Jiandae kwa kipindi Kipya Cha Matumaini.

Radio Fortune Africa-Kipindi Cha Matumaini

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kipindi Cha Matumaini..….

Jiandae Kipindi kipya Cha Matumaini katika Idhaa Ya Kiswahili Ya Radio Fortune Africa.

1Samweli 1:20
Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA.

Mpendwa kuna ambo Mungu huwa anayafanya sawasawa au kuringana na aina ya majira, usiogope kuna mambo yape muda majira yake yatafika tuu.

Biblia inasema ikawa wakati ulipowadia Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanaume. Kwahiyo wakati wa Hana kuzaa ulikuwepo ila ulikuwa haujawadia

Wakati ulipowadia yeye aliyechekwa na Penina, yeye aliyetemewa mate na kusemwa kila aina ya maneno nyakati zilibadirisha kila kitu

Nimetumwa kukwambia maneno haya

Never judge someone based on Season, one season Hana alichekwa kwasababu hakuwa na mtoto, the next season aliheshimika kwasababu ya kuzaa mtoto aliyekuwa bora kuliko mtoto wa Penina

One season David was a Shepherd and the next season he was a king, My dear majira yanabadirika usikubali kamwe mtu akucheke kwasababu leo unachunga kondoo

It is about season’s leo nachunga kondoo but next season nitakuwa mfalme, leo sina mtoto na unanicheka kesho nitamzaa samweli my time is coming

Acha kulia ni kweli leo unachunga kondoo,ni kweli leo unadharauliwa, ni kweli leo unatemewa mate, ni kweli leo unachekwa na kina Penina usilie inuka jipige kifua sema my time is coming

Majira yako yamewadia inuka, usikubali kufia hapo kwasababu tu ya majira unayoyapitia leo nooooo, your season is coming ni swala la muda tu

Chukua dakika chache mchana huu comment “my time is coming”

Kisha watagi marafiki zako wambie “your time is coming” na usiache kushare ujumbe huu na kwa wengine Mungu atakubariki sana sana

Jumatatu Hadi Ijumaa 4am-6am mida ya Afrika Mashariki na 3am-5am mida ya saa ya Afrika ya Kati na kote dunia kuambatana na kronomitabya hapo ulipo Hii Ni Idhaa Ya Kiswahili Ya Radio Fortune Africa.
Tufollow kwenye Facebook Page yetu Radio Fortune Africa

GoodMorningAfrica

GoodMorningAmerica

GoodMorningEveryone

goodmorningcanada

GoodMorningAsia

GoodMorningIsrael

GoodMorningEurope

TheHeartBeatofAfrica

Radio Fortune Africa

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Bao La Asubui

Upo uhusiano mkubwa sana baina ya namna unavyofikiri na hali yako ya kimaisha au na jinsi unavyoishi.

Kushindwa kwako, hakutegemeani na nguvu yoyote ulivyonayo isipokuwa ufahamu wako.

Kuanguka kwako hakutegemei maadui wengi ulionao, isipokuwa aina ya mtazamo ulionao.

Kurudi nyuma kwako hakutegemei historia yoyote uliyowahi kuwa nayo, isipokuwa namna unavyoendekeza mawazo yako ya kushindwa.

Naelewa kwamba panahitaji mjadala wa kina kuhusu kipi kinachomtawala mwenzie: mawazo yetu ndiyo yanayotuongoza ama ni sisi ndio tunayaongoza mawazo.

Hapo inapidi tushukie penye uelewa na namna mawazo yetu yanavyojengeka vichwani mwetu.

Kwa haraka haraka, nadhani, twawaza vile tulivyoviingiza ubongoni iwe kwa hiari yetu wenyewe ama pasipo hiari hiyo. Kwa maneno mengine sisi ndio watawala wa mawazo yetu.

Hiyo ni kusema kwamba unavyojiona, ndivyo ulivyo. Ukijidharau, hakuna mtu atakuja kukufanyia kazi ya kukuonyesha thamani uliyonayo.

Ukianza leo kujiona masikini, ni wazi kuwa akili yako itakubaliana nawe na kusema kweli, utakuwa umeukaribisha umasikini wako kwa mikono yako miwili.

Ningependa kukuachia ujumbe huu mchana wa leo;

Katika kila unalojaribu kulifanya, dhania kwamba haiwezekaniki jambo hilo likashindwa kwa namna yoyote.

Kwa sababu, haiwezekani ukashindwa katika jambo lolote, isipokuwa kama utakubali akilini mwako kwamba umeshindwa.

Achana na mawazo ya kushindwa shindwa. Achana na watu ambao hawaishiwi stori za ubaya ubaya. Amua kuyaelekeza mawazo yako kwenye mafanikio.

Kwa sababu mawazo yako ndiyo nguvu yako kuu uliyonayo! Itumie nguvu hiyo!

Jitamkie mchana wa leo kwa imani “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu”

Watag marafiki zako wambie kwa imani hata kama wamejikatia tamaa wambie ” Unayaweza mambo yote katika yeye akutiae nguvu”
Salamu zangu ziwafikie wenyeji wa Karatu Arusha Nchini Tanzania.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment