Jiandae kwa kipindi Kipya Cha Matumaini.

Radio Fortune Africa

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Leo nasikia kusema jambo hili kwamba kama ni Mungu amekupitisha kwenye jaribu au kwenye mtihani kwa sababu ya baraka au hatima njema iliyoko mbele yako,fahamu hiyo ndio Paradox of life.

Kwanza hatakupa jaribu au mtihani mkubwa kuliko uwezo wako, lazima uwe ni mtihani ambao unaendana na wewe au na level yako ili uweze kustahimili maana yake uweze kuushinda

Kwa hiyo huo mtihani ni saizi yako kabisa hahahahaha, my dear pambana uushinde kwa sababu usiposhinda hutaenda kiwango kipya cha kimaisha jitahidi sana sana ushinde

1 Wakorintho 10:13
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

Pili hata kama ni jaribu au mtihani mgumu au mzito kiasi gani uwe na amani lazima Bwana atakufanyia mlango wa kutokea ili usije ukaangamia

Ndio maana hata yale majaribu uliyowahi kuyapitia yalikuwa makubwa sana na mazito sana lakini Mungu alikufanyia mlango wa kutokea hukuangamia ulivuka

Amini tu utavuka, amini tu upo mlango wa kutokea, amini tu hutaangamia, amini tu hapo sio mwisho, amini tu mlango wa kutokea utafunguka nawe utavuka katika jina la Yesu

Kama unaamini omba maombi haya pamoja nami kwa imani na itakuwa

“Baba asante kwa mlango wa kutokea unaonifanyia mbele yangu”

Kisha watagi ndugu,na marafiki zako kwa imani wambie “Upo mlango wa kutokea usikate tamaa”.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment