Empowerment Mathematics-Una ndoto kubwa unataka kuitimiza, dunia inataka ubora.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wale waliokuumiza huwa wanatamani kukuona ukiwa umechakaa na unaendelea kulia,fungua ukurasa mpya na usiwape wanachota.

Kama wewe ni KIJANA hakikisha unasoma ujumbe huu mpaka mwisho…

Una NDOTO KUBWA Unataka Kuitimiza?

Inaweza kuwa kwenye KIPAJI ulichonacho…

Inaweza kuwa kwenye BIASHARA unayofanya…

Inaweza kuwa kwenye AJIRA yako…

Tunapoazimisha Siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani ni muhimu kuhakikisha tunaongeza UBORA wa tunachofanya kila siku.

Kabla ya kulipwa kiasi fulani cha fedha kwenye jambo fulani…

…ni muhimu kuhakikisha umejenga UBORA wako na kuweza kutengeneza thamani zaidi ya kile unachotaka kulipwa.

Dunia inataka watu BORA kwenye kila eneo bila kujali umri.

Ndio maana leo kuna vijana wadogo wenye biashara KUBWA za mabilioni.

Leo kuna vijana wadogo wanafanya majukumu MAKUBWA kwenye kampuni mbalimbali duniani.

Leo chagua uneo unalotaka kuwa BORA.

JINOE kwa bidii yote.

Nina uhakika ukifanya hivyo UTATIMIZA NDOTO ZAKO.

Majira magumu zaidi kwenye kupambania ndoto yako ni pale ambapo watu wako wa karibu sana ndio ambao hawakuamini au hawakusapoti na wanakukatisga tamaa.
Ndoto za wengi zimefia hapa. Ni muhimu kujifunza kuwa sio lazima watu wako wa karibu wawe sehemu ya mchakato wa kuinuka kwako.Kuba wengine watarudi ukishafima juu.”Ndio wataanza kusema ni mtu wangu/Ndugu yangu yule.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment