Afrika Leo Mchana-Radio Fortune Africa.
Na Cantona Joseph;Juni 21,2024

- Michezo Na Burudani

DRC yaongoza kwa ubora wa Soka Afrika Mashariki
Kulingana na viwango vya ubora wa soka ulivyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), DRC inashika nafasi ya 61 ulimwenguni na nafasi ya kwanza kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya DRC./Picha: Fecofa X
Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ndio timu bora zaidi kwa upande wa Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa viwango vya ubora wa soka wa mataifa mbalimbali uliotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Juni 20, 2024, DRC inashika nafasi ya 61, ikiwa imepanda juu kwa nafasi mbili, na hivyo kuongoza ukanda wa Afrika Mashariki.
Chui hao kutoka DRC walishika nafasi ya nne katika makala ya 34 ya michuano ya AFCON 2023 yaliyofanyika nchini Ivory Coast ikiwa imedondoka kwa nafasi mbili ulimwenguni, Uganda iko katika nafasi ya 94 na ni ya pili kwa ubora wa Soka katika ukanda wa Afrika Mashariki, ikifuatiwa na Kenya, ambayo imeporomoka kwa nafasi moja chini na kuwa ya 108 duniani.
Nafasi ya nne kwa ubora wa soka katika ukanda wa Afrika Mashariki inakwenda kwa Tanzania, ambaye imepanda kwa nafasi tano hadi ya 114 duniani. Hivi karibuni, Taifa Stars iliifunga Zambia goli 1-0 katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia kwa mwaka 2026.
Kama ilivyo kwa DRC, ‘Taifa Stars’ nayo ilishiriki michuano ya AFCON 2023. Hata hivyo, Tanzania ilikuwa ya mwisho kwenye msimamo wa kundi F, baada ya kuambulia alama mbili kwenye mashindano hayo makubwa na yenye hadhi barani Afrika.
Rwanda ni ya tano kwa ubora ikiwa na alama 132, ikifuatiwa na Burundi ambayo ipo katika nafasi ya 140 duniani, wakati Sudan ya Kusini na Somalia zikiambulia nafasi ya 167 na 202 mtawalia.
Pata habari zaidi kupitia whatsapp channels
Radio Fortune Afrika
Habari zinazohusiana

Vijana na mchezo wakuteleza ili kusahau machungu ya vita DRC

FIFA imepokea zabuni nne za Kombe la Dunia la Wanawake la 2027

Adama Bojang ‘The Hurricane’ anyakua nafasi adhimu katika historia ya FIFA
Mshambuliaji huyo wa miaka 19, tayari ameibuka kuwa mchezaji nyota katika soka barani Afrika.

Fatma Samoura wa Senegal kujiuzulu kama katibu mkuu wa Fifa
Fatma Samoura ndiye mwanamke wa kwanza kupanda hadi cheo hicho katika shirikisho la soka Duniani
Makala yanayovuma katika kategoria hii

Uturuki kumenyana na Georgia katika mechi yao ya ufunguzi, Euro 2024

Kenya: Wadada U 17 wafuzu kombe la dunia mara ya kwanza

Uingereza yaichapa Serbia, michuano ya EURO 2024
Bao la kichwa la Jude Bellingham lilitosha kuwapa vijana wa Gareth Southgate uongozi wa Kundi C.

Warusi 14 kushiriki Paris Olimpiki kama ‘watu wasiokuwa na nchi’
Nini kingine ungependa kujua?
Vile vile

Vijana na mchezo wakuteleza ili kusahau machungu ya vita DRC

FIFA imepokea zabuni nne za Kombe la Dunia la Wanawake la 2027

Adama Bojang ‘The Hurricane’ anyakua nafasi adhimu katika historia ya FIFA

Fatma Samoura wa Senegal kujiuzulu kama katibu mkuu wa Fifa

Ligi Kuu Uturuki: Chaguo jipya la wanasoka wa Kiafrika
Habari Maarufu.
Katika Picha: Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza
DRC: Jeshi la Kongo lataka ushirikiano wa raia ili kuwadhibiti wanamgambo
Ukame wapelekea changamoto ya kiafya nchini Somalia
Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali
Raia wa Nigeria waanza mfungo wa Ramadhani.
Majukumu ya Kisheria
Habari Pichani.




Tovuti hii hutumia vidakuzi. Kwa kuendelea kuangalia tovuti hii, unakubaliana na utumizi wa vidakuzi.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd|2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.