Bao La Asubui -SIO Kila Siku Utakuwa SAWA…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna siku utaamka asubuhi na hautakuwa sawa kama ulivyozoea…

Ndio, yaani utaona hauna NGUVU ambazo UMEZOEA kuwa nazo.

Utaona kama ile HAMASA ambayo kila siku unakuwa nayo, haipo tena.

Siku kama hizi, unaweza kujaribiwa KUKATA TAMAA.

Unaweza kujaribiwa KUISHIA NJIANI.

Unaweza kuanza kuwaza KUACHA UNACHOFANYA.

Kumbuka, Hizi ni siku za KUJITOFAUTISHA.

Kila unayemuona ambaye AMEFIKA JUU SANA…

…lazima kuna siku ambayo aliamka na HAKUJISIKIA KUENDELEA.

Wale waliojilazimisha katika siku hizo ndio WALIIBUKA WASHINDI…

…na wale ambao walikata tamaa ndio WALIFELI.

Ni kweli kuna KUCHOKA…

…ila usisahau ukichoka HAUTAKIWI KUACHA, unatakiwa KUPUMZIKA.

Hii ndio maana kwenye MECHI ya MPIRA huwa kuna MAPUMZIKO…

Ili KUKUSANYA NGUVU.

Ni kweli hauko sawa, PUMZIKA KIDOGO…

…kisha ENDELEA NA SAFARI.

Mwandishi maarufu na mshauri wa mambo ya kifedha Howard Ruff aliwahi kusema kuwa…

“ It wasn’t raining when Noah built the ark”

(Wakati Nuhu Anajenga Safina Mvua haikuwa inanyesha).

Msemo huu una maana kubwa sana kwa kila anayetaka mafanikio.

Tabia ya watu wengi sana ni kuanza kujiandaa pale wanapoziona fursa ama zinapowakaribia.

Ukiwa wa namna hii utajikuta kila siku unachelewa.

Wakati sahihi wa kujenga safina ni wakati ambako hakuna mvua.

Usisubiri usikie kuna kupandishwa cheo ndio uanze kutafuta kuongeza elimu.

Usisubiri uambiwe kuna mchongo ndio uanze kutafuta ujuzi.

Jiulize sasa hivi unahitaji nini?

Na anza kufanyia kazi ili fursa yako inapokuja ikukute ukiwa tayari.

Kuna watu wanadhani muda ambao hawana kitu cha kufanya basi ni muda wa kulala siku nzima…
.
…kuzurura ama kuangalia movie tu n.k

Ukijigundua uko kwenye kipindi kinachoonekana kama hauna cha kufanya, kumbuka ni muda wa kujiandaa Mungu amekupa.

Usiutumie vibaya, kwa sababu kuna fursa iko njiani itakuja baada ya hapo.

Ikukute ukiwa tayari.

Je, wewe Unajiandaa au Unapoteza muda?

Salamu ziwafikie wenyeji wa Mwanza Nchini Tanzania na Hili ndilo bao La Asubui.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment