Afrika Leo Mchana

Radio Fortune Africa

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

  • Habari
  • Kipenga Cha Michezo
  • Makala Maalum
  • Afya Na Jamii
  • Ukweli Na Burudani
  • Video CantonaCast Television
  • Video Fortune Television
  • Vipindi vya Radio Fortune Africa
  • Bao La Asubui
  • Good Morning Afrika
  • Kipindi Cha Matumaini
  • Sayansi Na Teknolojia

Moja kwa moja,Obama amuunga mkono Kamala Harris kuwa rais

Barack na Michelle Obama wanasema Bi Harris ana “uwezo ambao unahitajika katika kipindi hiki kigumu”.

Muhtasari

  • Obama amuunga mkono Kamala Harris kuwa rais
  • Je Ruto na Blinken walizungumza kuhusu nini kwa njia ya simu?
  • Genge lawauwa wanawake na watoto katika mauaji ya Papua New Guinea – ripoti
  • ‘Vikwazo havitatuondoa kwenye vita’ – Mkuu wa waasi DRC kuhusu vikwazo vya Marekani
  • China na Urusi zafanya doria ya kwanza ya pamoja ya ndege za mashambulizi karibu na Alaska
  • Wadukuzi wa Korea Kaskazini wanaojaribu kuiba siri za nyuklia, Marekani na Uingereza zaonya
  • Kiongozi wa genge linalouza dawa za kulevya nchini Mexico akamatwa Texas
  • Harris amwambia Netanyahu ‘

Na Cantona Joseph

  1. Watu waonyesha kuchukizwa na hatua ya Waziri Mkuu wa Bangladesh kulia kwa sababu ya uharibifu wa kituo cha trenithCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESKiongozi wa Bangladesh ameshutumiwa kwa kulia “machozi ya mamba” baada ya kupigwa picha akilia kwenye kituo cha treni ambacho kiliharibiwa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali.Takriban watu 150 wameuawa kutokana na mapigano ya nchi nzima kati ya polisi na wanafunzi wa vyuo vikuu, huku vikosi vya usalama vikituhumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi.Waandamanaji wamekuwa wakitaka mfumo wa upendeleo wa nafasi za kazi serikalini kufutwa.Mtandaoni, wengi walimshutumu Bi Hasina kwa kutoonyesha kiwango sawa cha huruma kwa waliokufa, au familia zao.Picha hizo zilipigwa wakati wa ziara ya Bi Hasina katika kituo cha treni cha metro katika jiji la Mirpur siku ya Alhamisi, ambapo mashine za kuuza tikiti na kituo cha kudhibiti ishara zilivunjwa. Bi Hasina alipigwa picha akiwa amekunja uso na kujifuta machozi kwa karatasi ya tishu.”Ni aina gani ya mawazo inawaongoza kuharibu vituo vinavyorahisisha maisha ya watu? Jiji la Dhaka lilikuwa limejaa msongamano wa magari. Reli ya metro ilitoa ahueni. Siwezi kukubali kuharibiwa kwa kituo hiki cha usafiri kilichotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa,” gazeti la kila siku la Bangladeshi The Business Standard lilimnukuu waziri mkuu akisema.Maoni haya yalikasirisha watumiaji wa mtandao wa Bangladeshi.
  2. Dakika 52 zilizopita
  3. Obama amuunga mkono Kamala Harris kuwa rais.CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESBarack Obama amemuunga mkono Makamu wa Rais Kamala Harris kuwa mgombea urais wa chama cha Democratic, na hivyo kumaliza uvumi kuhusu iwapo angemuunga mkono.Rais wa zamani Obama na aliyekuwa Mama wa Taifa Michelle Obama walisema katika taarifa ya pamoja kwamba wanaamini Bi Harris ana “maono, tabia, na uwezo ambao unahitajika katika kipindi hiki kigumu”.Bw Obama aliripotiwa kuwa miongoni mwa zaidi ya Wanademokrasia 100 mashuhuri, Bi Harris alizungumza nao baada ya Rais Joe Biden kutangaza Jumapili iliyopita kuwa anajiondoa katika kinyang’anyiro hicho.Katika taarifa wakati huo, Bw Obama alipongeza kuondoka kwa Bw Biden, lakini hakumuunga mkono Bi Harris.Makamu wa rais wa Marekani tayari amepata uungwaji mkono wa wajumbe wengi wa chama cha Democratic, na hivyo kumweka katika nafasi nzuri ya kuteuliwa rasmi katika kongamano la chama hicho mwezi Agosti.Akina Obama walisema katika taarifa ya Ijumaa kwamba ni “furaha isiyokifani kumuunga mkono” Bi Harris. Waliapa kufanya “kila tuwezalo” kumchagua.”Tunakubaliana na Rais Biden,” ilisema taarifa ya wanandoa hao, “kumchagua Kamala ilikuwa mojawapo ya maamuzi bora aliyofanya. Ana wasifu wa kuthibitisha kuwa anaweza.”Walitaja rekodi yake kama mwanasheria mkuu wa California, seneta wa Marekani na kisha makamu wa rais.”Hakuna shaka katika akili zetu kwamba Kamala Harris ana kile kinachohitajika kushinda uchaguzi huu na kutimiza matarajio ya watu wa Marekani.
  4. Soma zaidi:Harris amwambia Netanyahu ‘ni wakati’ wa kumaliza vita vya GazaJe, Kamala Harris ana uwezo na sifa za kumshinda Trump?Kamala Harris ni nani, makamu wa rais ambaye Biden anamuunga mkono kuwa rais?
  5. Saa 2 zilizopita
  6. Je Ruto na Blinken walizungumza kuhusu nini kwa njia ya simu?gCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESMaelezo ya picha,Rais William Ruto akiwa na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken wakati wa ziara ya Rais Ruto nchini MarekaniRais William Ruto na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken Alhamisi walifanya mazungumzo kwa njia ya simu kuhusu hali ya mambo nchini nchini Kenya.Kulingana na msemaji wa Blinken, Matthew Miller, wawili hao walijadili haja ya kulinda sauti za vijana wa Kenya na mashirika ya kiraia.Blinken alisisitizia umuhimu wa kutetea vyombo vya habari pia.Miller alisema Waziri huyo wa mambo ya nje ya Marekani pia alimtaka Ruto kuhakikisha kuwa vikosi vya usalama nchini vinawajibika kwa vitendo vyao.” Katika wito na Rais wa Kenya Ruto @SecBlinken alisisitiza haja ya kutetea na kulinda sauti za vijana, mashirika ya kiraia, na vyombo vya habari. Katibu pia alisisitiza kwamba vikosi vya usalama vinahitaji kuwajibika,” msemaji alisema katika taarifa ya X (zamani ikiitwa Twitter.hCHANZO CHA PICHA,@SECBLINKEN
  7. Haya yanajiri baada ya serikali ya Kenya kuuandikia Wakfu wa Ford kutaka majibu kuhusu kile ilichosema kuwa ni ufadhili uliotolewa na wakfu huo kwa baadhi ya mashirika nchini Kenya ambao Serikali inashuku ulitumiwa kufadhilimaandamano ya hivi karibuni.Serikali ya Kenya iliorodhesha mashirika 16 yasiyo ya kiserikali iliyodai kuwa yalidhaminiwa na Wakfu wa Ford kwa ajili ya kuchochea maandamano hayo.Wakfu wa Ford, hata hivyo, ulitetea vigezo vyake vya ufadhili kwa mashirika ingawa ulielezea msimamo wake dhidi ya machafuko.Kulingana na Tume ya Taifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNHRC) kufikia Alhamisi, takriban watu 60 walikuwa wamefariki kutokana na maandamano hayo. Watu wengine 66 hawapo na hawawezi kufuatiliwa.Maandamano hayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja.Unaweza pia kusoma:
  8. Kwa nini Wakenya bado wanaandamana?Kenya inaweza kujifunza nini kwa mfumo wa uongozi wa Rwanda?‘Sina damu mikononi mwangu,’ asema RutoJinsi zana hizi tatu zilivyotumiwa na Gen Z kuishinikiza serikali ya Kenya
  9. Genge lawauwa wanawake na watoto Papua New Guinea – ripotigCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESMaelezo ya picha,Mashambulizi hayo yametokea katika jimbo la East Sepik, nchini Papua New GuineaMakumi ya wanakijiji wameripotiwa kuuawa baada ya genge la vijana kufanya mashambulizi katika eneo la mbali la Papua New Guinea.Walionusurika katika mauaji hayo wameelezea kusikia vilio vya majirani zao vya maumivu, na kuwatazama wengine wakichomwa mikuki walipokuwa wakijaribu kulikimbia genge hilo kwa mitumbwi.Takriban watu 26 – ikiwa ni pamoja na watoto 16 – wameuawa, vyombo vya habari vya ndani viliripoti, na kuna hofu kwamba idadi ya watu waliokufa inaweza kuongezeka hadi kufikia 50. Msako wa kuwatafuta manusura unaendelea.Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema ghasia hizo “za kutisha” zilionekana kuwa “matokeo ya mzozo kuhusu umiliki wa ardhi na ziwa na haki za watumiaji” na kutoa wito kwa maafisa “kuhakikisha waliohusika wanachukuliwa hatua”.
  10. ‘Vikwazo havitatuondoa kwenye vita’ – Mkuu wa waasi DRC kuhusu vikwazo vya MarekanigCHANZO CHA PICHA,AFCMaelezo ya picha,Corneille Nangaa (kushoto) na Bertrand Bisimwa (kulia) wamewekewa vikwazo na Marekani.Mkuu wa muungano wa muungano wa waasi wa DRC wa Alliance Fleuve Congo (AFC) unaojumuisha kundi la M23, Corneille Nangaa, amesema kwamba vikwazo vya Marekani havitawazuia katika mapambano yao ya “kuirejesha uthabiti wa nchi ” na kusema: “lengo ni Kinshasa, tutafika huko”.Siku ya Alhamisi, Ofisi ya udhibiti wa mali za kigeni katika wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza kuwa serikali ya Marekani imewawekea vikwazo viongozi watatu wa makundi yenye silaha mashariki mwa Congo.Waliowekewa vikwazo hivyo ni Corneille Nangaa, mkuu wa AFC, Bertrand Bisimwa, mkuu wa kitengo cha siasa katika M23, na Kanali Charles Sematama, mmoja wa viongozi wa kundi la Twirwaneho(Tujipiganie), linaloendesha harakati zake katika jimbo la Kivu Kusini.Serikali ya Marekani inashutumu watatu hao kwa kuchangia vita, ghasia, na kuwadhuru raia “ili kufikia malengo yao ya kisiasa”.Mzozo wa DRC: Je inawezekana kuyamaliza makundi ya wapiganaji Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo?DR Congo: Vikosi vya SADC vyatishia ‘kuwaangamiza’ waasi wa M23Mambo matano muhimu kuhusu mzozo wa Mashariki mwa DR Congo
  11. China na Urusi zafanya doria ya kwanza ya pamoja ya ndege za mashambulizi karibu na MarekanihCHANZO CHA PICHA,RUSSIAN DEFENCE MINISTRY
  12. Maelezo ya picha,Ndege ya Kichina ya mashambulizi aina H-6K na ndege ya kivita ya Urusi ya Sukhoi Su-30CM wakati wa doria siku ya Jumatano karibu na Alaska.Urusi na China zimefanya doria ya pamoja katika Bahari ya Pasifiki ya kaskazini na Bahari ya Bering karibu na pwani ya Alaska.Nchi hizo mbili zimefanya doria kadhaa za pamoja hapo awali, na Urusi mara kwa mara hupeleka ndege zake za mashambulizi kwenye Bahari ya Bering.Lakini doria ya pamoja ya Jumatano ilikuwa ya kwanza iliyojumuisha ndege za mashambulizi kutoka nchi zote mbili katika eneo la kaskazini mwa Pasifiki.Urusi na China zilisema “hazikulenga mtu wa tatu”, huku kituo cha pamoja cha ulinzi wa anga cha Marekani na Canada (NORAD) kikisema ndege za mashambulizi ambazo kilizizuia zilikaa katika anga ya kimataifa na “hazikuonekana kama tishio”.Lakini Seneta wa Alaska Lisa Murkowski alielezea tukio hilo kama “uchochezi ambao haujawahi kufanywa na wapinzani wetu”, na kuongeza kuwa “ilikuwa mara ya kwanza kuzuiwa kufanya kazi pamoja.”China imesema doria hiyo “haina uhusiano wowote na hali ya sasa ya kimataifa na kikanda”.
  13. Doria ya pamoja ya Urusi – China yazua tumbo joto Japan na Korea KusiniKorea Kaskazini: Tunaweza kushambulia eneo lolote Marekani
  14. Wadukuzi wa Korea Kaskazini wanaojaribu kuiba siri za nyuklia, Marekani na Uingereza zaonyahCHANZO CHA PICHA,BILL HINTONWadukuzi wa Korea Kaskazini wanajaribu kuiba siri za nyuklia na kijeshi kutoka kwa serikali na makampuni ya kibinafsi duniani kote, Uingereza, Marekani na Korea Kusini zimeonya.Wanasema kundi hilo – linalojulikana kwa majina Andariel na Onyx Sleet – linalenga vyombo vya ulinzi, anga, nyuklia na uhandisi kupata habari za siri, kwa lengo la kuendeleza mipango na malengo ya kijeshi na nyuklia ya Pyongyang.Kundi hilo limekuwa likitafuta taarifa katika maeneo mbalimbali – kuanzia usindikaji wa uranium hadi mizinga, nyambizi na torpedo – na limelenga Uingereza, Marekani, Korea Kusini, Japan, India na kwingineko.Kambi za jeshi la anga la Marekani, NASA na kampuni za ulinzi zinasemekana kulengwa.Onyo la hali ya juu kuhusu kundi hili mahususi linaonekana kuwa ishara kwamba kazi yake kufanya ujasusi sambamba na shughuli ya kutafuta pesa inawatia hofu maafisa kwasababu ya athari zake kwenye teknolojia nyeti na maisha ya kila siku.Marekani inasema kundi hilo linafadhili shughuli zake za ujasusi kupitia operesheni za programu inayozuia utendaji wa kompyuta dhidi ya taasisi za afya za Marekani.Onyo hilo la pamoja lililotolewa na Marekani, Uingereza na Korea Kusini linatoa ushauri wa kusaidia kujilinda dhidi ya wadukuzi wa Korea Kaskazini, linasema pia kwamba wamekuwa wakitafuta taarifa kuhusu mashine za roboti, mitambo ya silaha na machapisho ya 3D.
  15. Unaweza pia kusoma:Kwa nini ni nadra sana kusikia kuhusu uvamizi wa mtandaoni nchi za Magharibi?Uhalifu wa mtandao:Donda sugu ambalo linazidi kuligharimu bara la AfrikaNato yachunguza udukuzi dhidi ya kampuni ya kutengeneza makombora
  16. Kiongozi wa genge linalouza dawa za kulevya nchini Mexico akamatwa TexasfCHANZO CHA PICHA,DEA/ICE
  17. Maelezo ya picha,Ismael “El Mayo” Zambada (kushoto) na Joaquin Guzman LopezMmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya duniani, Ismael “El Mayo” Zambada, anayeongoza genge llinalofahamika kama Sinaloa la Mexico, amekamatwa na mawakala shirika upelelezi la Marekani Marekani katika eneo la El Paso, Texas.Zambada, mwenye umri wa miaka 76, alianzisha genge hilo la uhalifu na Joaquin “El Chapo” Guzman, ambaye kwa sasa amefungwa nchini Marekani.Zambada alikamatwa siku ya Alhamisi akiwa pamoja na mtoto wa kiume wa Guzman, Joaquin Guzman Lopez, ilisema wizara ya sheria ya Marekani.Mnamo Februari, Zambada alishtakiwa na waendesha mashtaka wa Marekani kwa njama ya kutengeneza na kusambaza fentanyl, dawa ya kulevya yenye nguvu zaidi kuliko heroini ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa mgogoro wa matumizi ya opioid (kundi la dawa zinazojumuisha fentanyl; dawa za kutuliza maumivu ambazo kwa kawaida zinapatikana kisheria kwa maagizo, kama vile oxycodone, hydrocodone, codeine, morphine) nchini Marekani.
  18. Harris amwambia Netanyahu ‘ni wakati’ wa kumaliza vita vya GazagMakamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris – ambaye anatarajiwa kuwa mgombea mteule wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa rais wa Novemba – amefanya kile alichokiita “mazungumzo ya wazi na yenye kujenga” na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.Akiwa na sauti kali zaidi kuliko Rais Joe Biden, Bi Harris alisema aliweka wazi “wasiwasi wake mkubwa” kuhusu majeruhi huko Gaza, akimweleza Bw Netanyahu kuwa ilikuwa muhimu kwa Israeli kwa Israel kujitetea.”Ni wakati wa vita hivi kumalizika,” alisema baada ya mazungumzo yao ya ana kwa ana katika Ikulu ya White House.BiHarris pia alisisitiza juu ya haja ya njia ya suluhisho la serikali mbili, huku akitoa wito kwa Wamarekani kufahamu “suala la utata ” juu ya mzozo huo.Mapema siku ya Alhamisi, Bw Netanyahu alikutana na Bw Biden, ambaye alijiondoa katika kampeni ya kuchaguliwa tena kama rais wa Marekani siku ya Jumapili.Mikutano ya Bw Netanyahu katika Ikulu ya White House ilifanyika siku moja baada ya kutoa hotuba kali kwa Congress, akiapa “ushindi kamili” dhidi ya Hamas, huku maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina wakiandamana nje ya bunge.Unaweza pia kusoma
  19. Vita vya Israel na Gaza: Kwanini inaonekana kuwa vigumu zaidi kufikia amani kuliko wakati mwingine wowoteVita vya Gaza: Ni mambo gani yanayokwamisha mapatano ya Israel na Hamas?Je, Israel iko tayari kwa taifa huru la Palestina?‘Hiki ndicho anachotaka Netanyahu’ – Gazeti la
  20. Natumai upo salama, tunakukaribisha tena kwa matangazo yetu ya mubashara tuki

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment