Radio Fortune Africa -Bao La Asubui
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph

Wapo watu wengi sana ambao wanahitaji MSAADA na wanatamani KUONGEA, ila wanaogopa sana KUHUKUMIWA.
Dunia yetu imejaa watu wa KUHUKUMU kuliko wa KUFARIJI, hii ndio maana kuna watu wengi wanaona bora wabakie na matatizo yao kuliko kuyasema.
Mbaya zaidi, wale tunaowaamini kuwa wangeweza KUFICHA AIBU zetu, Kutunza SIRI ZETU na KUTUTIA MOYO, ndio wanakuwa MSTARI wa mbele KUTUHUKUMU na KUTUTANGAZA kila mahali.
Kama unataka KUWASAIDIA watu wako wa karibu, ni muhimu sana kuwatengenezea “Safe Space”.
Yaani, kuwatengenezea MAZINGIRA ambayo watajisikia wako SALAMA Kusema MADHAIFU au MAKOSA YAO.
Usipofanya hivyo, utashangaa mtu wako wa karibu ana matatizo, na anaenda kutafuta MSAADA MBALI SANA na wewe, hadi UNASHANGAA.
Nimeshakutana na kesi nyingi sana za watu ambao kwa sababu ya kutotengenezewa mazingira salama, wameamua WAFE na STRESS zao tu.
Umeshawahi kuwa na CHANGAMOTO na unatamani UMWAMBIE MTU WAKO WA KARIBU, ila UNAOGOPA namna ambavyo ATALICHUKULIA?
Salamu ziwafikie wakaazi wa Kahama Nchini Tanzania.
Hii Ni Idhaa Ya Kiswahili Ya Radio Fortune Africa.Na hili ndilo bao la Asubui.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.