Radio Fortune Africa
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hii Nayo Ni MBINU Ya KUKUFELISHA…
Kuna watu ambao wameshagundua kuwa…
HAWANA NGUVU za KUKUKABILI USO KWA USO.
Yaani, wameshajipima na wameona…
…wakiamua kupigana na wewe moja kwa moja, UTAWASHINDA.
Kwa sababu hiyo, wamebuni mbinu TOFAUTI ya kuhakikisha WANAPATA USHINDI…
…hata kama wewe una NGUVU zaidi na RASILIMALI zaidi Yao.
Mbinu Yao Ni KUKUSUMBUA usifikie makusudi na maono ulionayo.
Yaani wanahakikisha kila siku UNADEAL nao ili usifocus Katika kujenga mnara wa maono uliyo nayo.
Wanakuanzishia ISHU MOJA baada ya NYINGINE.
Inaweza ikawa ni kwenye MFUMO wa kukuzushia ili uanze KUJITETEA…au KUGOMBANA NAO.
Inaweza kuwa ni kukuanzishia KESI ambazo wanajua kabisa HAWATASHINDA…
Ila wana uhakika ZITAKUPOTEZEA MUDA na NGUVU zako.
Ni muhimu kujua MAPEMA hii mbinu kwa sababu…
Kwao USHINDI sio MATOKEO ya mwisho…
…bali ni kile UNACHOENDELEA kukipoteza kwa KUKABILIANA nao usikijenge.
Yaani, mwishoni unaweza kujiona UMESHINDA hoja, Kesi n.k…
…Ila kiukweli unakuwa UMEPOTEZA SANA MUDA.
Washtukie MAPEMA!
Salamu ziwafikie wakaazi wa Kechire, Kapsabet Kauti ya Nandi.
Na hili ndilo bao la Asubui .Hii Ni Idhaa Ya Kiswahili Ya Radio Fortune Africa -Ukweli Na Burudani.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.