UIsmail Haniya kiongozi wa Hamas ameuuawa katika shambulio nchini Iran

Radio Fortune Africa -Afrika Leo Mchana

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

HABARI INAYOTOKEA SASA HIVI ULIMWENGUNI NA CANTONA JOSEPH

SIKILIZA RADIO FORTUNE AFRICA

  • Makala Maalum
  • Habari kwa Kina
  • Ukweli Na Burudani

HABARI ZA AFRIKA

Kiongozi wa Hamas auwawa.

KIONGOZI wa kundi na wapiganaji la Hamas, Ismail Haniyeh, ameuawa nchini Iran, kundi hilo la wanamgambo wa Palestina lilisema  Jumatano, Julai 31, 2024 na kutaja shambulio hilo kama “ongezeko kali la mapigano” ambalo halitaafikia malengo yake.

Kikosi cha Revolutionary Guards cha Iran kilithibitisha kifo cha Haniyeh, saa chache baada ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo, na kusema kuwa kinafanya uchunguzi.

Hakukuwa na maoni ya mara moja kutoka kwa mamlaka ya Israeli.

Ikulu ya White House, Amerika haikujibu mara moja ombi la kutoa maoni kuhusu kuuawa kwa Haniyeh.

Habari hizo, ambazo zilijiri chini ya saa 24 baada ya Israeli kudai kumuua kamanda wa Hezbollah ambaye ilisema ndiye aliyehusika na shambulio baya katika milima ya Golan inayokaliwa na Israeli, zinaonekana kurudisha nyuma uwezekano wa makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza.

“Mauaji haya yaliyofanywa na Israel kwa ndugu Haniyeh, ni ongezeko kubwa la mapigano ambalo linalenga kuvunja moyo Hamas,” afisa mkuu wa Hamas Sami Abu Zuhri aliambia Reuters.

Alisema Hamas itaendelea na njia iliyokuwa ikifuata, na kuongeza: “Tuna uhakika tutaibuka na ushindi.”

Haniyeh, ambaye kwa kawaida anaishi Qatar, amekuwa akihusika na diplomasia kimataifa katika kundi  hilo la Palestina huku vita vilivyoanzishwa na shambulio la Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7  vikipamba huko Gaza, ambapo wanawe watatu waliuawa katika shambulio la angani lililotekelezwa Israel.

Akishikilia wadhifa wa juu katika Hamas  alioteuliwa mwaka 2017, Haniyeh amekuwa akihamia kati ya Uturuki na mji mkuu wa Qatar Doha, akikwepa njia za usafiri za Ukanda wa Gaza uliozingirwa na kumwezesha kuwa mpatanishi katika mazungumzo ya kusitisha mapigano au kuzungumza na mshirika wa Hamas, Iran.

Kundi la Hamas, limethibitisha kuuawa kwa kiongozi wake Ismail Haniya, katika shambulio linalodaiwa kutekelezwa na Israel

Aidha haifahamiki ni namna gani nchi ya Iran itajibu kilichofanywa na Israel, ambayo ni wazi sasa itakuwa Katia hali ya tahadhari zaidi.
Aidha haifahamiki ni namna gani nchi ya Iran itajibu kilichofanywa na Israel, ambayo ni wazi sasa itakuwa jaribio Kali.

Katika tarifa yake, kundi hilo limesema Kaka na kiongozi wa vuguvugu lao Ismail Haniya, ameuawa katika shambulio la Kizayuni lililolenga makazi yake mjini Tehran baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa rais mpya.

Taarifa ya Hamas pia imethibitishwa na jeshi la Iran, ambalo limethibitisha makazi ya kiongozi huyo wa juu wa Hamas kushambulia, katika tukio ambalo wanalichunguza.

Inahofiwa kuwa kifo cha kiongozi wa Hamas,  Ismail Haniyeh, huenda kikazua mzozo zaidi katika Ukanda wa Gaza.
Inahofiwa kuwa kifo cha kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, huenda kikazua mzozo zaidi katika Ukanda wa Gaza. © Ministère iranien des Affaires étrangères / HO / AFP

Kuuawa kwake kumeibua maswali zaidi kuhusu mustakabali wa amani kwenye eneo la Gaza, hasa kwa kuwa Haniya ndiye aliyekuwa akiongoza mazungumzo ya amani.

Aidha haifahamiki ni namna gani nchi ya Iran itajibu kilichofanywa na Israel, ambayo ni wazi sasa itakuwa Katia hali ya tahadhari zaidi.

Haniya, alichukua uongozi wa kundi hili kutoka kwa Sheikh Ahmed Yassin, ambaye aliuawa katika mashambulio ya Israel mwaka.

Soma zaidi mada inayofanana:

Kuhusu mada hiyohiyo

Aidha haifahamiki ni namna gani nchi ya Iran itajibu kilichofanywa na Israel, ambayo ni wazi sasa itakuwa Katia hali ya tahadhari zaidi.

Ismail Haniya kiongozi wa Hamas ameuuawa katika shambulio nchini Iran

 KUTOKANA na hali ngumu ya maisha nchini, kumeshuhudiwa vifo vingi vya akina mama wakati wakichimba dhahabu kwenye migodi katika Kaunti ya Pokot Magharibi.

Kulingana na mila za jamii ya Pokot, wanawake wako na jukumu la kutafutia na kulisha familia huku wanaume wakichunga mifugo.

Wakiwa na shoka, jembe, beleshi na mabaseni ya mabati wanaelekea kwenye mito ama maeneo ya migodi kusaka bidhaa hiyo.

Wao huchimba mashimo na wakiwa na watoto migongoni, hutembea mwendo mrefu na kuchomwa na jua kali.

Akina mama husukumwa kwenye migodi kutokana na hali ya umaskini na njaa kutokana na uzembe wa wanaume wao.

Ukosefu wa mvua umesababisha baa la njaa huku akina mama, watoto na wakongwe wakifanya kazi hiyo.

Hata hivyo, kazi hiyo imechangia wanawake wengi kuuawa na majangili ama kukufia kwenye migodi wakisaka dhahabu.

Wakati mwingine, hufunikwa na udongo huku wanaume wao wakiwa wanaota jua.

Akina mama wakiwa wamejihami na vifaa wanazohitaji katika uchimbaji wa dhahabu kwenye migodi Pokot Magharibi. Picha| Oscar Kakai

Ann Chepurai, mama wa watoto sita, mkazi wa eneo la Kases anasema kuwa yeye kutumia siku nzima mtoni na siku ya mwisho huuza dhahabu kwa wachuuzi kwa Sh200.

“Mimi husaka dhahabu sababu ya njaa, watoto hawana chakula. Mwaka jana hatukuvuna. Jua liliangamiza mazao,” alisema.

Bi Chepurai anasema kuwa kwa wiki moja yeye kupata Sh600 na yote ananunua chakula.

“Kazi hiyo ni ngumu. Unachimba mashimo na unaumwa na mgongo na kuchoka pakubwa,” anasema.

Anasema kuwa mabadiliko ya hali ya anga na wizi wa mifugo huharibu maisha ya wakazi.

Mary Chemsuto, mchimba dhahabu anasema kuwa wao hufanya kazi hiyo kwa makundi.

“Ni kazi ya kubahatisha. Tunategemea dhahabu kulisha, kuelimisha na kuvisha familia,” anasema.

Bi Chemusto anasema kuwa alianza kazi akiwa msichana mdogo lakini bado anaishi maisha ya uchocho.

Anapambana kuelimisha wanawe wawili ambao wako shule ya upili.

Anasema kuwa mamba na nyoka huwasumbua wakiwa kwenye mito.

Easter Chepukorio, mama wa miaka 45 anasimulia jinsi amekuwa aking’ang’ana kulisha wanawe nane huku mzee wake akishughulika na kuchunga mifugo.

“Nimefanya kazi hiyo kwa miaka kumi kulisha familia,” anasema.

Cheptoo Lotudo, msichana wa miaka 18 kutoka eneo la Alale ambaye aliponea kifo chupuchupu akisaka dhahabu na wenzake anasema kuwa alianza kazi hiyo akiwa na miaka nane.

“Sisi hufika hapa asabuhi na mapema na kufanya kazi siku nzima. Siku moja niliponea kifo chupuchupu baada ya kuangukiwa na udongo,” anasema.

Anasema kuwa kuna wachuuzi ambao huwanyanyasa kwa kununua bidhaa hiyo kwa bei ya chini.

Haya yanajiri baada ya akina mama wawili kuuawa na majangili wakisaka dhahabu katika kijiji cha Kases, eneo la Ombolion wiki jana.

Mwaka wa 2022, akina mama 3 walifunikwa

MGAWANYIKO mkubwa umezuka kati ya viongozi wa jamii ya Mulembe kuhusu hatua ya Rais William Ruto kuwajumuisha baadhi ya viongozi wa ODM ndani ya serikalini.

Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya ameongoza mrengo wa wanasiasa kutoka Magharibi kutaka utawala wa Kenya Kwanza utekeleze ahadi ya kutoa asilimia 30 za nyadhifa kwa wakazi wa eneo jinsi ilivyosema wakati wa kampeni za 2022.

Bw Natembeya amesema ni wazi kuwa Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula na Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi, wameshindwa kutoa uongozi bora kwa wakazi wa eneo hilo na sasa ni wakati wa kupisha uongozi mpya.

“Tunataka kujua jinsi eneo hili linanufaika kisiasa chini ya Wetang’ula na Mudavadi. Tunataka watuambie miradi ambayo wameanzisha au ile ambayo imetekelezwa tangu waingie mamlakani,” akasema Bw Natembeya.

Gavana huyo ambaye ameanzisha vuguvugu la tawe ameanza kuwavutia Katibu wa UDA Cleophas Malala, mfanyabiashara nguli wa Kakamega Cleophas Shimanyula ‘Toto’ na waziri wa zamani wa michezo Rashid Echesa katika mrengo anaouongoza.

“Mudavadi na Wetang’ula wote wanadai kuwa wana nyadhifa kuu serikalini ilhali viwango vya umaskini Magharibi vinaendelea kupanda. Sasa ni dhahiri wawili hao wanashughulikia maslahi yao wala si ya wananchi,” akaongeza.

Wanasiasa hao wanasema wakati umefika ambapo Mabw Mudavadi, Wetang’ula na waziri mteule wa vyama vya ushirika na biashara ndogondogo Wycliffe Oparanya kuwapisha wanasiasa chipukizi.

“Sasa kwa sababu mirengo yote ya Mulembe ipo serikali, tunataka kufahamu jinsi ambavyo watu wetu watanufaika,” akasema Bw Malala ambaye pia alikuwa katika mkutano huo ambao ulifanyika mjini Kakamega wikendi.

Bw Echesa naye ametofautiana na Rais Ruto akisema kuwa amewasaliti watu ambao walihakikisha anapata kura za maana Magharibi wakati ambapo ilikuwa vigumu kuvumisha UDA eneo hilo.

“Nilipewa wadhifa ambao nalipwa Sh50,000 kila mwezi na Sh54,000 kwa kila kikao tunachoandaa japo vikao hivyo havizidi nne kwa mwaka. Hili ni jambo la kuchekesha,” akasema Bw Echesa.

Hata hivyo, viongozi ambao wanaunga mkono ushirikiano kati ya Raila Odinga na Rais William Ruto wamesema kuwa wanaunga mkono uteuzi wa Bw Oparanya kama waziri.

Naibu Gavana wa Kakamega Ayub Savula na Mbunge wa Mumias Masharki Peter Salasya walisema kuwa Mabw Mudavadi na Wetang’ula ndio wataongoza mkutano wa kusherehekea uteuzi wa Bw Oparanya.

Bw Savula alidai kuwa Bw Natembeya anadhaminiwa na baadhi ya wanasiasa wakuu serikalini ili kuwadhalilisha Mabw Mudavadi na Wetang’ula na kusambaratisha umoja wa Waluhya.

“Tunawajua na wale ambao wanawadhamini na hawataenda mbali. Nimekuwa mbunge na sasa naibu gavana na najua Malala, Echesa na Natembeya hawaendi popote. Wangemakinikia kujijenga kisiasa badala ya kutumiwa kuwapiga vita Waluhya,” akasema Bw Savula.

RAIS William Ruto alimaliza ziara yake eneo la Pwani kwa kujaribu kuzima joto la kisiasa kati ya viongozi wa chama chake tawala cha UDA na wale wa upinzani, ambalo lilizuka upya baada ya kumteua Naibu Kinara wa ODM, Bw Hassan Joho kama waziri.

Rais ambaye aliandamana na wanasiasa wa mrengo wa Kenya Kwanza wakiwemo Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Hassan Omar, mwenzake wa Nyali Mohammed Ali na wengineo, aliwarai viongozi hao kufanya kazi kwa karibu na wenzao wa upinzani ambao amewateua kwenye baraza lake la mawaziri.

Dkt Ruto aliweka wazi kuwa hakuna mbabe wa kisiasa katika chama chake tawala cha UDA eneo la Pwani, kufuatia mzozo ambao umekithiri kati ya Bw Omar na Bw Ali.

Ubabe na uhasama wa kisiasa kati ya Bw Ali na Bw Omar umekithiri kwa muda sasa hasa ikikisiwa kuwa wawili hao wanaazimia kuwania ugavana wa Mombasa.

Chama cha UDA kimejaribu kusuluhisha joto hilo la kisiasa bila mafanikio. Hata hivyo, kuingia kwa Bw Joho serikalini huenda kukaongeza uhasama huo huku ikikisiwa mwanasiasa huyo ambaye ni kigogo wa siasa atazima ndoto za wanasiasa wa Pwani kufuatia umaarufu wake, utajiri na ufuasi mkubwa alionao.

Rais Ruto aliwataka viongozi wote wa Mombasa kumakinikia uongozi bora na kutumikia wananchi.Dkt Ruto alisema hayo kufuatia cheche za kupigania tiketi ya chama cha UDA katika uchaguzi wa ugavana wa 2027 baina ya Bw Ali na mwenzake Omar.

Gavana wa sasa Bw Abdulswamad Nassir pia anapania kugombea kiti chake.“Nimeshuhudia ubabe wa kisiasa lakini naomba tudumishe amani, tushirikiane na tufanye kazi pamoja badala ya kuangalia umaarufu wa wanasiasa. Naomba viongozi wadumishe siasa za amani na tuunganishe wakazi,” aliongeza.

Aliwatata wabunge Bw Omar, na Bw Ali, na viongozi wengine wa UDA kuweka tofauti zao za kisi Wakenya kazi.“Ni wapigakura ambao wataamua nani atakuwa mjumbe wao, diwani, Gavana, Seneta na Rais,” alisema Rais.

Hata hivyo, Bw Ali, alisema licha ya kuwa wamewakaribisha wanasiasa wa ODM serikalini, wanafaa kuwatumikia Wakenya wote kazini.

“Tumemkaribisha Bw Joho, lakini asifanyie wakazi wa Mombasa kazi bali Wakenya wote. Wakazi wa Mombasa wanalia sababu ya uongozi mbaya ambao hauna maendeleo. Nitaendelea kutathmini utendakazi wa serikali ya kaunti,” alisema Bw Ali.

Alisema hatanyamaza akiangalia uongozi mbaya ukiendelezwa Mombasa.Bw Ali ambaye anahudumu kama Mbunge wa Nyali kwa muhula wa pili alimtaka Rais kutoingilia siasa za Mombasa na awachane na viongozi hao kumenyana.

“Wakazi wa Mombasa wameteseka sana hasa katika swala la maendeleo. Uongozi ulioko umeshindwa kuwajibika, ni miaka miwili tangu wachukue hatamu lakini hakuna maendeleo yoyote,” alisema Bw Ali.

Alisema Bw Nassir ameshindwa kuleta maendeleo hata kujenga choo cha umma ilhali ameweza kujenga shule za umma.Alisema yuko tayari kumenyana na Gavana Nassir, Bw Omar, na Bw Joho kisiasa.

Hata hivyo, Bw Omar, alisema viongozi wa UDA wanafaa kuacha uhasama wa kisiasa na kujipiga kifua na badala yake kushirikiana.

Habari za Kitaifa Zaidi

WAKENYA wameshauriwa kujiandaa kwa mvua kubwa na baridi kali katika baadhi ya maeneo katika kipindi cha siku saba zijazo.

Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa Kenya imetabiri kuwa mvua kubwa itanyesha kuanzia Julai 30 hadi Agosti 5 katika baadhi ya maeneo ikiwemo Kaunti ya Nairobi.

Katika utabiri wake, idara hiyo ilisema kuwa baadhi ya maeneo nchini yatapokea mvua kubwa na ya wastani.

Miongoni mwa maeneo yanayotabiriwa kupata mvua ni pamoja na Nyanda za Juu za Kati, Magharibi mwa Kenya, Bonde la Ufa, Kaskazini-magharibi mwa Kenya, na Pwani.

Kaunti za maeneo haya ni pamoja na Nyandarua, Laikipia, Nyeri, Kirinyaga, Murang’a, Kiambu, Meru, Embu, Tharaka na Nairobi.

Kaunti nyingine ni pamoja na Siaya, Kisumu, Homabay, Migori, Kisii, Nyamira, Trans Nzoia, Baringo, Uasin Gishu, Elgeyo-Marakwet, Nandi, Nakuru.

Kaunti za Narok, Kericho, Bomet, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Busia na Pokot Magharibi zinatarajiwa kupata mvua kubwa kwa siku tano zijazo.

“Vipindi vya jua vinatarajiwa wakati wa mchana hali usiku huenda kukawa na mawingu kiasi ingawa mara kwa mara manyunyu na ngurumo za radi zinaweza kutokea katika maeneo machache,” idara hiyo ilitangaza.

Wakati huo huo, sehemu nyingine za nchi zinatarajiwa kubaki kavu kwa jumla huku hali ya jua ikitarajiwa katika maeneo mbalimbali.

Wakenya wanaoishi katika kaunti zilizotajwa hapo juu pia walionywa kuhusu majira ya baridi kali ya usiku ya chini ya nyusi 10.

Kaunti zinazotarajiwa kupata viwango vya juu vya joto mchana ni pamoja na; Mombasa, Tana-River, Kilifi, Lamu, Marsabit, Mandera, Wajir, Garissa Isiolo na Kwale.

“Hali ya baridi na mawingu inatarajiwa katika maeneo ya Nyanda za Juu za eneo la Kati, Magharibi mwa Kenya, nyanda za chini Kusini-mashariki na Bonde la Ufa,” idara ilisema.

WASAIDIZI watatu wa karibu wa Naibu Rais Rigathi Gachagua Jumanne walihojiwa na polisi kuhusiana na maandamano ya hivi majuzi yaliyoongozwa na vijana huku kukiwa na mazungumzo ya kupanga njama ya kumuondoa ofisini.

Watu hao waliandikisha taarifa kwa maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) katika Kituo cha Polisi cha Karen kuhusu madai ya kuingilia na kufadhili maandamano yaliyomlazimu Rais William Ruto kuondoa Mswada wa Fedha wa 2024 na kuvunja Baraza lake la Mawaziri.

Orodha ya waliohojiwa awali ilikuwa na wafanyakazi watano lakini ilipunguzwa hadi watatu na wapelelezi baada ya kuwaondolea wawili lawama.

Mmoja wa wale waliotakaswa alikuwa amesafiri hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika kilele cha maandamano na maafisa walitaka kujua maelezo zaidi kuhusu ziara hiyo. Inasemekana alitoa maelezo ya kuridhisha.

Afisa mwingine aliombwa kueleza shughuli ‘zinazotiliwa shaka’ alizofanya wakati wa kilele cha maandamano hayo.

Afisa mkuu wa DCI, ambaye ni miongoni mwa waliochukua taarifa hizo, aliambia Taifa Leo kwamba gavana wa zamani na mbunge maarufu wa Nairobi pia wamehojiwa kuhusiana na hilo.

Walihojiwa siku ambayo washirika wa Bw Gachagua walidai kuwa tayari kuna mipango ya baadhi ya washirika wa Rais Ruto kumuondoa Naibu Rais mamlakani.

Rais Ruto aliwahi kudai kuwa maandamano ‘halali’ ya Gen Z dhidi ya mapendekezo ya ushuru yalitekwa nyara na ‘wahalifu waliopangwa’.

Siku ambayo Rais aliondoa Mswada wa Fedha wa 2024, naibu wake ambaye alihutubia taifa kutoka Mombasa dakika chache baada ya hotuba ya kiongozi wa nchi alidai kulikuwa na majaribio ya kumhusisha na maandamano. Alimshutumu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ujasusi (NIS) Noordin Haji kwa kujaribu kumhusisha pamoja na aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta.

“Noordin Haji alikuwa anajaribu kutoa propaganda na kuhusisha viongozi na machafuko hayo akiwemo mimi na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta. Ni wazi kabisa na Rais amekiri kuwa maandamano hayo yalisababishwa na hasira za Wakenya kuhusu Mswada wa Fedha,” Bw Gachagua alisema.

Mbunge wa Embakasi Kaskazini Bw James Gakuya Jumanne aliambia Kameme FM kwamba ‘kuna mwanasiasa kutoka Kaunti ya Kiambu ambaye amekuwa akikusanya saini ili kuanzisha mchakato wa kumuondoa Bw Gachagua ofisini’.

Alisema washirika wa Bw Gachagua wanasubiri kuona jinsi mpango huo utakavyokuwa, akisema eneo la Mlima Kenya lazima lisalie macho kwani hilo litakuwa janga la kisiasa iwapo litatimia.

Alisikitikia kile alichodai kuwa tabia ya Mlima Kenya ya kupiga vita viongozi wa kutoka eneo hilo akisema kuna ‘viongozi wa eneo hilo ambao wamekuwa wakipiga Bw Gachagua ili kuwafurahisha wafadhili wao ambao wana nia mbaya kwa watu wetu’.

Kulingana na Mbunge Maalum Sabina Chege, mpango huo anaoutaja kama ‘bahati mbaya’ unapendekezwa na iwapo utatimia, utaonyesha jinsi “siasa za ulaghai” zinatekelezwa.

“Hata kuta zina masikio, mazungumzo hayo yamekuwa yakiendelea. Rais Ruto anapaswa kuwa mwangalifu sana kuhusu ushauri kutoka kwa marafiki na washauri wake. Natumai hajasahau mashaka yake ya 2018-2022 ya kufanya kazi kama Naibu Rais na mkubwa wake ambaye alikuwa akimhujumu.”

“Rais Ruto anapaswa kukumbuka kuwa hata wakati tofauti zake na Rais Kenyatta zilipofikia kilele, hakuna aliyewasilisha hoja ya kumfukuza kutoka kwa wadhifa wake wa pili wa uongozi,” alisema Bi Chege.

Bi Chege alisema, “ikiwa hoja itawasilishwa na kufikia umma, basi anayepaswa kuisimamisha mara moja ni rais mwenyewe.”

Bi Chege alisema kwamba udhaifu mkubwa ambao huenda ukamsababishia Bw Gachagua kuangamia ni kwamba “sisi jamii ya Agikuyu hatupendani tofauti na jamii zingine”.

Majina kadhaa yameorodheshwa kama yanayoweza kuchukua nafasi ya Bw Gachagua. Miongoni mwao ni pamoja na waziri mteule Alice Wahome, mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro, waziri wa usalama mteule Kithure Kindiki, gavana wa Kirinyaga Bi Anne Waiguru na mwenzake wa Embu Cecil Mbarire.

sabina chege

DCI

James Gakuya

Maandamano ya Gen Z

Rais William Ruto

Rigathi Gachagua

RAIS RUTO WA KENYA ATEUA MWANAMKE WA KWANZA KUWA MKUU WA SHERIA

RAIS William Ruto amemteua wakili Dorcus Agik Oduor kuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza mwanamke.

Rais Ruto alimteua Bi Oduor, mwenye tajriba ya juu na mweledi katika masuala ya sheria na uendelezaji wa kesi za umma kutwaa wadhifa huo ulioachwa wazi baada ya kutimuliwa kazini kwa aliyekuwa AG Justin Muturi alipovunja baraza lote nzima la mawaziri.

Jina la Bi Oduor limepelekwa katika bunge la kitaifa kupigwa msasa pamoja na mawaziri wengine aliowateua hivi majuzi katika zoezi litakaloanza Agosti 1, 2024.

Katika taarifa kwa wanahabari kutoka kwa Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, Rais Ruto alisema alimteua Bi Oduor kutokana na “ukwasi, ujuzi na weledi wake katika sheria” aliosema unatakiwa katika utekelezaji wa majukumu ya AG.

Bi Oduor ambaye amehudumu katika sekta ya umma kama wakili wa serikali kwa miaka 30 amepata umaarufu kama kiongozi wa mashtaka katika kesi mbali mbali za uhalifu.

“Nimemteua Bi Oduor kutwaa wadhifa wa mwanasheria mkuu ulio wazi, kutokana umahiri, weledi na kujitolea kwake kustawisha sheria nchini,” Rais Ruto alisema katika taarifa kwa wanahabari.

Bi Oduor, Rais Ruto alisema, amekuwa katika mstari wa mbele kustawisha sekta ya sheria kwa kuongoza na kushiriki katika kamati mbali mbali za kuangazia dosari na mapungufu ya sheria katika masuala kama vile changamoto za kiakili.

Bi Oduor aliyewahi kuteuliwa kuwa naibu wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) amehudumu kwa miaka 30 katika afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma.

Bi Oduor aliapishwa kuwa wakili wa Mahakama kuu 1992 baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu cha Nairobi alipofuzu katika taaluma ya uanasheria baada ya kuhitimu 1990.

Bi Oduor, anayetoka eneo la uwakilishi bungeni la Nyando anajulikana kwa ukakamavu wake katika utenda kazi katika Mahakama nchini.

Kabla ya uteuzi kuwa AG, Bi Oduor alikuwa Katibu katika masuala ya uendelezaji wa kesi za umma afisi ya DPP.

Bi Oduor, OGW, EBS, SC, Kamishna katika kamati ya sheria (KLRC) yuko na digirii ya uzamili masuala ya usimamizi wa hali tata.

Bi Oduor aliwahi kuhudumu kama naibu wa mkurugenzi wa kesi za umma (ODPP) Bw Keriako Tobiko alipokuwa DPP na pia alikuwa naibu wa Jaji Mkuu (CJ) Bernard Chunga alipokuwa DPP.

Pia amehudumu katika asasi mbali mbali na pia tume ya makabiliano ya masuala ya ardhi ya- Jaji (marehemu) Akilano Akiwumi, tume ya huduma za polisi (Ransely Commission) bodi ya kamati ya kutathmini masuala ya changamoto za akili, tume ya uchunguzi wa Kashfa ya Golden almarufu (tume ya Jaji (mstaafu) Samuel Bosire ya 2003, tume ya Kiruki ya kuwachunguza Artur Brothers almaarufu Mamuluki.

Bi Oduor atakuwa wa msaada mkuu kutokana ujuzi na uzoevu wa kazi katika sekta ya sheria.

Mbali na Bi Oduor Rais Ruto pia alimteua Bi Beatrice Asukui Moe kuwa Waziri wa Masuala ya Jumuia ya Afrika Mashariki.

NI rasmi sasa kwamba Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga atawania wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) Februari mwaka ujao.

Hii ni baada ya serikali ya Kenya Jumatatu kuwasilisha rasmi jijini Addis Ababa, Ethiopia, ombi lake la kutaka kushiriki kinyang’anyiro hicho.

Ombi hilo liliwasilishwa na Katibu wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni Korir Sing’oei kwa Afisi ya Mshauri wa Kisheria wa Umoja wa Afrika (AU), kupitia msimamizi wa Eneo la Mashariki mwa Afrika Dharmraj Busgeeth, ambaye pia ni Balozi wa Mauritius.

“Chini ya mamlaka ya serikali ya Kenya na kulingana na Sheria na Kanuni za Tume ya Umoja wa Afrika, leo tumewasilisha stakabadhi za mteule wa Kenya kwa wadhifa wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mheshimiwa Raila Amolo Odinga,” Dkt Sing’oei akasema kwenye taarifa.

“Uamuzi huo unatokana na sifa za Bw Odinga kama mtetezi sugu wa masilahi ya Afrika, ufaafu wake, ufahamu alionao kuhusu masuala kuhusu mataifa mbalimbali na uwezo wake wa kuongoza AUC ambayo ni asasi kuu katika Umoja wa Afrika,” akaongeza.

Katika ombi lake, Bw Odinga ameelezea maono yake kwa AUC yanayohimiliwa katika nyanja mbalimbali zikiwemo; utangamano wa Afrika, ustawishaji wa miundo msingi, ustawi wa kiuchumi, kuendelezwa kwa biashara baina ya mataifa ya Afrika, kujitegemea kwa Afrika kifedha na nyanja za usawa wa kijinsia.

Nyanja zingine katika maono ya Bw Odinga ni maendeleo ya sekta ya kilimo, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Amani na Usalama na uwezeshwaji wa vijana.

“Bw Odinga atatoa kipaumbele kwa mchakato wa matumizi ya utajiri wa rasilimali ya kibinadamu na kiasili zilizoko Afrika ili kuiweza bara la Afrika kufikia upeo wa ufanisi. Analenga kuigeuza Tume ya Umoja wa Afrika ili iweze kuandikisha ufanisi kwa manufaa ya bara letu,” Dkt Sing’oei akasema.

Miongoni mwa stakabadhi zilizowasilishwa jijini Addis Ababa ni Wasifu Kazi wa Bw Odinga, uliotafsiriwa kwa lugha sita zinazotambuliwa na AU, kulingana na hitaji la Afisi ya Mshauri wa Kisheria katika umoja huo.

Lugha hizo ni; Kiswahili, Kiingereza, Kiarabu, Kifaransa, Kireno na Kihispania.

Kuwasilishwa rasmi kwa ombi la Bw Odinga sasa kumeondoa dukuduku kuhusu kujitolea kwa Rais William Ruto na serikali yake katika kumuunga mkono kiongozi huyo wa upinzani kwa wadhifa huo.

Awali, serikali ilikuwa imeahidi kuwasilisha rasmi ombi hilo, na stakabadhi hitajika, kabla ya Juni 30, mwaka huu.

Hata hivyo, ilifeli kutimiza ahadi hiyo na hivyo kuibua wasiwasi kuhusu kujitolewa kwa serikali kumuunga mkono Bw Odinga.

Hata hivyo, muda rasmi wa makataa ni Agosti 7, mwaka huu.

KIPENGA CHA MICHEZO -TETESI ULAYA

PHILADELPHIA, Amerika

BEKI matata wa kimataifa, Riccardo Calafiori wa Italia amesema imekuwa ndoto yake kuchezea klabu ya Arsenal tangu akiwa na umri wa miaka 12.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 amejiunga na Arsenal kwa mkataba wa muda mrefu akitokea klabu ya Bologna ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kwa kandarasi iliyogharimu kiasi cha Sh4.2 bilioni pamoja na nyongeza nyingine za marupurupu.

Akichezea Arsenal, Calafiori aliyekuwa katika kikosi cha Italia kilichoshiriki Euro 2024, atakuwa akivalia jezi nambari 33 kuanzia msimu ujao wa 2024/2025.

“Beki wa kimataifa Riccardo Calafiori amejiunga nasi kutoka Bologna ya Serie A kwa mkataba wa muda mrefu,” taarifa fupi ya klabu ya Arsenal ilisema.

Calafiori alikuwa nguzo ya safu ya Bologna, akiibuka kama mmoja wa wachezaji wenye nguvu na thabiti katika ligi ya Serie A, lakini kocha Mikel Arteta amesisitiza kwamba hatamharakisha kucheza Jumatano dhidi ya Liverpool ugani Lincoln Financial Field.

“Huu ni mwanzo wa mambo makubwa zaidi maishani mwangu, kwa hakika nimefurahia kujiunga na Arsenal, timu niliyopenda tangu nikiwa mtoto mdogo,” alisema staa huyo aliyetambulishwa kwa wachezaji wenzake ugani Philadelphia Union Subaru Park ambapo kikosi cha Arsenal kimepiga kambi ya mazoezi kujinoa kwa msimu mpya.

“Nilizungumza na kocha pamoja na Edu (mkurugenzi wa michezo wa klabu) ambapo niliwaeleza hamu yangu ya kutaka kujiunga na Arsenal haraka iwezekanavyo,” alisema beki huyo.

“Kuna klabu nyingi zilizonihitaji, lakini sasa nimetua mahali nilikotaka. Niko hapa kwa ajili ya kusaidia Arsenal kutwaa mataji. Naipenda hii timu kwa sababu ina wachezaji wengi wa umri mdogo ambao watanipa matumaini makubwa ya kushinda mataji,” aliongeza Calafiori.

“Naweza kucheza katika nafasi tofauti. Popote kocha ataniweka, nitacheza. Nilishuhudia Arsenal ikicheza na Crystal Palace nikafurahia uchezaji wao. Nitajitahidi mazoezini ili nirejee katika kiwango changu bora, huku nikitarajia kusaidia timu kikamilifu,” alisema.

Usajili wake umekuja wakati kiungo Emile Smith Rowe anaondoka kujiunga na Fulham kwa mkataba unaosemekana kuwa wa thamani ya Sh3.4 bilioni pamoja na nyongeza za marupurupu.

Juhudi za Arsenal kumshawishi Rowe asalie klabuni ziligonga mwamba baada ya nyota huyo kukataa akisisitiza lazima atafute maisha mapya kwingineko.

Akizungumza kuhusu shughuli za usajili, kocha Arteta alisema hana mpango wa kuleta mastaa kwa sasa.

“Iwapo itawezekana, tutaimarisha kikosi, lakini kwa sasa nimetosheka na wachezaji nilionao. Hatutarajii kuleta majina makubwa kiwango cha akina Declan Rice kwa sasa.”

“Tuligundua ulegevu wetu kikosini mwezi Februari na Machi,” alisema Arteta, ingawa kulikuwa na uvumi kwamba Mhispania huyo anamfuatilia mshambuliaji Victor Osimhen wa Napoli mwenye umri wa miaka 25.

Wakati huo huo, mshambuliaji Julian Alvarez amesema ataamua hali yake ya baadaye baada ya kumalizika kwa Michezo ya Olimpiki za Paris 2024.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 alitarajiwa kuwa kikosini dhidi ya Ukraine jana katika mechi ya Olimpiki jijini Lyon.

HABARI ZA KAUTI NCHINI KENYA

BUNGE la Kaunti ya Meru jana lilipata pigo baada ya Mahakama Kuu kuahirisha uamuzi kuhusu hoja ya kumtimua Gavana Kawira Mwangaza na kuamrisha suala hilo lishughulikiwe na Baraza la wazee wa Njuri Ncheke.

Hii ina maana kuwa kuna uwezekano mkubwa Bi Mwangaza atanusurika nia ya kutimuliwa na madiwani kwa mara ya nne kwa sababu kisheria madiwani walikuwa na makataa ya hadi leo kuijadili hoja hiyo.

Kisheria, hoja ya kumbandua gavana inastahili kujadiliwa siku 10 baada ya kuwasilishwa kwake bunge la kaunti.

Bi Mwangaza alikuwa amesema kuwa hoja hiyo ilikuwa hafifu kwa sababu baadhi ya saini zilighushiwa, hakusikizwa na baadhi ya masuala yaliyojumuishwa yalikuwa kortini.

Jaji Linus Kassan Jumatatu alitoa amri ya kuzima hoja hiyo na kusema atatoa uamuzi wake mnamo Agosti 20.

“Njuri Ncheke ambalo ni baraza la juu la wazee Wameru linaamrishwa liwasilishe ripoti yake ya kupatanisha pande zote mbili jinsi ilivyoamrishwa na Rais wa Kenya. Wanastahili kuwasilisha ripoti hiyo kwa muda usiozidi wiki tatu kutoka sasa,” akasema Jaji Kassan.

Pia aliamrisha pande zinazozozana kufika mbele ya Njuri Ncheke kabla ya Jumatano wiki hii ili kusuluhisha utata kati ya madiwani na uongozi wa kaunti.

Amri hiyo ya korti ilitolewa kwa msingi kuwa Bi Mwangaza alisema hoja ya kumtimua ilikuwa inavuruga juhudi za upatanishi ambazo zimekuwa zikiendelea.

Mnamo Aprili, uhasama wa kisiasa kati ya gavana na bunge la kaunti ulipofikia kilele, wazee wa Njuri Ncheke na viongozi wa kidini kutoka Kaunti ya Meru walikutana na Rais Ruto katika ikulu ndogo ya Sagana ili kupata mawaidha yake kuhusu maridhiano.

“Tumekuja kwako kama baba wa Wameru kwa sababu nyumba yetu inateketea na hatuwezi kuangalia upande mwingine,” ikasema barua iliyowasilishwa kwa Rais kutoka kwa viongozi hao wa kidini na Njuri Ncheke.

Kwa mujibu Katibu Mkuu wa Njuri Ncheke Josephat Murangiri, Rais aliwapa wazee hao na viongozi wa kidini idhini ya kuwaunganisha wanasiasa wa kaunti hiyo.

Kati ya wanasiasa ambao walikuwa wafike kwenye kamati ya maridhiano yenye wazee 25 na maaskofu ni Gavana Mwangaza, aliyekuwa waziri wa kilimo Mithika Linturi, Naibu Gavana Isaac Mutuma na wabunge na madiwani wote wa kaunti hiyo.

Bi Mwangaza amekuwa haonani uso kwa macho na naibu wake huku madiwani 56 kati ya 69 wakiwa wanampinga.

“Rais alituamrisha tukutane na viongozi wote kusuluhisha masuala tata. Pia alisema tuwasilishe ripoti kwake ili aitekeleze,” akasema Bw Murangiri.

“Ripoti iko tayari baada ya kukutana na viongozi wote na tumetoa mapendekezo yetu kwa Rais Ruto baada ya kuwasikiza wote. Hatuwezi kuruhusu kaunti yetu isambaratike,” akaongeza.

Wiki jana, madiwani 10 walijiondoa katika mchakato wa kumtimua gavana wakisema ni vyema kamati ya upatanishi inayoongozwa na Njuri Ncheke na viongozi wa kidini ipewe muda wa kufanya kazi yake.

AJABU MWANAUME AMUUA MKEWE,KISHA KUJITOA UHAI KISUMU KENYA

  • WAKAZI wa eneo la Metameta katika mtaa wa Manyatta Kaunti ya Kisumu Jumatatu waliamkia habari za kushangaza baada ya watoto kuwaeleza majirani jinsi baba yao alivyomuuwa mama yao wakishuhudia na kisha kujitoa uhai.
  • Hii ilibainika baada ya majirani kuwaona watoto hao wakicheza nje asubuhi bila kuwaona wazazi wao, jambo ambalo halikuwa kawaida yao.
  • Awali, mhudumu wa bodaboda ambaye huwapeleka watoto hao shuleni alifika kuwachukua lakini akaondoka mara baada ya kifungua mimba mwenye umri wa miaka 6 kumwambia kuwa, ‘watu wamekufa hapa ndani.’ Alifikiri mvulana huyo anatania, hivyo akaondoka.
  • Mtu aliyefuata kuwauliza watoto hao kuhusu wazazi wao ni landledi, Margaret Otieno.
  • “Nilikuwa nimeanza kufua nguo nje ya nyumba yangu nilipoona watoto wanacheza, nikataka kujua kwanini hawaendi shuleni na wazazi wao waliko, waliniambia kuwa wazazi wao wamefariki. Nilidhani wanacheza hadi nilipoingia ndani ya nyumba yao,” alisema Bi Otieno.
  • Alipomwona baba wa watoto hao akiwa amelala sakafuni, Bi Otieno alitoka mbio na kuelekea moja kwa moja hadi nyumbani kwa jirani yake ambaye ni daktari aliyetambulika kama Bw George Omondi.
  • “Mwanaume huyo alikuwa amelala chini, sikutaka kumgusa hivyo nikammulika na tochi yangu na kugundua kuwa macho yake yalikuwa yametulia, hayapepesi, alionekana kutokwa na povu mdomoni pia,”
  • “Sikujua kuwa mkewe marehemu pia alikuwa ndani ya nyumba hadi nilipouona mwili wake kitandani ukiwa umejaa damu huku kisu kikiwa karibu naye,” akasimulia Bw Omondi.
  • Kwa kutaka kujua kilichojiri katika nyumba hiyo, Bw Omondi na Bi Otieno waliamua kuzungumza na watoto hao.
  • Kifungua mimba wao aliwasimulia jinsi alivyomuona baba yake akimshika mama yao mdomoni na kumchoma kisu mara kadhaa.
  • Kijana huyo pia aliwasimulia majirani waliokuwa wamechanganyikiwa jinsi alivyomwona babake akijaribu kujinyonga kwa kamba lakini akashindwa na hatimaye kuanza kunywa sumu.
  • Kulingana na ripoti ya polisi iliyowasilishwa katika Kituo cha Polisi cha Kondele wawili hao hawakuwa na mvutano wa kinyumbani hivyo ikafanya hata majirani kukosa kusikia yaliyotendeka.
  • Ripoti ya polisi ilisema zaidi kwamba mwanamume huyo aliyetambuliwa kama Felix Owiti, 32, alionekana akiwa na hasira kazini siku ya Jumapili.
  • “Mwajiri wa mwathiriwa, mmiliki wa baa, alibainisha kuwa marehemu alikuwa na hasira usio wa kawaida akiwa kazini na hata kumwitisha mwajiri wake pesa ambazo zinaaminiwa alitumia kununua sumu,” ilisema taarifa hiyo ya polisi.
  • kisumu
  • mauaji
  • Metameta
  • Wanandoa
  • watoto

Katika picha hii iliyochapishwa na tovuti rasmi ya Ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Rais Mteule Masoud Pezeshkian, kushoto, ameketi karibu na Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei wakati wa sherehe pamoja na picha ya Hayati Rais Ebrahim Raisi imewekwa katikati, huko Tehran, Iran, Ijumaa, Julai 12, 2024.

Rais wa Iran kuapishwa: Baada ya miezi miwili madarakani, Massoud Pezeshkian ashindwa kujizatiti

Safari za ndege za mashirika ya ndege ya Ujerumani - Lufthansa, Eurowings na Uswisi - kwenda mji mkuu wa Lebanon "zimefutwa hadi Agosti 5 kutokana na hali ya sasa ya Mashariki ya Kati," msemaji wa shirika moja la  ndege ameliambia shirika la habari la  AFPsiku ya Jumatatu.

Lufthansa na Air France zasitisha safari zao katika mji wa Beirut

Huko Majdal Shams, maelfu ya watu waliovalia mavazi meusi walikusanyika siku ya Jumapili, Julai 28, kwa mazishi ya vijana 12 waliouawa kwa shambulio la roketi siku ya Jumamosi.

Benjamin Netanyahu azuru eneo la Golan lililoshambuliwa shambulio kwa roketi na kuua watu 12

Roketi zilizorushwa kutoka mpaka wa Lebanon na Israel ziliua watu tisa katika uwanja wa soka huko Majdal Shams, kijiji cha Druze kwenye Milima ya Golan inayokaliwa na Israel, Julai 27, 2024.

Israel: Watu 11 waangamia baada ya roketi kupiga kwenye uwanja wa mpira Galan

Wapalestina wakiomboleza miili ya wapendwa wao waliouawa wakati wa mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza, katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali moja huko Deir el-Balah, Julai 16, 2024.

Gaza: Shambulio la Israel katika shule moja laua watu thelathini

Francesca Albanese, ripota maalum kuhusu hali ya haki za binadamu katika Maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu tangu mwaka 1967, Geneva Julai 2023.

Israel yamtuhumu mtaalamu wa Umoja wa Mataifa aliyemlinganisha Hitler na Netanyahu

Kwa mujibu wa Netanyahu, Marekani na Israeli kwa sasa zinaweza kuunda muungano wa kiusalama Mashariki ya Kati kukabiliana na tishio la Iran.

Iran yakashifu ziara ya Benjamin Netanyahu wa Israeli nchini Marekani

(Kutoka kushoto) Mahmoud al-Aloul, makamu mwenyekiti wa kamati kuu ya chama cha siasa cha Palestina na chama cha siasa cha Fatah, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na Mussa Abu Marzuk, mwanachama wa kundi la wapiganaji wa Kipalestina la Hamas, wanahudhuria hafla huko Diaoyutai State Guesthouse mjini Beijing Julai 23, 2024. Mnamo Julai 23, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alikaribisha makubaliano ya pande 14 za Palestina kuanzisha "serikali ya mpito ya maridhiano ya kitaifa" ili kuitawala Gaza baada ya vita.

Beijing: Hamas yatangaza makubaliano ya ‘umoja wa kitaifa’ na mahasimu wake kutoka Palestina

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anahudhuria kikao cha Knesset, Bunge la Israel, mjini Jerusalem, Julai 17, 2024.

Israel: Netanyahu nchini Marekani kujaribu kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili

Mtu huyu akisimama mbele ya moto kwenye matangi ya kuhifadhia mafuta, Julai 21, 2024, siku moja baada ya mashambulizi ya Israel kwenye bandari ya mji wa Houthi wa Hodeida nchini Yemen.

Shambulio la Israel nchini Yemen: Waasi wa Houthi watishia kufanya mashambulizi zaidi

Hii itakuwa ni mara ya nne kwa Waziri Mkuu huyo wa Israeli kuhotubia kwa pamoja mabunge yote mawili nchini Marekani.

Benjamin Netanyahu anaelekea nchini Marekani ambapo atakutana na Biden

Benjamin Netanyahu anarejelea mara kwa mara kwamba hakuna kitakachoizuia Israel kufikia lengo lake la kutokomeza Hamas na kuwaachia huru mateka.

Netanyahu atangaza kutuma wajumbe kujadili makubaliano

INATOKEA SASA HIVI ULIMWENGUNI

JAMII NA UTAMADUNI

Historia ya kabila la Wadigo wa Kenya na Tanzania katika Makala Maalum.

UCHUMI NA BIASHARA

Kuberoshwa kwa huduma ya intaneti Kenya na ilivyochochea ubunifu.

SANAA YA AFRIKA

Ambwene Mwasongwe Muimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania.

AFYA NA JAMII

Mpango wa afya kwa wote barani Afrika

Afrika Leo Asubui

Nchi ya Marekani, imesema haiungi mkono vita kati ya #israel na #lebanon , matamshi inayoyatoa saa chache baada ya #telaviv kutekeleza shambulio mjini ~#beiruti , ililodai limeua kamanda wa juu wa wapiganaji wa #Hezbollah , wanaolaumiwa kwa shambulio la mwishoni mwa juma lililopita kwenye eneo la #golanheights .

Hili ni shambulio la kwanza kwa #Israel kushambulia #beirut tangu ilipoanzisha vita kwenye eneo la #Gaza na maeneo yake ya mpakani na nchi ya #lebanon .

  • AfrikaLeoAsubui
  • Nchini #DRC , Waziri wa Sheria Constant Mutamba punde baada ya kuwasili katika mji wa Kisangani kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, hapo jana aliamuru Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Rufaa ya Jimbo la Tshoppo kuanzisha kesi dhidi ya tume ya usimamizi ya Mfuko kwa ajili ya malipo na fidia ya wahanga wa vita vya siku sita, ambapo majeshi ya #Uganda na #Rwanda yalipigana kati ya Juni 5 na 10, mwaka wa 2000 na kusababisha uharibifu mkubwa wa mji huo wa #Kisangani huku
  • #AfrikaLeoAsubui
  • Jumuiya ya Afrika Mashariki, imetoa tahadhari kuwa wanachama wake kuwaelimisha raia dhidi ya Ugonjwa wa Monkey Pox, baada ya shirika la afya duniani WHO kutangaza kwamba mataifa wanachama ambao ni #DRC na #Burundi , wanashuhudia mlipuko wa
  • #afrikaleoasubui
  • Hitilafu ya umeme katika njia ya reli ya SGR iliyojitokea Jumanne usiku kati ya stesheni ya Kilosa na Kidete na ilisababisha treni ya SGR iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili kabla ya mafundi kurekebisha hitilafu na treni kuendelea na safari. Taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) imethibitisha kutokea kwa hitilafu hiyo. “Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.Taarifa ya TRC imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na imeelezea zaidi kuwa huenda ngegere na bundi walisababisha hitilafu hiyo.
  • Kipenga Cha Michezo
  • Mwanasoka wa Tanzania Novatus Dismas Miroshi anaoneakana kushika kasi katika klabu yake mpya ya Superlig, Ligi kuu ya soka ya Uturuki ya Göztepe, mjini Izmir.
  • Miroshi ni kati ya wasajiliwa wapya wa klabu hiyo inayotegemea matokeo mazuri kwenye Ligi hiyo msimu ujao wa 2024-2025.

  • SISI NI NANI

HUDUMA

MAOMBI

  • Pakua RFA kwenye simu na Kompyuta yako.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment