Afrika Leo Asubui-Agosti 2,2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Muhtasari

  • Wamarekani walioachiliwa huru Urusi kwa mabadilishano ya wafungwa waungana na familia
  • Mashindano ya Olimpiki: Biles ashinda taji lingine na kufikisha jumla ya medali sita za dhahabu
  • Nigeria: Watu kadhaa wauawa kwa kupigwa risasi katika maandamano ya gharama ya maisha
  • Ushahidi mkubwa waonyesha upinzani ulishinda uchaguzi Venezuela – Blinken
  • Kiongozi wa Hezbollah asema mzozo na Israel upo katika ‘awamu mpya’ baada ya mauaji
  • Wafungwa 24 waachiliwa katika mabadilishano makubwa kati ya Urusi na nchi za Magharibi tangu VWamarekani walioachiliwa huru Urusi kwa mabadilishano ya wafungwa waungana na familia.CHANZO CHA PICHA,EPA
  • Wamarekani watatu akiwemo mwandishi wa jarida la Wall Street Journal Evan Gershkovich, ambao waliachiliwa katika makubaliano ya kubadilishana wafungwa na Urusi, wamewasili nchini Marekani.Bw Gershkovich, 32, alikuwa mmoja wa wafungwa 16 waliobadilishwa na wafungwa wanane wa Urusi katika kile kinachoelezwa kuwa mabadilishano makubwa zaidi tangu kumalizika kwa Vita Baridi kati ya Urusi na nchi za Magharibi.Mabadilishano hayo katika uwanja wa ndege nchini Uturuki pia yalijumuisha kuachiliwa kwa mwanajeshi wa zamani wa Marekani Paul Whelan, na mwandishi wa habari wa Urusi na Marekani Alsu Kurmasheva.Baada ya kuwasili kwa ndege iliyokuwa imewabeba katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Joint Base Andrews, Maryland, Bw Gershkovich, Bi Kurmasheva na Bw Whelan walitoka na kushangiliwa na waliokuwepo.Soma zaidi:
  • Wafungwa 24 waachiliwa katika mabadilishano makubwa kati ya Urusi na nchi za MagharibaridiPaul Whelan: Askari wa zamani wa Marekani anadai ametumiwa katika kesi ya ujasusi ya UrusiKwa nini Putin anamtaka ‘muuaji wa baiskeli’ anayehusishwa na FSB kurejeshwa Urusi?Mmarekani anayeshikiliwa Urusi anahisi nchi yake ‘i Wapenzi wa paka Kenya wana wasiwasi kuhusu Wapenzi wa paka katika mji mkuu wa Kenya ,Nairobi wamekuwa na wasiwasi juu ya tishio la kile kinachochukuliwa kuwa “kodi ya paka” – na mazungumzo yoyote ya ushuru katika taifa hilo la Afrika Mashariki yanaibua hofu.Pendekezo hilo linakuja kupitia Kaunti ya Jiji la Nairobi ambayo inataka paka wote wasajiliwe na wamiliki wao – jambo ambalo wengine wanalalamika kuwa ni ‘janga’Itawahitaji wamiliki wa paka jijini Nairobi kuchukua leseni ya kila mwaka – inayogharimu shilingi 200 za Kenya ($1.50; £1.20) pamoja na uthibitisho kwamba mnyama huyo amepata chanjo ya kichaa cha mbwa.Kulingana na Mswada wa Udhibiti wa Wanyama na Ustawi wa jiji hilo, watalazimika kuhakikisha wanyama wao kipenzi “hawapigi mayowe au kulia kwa njia ambayo inavuruga amani” ya wakaazi.Pia watahitajika kuwafungia paka wao ‘walio kwenye joto la kutaka kujamiiana’Sheria inayopendekezwa inalenga kuboresha ustawi wa paka, lakini baadhi ya wakazi wa jiji hilo wenye mashaka wanahitaji kushawishiwa.Hivi majuzi Wakenya walilazimisha serikali kuondoa mswada wa fedha wa uliopendekeza msururu wa ushuru wenye utata- na mpango huu wa kaunti ya Nairobi unaonekana na baadhi ya watu kama sehemu ya hamu ya serikali kujiongeza mapato zaidi.”Kwanza ushuru kwa bidhaa za vitambaa va hedhi , sasa mnatoza ushuru kwa wamiliki wa paka. Muacheni paka wangu!”Khadija M Farah alisema kwenye X, akirejelaa muswada wa fedha ulioangushwa sasa.Baadhi ya Wakenya pia wanaibua maswali kuhusu jinsi inavyoweza kutekelezeka, ikizingatiwa idadi kubwa ya paka waliopotea au wa mwituni.

    Nigeria: Maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama ya maisha yamefanyika

    Nchini Nigeria, polisi wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji waliojitokeza nchi nzima kuan

    Maandamano yameshuhudiwa kwenye jiji kuu Abuja,jiji la piki kwa ukubwa la Kano, mji mkuu wa kibiashara Lagos na miji mingine ambapo mamia ya waandamanaji wengi vijana waliotikia wito wa kuandamana wakiwa na ujumbe wa kumaliza uongozi mbaya nchini Nigeria.

    Maandamano yameshuhudiwa kwenye jiji kuu Abuja, jiji la pili kwa ukubwa la Kano, mji mkuu wa kibiashara Lagos na miji mingine ambapo mamia ya waandamanaji wengi vijana waliitikia wito wa kuandamana wakiwa na ujumbe wa kumaliza uongozi mbaya nchini Nigeria.

    Kuelekea maandamano haya yaliyohamasishwa na yale yaliyotokea nchini Kenya, vijana wamekuwa wakijipanga kupitia mitandao ya kijamii kujitokeza na kuandamana dhidi ya serikali ya rais Bola Tinubu kuanzia Agosti tarehe 1 hadi tarehe 10.

    Vijana hao wamehamisha maandamano hayo kupitia kwenye mitandao ya kijamii sawa na yale yaliofanyika nchini Kenya.

    Jijini Abuja, maafisa wa usalama walifunga barabara kuu za kwenda kwenye bustani ya kihistoria ya Eagle Square na kuwalazimu waandamanaji kujikusanya kwneye uwanja wa taifa wa Michezo.

    Maandamano haya yameanza wakati wananchi wa kawaida nchini Nigeria, wakilalamikia kupanda kwa gharama ya maisha, baada ya kuongezeka kwa bei ya mafuta, uongozi mbaya na utovu wa usalama hasa maeneo ya Kaskazini.

    Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji jijini Lagos.
    Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji jijini Lagos. REUTERS – Marvellous Durowaiye

    Licha ya wito wa rais Tinubu, kuwataka waandamanaji kumpa muda wa kutekeleza ahadi zake, waandamanaji wanasema wataendelea na shinikizo hadi pale serikali itakaposikia kilio chao.

    Takriban waandamanaji watatu wameuawa katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria, shirika la habari la Reuters ana mashuhuda wamesema, wakati waandamanaji walipoandamana katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wakipina kupanda kwa gharama za maisha na masuala ya utawala.

    Msemaji wa polisi wa jimbo la Kaduma Mansur Hassan emesema, polisi warusha mabomu ya kutoa machozi na siyo risasi. Polisi pia waliutawanya umati wa waandamanaji kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi katika mji mkuu wa Abuja, kulingana na akaunti za shuhuda

    Yakiwa wamehamasishwa na maandamano ya Kenya mwezi June ambayo yalisababisha serikali nchini humo kuondoa baadhi ya ongezeko la kodi zilizokuwa zimepangwa,.

    Wanigeria wamekuwa wakihamasisha mitandaoni kutaka kurudishwa kwa ruzuku ya mafuta ya petroli na umeme, elimu ya bure kwa shule za msingi na sekondari na kuchuliwa hatua kupambana na ukosefu wa usalama na matakwa mengine.

    VIJANA wa  kizazi cha Gen Z nchini Nigeria wameanza rasmi maandamano yao ya siku 10 ya kupinga serikali ya Rais Bola Tinubu na kupanda kwa gharama maisha.

    Maelfu ya vijana hao, jana Agosti 1, 2024,  walijitokeza katika majimbo na miji mingi nchini humo kuandamana kupinga utawala mbaya wa Rais Tinubu.

    Vijana hao sasa wanaonekana kufuata nyayo za wenzao kutoka Kenya, Uganda na Bangladesh.

    Vijana hao walikaidi agizo la Rais Tinubu la kuwataka wasitishe maandamano hayo huku akiwasihi wampe muda wa kufanya mageuzi katika serikali yake.

    Baadhi ya maafisa wakuu katika serikali ya Tinubu walitaja maandamano hayo kuwa hayafai na kudai kuwa yamechochewa kisiasa.

    Waandalizi wa maandamano hayo wanatoa wito kwa serikali itatue suala la ongezeko la bei ya mafuta, kurejeshwa kwa ushuru wa bei nafuu wa umeme, na kupunguzwa kwa ushuru wa uagizaji wa bidhaa miongoni mwa matakwa mengine.

    Vikundi hivyo pia vinataka kubatilishwa kwa sheria ya kupandisha karo za elimu ya juu.

    Pia wanadai uwazi na uwajibikaji katika utawala wa rais wao, ikiwa ni pamoja na kupunguzwa kwa mishahara na marupurupu ya maafisa wa umma na kutengwa kwa hazina ya dharura ili kuwasaidia wafanyabishara ndogo ndogo.

    “Tunaandamana kwa sababu tuna njaa,” mwanaharakati wa Nigeria Banwo Olagokun aliliambia shirika moja la habari.

    Yeye ni sehemu ya Vuguvugu la Take It Back, mojawapo ya makundi ambayo yameitisha maandamano hayo ya siku 10.

    “Tunaandamana kwa sababu bei za bidhaa zinaendelea kupanda jambo ambalo linatufanya tushindwe kujikimu kimaisha, Hatuwezi kununua vifaa kama vile chakula, maji, nguo na matibabu,” Bw Olagokun, aliongeza.

    Nigeria inakabiliwa na suala la kupanda kwa gharama ya maisha.

    Mfumuko wa bei wa kila mwaka ni asilimia 34.19, ambayo ni juu zaidi katika karibu miongo mitatu.

    Bei za vyakula zimepanda kwa kasi zaidi – kwa mfano, bei ya viazi vikuu Lagos ni karibu mara nne zaidi ya bei ya bidhaa hiyo mwaka jana.

    WAZIRI Mteule katika Wizara ya Ulinzi Roselinda Soipan Tuya ameambia kikao cha Bunge kwamba anafahamu hana ujuzi mkubwa katika idara ya ulinzi, lakini yupo radhi kujifunza na kutekeleza wajibu wake iwapo ataidhinishwa.

    Akijibu maswali katika kikao cha kupigwa msasa kubaini ufaafu wake katika wadhifa huo kilichoongozwa na Spika Moses Wetang’ula, Bi Tuya alisema yeye ni mtu anayejifunza mambo upesi na kwamba ana uwezo mkubwa wa kushirikiana na wengine ili kufanikisha majukumu.

    “Mimi hushika mambo upesi na hushirikiana sana kwa karibu na wenzangu. Kuna mengi ambayo nitahitaji kujifunza kuhusu masuala ya ulinzi…nitafahamu vizuri hali ya mambo bila kuingilia majukumu ya wanajeshi. Hilo nawahakikishia,” akajibu.

    Bi Tuya, kama wenzake waliotangulia kupigwa msasa Alhamisi, alisema utajiri wake umeongezeka kutoka Sh156 milioni alizofichua alipopigwa msasa 2022, hadi Sh243 milioni kwa sasa akisema nyongeza hiyo imetokana na faida kutoka kwa mali kama vile nyumba na biashara zingine za kibinafsi.

    Wengine waliopigwa msasa Alhamisi ni Kithure Kindiki (Wizara ya Usalama wa Ndani), Deborah Barasa (Afya) Alice Wahome (Ardhi) na Julius Ogamba (Elimu).

    INATOKEA SASA HIVI

    SIKILIZA RADIO FORTUNE AFRICA

    HABARI ZINAZOTOKEA

    Rais wa Angola amezungumza na wenzake kutoka DR Congo na Rwanda

    Rais wa Angola, Joao Lourenco, wiki hii amekuwa na majadiliano kwa njia ya simu na rais wa Rwanda, Paul Kagame na mwenzake wa DRC, Felix Tshisekedi, mazungumzo yaliyojikita katika makubaliano ya hivi karibuni ya usitishaji mapigano baina ya pande hizo mbili mjini Luanda.

    Rais wa Angola Joao Lourenco na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi wamezungumzia suala la usalama wa mashariki ya DRC.
    Rais wa Angola Joao Lourenco na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi wamezungumzia suala la usalama wa masharik

    Siku moja kabla ya kikao cha juma hili, rais wa Angola alikutana na mwenzake wa DRC kuzungumzia suala hili hili la usitishaji mapigano.

    Aidha makubaliano haya yamepokelewa vizuri na viongozi wengine wa nchi za ukanda, ambao wanaamini kuwa ikiwa yatatekelezwa kikamilifu kuanzia Agosti 04, yatamaliza rasmi kile kilichokuwa kinasemwa kuhusu vita kati ya DRC na Rwanda.

    Paul Kagame wa Rwanda , João Lourenço wa Angola na Felix Thisekedi wa DRC katika mkutano wa awali
    Paul Kagame wa Rwanda , João Lourenço wa Angola na Felix Thisekedi wa DRC katika mkutano wa awali AFP – JORGE NSIMBA

    Wakati huu ambapo mchakato wa mazungumzo ya Nairobi, ukionekana kukwama, uamuzi wa viongozi hawa kuridhia kusitisha mapugano kunatoa nafasi ya mazungumzo zaidi kuelekea suluhu ya kudumu.

    Haya yanajiri wakati huu wataalamu wa masuala ya usalama kutoka AngolaRwanda na DRC wanatarajiwa kukutana Agosti 7, kutathmini utekelezwaji wa makubaliano

    Soma zaidi mada inayofanana:

    Kuhusu mada hiyohiyo

    Mawaziri wateule wanapigwa msasa na bunge kabla ya kuidhinishwa katika wadhifa huo.

    MAWAZIRI watatu wateule wamefichua jinsi thamani ya utajiri wao ilivyoongezeka kwa mamilioni katika kipindi cha miaka miwili walipokuwa wakihudumu kabla ya Rais William Ruto kuwapiga kalamu.

    Profesa Kithure Kindiki na Bi Alice Wahome waliobahatika kupatiwa fursa ya pili kuhudumu tena kama mawaziri wa usalama wa ndani na ardhi, mtawalia, katika baraza jipya, wamekiri kuwa utajiri wao uliongezeka kwa zaidi ya Sh100 milioni.

    Kamati Maalum ya Bunge la Kitaifa ilisikia Alhamisi kuwa utajiri wa Profesa Kindiki uliongezeka kwa Sh150 milioni hadi kufikia Sh695 tangu alipochukua usukani kama waziri wa usalama wa ndani.

    Hata hivyo, Profesa Kindiki, akipigwa msasa na kamati hiyo inayoongozwa na Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula, alikanusha kuwa utajiri wake umeongezeka kutokana na shughuli haramu.

    “Jinsi nilivyosema nilipohojiwa mara ya kwanza, utajiri wangu ulikuwa Sh544 milioni kabla ya uteuzi wangu. Sasa umeongezeka hadi Sh694 milioni,” alisema Profesa Kindiki.

    “Sijanufaika kutokana na biashara yoyote haramu na sijawahi kufanya biashara yoyote na serikali.”

    Aidha, Profesa Kindiki anayemiliki shirika la mawakili alikana kwamba utajiri wake umeongezeka kutokana na mshahara au malimbikizi aliyokuwa akipata kama waziri.

    “Ingawa kwa sasa sihudumu kama wakili, shirika langu la sheria lingali hai na linafanya kazi,” alisema.

    “Mshahara wangu wote unatumika kulipa bili.”

    Bw Kindiki vilevile alifichua kuwa deni alilolipwa miezi miwili tu baada ya kuteuliwa kama waziri kwa mara ya kwanza, lilichangia kuongeza mali yake.

    Kando na Shirika lake la mawakili, Bw Kindiki alisema kuwa anamiliki biashara ndogondogo akisisitiza kuwa, “hakuna utajiri wangu umetokana na mshahara au malimbikizi.”

    Alisema jumla mali anayomiliki inajumuisha majumba mawili yenye thamani ya Sh235 yaliyopo jijini Nairobi na Tharaka Nithi, magari yenye thamani ya Sh17 milioni, akiba katika mashirika ya Sacco na mapato kutokana na shirika lake la mawakili.

    Kwa upande wake Bi Wahome, alisema thamani ya utajiri wake, unaojumuisha mali yake pamoja na mume wake, iliongezeka kwa Sh103 milioni hadi kufikia Sh327 milioni kutoka Sh224 milioni katika muda wa miaka miwili alipoongoza Wizara ya Ardhi.

    “Utajiri wangu umeongezeka kutokana na kuimarika kwa sekta ya ustawishaji na malipo ya malimbikizi ya kodi,” alifafanua Bi Wahome.

    Waziri mteule kwa wizara ya ulinzi, Bi Soipan Tuya, alisema kuwa thamani ya utajiri wake iliongezeka hadi Sh243.4 milioni kutoka Sh156 milioni alipochukua usukani kama waziri wa mazingira miaka miwili iliyopita.

    Wengine waliotangaza thamani ya utajiri wao ni pamoja na Bi Debora Barasa, waziri mteule wa afya aliyefichua kuwa thamani ya mali anayomiliki pamoja na mume wake ni Sh455 milioni.

    Bw Julius Migos, waziri mteule anayetazamiwa kumrithi aliyekuwa waziri wa elimu, Ezekiel Machogu, alitangaza vilevile utajiri wake kiasi cha Sh790 milioni.

    Habari za Kitaifa Zaidi

    Mimi SI MKALI kwa mkenya anayetii sheria

    PROFESA Kithure Kindiki, amefafanua kuhusu matamshi makali aliyotumia alipokuwa akihudumu kama waziri wa usalama wa ndani.

    Bw Kindiki ameshutumiwa kwa kutumia matamshi kama vile “tutawabonda, tutawaangamiza,” yanayodaiwa kuchochea ukatili wa polisi dhidi ya raia hasa katika maeneo yanayokumbwa na ghasia na katika maandamano ya amani.

    Bw Kindiki Alhamisi alieleza Kamati Maalum kuwa matamshi yake mazito yalidhamiriwa magaidi, majangili, majambazi na wahalifu wote kwa jumla, na wala sio Wakenya wanaotii sheria.

    “Ni kweli nimetumia lugha ya kipekee mno. Watu ninaolenga si Wakenya wanaotii sheria. Huwa ninalenga magaidi, majangili, majambazi, hao ndio ninawaeleza nitawabonda na ninamaanisha hivyo,” alisema Profesa Kindiki.

    Akirejelea operesheni ya kuangamiza majangili katika eneo la Bonde la Ufa, Bw Kindiki alisema kuwa, “nilisema nitavunja na kunyoosha miamba na nilifanya hivyo.”

    “Nimebomoa na kufurusha majangili na wahalifu waliokuwa wakikimbilia mafichoni kila mara kwenye milima ya Korkor na Nyalecha.”

    Kuhusu visa vya polisi kutumia nguvu kupita kiasi, alieleza Kamati hiyo inayoongozwa na Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula kuwa polisi wanapaswa kutumia nguvu kwa kiwango kinachoruhusiwa kisheria.

    “Wanapokumbana na wahalifu wanapaswa kwanza kuwaamuru wajisalimishe. Wakikaidi na kumtaka kuua polisi, hapo basi sheria inaruhusu wakabiliwe vikali.”

     MIONGONI mwa mawaziri  walioteuliwa na Rais William Ruto Bw Kipchumba Murkomen, Bw Hassan Joho na Bw Aden Duale ndio wanaopingwa zaidi na Wakenya.

    Bw Murkomen ameteuliwa kama wizara ya Masuala ya Vijana, uchumi wa ubunifu na michezo, Bw Joho (Madini na Uchumi wa Majini) huku Duale akiteuliwa Waziri wa Mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa na misitu.

    Kulingana na uchambuzi uliofanywa na Bunge na kuonekana na Radio Fortune Africa, kuna barua 92 za kupinga uteuzi wa Murkomen,  72 za kupinga Joho na 69 za kupinga Duale.

    Wakenya waliwasilisha maombi 68 ya kupinga Waziri mteule wa Masuala ya Ndani Kithure Kindiki huku maombi 58 yakipinga  uteuzi wa David Chirchir ambaye amependekezwa Waziri wa Barabara

    Waziri mteule wa Ulinzi Soipan Tuya alipingwa kupitia maombi 48 huku mwenzake wa Ardhi, Alice Wahome akipingwa  kupitia  malalamishi 40 yaliyowasilishwa dhidi ya uteuzi wake.

    Wycliffe Oparanya alikuwa na maombi 33 yaliyowasilishwa dhidi ya uteuzi wake, John Mbadi, waziri mteule wa Fedha alikuwa na malalamishi 31, uteuzi wa Alfred Mutua (Leba na ulinzi wa kijamii) ulipingwa kupitia malalamishi 23, na Waziri mteule wa Elimu Julius Ogamba alipingwa kwa maombi 21 huku Salim Mvurya (biashara na uwekezaji) na Rebecca Miano (utalii na wanyamapori) wote wakipingwa kwa maombi 19 ya kupinga uteuzi wao.

    Opiyo Wandayi ambaye ameteuliwa kuhudumu kama Waziri wa Nishati na Petroli alipokea maombi 11 ya kupinga uteuzi wake, Justin Muturi (utumishi wa umma) alipokea maombi 16, na mgombea wa Waziri wa Afya Debra Mulongo alikuwa na maombi sita ya kupinga uteuzi wake.

    Margaret Nyambura Ndung’u ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia) na Andrew Mwhia Karanja (kilimo na mifugo) walikuwa na ombi moja tu la kupinga uteuzi wao.

    Bunge lilipokea jumula ya malalamishi 1,368 kupinga uteuzi wa mawaziri hao.

    Hata hivyo, jumla ya risala 157 zilizotumwa kwa njia ya barua pepe zilibainika kutozingatia kifungu cha 6 (9) cha sheria ya vibali vya bunge.

    Kifungu cha 6 (9) cha Sheria ya Uteuzi wa Umma (Idhini ya Bunge), 2021 kinasema kwamba “mtu yeyote anaweza kabla ya kusikilizwa kwa idhini na kwa maelezo ya maandishi juu ya kiapo, kumpa karani ushahidi wa kupinga kufaa kwa mgombea kushika nafasi hiyo ambayo mgombea ameteuliwa.

    USIKU wa Juni 25, mbunge wa Kieni Njoroge Wainaina asema aliamka akiwa tajiri lakini akalala maskini.Ilikuwa siku ya kwanza ya maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024 yaliyoongozwa na vijana wa Gen Z ila mbunge huyo hakujua kilichokuwa kikimsubiri jioni hiyo.Kwa mara ya kwanza, Bw Wainaina ameeleza jinsi maandamano ya Juni 25 yalivyomwacha maskini baada ya maduka yake mawili makubwa katika miji ya Nyeri na Nanyuki kuporwa na kuharibiwa.“Huko Nanyuki, walichoma jengo langu la ghorofa tano. Siku hiyo niliamka milionea, lakini nikalala nikiwa mtu maskini,” asema na kuongeza kuwa alipoteza mali ya zaidi ya Sh500 milioni.Mbunge huyo anasema alikataa kulipiza kisasi dhidi ya waporaji, na “badala yake nilichagua kumuomba Mungu aelekeze baraka zilizokusudiwa kwao kwangu” kuashiria kwamba bado anaumia kutokana na hasara hiyo.Ametoa wito kwa kanisa kuwashawishi waumini kurejesha bidhaa zilizoibwa kutoka kwa biashara zake.Wainaina alizungumza kwa mara ya kwanza Jumatano wakati wa mazishi ya Charles Kariuki mwenye umri wa miaka 81 katika kijiji cha Muruguru katika Kaunti ya Nyeri.Wakati wa ibada, Bw Wainaina alitoa wito kwa makasisi wa kanisa la Presbyterian Church of East Africa kumuombea na kuombea jamii ya eneo hilo.Wakazi wameficha mali yake nyumbani kwao“Niliibiwa na watu wale wale mnaowahubiria. Nyumba hizi zimejaa friji zangu, meko na mashine za kuosha nguo kutoka dukani kwangu. Waambieni wahusika wazirudishe. Wkifanya hivyo kwa moyo safi, sitawashirikisha polisi,” alisema.Akielezea masaibu hayo, mbunge huyo alifichua kwamba haamini kuwa watu wale ambao alikuwa amewasaidia kwa hiari kabla ya kuingia kwenye siasa walikuwa wamemgeuka.Alisimulia jinsi mnamo 2020 wakati wa janga la Covid-19 alitoa lori tatu za vyakula katika maeneo tofauti.Aliendelea: “Nimekuwa Mkristo katika maisha yangu yote lakini kwa yale yaliyonipata siku hiyo, sasa naanza kutilia shaka Ukristo. Uporaji huo haukuwa wa kumcha Mungu”Bw Wainaina alikuwa aliandamana na Naibu Rais Rigathi Gachagua na wanasiasa wengine wa kitaifa na kaunti akiwemo Mbunge wa Nyeri mjini Duncan Mathenge, Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti Rahab Mukami, Seneta Wahome Wamatinga, Spika wa Bunge la Kaunti ya Nyeri James Gichuhi na Magavana Mutahi Kahiga na aliyekuwa gavana wa Nyandarua Francis Kimemia wakati wa mazishi hayo.#HasaraYaMaandamanoMbunge wa KieniNjoroge WainainaUporaji

    IRAN YAAPA KULIPIZA KISASI DHIDI ISRAEL

    IRAN imeapa kujibu shambulio la Israeli lililomwangamiza kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Hamas, Ismail Haniyeh.

    Wakati huo huo, Hamas pia imeapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya kiongozi wao.

    Haya yanajiri huku mamia ya Wapalestina wakiandamana katika mji wa Istanbul, Uturuki

    wakitaka haki itendeke baada ya Israeli kumwangamiza Haniyeh.

    Jeshi la Israeli, hata hivyo, halijatoa taarifa yoyote kuhusu tukio hilo.

    Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu jana alisema nchi yake imetoa “pigo kali” kwa maadui zake katika siku za hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuuawa kwa kamanda mkuu wa Hezbollah nchini Lebanon saa chache kabla ya shambulio la Tehran.

    Netanyahu pia aliwaonya Waisraeli “wajiandae kwa lolote litakalotokea”, huku kukiwa na hofu kuwa mzozo huo huenda ukaenea na kuwa mbaya zaidi.

    “Tuko tayari kwa hali yoyote na tutasimama kwa umoja na kuchukua hatua mwafaka kujilinda.”

    Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alionya dhidi ya kuongezeka kwa uhasama katika eneo hilo.

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipaswa kukutana Jumatano jioni kujadili hali hiyo.

    Haniyeh, ambaye kwa kawaida anaishi Qatar, amekuwa akihusika na diplomasia ya kimataifa katika kundi hilo la Palestina huku vita vilivyoanzishwa na shambulio la Hamas dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7 vikipamba eneo la Gaza, ambapo wanawe watatu waliuawa katika shambulio la angani lililotekelezwa na Israel.

    Akishikilia wadhifa wa juu katika eneo hilo alioteuliwa mwaka 2017, Haniyeh amekuwa akihamia kati ya Uturuki na mji mkuu wa Qatar, Doha, akikwepa njia za usafiri za Ukanda wa Gaza uliozingirwa na jeshi la Israeli kumwezesha kuwa mpatanishi katika mazungumzo ya kusitisha mapigano.

     

    AFISA wa zamani wa Jeshi (KDF) alizua kioja mahakamani Jumatano, Julai 30, 2024 alipoeleza makosa anayoshtakiwa nayo sio yake ni ya mtu mwingine.

    “Mheshimiwa nimeshangaa sana kusikia eti nimeshiriki ulaghai wa chakula cha Sh4 milioni,” Samuel Ouko Rangwa alimweleza Hakimu Mkuu katika mahakama ya Milimani Bernard Ochoi.

    Rangwa aliyestaafu kutoka KDF miaka miwili iliyopita aliambia korti, “nidhamu niliyopata kama afisa wa KDF hainiruhusu nishiriki uhalifu.Haya makosa sio yangu.Mwenyewe asakwe na polisi ”

    Rangwa alikabiliwa na mashtaka ya kula njama za kushiriki uhalifu na kupokea bidhaa za thamani ta Sh4 milioni kwa njia ya ulaghai .

    Rangwa alikana kati ya Desemba 6 na 11, 2023, akiwa na watu wengine, walikula njama kumlaghai Caroline Mwoni Amusala bidhaa za Sh4,026,700.

    BW Ochoi alielezwa na kiongozi wa mashtaja James Gachoka bidhaa Rangwa alizopokea ni magunia 600 ya mchele,mitungi 500 ya lita 20 kila mmoja ya mafuta ya kupika ya thamani ya Sh4,026,700.

    Mahakama iliambiwa Rangwa alimweleza bidhaa hizo zilikuwa za chama cha wadumishao amani almaarufu Kenya Veterans For Peace( KVFP).

    Shtaka lilisema Rangwa alijua anandanganya. Rangwa aliomba aachiliwe kwa dhamana.

    Gachoka alipinga akisema Rangwa huzuru mataifa ya kigeni na atatoroka.

    Lakini Rangwa alipinga akisema yeye ni mkazi wa Kaunti ya Nyanza na alisafiri nje ya Kenya akienda kudumisha amani Siera Leone na hajawahi safiri tena.

    Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh500,000 pesa tasilimu hadi Agosti 13, 2024 kesi itakaposikizwa.

    Taarifa kutoka Wizara ya afya nchini kenya haijaeleza kwa undani kuhusu abiria huyo, lakini imesema kwamba aligundulika na maambukizo hayo.

    UGONJWA wa homa ya tumbili (Monkeypox) uligunduliwa 1958 katika maabara nchini Denmark miongoni mwa koloni za tumbili zilizokuwa zinafanyiwa utafiti.

    Kisha, kisa cha kwanza kuambukiza binadamu kilishuhudiwa kwa mvulana wa miezi 9 nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) 1970.

    Nyakati hizo hakukuwa na tashwishi kuhusu matumizi ya jina la ugonjwa huo kuwa Monkeypox.

    Lakini, Shirika la Afya Duniani (WHO), lilisikitishwa na visa vya matamshi ya ubaguzi wa rangi na unyanyapaa baada ya ugonjwa huo kusambaa katika zaidi ya mataifa 100.

    WHO ilifichua kuwa watu na mataifa mengi yalitaka jina la monkeypox libadilishwe.

    Visa 98,001 vya ugonjwa huu vimeripotiwa katika nchi 118 duniani.

    Kati yao, watu 183 walioambukizwa walifariki katika mataifa 27.

    Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) nchini Amerika.

    Kutoka Monkeypox hadi Mpox

    Ilichukua miaka 64 kwa WHO kubadili jina na kutaka dunia itumie neno Mpox kurejelea ugonjwa wa homa ya tumbili.

    Mnamo Novemba 2022, shirika hili la Umoja wa Mataifa (UN) lilitangaza majina yote mawili yatumike kwa pamoja kwa kipindi cha mwaka mmoja kisha yaondolewe kabisa.

    “Baada ya mfululizo wa mashauriano na wataalamu wa kimataifa, hatimaye WHO litaanza kutumia jina MPOX (kwa Kingereza) badala ya ‘Monkeypox’ au ‘homa ya Ndui ya Nyani’ kufuatia mapendekezo ya kubadilishwa kwa jina hilo kwa maelezo ya kwamba lilikuwa na athari hasi kadhaa ukiwemo unyanyapaa,” ilisema taarifa ya WHO ya Novemba 28, 2022.

    Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus alipendekeza kuwa jina “Monkeypox’ halitafutwa kabisa kwenye rekodi ya Mfumo wa Kimataifa wa Uainishaji wa Magonjwa (ICD) ili kuhifadhi historia.

    Ugonjwa kuwa na jina jipya ni nadra

    Kubadili jina la maradhi hufanyika kwa nadra sana. Huu ni wajibu wa WHO na ICD kupitia mchakato wa mashauriano unaojumuisha nchi wanachama wa shirika hilo.

    Mchakato huu hufanyika kwa miezi kadhaa hadi zaidi ya mwaka mmoja kutegemea na uzito wa ugonjwa, upatikanaji wa ushahidi wa kisayansi na athari ya ugonjwa duniani.

    Lakini kwa Monkeypox, mchakato ulifanywa upesi kwa sababu kulikuwa na haja ya kukabili ubaguzi na kufuata kanuni bora za uainishaji.

    Kisa cha kwanza Kenya

    Mnamo Julai 31, 2024, Kenya ilithibitisha kisa cha kwanza cha Mpox katika mpaka wa Taveta na Tanzania.

    Kisa cha kwanza cha Mpox katika mpaka wa Taveta na Tanzania.Picha| Maktaba

    Virusi hivyo viligunduliwa kwa mtu aliyekuwa akisafiri kutoka Uganda kwenda Rwanda kupitia Kenya.

    Tahadhari 

    Ili kuepuka maambukizi, watu wanashauriwa kuzingatia masharti ya afya wanapokuwa maeneo ya umma.

    Vile vile, madaktari wanasisitiza umuhimu wa kunawa mikono kwa sabuni na maji mara kwa mara ili kulinda afya.

    Watu wenye dalili za ugonjwa huu wanatakiwa kufuata miongozo ya afya.

    Maelekezo haya yanashusisha kutokaribia wengine, kabla ya kufika katika kituo cha afya kilicho karibu kutibiwa.

    Maambukizi haya huenea watu wanapokaribiana na waathiriwa wenye dalili za mafua na upele.

    Kulingana na CDC, kwa sasa hakuna tiba mahususi iliyoidhinishwa ya maambukizi ya virusi hivi.

    Kwa wagonjwa wenye kinga thabiti wasio na maradhi ya ngozi, uangalizi wa kawaida wa kudhibiti uchungu bila matibabu unaweza kuwasaidia kupona.

    Chanjo ya Mpox inaweza kusaidia kuepuka maambukizi. Picha| Hisani

    Kwa mujibu wa WHO, chanjo ya Mpox inaweza kusaidia kuepuka maambukizi.

    Chanjo hutolewa ndani ya siku nne baada ya mtu kukaribiana na mwathiriwa (ama hadi siku 14 kama hakuna dalili).

    Baadhi ya mataifa barani Afrika ambayo yameripoti kuwa na visa vya Mpox ni DRC, Burundi, Central African Republic, Nigeria, Afrika Kusini na Sierra Leone.

    Kadhalika Visa vimeripotiwa katika mabara mengine duniani yakiwemo Ulaya, Asia, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Asia, na Australia.

    maambukizi

    #Monkeypox

    #MPOX

    afya

    chanjo

    KiPENGA CHA MICHEZO

    TIMU ya voliboli ya wanawake almaarufu Malkia Strikers bado inaendelea kuteleza kwenye Michezo ya Olimpiki inayoendelea jijini Paris, Ufaransa baada ya kupokezwa kichapo kingine katika mechi za Kundi B.

    Juhudi za warembo hao wa makocha, Japheth Munala na James Barasa kuandikisha historia ya kusajili angalau hata ushindi wa seti moja kwenye kipute hicho ziligonga ukuta usiku wa kuamkia jana walipozabwa seti 3-0 na Poland kwenye mechi yao ya pili.

    Kina dada hao chini ya nahodha Trizah Atuka walikubali kichapo cha 25-14, 25-17, 25-15, baada ya hapo awali kushindwa seti 3-0 na Brazil katika mechi ya utangulizi.

    Katika mechi hizo mbili walishindwa kwa muda sawa kwani Brazil ilitumia dakika 56 kuzima Malkia Strikers huku Poland ikitumia dakika 58 pekee kumaliza mchezo wao.

    Malkia Strikers walianza michuano ya Olimpiki kwa kuchuana na Brazil ambapo pia walishindwa. Picha|Reuters

    Matokeo hayo yanaashiria kuwa bado Malkia Strikers haina uwezo wa kung’ata wapinzani wao katika viwango vya dunia.

    Kwenye mechi hizo mbili Sharon Chepchumba hakupewa nafasi licha ya kutarajiwa kuwa yeye ni kati ya wachezaji wawili wa kimataifa wanaotazamiwa kusaidia kikosi hicho.

    ”Bado tuna mechi moja dhidi ya Japan tunakolenga kujituma kisabuni kwenye juhudi zetu za kusaka angalau ushindi wa seti moja,” alisema nahodha wa kikosi hicho, Atuka.

    Kenya imepangwa katika Kundi B linaloshirikisha Brazil, Japan na Poland. Nalo Kundi A linajumuisha: Ufaransa, Serbia, Marekani na Uchina. Uholanzi, Uturuki, Italia na Jamhuri ya Dominika zimepangwa katika Kundi C.

    Kwenye makala ya mwaka 2020 jijini Tokyo, Japan Malkia Strikers walishindwa kufana na kumaliza katika nafasi ya 12.

    BINGWA wa zamani wa Afrika wa kutembea haraka kilomita 20 Samuel Gathimba, Alhamisi aliambulia pakavu katika vita vya kuwania tuzo ya Sh6.4 milioni (Dola za Amerika 50,000) anazopata mshindi katika riadha kwenye Michezo ya Olimpiki jijini Paris, Ufaransa.

    Afisa huyo kutoka Idara ya Magereza amekamata nafasi ya 22 kwa saa 1:21:26 kati ya washiriki 49, huku Brian Pinado (Ecuador), Caio Bonfim (Brazil) na bingwa wa dunia Alvaro Martin (Uhispania) wakifagia medali kwa 1:18:551:19:09 na 1:19:11 mtawalia katika usanjari huo.

    Gathimba anajivunia medali tatu za dhahabu kutoka Riadha za Afrika na moja katika Michezo ya Afrika pamoja na fedha mbili za Michezo ya Afrika na moja kwenye Riadha za Afrika na shaba moja ya Michezo ya Jumuiya ya Madola.

    Muda wake bora mwaka huu kabla ya Olimpiki ulikuwa 1:28:06 kumaanisha aliuimarisha, lakini hiyo haikutosha hata kuwa karibu na mduara wa medali.

    Gathimba alishiriki Olimpiki kwa mara ya kwanza mjini Rio de Janeiro nchini Brazil mwaka 2016, lakini hakumaliza mashindano.

    Alikosa makala yaliyopita mjini Tokyo nchini Japan mwaka 2021 kwa njia ya kutatanisha kabla ya kufuzu kushiriki makala haya ya 33.

    Hakuna Mwafrika amewahi kuibuka mfalme wa kutembea kwa haraka kwenye Olimpiki tangu fani hiyo ijumuishwe kwa mara ya kwanza mwaka 1956.

    Mbali na Gathimba, Wakenya wengine wanaume waliojaribu bahati katika fani hiyo ya kutembea kwa haraka katika Olimpiki, ni Pius Munyasia mjini Los Angeles nchini Amerika mwaka 1984, na David Kimutai, Justus Kavulanya na Julius Sawe mjini Atlanta nchini Amerika mwaka 1996.

    Kimutai na Sawe pia walishiriki makala ya Sydney nchini Australia mwaka 2000. Isitoshe, Kimutai alishiriki makala ya 2008 mjini Beijing, Uchina naye Simon Wachira hakumaliza mbio mwaka 2016.

    RATIBA YA OLIMPIKI AGOSTI 2:

    11.35am – michujo ya 100m (wanawake)

    12.10pm – michujo ya 1,500m (wanaume)

    7.10pm – michujo ya 5,000m (wanawake)

    8.10pm – 4x400m (mseto)

    8.45pm – michujo ya 800m (wanawake)

    10.00pm – fainali (wanaume)

    • TETESI ZA UHAMISHO ULAYA
    • West Ham wapo ukingoni kusaini mikataba miwili, timu inayoshiriki Ligi Kuu ya England imefikia makubaliano ya kumsajili Romelu Lukaku na Arsenal wakaribia kumnunua Mikel Merino.
      Arsenal, Real Madrid na Atletico Madrid wote wanamtaka kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Juventus. (Gazetta, kwa Kiitaliano)
      West Ham wanakaribia kuwasajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani Niclas Fullkrug, 31, na fowadi wa Leeds wa Uholanzi Crysencio Summerville, 22. (Sky Sports).
      Nottingham Forest hailengi kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Gibbs-White, 24, licha ya Newcastle, Arsenal, Aston Villa na Chelsea kutaka kumnunua. (HITC)
      MATANGAZO

      THCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
      West Ham wamekubali masharti ya kibinafsi ya kumsajili beki wa kulia Aaron Wan-Bissaka, 26, lakini bado hawajakubaliana ada na Manchester United, ambao wanataka £18m badala ya £10m iliyotolewa. (Sky Sports Ujerumani)
      Fulham wapo kwenye mazungumzo ya hatua ya juu kumnunua beki wa kati wa Villarreal Mhispania Jorge Cuenca, 24, kwa £6.7m. (Standard)
      Napoli wana ofa ya euro 12m (£10.2m) tayari kwa kiungo wa kati wa Brighton na Scotland Billy Gilmour mwenye umri wa miaka 23 na wanasubiri wachezaji kuondoka katika klabu hiyo kabla ya kuitoa. (Sky Sports Italia)
      Roma wamekubali mkataba na Girona kumsajili mshambuliaji wa Ukraine Artem Dovbyk, 27, kwa £28.8m – huku AC Milan ikionyesha nia ya kumsajili fowadi wa Roma wa Uingereza Tammy Abraham, 26. (Repubblica,
    • Arsenal wanakaribia kufikia dili la £25m kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Mikel Merino, 28, kutoka Real Sociedad. (Mirror)
      Stuttgart wataondoa nia yao ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Ujerumani Deniz Undav, 28, na kuangalia walengwa wapya hivi karibuni ikiwa hawawezi kufikia makubaliano na Albion. (Kicker, kwa Kijerumani)
      Newcastle wapo kwenye hatua ya juu ya mazungumzo na Sheffield United ili kumsajili mshambuliaji wa Blades wa Denmark William Osula, 20 kwa dau la awali la £10m. (Telegraph – usajili unahitajika)
      Leipzig itakataa ombi la pili kutoka kwa Barcelona kumnunua kiungo wa kati wa Uhispania Dani Olmo, 26. (Sport, kwa Kihispania)
      THCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
      Aston Villa wamefikia makubaliano na Chelsea kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anataka kujiunga na Napoli ya Antonio Conte. (Il Mattino, kwa Kiitaliano – usajili unahitajika)
      Bristol City, Stoke na Birmingham City wanavutiwa na mlinzi wa Burnley raia wa Ireland Luke McNally, 24. (Football Insider)
      Stoke City inamtaka kiungo wa kati wa Blackburn Rovers Muingereza Lewis Travis, 26. (Teamtalk)
      Kiungo wa kati wa Manchester City Muingereza Jacob Wright, 18, amekubali kuhamia Peterborough United kwa mkopo. (Football Insider)

     Habari zinazovuma Afrika Mashariki

    Kwa mujibu wa rais Ruto, muswada wa mwaka uliopita ulilenga kukusanya kiasi cha dola za Marekani bilioni 2 na laki moja, kusaidia nchi hiyo kulipa madeni yake.

    Kenya: Muswada wa fedha wa mwaka wa 2023 ulikuwa kinyume cha sheria: Mahakama

     

    Rais wa Rwanda Paul Kagame, João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi wa Kongo wakati wa mkutano wao wa pande tatu mjini Luanda, Julai 6, 2022, kuhusu mvutano mashariki mwa DRC.

    Rwanda na DRC zakubaliana kusitishwa kwa mapigano mashariki ya DR Congo

     

    Uchimbaji kwa sasa unaendelea ili kuangalia ikiwa mafuvu mengine hayajazikwa karibu na hayo 17 ambayo tayari yamepatikana.

    Mafuvu ya binadamu yagunduliwa kwenye masanduku ya chuma nchini Uganda

    Mamlaka kwa sasa inaendelea na zoezi ya uchimbaji ilikuhakikisha kwamba hakuna mafuvu mengine katika eneo hilo.

    Uganda: Mafuvu 17 ya vichwa vya binadamu yagunduliwa katika eneo la ibaada

    Wataalamu wanasema baada ya uchunguzi wao, walibainisha kuwa usafiri wa anga ulitatizwa na Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) na M23.

    DRC yaituhumu Rwanda kwa lengo la kutatiza usafiri wa anga Kivu Kaskazini

     

    Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga wakati wa hafla ya kuwakumbuka wahanga wa maandamano ambayo yaiitikisa nchi ya Kenya kwa wiki kadhaa, Julai 26, 2023.

    Ruksa kwa Raila Odinga kuwania kiti cha uenyekiti wa AU

    Mashirika ya kiraia yamekuwa yakiripoti kwamba wafungwa wanapitia hali mbaya kwenye magereza kutokana na msongamano.

    Mamlaka kuwaachia wafungwa zaidi ya Elfu Moja nchini DR Congo

     

    Mahakama ya Kijeshi ya Kinshasa/Gombe siku ya Alhamis iliendelea na uchunguzi wa kesi inayomhusisha Corneille Nangaa.

    DRC : Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Corneille Nangaa kiongozi wa (AFC)

     

    Corneille Nangaa, kiongozi wa kisiasa wa Muungano wa (AFC), ambalo ni tawi la kisiasa la waasi wenye silaha wa M23.

    DRC: Kesi dhidi ya Corneille Nangaa imeanza katika mahakama ya kijeshi

     

    INATOKEA SASA HIVI ULIMWENGUNI

    DUNIA

    • SISI NI NANI

    HUDUMA

    MAOMBI

    Orodha

    10:00

    GURUDUMU LA UCHUMI

    04/03/2024

    Umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na uma

    10:04

    WIMBI LA SIASA

    20/03/2024

    Makala haya yanatupia jicho uchaguzi wa urais nchini Urusi, nini maana ya ushindi wa rais Vladimir Putin.

    09:56

    AFRIKA YA MASHARIKI

    28/10/2023

    Nishati inachangia asilimia kubwa kwa ukuaji wa Uchumi wa mataifa

    20:03

    CHANGU CHAKO, CHAKO CHANGU

    28/11/2023

    Historia ya kabila la Wadigo wa Kenya na Tanzania katika Makala Changu Chako na Florence Kiwuwa

    10:02

    GURUDUMU LA UCHUMI

    04/03/2024

    Kuberoshwa kwa huduma ya intaneti Kenya na ilivyochochea ubunifu

    20:04

    NYUMBA YA SANAA

    06/01/2024

    Ambwene Mwasongwe Muimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania

    10:19

    SIHA NJEMA

    21/11/2023

    Mpango wa afya kwa wote barani Afrika

    Moussa Dadis Camara, na washtakiwa wengine wakiingia katika chumba cha mahakama kabla ya hukumu kutangazwa wakati wa kesi ya mauaji yaliyotokea katika uwanja wa mpira mnamo mwaka 2009 huko Conakry, Guinea, Julai 31, 2024.

    Mauaji ya 2009 nchini Guinea: Mawakili wa dikteta wa zamani Camara watangaza kukata rufaa

    Maandamano yameshuhudiwa kwenye jiji kuu Abuja,jiji la piki kwa ukubwa la Kano, mji mkuu wa kibiashara Lagos na miji mingine ambapo mamia ya waandamanaji wengi vijana waliotikia wito wa kuandamana wakiwa na ujumbe wa kumaliza uongozi mbaya nchini Nigeria.

    Nigeria: Maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama ya maisha yamefanyika

    Jeshi nchini Sudan linasema Jenerali al-Burhan alilengwa na ndege isiyokuwa ya kivita kutoka kwa wanamgambo wa RSF.

    Sudan: Utawala wa kijeshi umesema hatahudhuria mazungumzo ya amani

     

    Washtakiwa 10 wakiwa mbele ya majaji wakati wa kusomwa  hukumu katika kesi ya mauaji ya Septemba 28, 2009, Julai 31, 2024 huko Dixinn.

    Guinea: Moussa Dadis Camara ahukumiwa miaka 20 jela kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Hadja Lahbib anazungumza na wanahabari mjini Brussels, Ubelgiji, Juni 26, 2023.

    Waasi wa M23 mashariki mwa DRC: Ubelgiji yakaribisha makubaliano ya kusitisha mapigano

    Mashtaka dhidi ya Camara na washirika wake, ni pamoja  na mauaji, ubakaji na utekaji nyara.

    Uamuzi unatarajiwa katika kesi ya kihistoria ya mauaji katika uwanja wa Conakry

    Khartoum, Mei 30, 2023. Jenerali Al-Burhane awatembelea wanajeshi wake.

    Shambulizi la ndege isiyo na rubani lalenga kambi moja wakati wa ziara ya mkuu wa jeshi la Sudani

    Mamlaka imetetea mpango wa kuwahamisha watu hao ikisema ni njia moja ya kuhifadhi eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO kutokana na uvamizi wa binadamu.

    Tanzania: Serikali inawaondoa kwa nguvu wamaasai kutoka katika ardhi yao: HRW

    Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Sudan, Desemba mwaka wa 2022.

    Sudan : Jeshi lataka masharti kadhaa kutimizwa kabala ya mazungumzo mjini Geneva

     

    Kiongozi wa zamani wa kijeshi nchini Guinea Moussa Dadis Camara.

    Guinea : Mahakama kutoa uamuzi wake dhidi ya Moussa Dadis Camara

     

    Mwonekano wa jumla unaoonyesha moja ya kmitaa ya Niamey, Niger, Agosti 2, 2023

    Niger: Mahakama yaagiza kuachiliwa kwa muda kwa mawaziri wanne wa zamani wa rais Mohamed Bazoum

    "Sisi ni mamilioni ya vijana wa Cameroon ambao kwa sasa tunateseka chini ya utawala wa CPDM kwa zaidi ya miaka 40," amelalama Junior Ngombe kwenye video aliyorekodi TikTok.

    Mwanaharakati wa Cameroon azuiliwa kwa machapisho yake kwenye Tiktok

    Sahara Magharibi, koloni la zamani la Uhispania, inadhibitiwa haswa na Morocco, ambayo inapendekeza mpango wa kujitawala chini ya uhuru wake.

    Sahara Magharibi: Algeria yatangaza ‘kumrejesha nyumbani’ balozi wake Paris

    INATOKEA SASA HIVI

    DUNIA

    SISI NI NANI

    TOVUTI ZA FRANCE MÉDIAS MONDE

    Umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na uma

    WIMBI LA SIASA

    Makala haya yanatupia jicho uchaguzi wa urais nchini MAREKANI, nini maana ya ushindi wa Makamu Rais Kamala Harris dhidi Rais wa zamani Donald Trump.

    09:56

    AFRIKA YA MASHARIKI

    Nishati inachangia asilimia kubwa kwa ukuaji wa Uchumi wa mataifa

    20:03

    CHANGU CHAKO, CHAKO CHANGU

    28/11/2023

    Historia ya kabila la Wadigo wa Kenya na Tanzania katika Makala Changu Chako .

    UCHUMI NA BIASHARA

    Kuberoshwa kwa huduma ya intaneti Kenya na ilivyochochea ubunifu

    SANAA YA AFRIKA

    Ambwene Mwasongwe Muimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania

    10:19

    AFYA NA JAMII

    Mpango wa afya kwa wote barani Afrika

    All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


    Discover more from cantonadigital

    Subscribe to get the latest posts sent to your email.

    Leave a comment