Radio Fortune Africa
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuuawa kwa kiongozi mkuu na wa kisiasa wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh aliyeshambuliwa na ndege isiyokuwa na rubani, akiwa katika makaazi yake jijini Tehran nchini Iran, kumelaumiwa kutekelezwa na Israeli na kuzua wasiwasi wa kusambaa kwa mzozo kati ya Israeli na Hamas.

Israel haijasema chochote kuhusu kuuawa kwa Haniyeh, huku wasiwasi ukizuka kuwa tukio hilo litageuza vita vya Israel na Gaza kuwa vya kikanda.
Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian, ambaye kiongozi huyo wa Hamas alikuwa amekuja kuhudhuria kuapishwa kwake, amesema Israel itaadhibiwa vikali, kauli ambayo imeungwa mkono na kiongozi wa kiroho Ayatollah Ali Khamenei.

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestine rais Mahmud Abbas ambaye ni mpinzani wake wa kisiasa, ameelezea kitendo cha kuuawa kwa kiongozi huyo wa Hamas kama kilichotekelewa na watu na kuwataka Wapalestina kuendelea kusimama pamoja dhidi ya uvamizi wa Israeli.
Nchi za Urusi na China, zimelaaniwa kuuawa kwa Haniyeh huku nchi za Qatar na Uturuki, zikisema kitendo cha kumuua kiongozi huyo ni cha aibu na uhalifu mkubwa.
Haniyeh mwenye umri wa miaka 62, amekuwa kwenye kundi la Hamas tangu miaka ya 80 na aliwahi kufungwa jela la Israeli miaka mitatu mwaka 1989 na baadaye kuwa huru baada ya mpango wa kubadiliana wafungwa na Hamas.
Amekuwa akishikilia wadhifa wa uongozi wa kisiasa wa kundi la Hamas tangu mwaka 2017.
Kusambaza :
Soma zaidi mada inayofanana kwingineko:
Kuhusu mada hiyohiyo
Jeshi la #Israel limedai kumuua mkuu wa kijeshi wa wapiganaji wa #Hamas Mohammed Deif katika shambulio lake la mwezi uliopita katika mji wa Khan Yunis kusini mwa #Gaza.
Madai ya #israeli kumuua Deif yamekuja ikiwa imepita siku moja baada ya kuuawa kwa mkuu wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh mjini #Tehran , maujai ambayo yalithibitishwa na Iran na Hamas.
📷Maktaba


Israeli imedai kumuua mkuu wa kijeshi wa Hamas Mohammed Deif katika shambulio

Kiongozi wa Hamas Ismaïl Haniyeh, aliyeuawa katika shambulio linalohusishwa Israel kuzikwa

Viongozi mbalimbali wamezungumzia vipi mauaji ya Ismail Haniyeh wa Hamas ?
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lajadili Mashariki ya Kati
Kifo cha kiongozi wa Hamas: Kiongozi mkuu wa Iran aahidi ‘adhabu kali’ kwa Israeli

Umoja wa Mataifa: Wafungwa wa Kipalestina nchini Israel waliteswa

Hofu yatanda Israel baada ya kifo cha kiongozi wa Hamas mjini Tehran

Mfahamu Ismaïl Haniyeh, kiongozi wa kihistoria wa Hamas aliyeuawa katika shambulio Tehran

Ismail Haniya kiongozi wa Hamas ameuuawa katika shambulio nchini Iran

Rais wa Iran kuapishwa: Baada ya miezi miwili madarakani, Massoud Pezeshkian ashindwa kujizatiti

Lufthansa na Air France zasitisha safari zao katika mji wa Beirut

Benjamin Netanyahu azuru eneo la Golan lililoshambuliwa shambulio kwa roketi na kuua watu 12
Israel: Watu 11 waangamia baada ya roketi kupiga kwenye uwanja wa mpira Galan
INATOKEA SASA HIVI
- DRC
- Uganda
- EAC
- Israeli
- Kenya
- WASILIANA NASI
- Facebook Page Radio Fortune Africa
- X @cantonadigital
- X @CANTONAJOSEPH
- @RadioFortuneAfrica
- YouTube
- Tune
MAKALA MAALUM
UCHUMI NA BIASHARA
Umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na uma
WIMBI LA SIASA
Makala haya yanatupia jicho uchaguzi wa urais nchini America, nini maana ya ushindi wa makamu Rais Kamala Harris shidi Rais wa zamani Donald Trump
AFRIKA YA MASHARIKI
Nishati inachangia asilimia kubwa kwa ukuaji wa Uchumi wa mataifa
CHANGU CHAKO, CHAKO CHANGU
Historia ya kabila la Wadigo wa Kenya na Tanzania katika Makala Changu Chako.
UCHUMI NA BIASHARA
Kuberoshwa kwa huduma ya intaneti Kenya na ilivyochochea ubunifu
SANAA YA AFRIKA
Ambwene Mwasongwe Muimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Tanza
AFYA NA JAMII
Mpango wa afya kwa wote barani Afrika
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.