Radio Fortune Africa
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Maombolezo 3:31-33
Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu
Hata milele.Maana ajapomhuzunisha atamrehemu,Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.
Wala kuwahuzunisha.
Nimehimizwa moyoni sana kuandika ujumbe huu siku ya leo na ninajua ni kwa ajili yako wewe unaesoma wakati huu,ujumbe huu hujakutana nao kwa bahati mbaya kuna chakwako hapa
Nimehimizwa moyoni kukukumbusha kwamba, Wewe na Mungu mmetoka mbali sana, na kama angekuwa mtu wa kukutupa angeshakutupa siku nyingi,kama angekuwa mtu wa kukuacha angeshakuacha siku nyingi
Lakini hajawahi kukuacha,hajawahi kukutupa na hawezi kukutupa kamwe wala hawezi kukuacha kamwe,ajapo kuhuzunisha atakurehemu kwa kadri ya wingi wa rehema zake,maana moyo wake haupendi kuwatesa wanadamu
Nimetumwa kukumbusha kwamba,kuna kipindi ulipita katika bonde la uvuli wa mauti mahali ambapo woote uliowategemea walikutupa,wengine wakakuacha na kukucheka
Lakini huyu Mungu hakukuacha,ulipolia alilia na wewe,wakati wa huzuni alikuwa faraja yako,wakati wa upweke alikuwa rafiki yako wa karibu na alikukumbatia na kukwambia mwanangu usiogope nipo pamoja na wewe
Kwanini umekata tamaa tena? Kwanini unaona kama Mungu amekuacha tena, kwanini unahisi kama Mungu amekutupa,kwanini umeruhusu moyo wako kuinama?
Niko hapa kukutia moyo wanaweza kukuacha woote lakini sio Mungu, wanaweza kukukimbia woote lakini sio Mungu,wanaweza kukuchukia wote lakini sio Mungu
Yupo pamoja na wewe, anakupenda na anakuwazia mema, na yeye ni msaada wako wa karibu atakutetea, atakutia nguvu na atakutengeneza na kukusimamisha tena katika jina la Yesu

Kama umepokea Neno hili mshukuru Bwana kwa maneno haya “Asante Yesu kwa Upendo wako kwangu Amen”.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.