Ni kipindi Kipya Cha Matumaini.Tulianza sio kwa kuona njia bali kutii sauti ya Mungu.

Radio Fortune Africa

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Aliyetufikisha hapa hata kule atatufikisha.

Matendo ya Mitume 17:28


Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.

Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu.tuko hivi tulivyo kwasababu Neema yake inatubeba

Kuna wakati tunamshukuru Mungu sio kwasababu amefanya ila nikwasabu tunajua yeye ni Mungu hata asipofanya anabaki wa kuaminiwa

Tulianza sio kwasababu tuliona njia ila ni kwasababu tulimwamini Mungu nae akatusaidia, Hata kule japo hatuoni njia tunamwamini atatufikisha tu

Hatuwazuii kusema ila tunajitahidi sana maneno yao yasituzuie kumsikia Mungu anaposema kwa maana Neno lake ndio taa na mwanga wa njia zetu

Kuna wakati tunashinda vita sio kwasababu ya nguvu za mwilini tulizonazo ila ni kwasababu ya Mungu tuliyenaye ambaye anatupigania na kutisaidia tunapochoka

Bwana akiwa upande wetu ni nani aliye juu yetu,tunacholinda kila siku ni Bwana awe upande wetu maana sisi ni kama samaki ambao ukiwatoa ndani ya maji wanaangamia

Nguvu zetu ziko ndani yake, tabasamu letu liko ndani yake, ushindi wetu uko ndani yake,kuendelea kwetu kuko ndani yeke,chukua vyote lakini tuachie Yesu, akiwa upande wetu atatusimamisha tena

Kwa msaada wake tutatenda makuu maana yeye ni rafiki yetu wa karibu, nguvu yetu, msaada wetu wa karibu na mtetezi wetu,aliyetufikisha hapa tunauhakika atatufikisha na kule.

Weka miadi kila siku ya Jumaa saa 4 am-6am Alfajiri na 3am-5am Alfajiri,mida ya Afrika Mashariki na Kati,na kote duniani kwa lisaa ya hapo ulipo.

All Rights Reserved ©Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment