Bao La Asubui- Agosti 6,2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Huhitaji Kubwa Tajiri Ili Ustaafu Ukiwa Na Kipato Cha Uhakika.

____Zaidi ya asilimia 70 ya watu wanapata STRESS kuhusu PESA – Hii ni kwa mujibu wa CNBC, Your Financial Confidence Survey.

Moja kati jambo kubwa linalokwamisha wengi kutimiza malengo yao ya kifedha ni KUKOSA BAJETI ILIYOANDIKWA NA KUITEKELEZA.

50/30/20 Ndio Njia Rahisi Zaidi Ya Kupanga Bajeti Yako Ili Utimize Malengo Yako Ya Kifedha Kwa Kasi.

Njia hii ilianzishwa na Seneta mmoja wa Marekani, jina lake anaitwa Elizabeth Warren.

Elizabeth alisema kwamba unapopanga Bajeti yako igawe katika Makundi 3 Makubwa.

1. Kundi La Kwanza Ni 50%

Kundi hili ni la kuweka kwenye Needs.

NEEDS ni mahitaji yako ya muhimu, ambayo HUWEZI kuishi bila hayo.

Mfano: Chakula, Mavazi na Makazi (Au Kodi ya nyumba) iwapo unaishi gulio, Bima Ya Afya n.k

“Ni muhimu kuhakikisa matumizi yako muhimu hayazidi 50% ya kipato chako”.

Yakizidi, ki bajeti tunasema wewe umeanza kwenda kwenye HATARI KUBWA.

2. Kundi La Pili Ni 30%

Kwenye kundi hii tunapeleka kwenye kitu kinachoitwa WANTS.

Wants ni mambo unayoyahitaji, ila SIYO YA LAZIMA sana.

Yani unaweza ukaishi BILA mambo hayo kuwepo kwenye maisha yako.

Mfano: Kila mwezi lazima ukaangalie Movie, Au lazima utoke Outing kula n.k

Hivi ni vitu ambavyo unaweza ukavifanya, ila SIO vya lazima.

Ukitaka kujua tofauti ya NEEDS Na WANTS jiulize hili swali…

“Je Naweza Kuishi Bila Kukifanya Hichi Kitu?”

Ukiona unaweza kuishi bila kukifanya Tafsiri yake hiyo ni WANT.

Maana yake unaweza kulisubirisha jambo hilo.

Ila kama huwezi kuishi bila kukifanya tafsiri yake inakuwa hiyo ni NEEDS.

3. Kundi La Tatu Ni 20%

Hapa kwenye kundi hili unafanya Saving unaweka Akiba, Uwekezaji wako au Unalipa madeni kwenye hii asilimia 20%.

Trick part ya hii budget iko hapa.

Ukiweza kupunguza 15% ya WANTS zako ina maana ile 15% ya Wants ukiipeleka kwenye Kundi la Tatu….

…na kuliongeza kutoka 20% mpaka kufika 35% kwenye saving, uwekezaji au kulipa madeni…

…ina maana utakuwa unaeleka kwenye Uhuru Wako Wa Kifedha kwa kasi sanaaa.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment