- Mashindano ya soka ya Olimpiki: Morocco na Misri zatinga nusu fainali
Chanzo cha picha,ReutersMaelezo ya picha,Achraf Hakimi (kushoto) na Ibrahim Adel (kulia) wote walifunga bao wakati Morocco na Misri zikitinga nusu fainali ya Olimpiki ya Paris 2024.Afrika itakuwa walau na medali moja katika mashindano ya soka ya Olimpiki ya wanaume baada ya Misri na Morocco zote kutinga nne bora.Morocco ilianza na mafanikio maradufu kwa ushindi murua wa 4-0 dhidi ya Marekani kwenye uwanja wa Parc des Princes mjini Paris.Mkwaju wa penalti kipindi cha kwanza wa Soufiane Rahimi – bao lake la tano kwenye michuano hiyo – uliipa Atlas Lions fursa ya kuongoza hadi wakati wa mapumziko.Lakini katika kipindi cha pili ambacho kilionekana kuwa na bahati ya mtende kwao, Ilias Akhomach, nahodha Achraf Hakimi na penalti nyingine iliyofungwa na Mehdi Maouhoub ilimalizia mambo kwa mtindo wa kipekee.Katika marudio ya mechi ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la Qatar 2022, Morocco sasa itamenyana na Uhispania mjini Marseille Jumatatu (16:00 GMT) kuwania nafasi ya kutinga fainali.Baada ya mechi hiyo, Hakimi alisifu uungwaji mkono mkubwa wa Morocco ambao umeisaidia timu hiyo nchini Ufaransa.”Mashabiki wamekuwa wakitufuatilia katika mashindano yote,” alisema mlinzi huyo ambaye anachezea soka uwanja wa Parc des Princes klabu la Paris St Germain.”Natumai wanaweza kutufuata hadi fainali. Tunataka kuwafanya wawe na fahari.”Pia unaweza kusoma:Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 03.08Makubaliano ya kukiri mashtaka ya watuhumiwa wa shambulio la 9/11 yabatilishwa
Chanzo cha picha,Getty ImagesWaziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin amebatilisha makubaliano ya kukiri mashtaka nje ya mahakama yaliyofikiwa na maofisa wa wizara hiyo pamoja na watuhumiwa wa shambulio la kigaidi la Septemba 11, 2001.Kupitia taarifa aliyoitoa jana Ijumaa, Bw Austin amesema pia kuwa ametengua mamlaka ya ofisa anayesimamia mahakama za kijeshi ambaye alisaini makubaliano hayo siku ya Jumatano.Makubaliano hayo, ambayo yanaripotiwa kuwa yalikuwa yanawakinga watuhumiwa hao na adhabu ya kifo, yalipingwa vikali na baadhi ya familia za waathirika wa shambulio hilo.Taarifa ya Waziri huyo imewataja washtakiwa watano ambao wote wanashikiliwa kwenye jela ya kijeshi ya Guantanamo, ikiwemo anayetuhumiwa kusuka mpango wa mashambulizi, Khalid Sheikh Mohammed. Makubaliano yenyewe yalihusisha watuhumiwa watatu tu.“Nimeamua kwamba, kwa kuzingatia uzito wa kuingia kwenye makubaliano ya nje ya mahakama na washtakiwa…Wajibu wa kufanya jambo hilo inabidi uwe wangu kama mtu mwenye mamlaka ya juu (katika wizara ya ulinzi),” Bw Lloyd alimuandikia Brigedia Jenerali Susan Escallier, ambaye ni kiongozi wa kamisheni inayosimamia mahakama za kijeshi huko Guantanamo.”Hivyo basi, natengua mamalaka yako. Na kuanzia sasa, kama sehemu ya kutekeleza mamlaka niliyonayo, ninafuta makubaliano yote matatu ya nje ya mahakama.”Ikulu ya White House ilijitenga na kuhusika kwa namna yeyote katika kufikiwa kwa makubaliano hayo siku ya Jumatano.Watuhumiwa hao watano waliotajwa kwenye taarifa ya Bw Austin ni: Khalid Sheikh Mohammed, Walid Muhammad Salih Mubarak bin Attash, Mustafa Ahmed Adam al-Hawsawi; na wawili ambao hawakutajwa kwenye makubaliano ya Jumatano ni: Ramzi bin al-Shibh na Ali Abdul Aziz Ali.Wanaume hao wamekuwa kizuizini bila kufunguliwa mashtaka kwa zaidi ya miongo miwili sasa. Moja ya sababu zinazotia ugumu wa kufunguliwa mashtaka rasmi ni tuhuma za matumizi ya mateso makali katika kuwahoji na kusaka ushahidi.Kwa pamoja wanatuhumiwa kukeleza msururu wa makosa ya jinai, ikiwemo kushambulia raia, mauji ya kinyume cha sheria za vita, utekaji nyara na ugaidi.Wanasiasa kadhaa kutoka chama cha Republican ambao walipinga makubaliano ya Jumatano wamempongeza Waziri Austin kwa kuyabatilisha.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.