Kipi hutokea kwenye ubongo mwanadamu anapokaribia kufa?

Maelezo kuhusu uchunguzi……..
Mwaka 2023, watafiti walichapisha utafiti uliochunguza wagonjwa wanne ambao walikuwa katika usingizi mzito (coma) wakiwa katika mashine.
“Walikuwa wakifa kutokana na magonjwa mbalimbali,” anasema mwanasayansi wa mishipa ya fahamu (neva), na Profesa wa Chuo Kikuu cha Michigan, Jimo Borjigin.
Madaktari na familia walipofikia makubaliano kwamba hawakuwa na jambo lolote la matibabu ambalo wangeweza kufanya, waliamua kuziondoa mashine. Kwa ruhusa kutoka jamaa zao, mitambo ya upumuaji iliondolewa.
Watafiti waligundua katika wagonjwa wawili, shughuli za ubongo zinazohusishwa na kazi za utambuzi zilionekana. Mawimbi ya gamma, katika ubongo yaligunduliwa, ambayo yanahusika katika uchakataji wa taarifa na kumbukumbu.Pia unaweza kusoma
- Mambo manne yanayoweza kusababisha kifo cha ghafla kwa binadamu26 Mei 2024
- Fumbo la kiroho kuhusu hali unayopitia ukikaribia kufa24 Oktoba 2023
Maeneo yanayoamka

Kwa wanadamu, ni sehemu fulani tu za ubongo zinazoamshwa unapokaribia kufa. Haya ni maeneo yanayohusiana na kazi za fahamu za ubongo.
Mojawapo ni sehemu ya nyuma ya ubongo inayowajibika kwa utambuzi wa hisia, fahamu na pia ndoto na maono ya kuona.
Eneo jingine ambalo waliona limeamshwa ni eneo linaloitwa Wernicke, linalohusishwa na lugha, kuzungumza na kusikiliza. Liko karibu na masikio yetu, sehemu hiyo ni muhimu sana si tu kwa kuhifadhi kumbukumbu, lakini kwa kazi nyingine za utambuzi.
Profesa anasema eneo la upande wa kulia la ubongo huhusika na ukuzaji wa huruma.
“Wagonjwa wengi ambao wamenusurika kifo kutokana na mshituko wa moyo ama walikaribia kufa, wanasema walipata hisia kubwa za huruma.”
Karibu na kifo

Katika historia, watu wengi ambao wamekaribia kufa wamezungumza juu ya kupata kukumbuka za wakati muhimu wa maishani mwao; wengi wameona mwanga mkali; wengine hujihisi wameiacha miili yao, wakiinuka na kuona kile kilichokuwa kikiendelea karibu nao.
Utafiti wa 2023 unabainisha kuwa katika kundi la watu waliopata mshtuko wa moyo, 20% au 25% waliripoti kuona mwanga, ikimaanisha ubongo uliamsha eneo la kuona.
“Baadhi ya wagonjwa walionusurika kifo wameripoti kusikia kilichokuwa kikiendelea wakati wa upasuaji wao au kile ambacho wahudumu wa afya waliowaokoa walichokuwa wakikisema.”
Inawezekanaje mtu anaweza kuona mwanga, kusikia sauti, kuhisi mwili umeondoka na kuelea hewani? “Hayo yote ni sehemu ya kazi ya ubongo,” anasema Profesa.
“Kwa sababu wataalamu wa matibabu wanafikiri ubongo haufanyi kazi wakati mtu anapokaribia kufa, kuna wale wanaoamini shughuli hizi zote hutokea nje ya mwili, yaani ni kitu kisicho cha kawaida.”
“2013 tulipochapisha utafiti wa kwanza wa wanyama, tuliandika, wazo kwamba hali hiyo hutokea nje ya mwili haliwezi kuthibitishwa.”
”Tangu awali, naamini matukio hayo hutokea kwenye ubongo, ingawa ni matukio ya kushangaza kwa sababu inadhaniwa kuwa ubongo haufanyi kazi wakati unapopata mshtuko wa moyo.”
“Ninaamini kwamba matukio ya karibu kufa huja kutokana na shughuli za ubongo ambazo hutokea kabla ya ubongo kukoma kufanya kazi kabisa,” anasema Borjigin.
Uelewa wa zamani

Borjigin anakubali kwamba utafiti wake kwa wanadamu ni mdogo sana na utafiti zaidi unahitajika juu ya kile kinachotokea katika ubongo tunapokufa.
“Ubongo, badala ya kuwa na shughuli kidogo, huwa na shughuli nyingi wakati wa mshtuko wa moyo. Tunahitaji kuboresha uelewa wetu kuhusu kazi ya ubongo wakati wa shida kama hiyo.”
Anafikiri ongezeko la shughuli za ubongo ni sehemu ya mbinu ya ubongo kuishi wakati unapokosa oksijeni .
“Wanyama, panya na wanadamu, wana utaratibu wa asili wa kukabiliana na ukosefu wa oksijeni.”
“Uelewa wetu wa sasa ni kwamba, moyo unaposimama, ubongo hufa tu, tunaamini ubongo hauwezi kukabiliana na kusimama kwa moyo.”
Lakini anasema – hatujui ikiwa hilo ni kweli.
Ubongo unataka kuishi

Borjigin anaamini ubongo haukati tamaa kwa urahisi. Na katika baadhi ya matukio, ubongo hupambana kuishi.
“Hibernation kwa kweli ni moja ya mifano bora ya kwanini nadhani ubongo una vifaa vya kustahimili shida ya ukosefu wa oksijeni, lakini hilo linahitaji kuchunguzwa.”
Fikiria familia ambayo, ghafla, inakabiliwa na mgogoro wa kiuchumi: wazazi wanapoteza kazi zao na hakuna mapato.
“Wanafanya nini? Wanapunguza gharama zao, wanaondoa vitu visivyo muhimu. Wanatumia pesa walizobakiza tu kwa kile kinachowaruhusu kuishi.”
“Sasa fikiria pesa ni oksijeni kwa ubongo. Ubongo nao hufanya vivyo hivyo. Kazi yake sio ya kuruhusu kucheza, kuongea, kutembea tu. Jambo la muhimu ni kupumua, kuruhusu moyo upige.”
“Nilipokuelezea nadharia yangu ya mfano wa familia ambayo inapaswa kufafanua vipaumbele vyake vya kifedha, ni kwa sababu naamini ubongo hufanya hivyo, naamini hukabiliana na ukosefu wa oksijini.”
“Kwa juu juu, tunajua kuwa kuna watu ambao hupatwa na mshtuko wa moyo na hupata matukio ya kushangaza, na taarifa zetu zinaonyesha matukio hayo ni kwa sababu ya kuongezeka kwa shughuli za ubongo.”
“Lakini, swali ni: kwa nini ubongo unaokufa unakuwa na shughuli nyingi namna hiyo?
“Tunahitaji kuchunguza, kugundua, kuelewa hilo kwa sababu tunaweza kufanya uchunguzi wa kifo kwa mamilioni ya watu, kwani bado hatuelewi mengi.”Pia unaweza kusoma
- Ni nchi ngapi ambazo bado zina hukumu ya kifo, na ni watu wangapi wameuawa?26 Januari 2024
- Kifo kwenye kivuko cha kuingia Uingereza – ni nini kilisababisha mvulana wa miaka 14 kufanya
Mada zinazohusiana
Habari kuu
- Tanzania: Baba, Paroko msaidizi miongoni mwa wanaotuhumiwa kumuua mtoto mwenye ualbino,
- Moja kwa moja,Mkataba na Korea Kaskazini utatulinda sisi sote dhidi ya uchokozi – Putin
- Zaidi ya mahujaji 500 wapoteza maisha kutokana na joto kali
Gumzo mitandaoni
Wanajeshi wa Korea Kaskazini wavuka mpaka, risasi za onyo zapigwa
AI: Kwa nini wanawake wa China wanaitegemea ChatGPT kwenye mapenzi?18 Juni 2024
Je Iran itajiunga na Hezbollah katika vita na Israel?17 Juni 2024
Hadithi ya mwanamke aliyelazwa kwa miaka 12 katika hospitali ya magonjwa ya akili kwa sababu hawakuielewa lugha yake16 Juni 2024
‘Wadukuzi walivujisha picha zangu za utupu baada ya kipakatalishi changu kuibiwa’17 Juni 2024
Putin ‘azitia tumbo joto’ nchi za Magharibi huku uvumi kuhusu ziara ya Korea Kaskazini ukiongezeka
Je, unakifahamu kisima cha kale ambacho Waislamu wanaamini maji yake ni matakatifu?14 Juni 2024
Eid al-Adha: Kwa nini kafara ya wanyama hufanyika katika dini15 Juni 2024
‘Mitandaoni wanatazama urembo badala ya kazi yangu’12 Juni 2024
Iliyosomwa zaidi
- Kipi hutokea kwenye ubongo tunapokaribia kufa?
- Tetesi za soka Ulaya Jumatano 19.06.2024
- Kwanini Urusi inazidisha vitisho vya nyuklia kwa Magharibi?
- Dawa 6 zinazopunguza nguvu za kiume na hutumiwa sanaImeboreshwa mwisho: 22 Julai 2022
- Euro 2024: Je, Ronaldo ni mchezaji wa kipekee Ureno au ni mzigo?
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd|2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.