Afrika Mwisho Juma

Radio Fortune Africa

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Natumai u Buheri wa afya popote ulipo duniani,karibu julai ya 27 Katika awamu Afrika Mwisho Juma, Naitwa Cantona Joseph

INATOKEA SASA HIVI

SIKILIZA RADIO FORTUNE AFRICA

HABARI

Haiti: Makundi mawili yenye silaha yatia saini makubaliano ya kumaliza mvutano

Viongozi wa makundi mawili yenye silaha nchini Haiti wameripotiwa kutia saini makubaliano ya kumaliza mzozo.

Dakika 2

Haiti imekuwa ikikabiliwa na machufuko yanayotokana na makundi ya watu wenye silaha yanayowahangaisha raia, baadhi ya wangine wakitekwa.
Haiti imekuwa ikikabiliwa na machufuko yanayotokana na makundi ya watu wenye silaha yanayowahangaisha raia, baadhi ya wangine wakitekwa. AP – Odelyn Joseph

Na: Radio Fortune Africa

MATANGAZO YA KIBIASHARA

Haiti imekuwa ikikabiliwa na machufuko yanayotokana na makundi ya watu wenye silaha yanayowahangaisha raia, baadhi ya wangine wakitekwa.

Hali ilikuwa mbaya zaidi mwezi Februari baada ya watu wenye silaha kutekeleza shambulio katika mji mkuu wa Port-au-Prince wakiwa na nia ya kumtimua madarakani aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo Ariel Henry.

Makundi yenye silaha yanaripotiwa kudhibiti sehemu kubwa ya taifa hilo ambapo yanatuhumiwa kwa kutekeleza mauaji, uporaji wa mali pamoja na utekaji wa raia ilikulipwa kikombozi.

Magenge ya watu wenye silaha yamekuwa yakiyumbisha usalama nchini Haiti kwa kipindi kirefu.
Magenge ya watu wenye silaha yamekuwa yakiyumbisha usalama nchini Haiti kwa kipindi kirefu. © Ralph Tedy Erol / Reuters

Kwa mujibu wa makubaliano hayo kati ya viongozi wa kundi la G9 na lile na G-Pep, vizuizi vya barabarani katika mji wa shantytown wenye karibia watu laki tatu viliondolewa.

Mchungaji Jean Enock Joseph, mwenye umaarufu katika eneo hilo, ameeleza kwamba makubaliano kama hayo yaliafikiwa mwaka wa 2023 kabla ya kuvunjika majuma kadhaa baadae.

Kama ilivyo kwa raia wengi katika mji wa  Port-au-Prince, wakazi wa Cite Soleil walikuwa wamezuiwa kutembea kwa uhuru katika mtaa wa mabanda  uliogawanywa katika mitaa zinazodhibitiwa na magenge hasimu kwa hofu ya kuathiriwa kwenye makabiliano.

Takriban watu 600,000 wamekimbia makazi yao nchini Haiti, kulingana na Umoja wa Mataifa, ongezeko la asilimia 60 tangu Machi.
Takriban watu 600,000 wamekimbia makazi yao nchini Haiti, kulingana na Umoja wa Mataifa, ongezeko la asilimia 60 tangu Machi. © REUTERS – Ralph Tedy Erol

Magenge ya G9 na G-Pep hayajaripotiwa kuingia katika makabiliano tangu Februari, walipojiunga na muungano ulioanzisha kumpindua Henry.

Jimmy “Barbecue” Cherizier, mkuu wa G9 na mmoja wa viongozi wa muungano huo, alisifu ujasiri wa viongozi wa genge la Cite Soleil siku ya Alhamisi.

Ghasia katika mji wa Port-au-Prince zimeongezeka katika miezi ya hivi karibuni, na kuzua mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Kenya imewatuma polisi wake kuongoza kikosi cha polisi wa kimataifa kusaidia kurejesha hali ya utulivu nchini Haiti.
Kenya imewatuma polisi wake kuongoza kikosi cha polisi wa kimataifa kusaidia kurejesha hali ya utulivu nchini Haiti. © Marckinson Pierre / AP

Takriban watu 600,000 wamekimbia makazi yao nchini Haiti, kulingana na Umoja wa Mataifa, ongezeko la asilimia 60 tangu Machi.

Tangu kuondoka kwa Ariel Henry, mamlaka za mpito zimeundwa ili kuirejesha utulivu na uongozi thabiti kwenye taifa hilo.

Kenya inaoongoza kikosi cha polisi wa kimataifa kujaribu kurejesha hali ya utulivu nchini Haiti

Soma zaidi mada inayofanana:

Habari zinazofanana

Makamu wa rais wa Marekani na mgombea urais anayependekezwa wa chama cha Democratic Kamala Harris na mke wa rais wa zamani wa Marekani Michelle Obama (kulia).

Barack Obama atangaza kumuunga mkono Kamala Harris katika uteuzi wa chama cha Democratic

Haiti imekuwa ikikabiliwa na machufuko yanayotokana na makundi ya watu wenye silaha yanayowahangaisha raia, baadhi ya wangine wakitekwa.

Haiti: Makundi mawili yenye silaha yatia saini makubaliano ya kumaliza mvutano

Homa ya Oropouche unaambukiza binadamu kupitia nzi na mbu.

Brazil: Brazil yarekodi vifo viwili vilivyotokana na Oropouche

Siku ya Alhamisi Kamala Harris alisema yuko tayari kufanya mdahalo na Donald Trump, mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais wa Marekani ambaye kwa upande wake anaona kuwa "haifai" kufanya mdahalo wa ana kwa ana na mpinzani wake mpya kabla ya kuteuliwa rasmi na Chama cha Democratic.

Marekani: Trump akataa mdahalo wowote na Kamala Harris kabla ya kuteuliwa rasmi na Democrats

Picha mbili zisizo na tarehe za Ismael Zambada Garcia anayejulikana kama "El Mayo".

Marekani yatangaza kukamatwa kwa ‘El Mayo’ na Guzman, viongozi wawili wa kundi la Sinaloa

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akipokelewa na Makamu wa Rais wa Marekani na mgombea wa chama cha Democratic Kamala Harris, Julai 25, 2024 mjini Washington.

Marekani: Kamala Harris aahidi “kutokaa kimya” kuhusu Gaza baada ya mazungumzo na Netanyahu

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu, Oktoba 18, 2023 mjini Tel Aviv.

Joe Biden ampokea Benjamin Netanyahu ili kujaribu kuendeleza mazungumzo kuhusu Gaza

Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa hotuba yake kwa taifa mnamo Julai 24, 2024, kutoka Ikulu ya White huko Washington.

Biden anaelezea kujiondoa kwake kwa hitaji la ‘kuunganisha’ chama chake na ‘kukabidhi mwenge’

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akizungumza katika mbele ya wabunge na maseneta katika makao makuu ya Bunge la Capitole huko Washington, Jumatano, Julai 24, 2024.

Benjamin Netanyahu aapa kuendelea na vita Gaza mbele ya Bunge la Marekani lililogawanyika

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris wakati wa hafla katika Ofisi ya serikali ya Eisenhower mnamo Juni 17, 2024 huko Washington, DC.

Marekani: Kamala Harris kufafanua msimamo wake ili kuvutia wanaounga mkono Palestina

Mkurugenzi wa Huduma ya Secret Service Kimberly Cheatle wakati wa kusikilizwa kwake kuhusu dosari katika jaribio la mauaji ya Donald Trump. Jijini Washington, Julai 22, 2024.

Mkurugenzi wa Huduma ya Secret Service ajiuzulu kufuatia jaribio la kumuua Trump

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris akizungumza kutoka kwa bustani ya White House huko Washington, Jumatatu, Julai 22, 2024, wakati wa hafla na wanariadha wa chuo cha NCAA.

Marekani: Kamala Harris ajivunia kuwa na uungwaji mkono wa kutosha ili kuteuliwa kuwa mgombea

USA-ELECTION/HARRIS-HOLLYWOOD

Marekani: Kamala Harris, amepata uungwaji mkono kutoka kwa chama cha DeMOCRATS

WIMBI LA SIASA MAREKANI

Makala haya yanatupia jicho uchaguzi wa urais nchini Marekani, nini maana ya ushindi wa Makamu Rais Kamala Harris

AFRIKA YA MASHARIKI

Nishati inachangia asilimia kubwa kwa ukuaji wa Uchumi wa mataifa.

UCHUMI NA BIASHARA

Kuberoshwa kwa huduma ya intaneti Kenya na ilivyochochea ubora.

SANAA YA AFRIKA

Ambwene Mwasongwe Muimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania asimulia Safari yake ya Sanaa ya nyimbo za kumwabudu Mungu,anavyotunga nyimbo Katika uhalisia wa matukio ya kila siku maishani,mfano hai ni katika wimbi wake majaribu ni Mtaji.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment