Radio Fortune Africa -Afrika Leo Mchana
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Natumai U Buheri wa Afya Popote pale Duniani,Karibu Katika Afrika Leo Mchana Jina Langu Cantona Joseph
Moja kwa moja,
Netanyahu atetea vita vya Gaza huku waandamanaji wakiandamana nje ya bunge la Marekani
Katika hotuba ya kihistoria aliyoitoka kwa Bunge la Congress Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwaambia wabunge wa Marekani kuwa “maadui zetu ni adui zenu”.
Muhtasari
Meli yenye bendera ya Tanzania yazama Taiwan
Polisi arekodiwa video akimkanyaga kichwani mtu kwenye uwanja wa ndege
Netanyahu atetea vita vya Gaza huku waandamanaji wRaia wa Ujerumani, Marekani, Uingereza na mataifa mengi 29 sasa watahitaji visa kuingia Namibia
Michelle Nehoya wa Namibia ametumia karibu $500 kwa ombi la visa ya kutembelea Canada – lakini karibu miaka miwili baadaye bado haijapata cheti hicho cha kusafiri.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 38, ambaye anaishi katika mji mkuu wa Namibia, Windhoek, anatamani sana kufika Quebec kumuona shangazi yake na binamu zake ambao hajawaona kwa karibu muongo mmoja.
Ombi la visa limehusisha kujaza fomu nyingi – na miongoni mwa mahitaji mengine, pia amelazimika kutoa miezi sita ya taarifa za benki, barua ya mwaliko pamoja na historia ya kina ya safari.
Hakuna njia ya kutuma ombi nchini Namibia, kwa hivyo hii inamaanisha kusafiri hadi Afrika Kusini kuwasilisha data yake ya kibayometriki, ambayo inahusisha kutoa alama za vidole na kupigwa picha.
Hali yake ni ya kawaida kwa Waafrika wengine wanaosafiri kwenda nchi za Magharibi.
Mwaka 2022, nchi saba kati ya 10 bora zilizo na viwango vya juu zaidi vya kukataa visa katika nchi za Ulaya inayojulikana kama eneo la Schengen zilikuwa za Kiafrika, kulingana na kampuni ya ushauri ya Henley and Partners.
“Kutafuta Visa imekuwa mchakato mrefu na wa kukatisha tamaa. Sijapewa sababu yoyote kwa nini imechukua muda mrefu,” Bi Nehoya aliambia Radio Fortune Africa
Hata hivyo, ikiwa familia yake huko Quebec itaamua kusafiri hadi Namibia kwa pasipoti za Canada, hawatakabiliana na chochote kama changamoto na gharama alizokabiliana nazo.
Raia wa Canada kwa sasa wanaweza kuingia Namibia bila visa.
Lakini hii itabadilika katika muda wa miezi minane.
Kuanzia Aprili ijayo, raia wa Canada, pamoja na wale kutoka Ujerumani, Marekani, Uingereza na nchi nyingine 29, watahitaji visa ili kuingia.
Hizi ni pamoja na “nchi zote zisizokubaliana” – ikimaanisha kuwa sheria mpya za visa zitaathiri raia kutoka nchi zote ambazo zinahitaji wamiliki wa pasi za Namibia kuwa na visa.
“Namibia imekuwa na nia njema na upendeleo kwa raia wa nchi mbalimbali. Hata hivyo, pamoja na juhudi hizi, mataifa fulani hayajakubali,” wizara ya uhamiaji ya Namibia ilisema mwezi Mei.
“Kwa kuzingatia tofauti hii, serikali imeona ni muhimu kutekeleza hitaji la visa ili kuhakikisha usawa katika mwingiliano wa kidiplomasia.
“Lakini wageni hawa wataweza kununua visa yao ya siku 90, inayogharimu dola 90, watakapowasili Namibia – tofauti na mahitaji magumu yanayowekwa kwa wamiliki wa pasipoti wa Kiafrika ambao wanahitaji kupata viza zao kabla ya kuingia Nchini humo.
Morocco yailaza Argentina katika mechi iliokumbwa na ghasia
Matatizo ya umati ya watu yalilazimisha mechi ya kwanza ya kandanda ya Olimpiki kusimamishwa kwa takriban saa mbili huku kukiwa na hali ya taharuki na wasiwasi, na mchezo huo ukakamilika katika uwanja mtupu.
Morocco walikuwa mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya Argentina, ambao walifunga bao moja na kuanza kutafuta bao la kusawazisha.
Cristian Medina baadaye alionekana kufanya matokeo kuwa 2-2 katika dakika ya 16 kati ya muda uliopangwa wa dakika 15 za majeruhi mwishoni mwa kipindi cha pili.
Baada ya umma kughadhabika mchezo ulianza tena bila mashabiki ndani ya uwanja huku VAR ikikataa bao la kusawazisha la Argentina, Morocco ilipata ushindi wa kutatanisha wa 2-1.
Hivi ndivyo fujo na machafuko yalivyotokea…•
Mara tu baada ya Medina kusawazisha na mambo kuwa 2-2, vikombe na chupa kadhaa zilirushwa kwa upande wa Argentina waliokuwa wakisherehekea kabla ya kile kilichoonekana kuwa moto kuanguka karibu na wachezaji na wakufunzi.
- Mashabiki kadhaa waliovalia rangi za Morocco pia waliingia uwanjani, huku wengine wakitolewa nje ya uwanja na wasimamizi.
- Askari wa kutuliza ghasia walisogea kando ya uwanja na mwamuzi akawatoa wachezaji mara moja.
- Mashabiki waliokuwa ndani ya uwanja wa Saint Etienne waliambiwa waondoke uwanjani na ujumbe kwenye skrini kubwa ulisema: “Kikao chako kimesitishwa tafadhali tokeni muelekee karibu la kutokea.”
- Haikuwa wazi iwapo mechi hiyo iliorodheshwa kuwa imekamilika, lakini ikabainika kuwa dakika tatu za mwisho zingechezwa kwenye uwanja usio na mashabiki.
- Kabla ya mechi kuchezwa hadi mwisho, ilitangazwa kuwa bao la kusawazisha lililokuwa na uwezo wa Argentina lilikuwa limekataliwa na uamuzi wa mwamuzi msaidizi wa video ambao ulionyesha mchezaji alikuwa ameotea kabla ya Medina kufunga.

ODM haijajiunga na serikali ya Ruto – Katibu mkuu wa chama cha ODM nchini Kenya
Kiongozi wa Chama cha ODM Raila Odinga
Katibu Mkuu wa chama cha ODM nchini Kenya Edwin Sifuna ameshikilia kuwa chama hicho hakijajiunga na serikali ya Rais William Ruto.
Bw Sifuna ameyasema hayo baada ya Rais William Ruto kuwateuwa viongozi 4 wa ODM kujiunga na serikali yake.
Akizungumza siku ya Alhamisi, Sifuna alisema kuwa hakuna uamuzi wowote ambao umefanywa na chama wa kujiunga na serikali ya Rais Ruto.
“Ukweli wa mambo ni kwamba hakuna uamuzi wa chombo chochote cha ODM kinachojiunga na serikali ya Ruto.”
Aliendelea kusema kuwa kumekuwa na juhudi za kukipaka matope chama cha ODM tangu kinara wa chama Raila Odinga alipohudhuria hafla ya kutiwa saini kwa Mswada wa mageuzi katika Tume ya Uchaguzi (IEBC) kuwa sheria.
Sifuna alivishutumu vyombo vya habari kwa kupotosha msimamo wa chama cha Chungwa kuhusu suala hilo.
Saa 4 zilizopita
Meli yenye bendera ya Tanzania yazama Taiwan
Moja ya meli nne za kigeni ambazo zilikwama
Maafisa wa uokoaji nchini Taiwan wanatafuta meli ya mizigo iliyokuwa na wafanyakazi tisa ambayo imezama kwenye pwani yake ya kusini.
Meli hiyo yenye bendera ya Tanzania ilikuwa imetoka katika bandari ya kusini ya mji wa Kaohsiung wakati Taiwan ilipokumbwa na kimbunga Gaemi.
Dhoruba hiyo pia imesababisha mvua isiyoisha nchini Ufilipino, ambapo meli ya mafuta iliyokuwa imebeba takriban lita milioni 1.5 za mafuta ya viwandani imepinduka.
Wafanyakazi kumi na sita wa MT Terra Nova yenye bendera ya Ufilipino wameokolewa huku mmoja akiwa bado hajapatikana, Katibu wa Uchukuzi Jaime Bautista alisema.
Kimbunga Gaemi, ambacho kilitua pwani ya mashariki ya Taiwan siku ya Jumatano, kimewaua watu watatu na kuwajeruhi mamia zaidi katika kisiwa hicho, maafisa wamesema.
Kabla ya kupiga Taiwan, kimbunga Gaemi kilisababisha mvua kubwa nchini Ufilipino, ambapo watu wanane wamekufa.
Kinatarajiwa kusababisha kutua katika maeneo ya bara ya China baada ya kupita Taiwan.
Walinzi wa Pwani wa Taiwan wanasema meli hiyo ya mizigo, Fu Shun, iliyopinduka pwani yakPolisi arekodiwa video akimkanyaga kichwani mtu kwenye uwanja wa ndege
Maelezo ya picha,Afisa huyo anaonekana kumpiga teke mara kwa mara mtu huyo, ambaye amelala kifudifudi
Afisa wa polisi amerekodiwa akimkanyaga na kumpiga kichwani mwanamume aliyekuwa amelala chini kwenye Uwanja wa Ndege wa Manchester nchini Uingereza.
Afisa huyo wa kiume aliyevalia sare anaonekana akiwa ameshikilia silaha aina ya Taser ( kifaa kinachotumika kujilinda bila kusabaisha madhara) juu ya mwanaume huyo, ambaye amelala kifudifudi, kabla ya kumpiga mara mbili huku maafisa wengine wakiwapigia kelele watazamaji , katika video iliyosambazwa sana mtandaoni.
Polisi wa Greater Manchester (GMP) walisema maafisa ealiojihami kwa bunduki walishambuliwa walipokuwa wakijaribu kumkamata mtu huyo baada ya makabiliano yaliyotokea kwenye uwanja wa ndege siku ya Jumanne.
Hasira kuhusu video hiyo imeendelea kuongezeka na mamia ya watu waliandamana nje ya kituo cha polisi huko Rochdale, Greater Manchester Jumatano kulaani kitendo hicho.
Netanyahu atetea vita vya Gaza huku waandamanaji wakiandamana nje ya bunge la Marekani
Katika hotuba ya kihistoria aliyoitoka kwa Bunge la Congress Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwaambia wabunge wa Marekani kuwa “maadui zetu ni adui zenu” .
Hotuba hiyo ililenga kutapata uungaji mkonowa Marekanikatika vita vya Gaza, lakini iliambatana na maandamano yaliyofanyika ndani na nje ya jengo la bunge la Capitol Hill.
“Tunapopigana na Iran, tunapambana na adui mkali zaidi, muuaji wa Marekani,” Bw Netanyahu alisema.
“Pambano letu ni pambano lenu, na ushindi wetu utakuwa ushindi wenu,” aliongeza.
Maelfu waandamana huku Netanyahu akihutubia bunge la Marekani
Kiongozi huyo wa Israel alipata mapokezi makubwa kutoka kwa wanasiasa wengi wao wakiwa wa chama cha Republican alipokuwa akitoa hotuba kwenye kikao cha pamoja cha Congress.
Lakini mgawanyiko wa kisiasa kuhusu vita huko Gaza ulisisitizwa na makumi ya wabunge wa Democratic wa Congress ambao hawakuhudhuria kwa makusudi huku maelfu ya waandamanaji wakiendamana mitaani nje.
Umati wa watu uliokusanyika kwenye jukwaa katika Capitol Hill ulibeba mabango yaliyoandikwa maandishi ya shutuma ikiwa ni pamoja na lile lililomtangaza kiongozi huyo wa Israel kuwa “mhalifu wa kivita anayetafutwa,” likilenga kukumbusha juu ya hati ya kukamatwa iliyotafutwa na mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.
Maafisa wa polisi wakiwa wamesimama mbele ya Bunge la Congress huku waandamanaji wanaounga mkono Palestina wakipinga hotuba ya Bw Netanyahu
Asante na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni Alhamisi ya Leo tarehe 25 mwezi Julai 2024
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.