Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

KOCHA wa zamani ambaye sasa ni mshauri wa klabu ya Ajax nchini Uholanzi, Louis van Gaal, 72, ametoa taarifa kuhusu jinsi anavyoendelea kupigana vita na saratani ya tezi dume.
Mkufunzi huyo wa zamani wa Barcelona, Bayern Munich na Manchester United aligunduliwa kuwa anaugua kansa mnamo 2021 lakini hapo awali akaweka hali yake ya afya kuwa siri.
Alishangaza wengi alipofunguka na kukiri kwamba alikuwa akipambana na ugonjwa wa saratani alipokuwa akiongoza timu ya taifa ya Uholanzi kwenye kampeni za Kombe la Dunia mnamo 2022 nchini Qatar.
“Nimekuwa nikiishi na ugonjwa huo kwa zaidi ya miaka mitatu. Imekuwa ni kuchomwa sindano za homoni mara kwa mara, upasuaji mmoja baada ya mwingine na kubeba mifuko ya mkojo.”
“Huenda ninachosema kisiaminike, lakini ndivyo ambavyo hali imekuwa. Nimesimama nisianguke na niliweza kufanya kazi hata wakati wa fainali zilizopita za Kombe la Dunia,” akasema.
Kama ilivyo kwa mamilioni ya wanaume wanaougua saratani ya kibofu, korodani au tezi ya kiume kote ulimwenguni, utendaji wa kimsingi wa kibinadamu ambao hapo awali ulikuwa wa kawaida sasa ni shida pia kwa Van Gaal.
Alisema: “Ninaendelea vizuri. Baada ya miaka mitatu ya matibabu ya mionzi, maambukizo ya figo na upasuaji wa tezi dume, hatimaye ninaweza kuudhibiti ugonjwa huu.”
“Ninaweza kwenda haja ndogo kwa namna ya kawaida, na hilo ndilo jambo muhimu. Lakini siwezi kabisa kushiriki tendo la ndoa. Nimeuaga huo mchezo wa ngono na hilo huenda liwe tatizo kwa mke wangu Truus ambaye nilimuoa 2008.”
Hata hivyo, kuwa na saratani hakujabadilisha mtazamo wa Van Gaal kuhusu maisha.

“Tazama, ninatoka katika familia ambayo sisi ni ndugu tisa wa kiume. Mimi ndiye mdogo kwa wote. Babangu alifariki nikiwa na umri wa miaka 11. Aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 53.”
“Mke wangu wa kwanza, Fernanda Obbes, alifariki akiwa na umri wa miaka 39. Na ndugu zangu wote waliaga mapema sana. Nimezoea kifo na ninajua ni sehemu ya maisha.”
Alipoulizwa iwapo anaogopa kifo wakati wa mahojiano yake na wanahabari wiki hii, Van Gaal alijibu: “Kweli, mtu hafi haraka hivyo kutokana na saratani ya kibofu. Japo kuna baadhi ya watu wanaofariki kutokana na ugonjwa huo, wengi wao hufa kutokana na matatizo mengine. Sijaogopa sana, lakini sijapata maisha yangu yakiwa ya kufurahisha tena.”
MAHAKAMA kuu imezima Polisi kumkamata na kumshtaki kiongozi wa Chama cha kisiasa cha Safina Jimi Wanjigi.
Na wakati huo huo Jaji Bahati Mwamuye aliwaagiza polisi wamwachilie mara moja Wanjigi endapo walifaulu kumkamata baada ya kupiga kambi katika makazi yake katika mtaa wa kifahari Muthaiga usiku wa Agosti 8,2024.
Jaji Mwamuye alitoa maagizo hayo baada ya Wanjigi kuwasilisha ombi katika mahakama kuu akiomba korti isambaratishe hatua za polisi za kumkamata na kumshtaki kwa kumili silaha hatari.
Wakili Nelson Osiemo aliwasilisha kesi dhidi ya Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli na Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) Mohamed Amin akisema “wametisha kumkamata Wanjigi.”

Bw Osiemo alieleza mahakama kwamba polisi walimwandama Wanjigi kutoka kati kati mwa jiji Agosti 8 baada ya kushiriki katika maandamano ya Nane Nane hadi katika makazi yake mtaani Muthaiga.
“Polisi walidai kwamba walipata grunedi nne zikiwa ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa nje ya nyumba yake,” Bw Osiemo alimweleza Jaji Mwamuye.
Wakili huyo alisema “Jimi Wanjigi kamwe hajui chochote kuhusu grunedi nne zilizokuwa kwenye gari lililokuwa nje ya makazi yake.”
Mahakama ilielezwa Wanjigi anahofia polisi watamkamata na kumzuilia kwa makosa asiyoyajua.
Bw Osiemo alisema hati za mlalamishi zitakandamizwa endapo mahakama haitazima hatua ya polisi kumshika.
Akitoa uamuzi Jaji Mwamuye alisema ametathmini kwamba huenda haki za mlalamishi (wanjigi) zikakandamizwa iwapo polisi watamkamata na kumzuilia bila kumweleza sababu.
Jaji huyo aliamuru kesi hiyo itajwe Agosti 16, 2024 kwa maagizo zaidi.
MASHIRIKA ya kijamii kaunti ya Kilifi, yametoa wito kwa juhudi za pamoja za kumaliza mauaji ya wazee kwa kushukiwa kuwa wachawi.

Mashirika hayo yanasikitika kuwa vijana katika kaunti hiyo wanaendelea kuwaua wazee na baadhi yao wamegeuza uhalifu huo kuwa ajira huku wakikodishwa kutekeleza mauaji kwa niaba ya watu wa familia za waathiriwa.
Wawakilishi wa mashirika yanayojumuisha Malindi District Cultural Association, the Malindi Gender-Based Violence (GBV) Network na Haki Yetu pia wameshinikiza kubadilishwa kwa sheria ya kuthibiti uchawi ili kujumuisha masuala ibuka.
Wakizungumza wakiwa kituo cha kitamaduni cha Mekatilili wa Menza kilichoko wadi yao Sabaki, Magarini, wakati wa ziara ya Kamati ya Watumiaji wa Korti viongozi wa mashirika hayo walisema mauaji ya wazee bado yanaendelea katika kaunti hiyo.
Kamati iliyoongozwa na Hakimu Mkuu wa Malindi Elizabeth Usui ilitembelea kituo hicho kutoa msaada wa chakula na bidhaa nyingine kwa wazee wanaohifadhiwa humo baada ya kutoroka boma zao kufuatia vitisho kutoka kwa watu wa familia zao na majirani wakishukiwa kuwa wachawi.
Katibu Mkuu wa MADCA, Bw Joseph Karisa Mwarandu alilalamika kuwa ukatili huo unaendelea kwa sababu haulaaniwi vya kutosha na viongozi wa kisiasa, kidini na maafisa wa utawala.
Alisema kwamba ni mashirika ya kijamii na kitamaduni ambayo yameachiwa vita dhidi ya dhuluma na ukatili unaotendewa wazee.
“Tatizo hili linaendelea kuzidi kwa kuwa hatusikii likilaaniwa na kila mtu. Hatusikii sauti za viongozi wa kisiasa, serikali na kidini na ndio sababu imekuwa vigumu kupigana na uhalifu huu,” alilalamika.
“Hili sio tatizo la kitamaduni. Ni suala la usalama kwa sababu kwa maoni yangu, vijana wengi wa kiume wamefanya mauaji ya wazee kuwa biashara,”alisema Mwarandu.
“Inasikitisha kwamba wauaji wanaongezeka kila siku ambao kwa sasa wanakodishwa, kwa sababu wamechukulia uhalifu huu kama shughuli ya kuwapa mapato,” alisema Bw Mwarandu ambaye ni wakili anayehudumu Malindi.
Maoni yake yaliungwa na wenzake wa Haki Yetu, Warda Zighe na Helder Lameck wa Malindi GBV Network, ambao walitaka Sheria ya Kuthibiti Uchawi ifanyiwe mabadiliko.
AjiraYaMauaji
HofuYatanda
MauajiYaWazee.
WashukiwaWachawi
KIPENGA CHA MICHEZO
Jedwali la medali ya mashindano ya Olimpiki ya Paris 2024
24 Julai 2024
Nani anayeshinda dhahabu nyingi? Wanariadha kutoka zaidi ya nchi 200 wanashindania medali 329 katika michezo 32 kwenye mashindano ya Olimpiki ya Paris.
Tazama mashindano yote ya Olimpiki katika BBC News Swahili
| Nafasi | Timu | Dhahabu | Fedha | Shaba | Jumla |
|---|---|---|---|---|---|
| 1 | 33 | 39 | 39 | 111 | |
| 2 | 33 | 27 | 23 | 83 | |
| 3 | 18 | 16 | 14 | 48 | |
| 4 | 16 | 8 | 13 | 37 | |
| 5 | 14 | 20 | 23 | 57 | |
| 6 | 14 | 20 | 22 | 56 | |
| 7 | 13 | 8 | 7 | 28 | |
| 8 | 13 | 6 | 10 | 29 | |
| 9 | 12 | 9 | 8 | 29 | |
| 10 | 11 | 12 | 13 | 36 | |
| 11 | 7 | 6 | 11 | 24 | |
| 12 | 6 | 7 | 2 | 15 | |
| 13 | 5 | 5 | 5 | 15 | |
| 14 | 5 | – | 3 | 8 | |
| 15 | 4 | 3 | 8 | 15 | |
| 16 | 4 | – | 3 | 7 | |
| 17 | 3 | 6 | 9 | 18 | |
| 18 | 3 | 4 | 4 | 11 | |
| 19 | 3 | 4 | 3 | 10 | |
| 20 | 3 | 4 | 1 | 8 | |
| 21 | 3 | 1 | 6 | 10 | |
| 22 | 3 | 1 | 3 | 7 | |
| 23 | 2 | 4 | 2 | 8 | |
| 24 | 2 | 2 | 1 | 5 | |
| 25 | 2 | 1 | 4 | 7 | |
| 26 | 2 | 1 | 3 | 6 | |
| 26 | 2 | 1 | 3 | 6 | |
| 28 | 2 | 1 | – | 3 | |
| 29 | 2 | – | 2 | 4 | |
| 29 | 2 | – | 2 | 4 | |
| 29 | 2 | – | 2 | 4 | |
| 32 | 2 | – | 1 | 3 | |
| 32 | 2 | – | 1 | 3 | |
| 34 | 2 | – | – | 2 | |
| 35 | 1 | 4 | 1 | 6 | |
| 36 | 1 | 3 | 3 | 7 | |
| 37 | 1 | 3 | 2 | 6 | |
| 37 | 1 | 3 | 2 | 6 | |
| 39 | 1 | 2 | 5 | 8 | |
| 40 | 1 | 2 | 2 | 5 | |
| 40 | 1 | 2 | 2 | 5 | |
| 42 | 1 | 2 | 1 | 4 | |
| 42 | 1 | 2 | 1 | 4 | |
| 44 | 1 | 2 | – | 3 | |
| 45 | 1 | 1 | 6 | 8 | |
| 46 | 1 | 1 | 5 | 7 | |
| 47 | 1 | 1 | 1 | 3 | |
| 47 | 1 | 1 | 1 | 3 | |
| 47 | 1 | 1 | 1 | 3 | |
| 50 | 1 | 1 | – | 2 | |
| 50 | 1 | 1 | – | 2 | |
| 50 | 1 | 1 | – | 2 | |
| 50 | 1 | 1 | – | 2 | |
| 50 | 1 | 1 | – | 2 | |
| 55 | 1 | – | 5 | 6 | |
| 56 | 1 | – | 2 | 3 | |
| 57 | 1 | – | 1 | 2 | |
| 57 | 1 | – | 1 | 2 | |
| 59 | 1 | – | – | 1 | |
| 59 | 1 | – | – | 1 | |
| 59 | 1 | – | – | 1 | |
| 62 | – | 3 | 3 | 6 | |
| 63 | – | 3 | 2 | 5 | |
| 64 | – | 3 | – | 3 | |
| 65 | – | 2 | 4 | 6 | |
| 66 | – | 2 | 2 | 4 | |
| 67 | – | 2 | 1 | 3 | |
| 67 | – | 2 | 1 | 3 | |
| 69 | – | 1 | 5 | 6 | |
| 70 | – | 1 | 3 | 4 | |
| 70 | – | 1 | 3 | 4 | |
| 72 | – | 1 | 1 | 2 | |
| 73 | – | 1 | – | 1 | |
| 73 | – | 1 | – | 1 | |
| 73 | – | 1 | – | 1 | |
| 73 | – | 1 | – | 1 | |
| 77 | – | – | 3 | 3 | |
| 78 | – | – | 2 | 2 | |
| 78 | – | – | 2 | 2 | |
| 80 | – | – | 1 | 1 | |
| 80 | – | – | 1 | 1 | |
| 80 | – | – | 1 | 1 | |
| 80 | – | – | 1 | 1 | |
| 80 | – | – | 1 | 1 | |
| 80 | – | – | 1 | 1 |
Rudi juu
Kumbuka: Medali wanazoshinda Wanariadha Wasioegemea upande wowote hazijajumuishwa kwenye jedwali hili.
Mada zinazohusiana
Muhtasari
- Ukraine yaendelea na mashambulizi yake dhidi ya Urusi
- Olimpiki 2024: Tola wa Ethiopia ashinda mbio za marathon kwa wanaume
- Makumi ya watu waripotiwa kuuawa katika shambulizi la Israel mjini Gaza
- Zimbabwe: Watu 160 wamekamatwa tangu katikati ya Juni
- Khelif ajishindia medali ya dhahabu licha ya mzozo wa ustahiki wa jinsia
- Brazil: 61 wafariki katika ajali ya ndege São Paulo
Moja kwa moja
- Dakika 27 zilizopita Ukraine yaendelea na mashambulizi yake dhidi ya Urusi
Chanzo cha picha,IZ.RU/ReutersWanajeshi wa Ukraine wanaendelea na mashambulizi yao katika eneo la Kursk magharibi mwa Urusi, huku mashambulizi yao ya kushtukiza ya kuvuka mpaka yakiingia siku ya tano.Urusi imetangaza operesheni ya “kukabiliana na ugaidi” katika maeneo matatu, huku ikijitahidi kukabiliana na uvamizi huo.Siku ya Ijumaa Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema kuwa “inaendelea kuwakabili” wanajeshi wa Ukraine, ambao ilidai kuwa wamepoteza zaidi ya wanajeshi 280 katika muda wa saa 24 zilizopita – idadi ambayo haijathibitishwa kikamilifu.Ripoti zinaonyesha kuwa wanajeshi wa Ukraine wanafanya kazi zaidi ya kilomita 10 ndani ya Urusi – hatua kubwa zaidi ya Kyiv tangu Moscow ilipoanzisha uvamizi wake kamili wa Ukraine mnamo Februari 2022.Ukraine haijakiri hadharani uvamizi huo, lakini Rais Volodymyr Zelensky alisema wiki hii kwamba Moscow lazima “ihisi” matokeo ya uvamizi wake.Soma pia:Kwa nini Ukraine imeanzisha mashambulizi ya mpakani dhidi ya Urusi?Je vita vya Urusi nchini Ukraine vinakwenda kama Urusi inavyotaka?Vita vya Ukraine: Droni zafungua aina mpya ya vita vya baadaye - Dakika 38 zilizopita. Olimpiki 2024: Tola wa Ethiopia ashinda mbio za marathon kwa wanaume
Chanzo cha picha,GettMwanaridha wa Ethiopia Tamirat Tola, ameshinda mbio za marathon za Olimpiki katika muda wa saa 2:06.26 na kupatia nchi yake medali ya kwanza ya dhahabu katika Michezo hii. - Saa 3 zilizopitaMakumi ya watu waripotiwa kuuawa katika shambulizi la Israel mjini Gaza
Chanzo cha picha,ReutersMaelezo ya picha,Ukanda wa Gaza unavyoonekana kwa mbali kutoka Israel Jumamosi asubuhiShirika la ulinzi wa raia linalodhibitiwa na Hamas katika ukanda wa Gaza linasema makumi ya watu wameuawa katika shambulio la anga la Israel dhidi ya makazi katika shule moja mjini Gaza.Jeshi la Israel lilimethibitisha kushambulia eneo hilo siku ya Jumamosi, na kuelezea lengo la shambulio hilo lilikuwa ni kuharibu kituo mawasiliano cha Hamas kilichowekwa katika shule hiyo.Kulingana na ajenti wa ulinzi wa raia wa Gaza, shambulio katika wilaya ya Daraj lilisababisha vifo vya takriban watu 90 na kuwajeruhi makumi ya wengine. BBC haijafanikiwa kuthibitisha takwimu hizo.”Idadi ya waliofariki sasa ni kati ya 90 hadi 100 na kuna makumi ya wengine waliojeruhiwa,” msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal aliliambia shirika la habari la AFP.”Roketi tatu za Israel zilipiga shule iliyokuwa inawahifadhi Wapalestina waliokimbia makazi yao.”Hapo awali katika chapisho la Telegram alielezea tukio hilo kama “mauaji ya kutisha” akisema wafanyakazi walikuwa wakijaribu kudhibiti moto ili kuwaokoa waliojeruhiwa.Wanajeshi wa Israel walisema “wamewashambulia magaidi wa Hamas wanaoendesha shughuli zao ndani ya kituo cha udhibiti wa Hamas kilichowekwa katika shule ya Al-Taba’een”.Unaweza pia kusoma:Israeli inasubiri na kujiandaa kujibu: Kwa nini Nasrallah alitishia mji wa Haifa?Nini kimewapata viongozi mashuhuri wa Hamas?Mauaji ya Haniyeh ni kikwazo kwa usitishaji mapigano - Saa 3 zilizopitaZimbabwe: Watu 160 wamekamatwa tangu katikati ya JuniMamlaka nchini Zimbabwe imewakamata zaidi ya watu 160 tangu katikati ya Juni kabla ya mkutano wa kilele wa kanda ya kusini mwa Afrika mjini Harare mwezi huu, mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema.Mashirika ya Human Rights Watch na Amnesty International yalipata ushahidi wa watu kuteswa na wanahofia kamata kamata hiyo huenda ikafanya hali kuwa tete.Mashirika hayo pia yanahoji kujitolea kwa jumuiya ya kikanda ya SADC kaimarisha haki za binadamu chini ya uenyekiti ujao wa Rais Mnangagwa wa Zimbabwe.Viongozi waliochaguliwa, wanachama wa upinzani, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wanafunzi ni miongoni mwa waliokamatwa.Katika taarifa ya pamoja mashirika hayo mawili ya kutetea haki za binadamu yaliwataka viongozi wa SADC kulaani ukiukaji wa haki za binadamu wa Zimbabwe na Vyombo vya habari kuachiliwa kwa wale waliokamatwa.Yanasema mwezi Juni Rais Mnangagwa alionya dhidi ya “vyama vya upinzani vinavyolenga kuchochea vurugu za kiraia, hasa kabla, wakati na baada ya mikutano ya kikanda na ya kimataifa.”Saa chache baadaye, polisi kjini Harare waliwapiga na kuwakamata waandamanaji waliokuwa wakifanya maandamano ya amani, kushinikiza kuachiwa kwa watu waliokamatwa.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.