza hata kujua mahali ambapo kifaru kinaendeshwa kwa alama za barabarani na idadi ya njia kwenye barabara karibu na kituo cha ukaguzi.Tunafahamu kuwa hii ilirekodiwa tarehe 6 Agosti kwa sababu picha za satelaiti zinazomilikiwa zinaonyesha majengo yote yakiwa salama tarehe 5 Agosti, na kuharibiwa tarehe 6 Agosti.Kwa kuangalia vivuli, shambulio hilo lazima liwe lilirekodiwa mapema jioni, kati ya kumi na moja unusu na saa moja za jioni , kwa saa za eneo.Upepo mdogo na wingu lililotawanyika pia vinaenddana sawia na ripoti za hali ya hewa za Sudzha kwa wakati huu.Unaweza pia kusoma:Ukraine iko ‘huru kutumia’ silaha za Uingereza kwenye ardhi ya Urusi – Wizara ya UlinziUkraine yaendelea kusonga mbele ndani ya eneo la UrusiUrusi: Hali katika eneo la Belgorod ‘ni tete’, – GavanaUrusi lazima ilazimishwe kuleta amani – ZelenskyPutin: ‘Lazima tumfukuze adui nje ya eneo letuWanajeshi wa Ukraine wapo kilomita 30 ndani ya eneo la UrusiKwa nini Ukraine imeanzisha mashambulizi ya mpakani dhidi ya Urusi?Steve Rosenberg: Uvamizi wa Ukraine unaonyesha vita vya Urusi haviendi kama ilivyopangwaUrusi yaongeza mashambulizi dhidi ya wakosoaji wake nje ya nMshirikishe mwenzako, Tazama: Picha ya video ya siku ya kwanza ya uvamizi wa Ukraine dhidi ya Mazungumzo ya kusitisha mapigano yaingia siku ya pili Doha huku Israel ikishambulia Ukingo wa MagharibigChanzo cha picha,ReutersMaelezo ya picha,Maandamano ya Wasraeli kudai kuhitimishwa kwa makubaliano ya kubadilishana wafungwa na kukomesha vita- Gaza, Agosti 15, 2024.Wapatanishi wa mzozo baina ya Israel na Hamas wataanza tena mkutano katika mji mkuu wa Qatar, Doha, kwa lengo la kufikia makubaliano ya mapatano katika Ukanda wa Gaza.Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar Majid Al-Ansari alisema siku ya Alhamisi kwamba mazungumzo kuhusu usitishaji mapigano na mateka huko Gaza yataendelea kwa siku ya pili mfululizo.Msemaji huyo ameongeza katika taarifa yake kuwa juhudi za wapatanishi wa Qatar, Misri na Marekani zinaendelea, akisisitiza kuwa wapatanishi hao wamedhamiria kusonga mbele katika juhudi zao za kufikia usitishaji wa vita katika Ukanda wa Gaza ambapo mateka hao wataachiliwa huru na kiasi kikubwa zaidi cha msaada wa kibinadamu kitaingia Gaza.Afisa wa Marekani, akizungumza na Reuters, alielezea siku ya kwanza ya mazungumzo kama “ya kujenga.”Wakati huo huo, Israel inaendelea na mashambulizi yake dhidi ya Gaza, na maafisa wa matibabu huko Gaza wanasema kuwa Wapalestina wasiopungua sita waliuawa Alhamisi jioni katika shambulio la anga la Israel kwenye nyumba moja huko Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.Unaweza pia kusoma:Tofauti yazuka kati ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wake wa Ulinzi – Kunani?Je, nguvu ya mashambulizi ya Iran inalinganishwaje na ya Israel?‘Mzozo unatokota’: Mauaji ya polisi ni sehemu ya vurugu zinazoendelea Ukingo wa MagharibiMshirikishe mwenzako, Mazungumzo ya kusitisha mapigano yaingia siku ya pili Doha huku Israel ikishambulia Ukingo wa Magharibi
  2. Saa 2 zilizopitaVita vya Ukraine: Urusi yadai kufanikiwa kushambulia vikosi vya Ukraine ndani ya UrusigChanzo cha picha,Getty ImagesMaelezo ya picha,Askari wa Ukraine akiwa amepumzika kwenye kifaru cha Marekani Stryker baada ya kurejea kutoka kwenye mapigano katika eneo la Kursk.Baada ya Ukraine kutangaza kuwa jeshi lake la anga limedungua droni 5 za Urusi, wizara ya ulinzi ya Urusi pia imejibu kupitia Telegram mapema leo asubuhi kuwa majeshi yake yamefanikiwa kushambulia wanajeshi wa Ukraine katika eneo la mpaka la Kursk nchini Urusi.Tangazo hilo limesema : “Wahudumu wa anga kwenye helikopta za Mi-28NM walifanya mashambulizi usiku dhidi ya wafanyikazi, magari ya kivita na vifaa vya kijeshi vilivyokuwemo ndani ya magari ya Wanajeshi wa Ukraine katika eneo la mpaka wa jimbo la Kursk.”Taarifa hiyo inasema pia kwamba ripoti za kijasusi zinaonyesha maeneo yote maalumu yaliyolengwa yameharibiwa.Soma zaidi:Ukraine iko ‘huru kutumia’ silaha za Uingereza kwenye ardhi ya Urusi – Wizara ya UlinziUkraine yaendelea kusonga mbele ndani ya eneo la UrusiUrusi: Hali katika eneo la Belgorod ‘ni tete’, – GavanaUrusi lazima ilazimishwe kuleta amani – ZelenskyPutin: ‘Lazima tumfukuze adui nje ya eneo letuWanajeshi wa Ukraine wapo kilomita 30 ndani ya eneo la UrusiKwa nini Ukraine imeanzisha mashambulizi ya mpakani dhidi ya Urusi?Steve Rosenberg: Uvamizi wa Ukraine unaonyesha vita vya Urusi haviendi kama ilivyopangwaUrusi yaongeza mashambulizi dhidi ya wakosoaji wake nje ya nchiMshirikishe mwenzako, Vita vya Ukraine: Urusi yadai kufanikiwa kushambulia vikosi vya Ukraine ndani ya Urusi
  3. Saa 2 zilizopitaDroni tano za Urusi zadunguliwa usiku, jeshi la anga la Ukraine lamesemagChanzo cha picha,Maxar Technologies/Handout via REUTERSKatika taarifa yake ya Telegram iliyotolewa asubuhi, jeshi la anga la Ukraine linasema kuwa limedungua ndege tano zisizo na rubani zilizorushwa na Urusi katika majimbo yake ikiwa ni pamoja na Odesa na Poltava.Taarifa hiyo pia inasema kuwa Urusi ilishambulia kwa makombora matatu ya balestiki ya Iskander-M.Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba gavana wa Kyiv hajaripoti uharibifu wowote au majeruhi.Pia kwenye Telegram, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilichapisha asubuhi ya leo kwamba “wameteka na kuharibu aina tano za ndege kwenye Bahari Nyeusi”.Pia walidai kuharibu boti mbili zinazo na nahodha zilizokuwa “zikielekea katika Rasi ya Crimea”.Unaweza pia kusoma:Ukraine iko ‘huru kutumia’ silaha za Uingereza kwenye ardhi ya Urusi – Wizara ya UlinziUkraine yaendelea kusonga mbele ndani ya eneo la UrusiUrusi: Hali katika eneo la Belgorod ‘ni tete’, – GavanaUrusi lazima ilazimishwe kuleta amani – ZelenskyPutin: ‘Lazima tumfukuze adui nje ya eneo letuWanajeshi wa Ukraine wapo kilomita 30 ndani ya eneo la UrusiKwa nini Ukraine imeanzisha mashambulizi ya mpakani dhidi ya Urusi?Steve Rosenberg: Uvamizi wa Ukraine unaonyesha vita vya Urusi haviendi kama ilivyopangwaUrusi yaongeza mashambulizi dhidi ya wakosoaji wake nje ya nchiMshirikishe mwenzako, Droni tano za Urusi zadunguliwa usiku, jeshi la anga la Ukraine lamesema
  4. Saa 3 zilizopitaMan Utd ‘hawako tayari’ kucheza dhidi ya Fulham leo – Ten Hag.Chanzo cha picha,Getty ImagesMaelezo ya picha,Meneja wa Man United Erik ten HagMeneja wa Manchester United Erik ten Hag ana wasiwasi kuwa timu yake “haiko tayari” kwa mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Fulham siku ya Ijumaa.Wachezaji wapya waliosajiliwa Matthijs de Ligt na Noussair Mazraoui watakuwa kwenye kikosi hicho lakini waliwasili Alhamisi.Wamekuwa na nafasi finyu ya kufanya mazoezi na wenzao wapya, na kumwacha meneja Ten Hag na kizungumkuti cha kuchagua wachezaji 11 wa kwanza watakaomenyana na Fulham Old Trafford.Wakati huohuo, beki Luke Shaw anauguza jeraha la mguu huku naye mlinzi mpya aliyenunuliwa kwa dau la £52m Leny Yoro akipata jeraha litakalomuweka nje kwa miezi mitatu naye fowadi Rasmus Hojlund pia akiguza jeraha la paja.United ilijitolea kutumia karibu pauni milioni 60 kuwaleta mabeki De Ligt na Mazraoui kwenye klabu kutoka Bayern Munich.“Timu haiko tayari lakini ligi inaanza,” alisema Ten Hag.”Kuna mameneja wengi zaidi ambao wanakabiliwa na tatizo hili lakini inabidi tuanze.”Hatuwezi kujificha. Hatuwezi kuikimbia. Tunapaswa kukabiliana nayo.”Mchezaji mwingine aliyesajiliwa na United majira ya kiangazi, mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkee, alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika wakati wa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester City na anaweza kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Fulham.Mazraoui anaweza kuwa jibu moja, huku Diogo Dalot na Lisandro Martinez wakiwa wametumika kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Jumamosi iliyopita.Licha ya kuwa kuna masuala kuhusu ni mchezaji gani anapaswa kuza katika kikosi cha kwanza Ten Hag bado anatarajia kupanga kikosi kikali”Sio kuhusu wachezaji ambao hawapatikani,” Mholanzi huyo alisema.”Pia ni kile nilichosema msimu uliopita – ni kuhusu wachezaji ambao wanapatikana na tuna kundi zuri, tunaweza kuchagua kikosi kikali.”Shaw hajaichezea United tangu Februari, hasa kwa sababu ya jeraha la misuli ya paja, ingawa hatimaye alikuwa vyema kuichezea England kwenye Euro 2024.Ten Hag ana uhakika Shaw atakuwa tayari hivi karibuni na anatazamia kurejea.”Atarejea baada ya muda mfupi,” Ten Hag alisema. “Haichukui muda mrefu.Mshirikishe mwenzako, Man Utd ‘hawako tayari’ kucheza dhidi ya Fulham leo – Ten Hag
  5. Saa 3 zilizopitaMbunge akosolewa kwa kuuliza kama wanaume wana ‘haki za unyumba’.Chanzo cha picha,Seneti ya UfilipinoSeneta mmoja nchini Ufilipino ameshutumiwa mitandaoni baada ya kuuliza bungeni ikiwa wanaume wana “haki za unyumba” kwa wake zao.Robin Padilla, mwigizaji wa zamani, aliuliza swali hilo kwa wakili maarufu wa haki za binadamu, ambaye alialikwa kama mtaalam kwenye kikao cha unyanyasaji wa kijinsia katika tasnia ya burudani.Pia aliuliza je, wanaume wanapaswa kufanya nini ikiwa “wanataka kuwa na wake zao” lakini wao hawataki – ambapo wakili Lorna Kapunan alijibu kwamba wanaweza “kutazama Netflix”.Wakili huyo aliongeza kuwa baadhi ya wanaume wanahisi kwamba wake zao wapo ili “kuwahudumia,” na kusema kuwa “sio wajibu wa mke kumhudumia mumewe”.Maoni ya Bw Padilla yalizua gumzo mtandaoni, huku mmoja akisema “anakera”.Katika mtandao wa X, mmoja alisema: “Je, hilo linafanya wake kuwa wafanyabiashara ya ngono kwa waume zao?””Wanaume hawana ‘haki za ngono’ zaidi ya wake zao. Wanawake wana haki sawa na uhuru wa kuchagua watakacho. Hapana inamaanisha hapana. Ni heshima tu,” alisema wakili wa haki za binadamu Jose Manuel Diokno kwenye mtandao wa X.Soma zaidi:Faida za kiafya za kushiriki tendo la ndoa mara kwa maraMshirikishe mwenzako, Mbunge akosolewa kwa kuuliza kama wanaume wana ‘haki za unyumba’
  6. Saa 4 zilizopitaOperesheni ya Ukraine huko Kursk ilipangwa na Nato na nchi za Magharibi – Urusi.Chanzo cha picha,Getty ImagesMsaidizi wa karibu wa Putin Nikolai Patrushev amenukuliwa na gazeti la Urusi la Izvestia akisema kuwa Nato na nchi za Magharibi zilihusika katika kupanga uvamizi unaoendelea wa Ukraine katika eneo la Kursk, kulingana na shirika la habari la Reuters.”Operesheni katika eneo la Kursk pia ilipangwa kwa ushirikiano wa Nato na huduma maalum za nchi za Magharibi,” gazeti la Izvestia limemnukuu Patrushev.”Taarifa za uongozi wa Marekani kwamba haikuhusika katika uhalifu wa Ukraine katika eneo la Kursk si za kweli… Bila ushiriki wao na usaidizi wa moja kwa moja, Kyiv isingeingia katika eneo la Urusi.”Mapema wiki hii, Ikulu ya Marekani ilisema kwamba haikuwa na taarifa ya mapema kuhusu operesheni hiyo na haikuhusika.Ukraine inasema vikosi vyake vinaendelea kusonga mbele katika eneo la Urusi na pande mbalimbali. Pia imeanzisha ofisi ya kijeshi ndani ya Urusi.Soma zaidi:Ukraine yafungua ofisi ya kijeshi katika ardhi ya UrusiUkraine iko ‘huru kutumia’ silaha za Uingereza kwenye ardhi ya Urusi – Wizara ya UlinziUkraine yaendelea kusonga mbele ndani ya eneo la UrusiUrusi: Hali katika eneo la Belgorod ‘ni tete’, – GavanaUrusi lazima ilazimishwe kuleta amani – ZelenskyPutin: ‘Lazima tumfukuze adui nje ya eneo letuWanajeshi wa Ukraine wapo kilomita 30 ndani ya eneo la UrusiKwa nini Ukraine imeanzisha mashambulizi ya mpakani dhidi ya Urusi?Steve Rosenberg: Uvamizi wa Ukraine unaonyesha vita vya Urusi haviendi kama ilivyopangwaUrusi yaongeza mashambulizi dhidi ya wakosoaji wake nje ya nchiMshirikishe mwenzako, Operesheni ya Ukraine huko Kursk ilipangwa na Nato na nchi za Magharibi – Urusi
  7. Saa 5 zilizopitaMatthew Perry: Watano washtakiwa kwa kifo kilichohusishwa na dawa za kulevya.Chanzo cha picha,Getty ImagesWatu watano wameshtakiwa katika kifo kilichohusiana na dawa za kulevya cha Matthew Perry mwaka jana, polisi wanasema, wakiwemo madaktari wawili na msaidizi wa kibinafsi wa mwigizaji huyo.Polisi walisema siku ya Alhamisi kwamba uchunguzi wao, ulioanza mnamo mwezi Mei, ulifichua “mtandao mpana wa uhalifu” wa wauzaji wa dawa za kulevya ambao walimpa kiasi kikubwa cha dutu za ketamine.Perry, 54, alifariki akiwa nyumbani kwake Los Angeles mnamo Oktoba. Uchunguzi wa maiti uligundua mkusanyiko mkubwa wa ketamine katika damu na kuhitimisha kuwa “athari za papo hapo” za dutu hiyo ndio chanzo cha kifo chake.”Washtakiwa hawa walitumia hali ya uraibu wa Bw Perry kujitajirisha,” Wakili wa Marekani Martin Estrada alisema Alhamisi. “Walijua wanachofanya ni kuhatarisha maisha ya Bw Perry, lakini walifanya hivyo.”Ketamine – ni dawa yenye nguvu ya ganzi – hutumiwa kama matibabu ya kutuliza msongo wa mawazo, wasiwasi na maumivu. Watu wa karibu wa Perry, ambaye aliigiza kama mmoja wa wahusika wakuu kwenye kipindi cha televisheni cha NBC Friends, walisema kwamba alikuwa akipata matibabu ya ketamine.Lakini alikuwa amepata matibabu ya mwisho zaidi ya wiki moja kabla ya kifo chake.Mkaguzi wa matibabu alisema ketamine katika mfumo wa Perry haiwezekani kuwa tiba aliyopata kwa sababu dawa hiyo huwa haikai kwa muda mrefu ndani ya mwili.Viwango vya ketamine katika mwili wake vilikuwa vya juu kama kiwango kilichotolewa wakati wakati wa matibabu ya ganzi, kulingana na mkaguzi wa matibabu.Soma zaidi:‘Dawa za kulevya zilinisababishia kukojoa damu na kuleta shida kwenye ubongo’Uraibu wa dawa za kulevya miongoni mwa vijana na wanawake nchini SomaliaMshirikishe mwenzako, Matthew Perry: Watano washtakiwa kwa kifo kilichohusishwa na dawa za kulevya
  8. Saa 6 zilizopitaBinti wa waziri mkuu wa zamani amekuwa kiongozi mdogo zaidi Thailand.Chanzo cha picha,Getty ImagesBunge la Thailand limemchagua Paetongtarn Shinawatra, binti wa bilionea na kiongozi wa zamani Thaksin, kuwa waziri mkuu.Akiwa na umri wa miaka 37, atakuwa Waziri Mkuu mdogo zaidi nchini na mwanamke wa pili katika wadhifa huo, baada ya shangazi yake Yingluck.Uteuzi wake umefanyika siku mbili tu baada ya Waziri Mkuu wa zamani Srettha Thavisin kufutwa kazi na mahakama ya kikatiba.Wote wawili wanatoka chama cha Pheu Thai, ambacho kilishika nafasi ya pili katika uchaguzi wa 2023 lakini wakaunda muungano unaotawala.Bi Paetongtarn anakabiliwa na kibarua kigumu cha kufufua uchumi uliokwama wa Thailand na kuepuka mapinduzi ya kijeshi na uingiliaji kati wa mahakama ambao umeondoa tawala nne zilizopita zikiongozwa na familia yake.Bi Paetongtarn, ambaye aliidhinishwa kwa kupata kura 319 dhidi ya 145 siku ya Ijumaa, ni wa nne wa ukoo wa Shinawatra kuwa waziri mkuu katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.Wengine watatu, akiwemo babake Thaksin na shangazi yake Yingluck, waliondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi au maamuzi ya mahakama ya kikatiba.Mahakama hiyo hiyo ilimuondoa Bw Thavisin Jumatano kwa kumteua wakili wake wa zamani ambaye aliwahi kufungwa katika baraza lake la mawaziri.Pia unaweza kusoma:Mwanamke kuwa kiongozi wa ThailandMshirikishe mwenzako, Binti wa waziri mkuu wa zamani amekuwa kiongozi mdogo zaidi Thailand
  9. Saa 7 zilizopitaJaji asimamishwa kazi kwa kumfunga pingu msichana aliyelala wakati wa ziara ya mafunzo mahakamani.Chanzo cha picha,36th District CourtJaji wa Detroit amesimamishwa kazi kwa muda baada ya kumlazimisha msichana mwenye umri wa miaka 15 kuvaa pingu na sare ya jela kwa sababu alionekana kusinzia wakati wa ziara ya shule mahakamani.Jaji wa Mahakama ya Wilaya Kenneth King alisema hakupenda “mtazamo” wa Eva Goodman na akaongeza kuwa alitaka kumwonyesha “mwenendo wake unavyotakiwa kuwa mahakamani”.Kijana huyo alikuwa akitembelea Mahakama ya Wilaya kwa ajili ya ziara iliyoandaliwa na shirika la kutoa msaada la mazingira la The Greening, ambalo ziara zake nyingine ni pamoja na kukayaki na kutazama ndege kwenye mazingira yao asili.Siku ya Alhamisi, hakimu mkuu wa Mahakama ya Wilaya,​​William McConico, alisema katika taarifa kwamba alikuwa amefanya “uchunguzi wa kina” wa tukio hilo na akaamua kumsimamisha kazi Bw King kwa muda ili apate “mafunzo ya msingi”.”Tunatumai kwa dhati kwamba tukio hili halitaharibu uhusiano wetu wa muda mrefu na shule za mitaa,” Jaji McConio alisema.Mama wa msichana huyo, Latoreya Hill, aliambia vyombo vya habari eneo hilo: “Je, ungependa mtu amtendee mtoto wako hivyo?”Kumdharau mbele ya ulimwengu mzima na marafiki zake, kumfanya ajisikie vibaya zaidi kuhusu hali yake.”Video kutoka mahakamani inamwonyesha Jaji King akimwambia bintiye Bi Hill: “Jambo moja utakalojifunza kuhusu mahakamani ni kwamba mimi si mwanasesere. Sitakiwi kuchezewa.”Mshirikishe mwenzako, Jaji asimamishwa kazi kwa kumfunga pingu msichana aliyelala wakati wa ziara ya mafunzo mahakamani
  10. Saa 8 zilizopitaHarris “atakuwa rais wa kupigiwa mfano” – BidenJoe Biden na Kamala HarrisChanzo cha picha,Getty Images
  11. Makamu wa Rais Kamala Harris na Rais Joe Biden wameonekana kwenye hafla pamoja kwa mara ya kwanza tangu rais alipojiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania muhula wa pili na Bi Harris kuchukua nafasi yake kama mgombeaji wa chama cha Democratic.Hafla hiyo ya chama cha Democratic iliyofanyika Alhamisi ilisherehekea makubaliano mapya ya serikali ya Biden ya kupunguza gharama ya dawa 10 za kawaida kwa mamilioni ya Wamarekani.Pia ilitoa taswira ya mabadiliko ya wawili hao, wiki kadhaa baada ya chama kujipanga upya.Ikulu ya White House ilisema takriban watu 2,300 walihudhuria mkutano wa Alhamisi huko Upper Marlboro, Maryland – ngome ya chama cha Democratic.”Nina mshirika wa kipekee katika maendeleo tuliyofanya,” rais alisema. “Atakuwa rais wa kupigiwa mfano.”Lakini zaidi ya tangazo la sera, Bw Biden alimwagia sifa makamu wake wa rais. Umati ulijipata ukisherehekea mara kadhaa.”Kuna upendo wa ajabu humu kwa rais wetu,” Bi Harris alisema. “Viongozi wachache kama Joe Biden katika taifa letu wamejitolea zaidi, katika masuala mengi, ikiwa ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa gharama nafuu.”Soma zaidi:Kocha wa zamani wa mpira wa miguu na mwalimu – sasa ndiye mgombea mwenza wa HarrisKamala Harris ni nani, makamu wa rais ambaye Biden anamuunga mkono kuwa rais?Mshirikishe mwenzako, Harris “atakuwa rais wa kupigiwa mfano” – Walowezi wa Israeli wateketeza kijiji cha Ukingo wa Magharibi.Chanzo cha picha,Reuters. Makumi ya walowezi wa Israeli wamechoma moto nyumba na magari kwenye kijiji kimoja katika Ukingo wa Magharibi kinachokaliwa kwa mabavu, huku wizara ya afya ya Palestina ikisema kuwa mtu mmoja ameuawa.Walowezi hao – baadhi yao wakiwa wamejifunika nyuso – walirusha mawe na aina ya bomu ambalo kawaida hujumuisha chupa iliyojazwa kioevu kinachoweza kuwaka na utambi unaowashwa kabla ya kurushwa, walipokuwa wakishambulia kijiji cha Jit, karibu na mji wa Nablus, Alhamisi jioni, Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) lilisema.Wizara ya afya ya Palestina ilisema mwanakijiji wa eneo hilo mwenye umri wa miaka 20 aliuawa na mtu mwingine kujeruhiwa vibaya kifuani.IDF ilisema inachunguza ripoti ya kifo hicho.Viongozi wa kisiasa wa Israeli wamelaani shambulizi hilo, na kuahidi kuwaadhibu wahusika. Raia mmoja wa Israeli alizuiliwa huko Jit, IDF ilisema.Kanda za video zimeibuka kwenye mitandao ya kijamii zinazodaiwa kuonyesha nyumba na magari yakichomwa moto huko Jit siku ya Alhamisi na moshi mwingi unaonekana ukipanda juu ya kijiji.Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ilisema katika taarifa yake kwamba “waliohusika na kitendo chochote cha uhalifu watakamatwa na kufunguliwa mashtaka”.Pia unaweza kusoma:Je, walowezi wa Israel wenye itikadi kali wanaolengwa na vikwazo vya Marekani na Uingereza ni akina nani?Walowezi wa Kiyahudi wanaotaka kujenga makazi huko GazaMshirikishe mwenzako, Walowezi wa Israeli wateketeza kijiji cha Ukingo wa Magharibi
  12. 16 Agosti 2024 –Ukraine yafungua ofisi ya kijeshi katika ardhi ya Urusi.Chanzo cha picha,Getty ImagesUkraine imefungua ofisi ya utawala wa kijeshi katika eneo la Kursk magharibi mwa Urusi, ambapo uvamizi wake wa kushtukiza katika ardhi ya Urusi unaendelea, kulingana na kamanda wake mkuu wa kijeshi.Jenerali Oleksandr Syrsky alisema ofisi hiyo “itadumisha sheria na utulivu” na “kukidhi mahitaji ya haraka” ya watu katika eneo hilo.Katika video iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii, Jenerali Syrsky anaonekana akiuambia mkutano ulioongozwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwamba ofisi hiyo imeanzishwa “kwenye maeneo yanayodhibitiwa na Ukraine”.Wakati huo huo, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Andrei Belousov amesema Urusi itatuma wanajeshi zaidi “kulinda” watu katika eneo hilo.Ukraine pia ilidai kuwa imepata mafanikio zaidi katika uvamizi wake siku ya Alhamisi.Wanajeshi wa Ukraine walikuwa kilomita 35 ndani ya eneo la Kursk, ambapo wanadhibiti eneo la kilomita za mraba 1,150, pamoja na makazi 82, Jenerali Syrsky alisema.Sasa katika siku yake ya 10, huu ni uvamizi mkubwa zaidi wa Ukraine ndani ya Urusi tangu ilipoanzisha uvamizi wake mnamo 2022.Lakini Ukraine imesema haina nia ya “kuchukua” eneo la Urusi.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment