Idhaa ya Kiswahili ya Radio Fortune Africa.

Na Cantona Joseph Juni 20,2024

  • Ushirikiano kati Urusi na Korea Kaskazini.

Moja kwa moja,Mkataba na Korea Kaskazini utatulinda sisi sote dhidi ya uchokozi – Putin

Baadhi ya maelezo yanaanza kujitokeza kupitia mashirika ya habari ya Urusi kuhusu kile kilichopo katika mikataba iliyotiwa saini na Urusi na Korea Kaskazini mjini Pyongyang.

Muhtasari

  • Ramaphosa kuapishwa kuiongoza Afrika Kusini kwa muhula wa pili
  • Kwa picha: Ziara ya Putin Korea kaskazini
  • Kim asema Korea Kaskazini ‘inaunga mkono kikamilifu operesheni ya Urusi nchini Ukraine’
  • Uvamizi wa Ukraine ulibadilisha mtazamo wa Putin kwa Korea Kaskazini – wachambuzi
  • Justin Timberlake akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa
  • TikTok yakabiliwa na madai mapya ya kukiuka faragha ya watoto
  • Biden ajikuta pabaya katika suala la uhamiaji
  • Putin na Kim wanawasili katika viwanja vya Kim Il Sung kwa ajili ya sherehe za makaribisho
  • Putin akaribishwa Korea Kaskazini huku akitarajiwa kufanya mazungumzo na Kim

Moja kwa mojA

  1. Saa 6 zilizopitaTanzania: Baba, Paroko msaidizi miongoni mwa wanaotuhumiwa kumuua mtoto mwenye ualbino,PinguCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Baba mzazi wa mtoto mwenye ualbino, Asimwe Novart, Paroko msaidizi wa Parokia ya Bugandika Elipidius Rwegoshora na Desideli Evarist ambaye ni mganga wa jadi ni miongoni mwa watu wanaoshikiliwa na polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mtoto mwenye ualbino wa umri wa miaka miwili na nusu.Taarifa ya polisi imesema, watuhumiwa hao walieleza namna walivyoshiriki katika tukio la mauaji ya mtoto Asimwe, tukio lililotokea mkoani humo.Polisi imesema kwa kushirikiana na raia walifanya msako mkali hadi usiku wa kuamkia Jumatano Juni 19 na kuwakamata watuhumiwa tisa wakiwa na viungo vinavyodhaniwa kuwa vya mtoto huyo wakiwa wamevihifadhi katika vifungashio vya plastiki wakitafuta mteja.Taarifa ya polisi inasema Paroko msaidizi, Elipidius Rwegoshora anadaiwa kumfuata na kumshawishi baba mzazi wa mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu.Pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.Mtoto Asimwe alichukuliwa nyumbani kwao kaskazini magharibi mwa nchi hiyo katika kijiji cha Bulamula, kata ya Kamachumu, wilayani Muleba mkoani Kagera Mei 30 majira ya saa mbili usiku.Baada ya tukio hili la mtoto Asiimwe, polisi mkoani Kagera wanasema wameimarisha ushirikiano na wananchi kupata taarifa za wahalifu kwa haraka na kuimarisha ulinzi kwa watu wenye ualbino.‘Kwa Kagera hili ndiyo limetokea, lakini sidhani kama yanaweza kutokea matukio mengine ya namna hiyo kwa mkoa huu kwa sababu polisi ipo karibu sana na wananchi na imejikita sana kwa polisi jamii na ile miradi yake lakini, kata zote zina wagakuzi kata na askari kata na vikundi shirikishi, kwa ujumla wananchi wamaeneo haya wamejipanga vizuri kwa sasa’Miaka kumi iliyopita, juhudi kubwa zilifanywa kukamata wahalifu na kutoa elimu kwa umma kukabiliana na mauaji haya ya kikatili. Mathalani mwanzoni mwa mwaka 2015, zaidi ya waganga wa jadi 200 walikamatwa, wakihusishwa na mauaji haya ya kinyama. Kuibuka kwa matukio haya mapya kunaashiria uhitaji tena kwa jamii na vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi na usalama wa watu wenye ualbino Tanzania.Matukio ya namna hiyo pia yamekuwa yakiripotiwa katika nchi Jirani ya Malawi.
  2. Saa 7 zilizopitaZaidi ya mahujaji 500 wapoteza maisha kutokana na joto kaliHujaji akijaribu kupoza joto kwa mtoto wake wa kiume huko MakkaTakribani mahujaji 577 wa mataifa tofauti walikufa walipokuwa wakitekeleza ibada ya Hija ya mwaka huu, wengi wao kutokana na sababu zinazohusiana na joto kali, kulingana na shirika la habari la Ufaransa Agence France-Presse.Shirika hilo limewanukuu wanadiplomasia wa Kiarabu kwamba takribani mahujaji 323 wa Misri walifariki walipokuwa wakitekeleza ibada ya Hijja huko Makka.Mmoja wa wanadiplomasia wanaoratibu mawasiliano ya nchi zao alisema kuwa “wote walikufa kutokana na joto” isipokuwa mtu mmoja ambaye alijeruhiwa vibaya wakati wa mkanyagano mdogo kati ya umati wa mahujaji, na kuongeza kuwa idadi hiyo ilitoka katika chumba cha maiti cha hospitali ya Al- Muaisem huko Makka.Mapema siku ya Jumanne, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ilisema kuwa Cairo inashirikiana na mamlaka za Saudia katika kuwatafuta mahujaji wa Misri waliotoweka katika msimu wa Hija.Ubalozi mdogo wa Jordan wa Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Wageni ulitangaza kuwa imetoa vibali 41 vya maziko kwa mahujaji wa Jordan kuzikwa Makka kulingana na matakwa ya familia zao, ikionesha kwamba “hawakuwa sehemu ya ujumbe rasmi wa Hajj wa Jordan. ”Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia imesema katika taarifa yake, “Idadi ya mahujaji wa Tunisia waliofariki katika msimu wa Hijja imefikia watu 35 hadi sasa, wakiwemo mahujaji 5 waliofika kupitia mfumo wa bahati nasibu, ambao serikali inaupitisha kuchagua mahujaji kwa kila mwaka, na 30 waliofika kwa ziara, au visa ya Umrah.” ” Wizara ya Mambo ya Nje imethibitisha kuwa ujumbe wa kidiplomasia huko Riyadh na Ubalozi mdogo wa Jeddah unashirikiana na mamlaka husika za Saudia na familia za mahujaji kukamilisha taratibu zinazohusiana na maziko yao.Mamlaka za Saudia ziliripoti kuwatibu zaidi ya mahujaji 2,000 wanaosumbuliwa na uchovu kutokana na joto, lakini hawajatoa maelezo zaidi ya idadi hiyo tangu Jumapili na hawajatoa taarifa kuhusu vifo.Unaweza kusoma;Nini ipi hatima ya mahujaji wanaofariki wakati wanapokwenda hijja Makka?
  3. Saa 7 zilizopitaMkutano wa Putin na Kim: Tunachojua kufikia sasa.CHANZO CHA PICHA,SPUTNIK/KREMLIN POOL/EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCKKumekuwa na shamrashamra na nderemo mjini Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini, kuadhimisha ziara ya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin.Yeye na mwenzake wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, wamekuwa wakitaka kuonyesha kuwa pande hizo mbili zina uhusiano mkubwa.Ziara hiyo bado haijaisha lakini huu hapa ni mukhtasari wa matukio muhimu:
    • Kiongozi huyo wa Urusi alikaribishwa katika sherehe rasmi iliyoshirikisha watoto wanaoimba, pamoja na gwaride la kijeshi.
    • Zawadi zilitolewa, huku Kim akiripotiwa kupokea gari lingine la kifahari.
    • Wawili hao walifanya biashara fulani ingawa – walizungumza kwa saa mbili, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.
    • Kisha walitia saini makubaliano ya kusaidiana katika tukio la “uchokozi” dhidi ya nchi yoyote ile – maneno ambayo mwandishi wetu wa masuala ya kidiplomasia Paul Adams anayaelezea kama “tata”.
  4. Saa 7 zilizopitaWanajeshi wa Ufilipino wapambana na walinzi wa pwani ya China ‘kwa mikono mitupu’Walinzi wa pwani wa China wakiwa doria katika Bahari ya China KusiniCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESWanajeshi wa Ufilipino walitumia “mikono mitupu” kupigana na walinzi wa pwani ya China waliokuwa na panga, mikuki na visu katika eneo linalozozaniwa la Bahari ya China Kusini, kamanda mkuu wa jeshi la nchi hiyo amesema.Jenerali Romeo Brawner alishutumu meli za China kwa kushambulia boti za Ufilipino, kisha kuzipanda na kukamata silaha.Mwanajeshi mmoja wa Ufilipino alipoteza kidole gumba wakati chombo chake kilipogongwa, jenerali huyo alisema.China ilikanusha madai hayo dhidi ya wafanyakazi wake ikisema “wamezuiliwa”.Mapigano hayo yalitokea wakati jeshi la wanamaji la Ufilipino na walinzi wa pwani walipokuwa wakipeleka vifaa kwa wanajeshi wa Ufilipino waliokuwa kwenye eneo la Second Thomas Shoal.Jenerali Brawner alisema wanajeshi waliripoti kuwaona walinzi wa pwani ya China wakiwa na visu, mikuki na mbao. Alisema ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Ufilipino kuona Wachina wakitumia aina hii ya silaha katika eneo hilo.”Tuliona kwenye video jinsi Wachina walivyotishia wafanyakazi wetu kwa kuwaelekezea visu,” Jenerali Brawner alisema.Wafanyakazi wa China pia walikamata bunduki kadhaa na kuharibu vitu, ikiwa ni pamoja na mota na kutoboa vyombo vya hewa.Tukio hilo, aliongeza, lilifikia hatua ya kuwa “uharamia”. “Hawana haki au mamlaka ya kisheria ya kuteka nyara shughuli zetu na kuharibu meli za Ufilipino zinazofanya kazi ndani ya eneo letu la kipekee la kiuchumi,” Jenerali Brawner aliwaambia waandishi wa habari.Lakini Beijing ilitupilia mbali madai hayo, ikisema wafanyakazi wake walikuwa na lengo la kuzuia “usafirishaji haramu” wa vifaa.”Hakuna hatua za moja kwa moja” zilizochukuliwa dhidi ya wanajeshi wa Ufilipino, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lin Jian aliwaambia waandishi wa habari mjini Beijing.”Hatua za utekelezaji wa sheria zilizochukuliwa na Walinzi wa Pwani ya China kwenye eneo hilo zilikuwa za kitaalamu na zilizuiliwa,” aliongeza.Katika taarifa yake ya awali, walinzi wa pwani wa China walisema Ufilipino “ilihusika kikamilifu” na tukio hilo, kwani wanajeshi “walipuuza maonyo ya mara kwa mara ya China … na kukaribia kwa hatari meli ya China iliyokuwa ikisafiri kwa kawaida kwa njia isiyo ya kitaalamu, na kusababisha mgongano. ”.
  5. Saa 7 zilizopitaMaandamano ya kupinga Muswada wa fedha yafanyika MombasaMaandamano ya #OccupyParliament dhidi ya muswada wa fedha wa 2024/2025 yaliingia katika siku yake ya pili baada ya wakaazi wa Kaunti ya Mombasa Jumatano kuandamana mitaani kupinga Muswada huo wa Fedha ambao unajadiliwa Bungeni.Wakiwa wamejihami kwa mabango, huku wakiimba nyimbo, Wakenya hao ambao hawajaridhishwa na mapendekezo ya muswada huo walitembea katika barabara za kaunti hiyo, wakiwataka Wabunge kukataa mswada huo tata. Wakaazi hao walikutana kuanzia saa mbili asubuhi katika maeneo tofauti mjini humo kabla ya kuanza maandamno hayo.Licha ya hali ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo, wakazi hao walitembea barabarani na kuwataka wabunge kuzingatia matakwa yao.Maafisa wa polisi, walitumwa kukabiliana na waandamanaji hao na walitumia vitoa machozi kujaribu kuwatawanya.Siku ya Jumanne, Wakenya waliochoshwa na muswada huo wa fedha walikabiliana na polisi katikati ya jiji la Nairobi walipokuwa wakiandamana kupinga mswada huo.Saa chache, maafisa wa polisi walitumia vitoa machozi na kufanikiwa kuwakamata baadhi ya waandamanaji ambao waliachiliwa baadaye.Kulingana na mabango yaliyosambazwa mtandaoni, maandamano ya #OccupyParliament yataendelea siku ya Alhamisi katika kaunti zingine kama vile Meru, Eldoret, Laikipia, Nakuru na Nyeri. Wabunge kwa sasa wanajadili muswada huo kwa awamu ya pili bungeni kabla ya kupiga kura ya kuupinga au kuunga mkono siku ya Alhamisi.
  6. Saa 8 zilizopitaBajeti ya EU yapendekeza msaada kwa Ukraine wa zaidi ya euro bilioni 15BenderaCHANZO CHA PICHA,STR/NURPHOTOTume ya Ulaya imependekeza rasimu ya bajeti ya Umoja wa Ulaya kwa mwaka wa 2025, ikitoa msaada kwa Ukraine kwa kiasi cha zaidi ya euro bilioni 15, ambayo “itatoa msaada thabiti kwa Ukraine.”Tume ya Ulaya imependekeza rasimu ya bajeti ya EU kwa mwaka 2025 kwa kiasi cha euro bilioni 199.7, ikiwa ni pamoja na msaada kwa Ukraine.Tume ilisema katika taarifa kwamba “€ 4.3 bilioni zitapatikana kwa njia ya ruzuku chini ya Mfuko wa Ukraine, inayosaidiwa na € 10.9 bilioni katika mikopo.” Baraza la EU mwezi Machi lilikubali kanuni za msingi za bajeti ya Umoja wa Ulaya ya 2025, ambayo hutoa “msaada endelevu kwa Ukraine.” “Baraza linathibitisha kwamba EU inasalia kujitolea, pamoja na washirika, kutoa usaidizi wa kifedha kwa Ukraine kwa muda mrefu iwezekanavyo.” Baraza la EU lilisema katika taarifa.Unaweza kusoma;Vita vya Ukraine: Je, Ukraine itamudu bila msaada wa Marekani?Je, kutumia silaha za Magharibi dhidi ya Urusi kutasaidia Ukraine kuvibadili vita?
  7. Saa 9 zilizopitaRamaphosa aapishwa kuwa rais wa Afrika Kusini kwa muhula wa piliCyril RamaphosaCHANZO CHA PICHA,EPACyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameapishwa kwa muhula wa pili wa urais, licha ya kushindwa kupata wabunge wengi katika uchaguzi wa mwezi uliopita wa chama chake cha African National Congress (ANC).Wabunge walimchagua tena kuwa rais wiki iliyopita kufuatia makubaliano kati ya ANC, mpinzani wake wa muda mrefu wa Democratic Alliance (DA) na vyama vingine kuunda serikali ya mseto.Chama cha ANC, ambacho kimetawala tangu mwisho wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994, kilipoteza wingi wa viti vya ubunge kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa Mei 29 kutotoa mshindi wa moja kwa moja.Viongozi wengi wakiwemo wakuu kadhaa wa mataifa ya Afrika wanahudhuria sherehe hizo.”Ninaapa nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Afrika Kusini… nitatii, nitazingatia katiba na sheria nyingine zote za jamhuri,” Bw Ramaphosa alisema.Kiapo hicho kilisimamiwa na Jaji Mkuu Raymond Zondo.Baada ya Bw Ramaphosa kula kiapo, bendi iliimba wimbo wa taifa uliofuatwa na salamu ya bunduki 21 na kuruka kwa helikopta za jeshi, kabla ya kutoa hotuba yake ya kuapishwa.Chama cha uMkhonto weSizwe (MK) kilichoundwa miezi sita iliyopita na Rais wa zamani Jacob Zuma kinasema maafisa wake hawatashiriki katika uapisho wa “kifahari”.Chama hicho, ambacho kilipata 15% ya kura na kupata viti 58 vya ubunge, pia kilisusia kikao cha kwanza cha bunge Ijumaa iliyopita.
  8. Saa 9 zilizopitaHabari za hivi punde,Mkataba na Korea Kaskazini utatulinda sisi sote dhidi ya uchokozi – Putin.CHANZO CHA PICHA,SPUTNIK/KREMLIN POOL/EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCKMaelezo ya picha,Rais Vladmir Putin na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong unBaadhi ya maelezo yanaanza kujitokeza kupitia mashirika ya habari ya Urusi kuhusu kile kilichopo katika mikataba iliyotiwa saini na Urusi na Korea Kaskazini mjini Pyongyang.La kushangaza zaidi, Rais Vladimir Putin amenukuliwa akisema “hati ya mafanikio” inajumuisha kifungu cha ulinzi wa pande zote: “Mkataba wa ushirikiano wa kina uliotiwa saini unatoa pamoja na mambo mengine, usaidizi wa pande zote katika tukio la uchokozi dhidi ya mmoja wa wahusika.”Mashirika hayo pia yanamnukuu Bw Putin akisema Korea Kaskazini ina haki ya kujilinda na kwamba huenda Urusi na Korea Kaskazini zikashirikiana kijeshi, ingawa makubaliano hayo ni “ya kiulinzi na ya amani”.Mkataba huu wa ulinzi wa pande zote unaweza kuwa na athari kwa vita vya Urusi huko Ukraine.Je, Urusi inaweza kuhusisha Korea Kaskazini kwa ujumla zaidi katika mzozo huo, ikitoa mfano wa mashambulizi ya Ukraine dhidi ya miji ya Urusi kama vile Belgorod au maeneo yaliyotwaliwa na Ukraine ambayo sasa inayachukulia kuwa ni eneo la Urusi.Maswali pia sasa yataulizwa kuhusu nini Urusi inaweza kufanya baada ya kuipunguzia vikwazo Korea Kaskazini.Maelezo yanayogonga vichwa vya habari zaidi, ni kwamba Kremlin inasema hati zingine zilizotiwa saini ni pamoja na makubaliano ya ujenzi wa daraja la mpakani na ushirikiano juu ya afya, elimu ya matibabu na sayansi.
  9. Saa 9 zilizopitaJeshi la Israel “laidhinisha mipango ya operesheni ya kuishambulia Lebanon”Hezbollah imekuwa ikijibizana kwa makombora kuvuka mpaka na Israel tangu kuzuka kwa vita vya Gaza miezi kadhaa iliyopita.CHANZO CHA PICHA,AFPJeshi la Israel lilitangaza Jumanne kwamba limeidhinisha “mipango ya uendeshaji” kwa ajili ya mashambulizi dhidi ya Lebanon, huku matamshi kati ya Israel na Hezbollah yakiongezeka ambayo yanaweza kusababisha vita.Jeshi lilisema: “Kama sehemu ya tathmini ya hali hiyo, mipango ya operesheni ya kushambulia Lebanon iliidhinishwa, na maamuzi yakafanywa kuhusu kuendelea kuinua utayari wa vikosi .”Siku ya Jumanne, Hezbollah ilichapisha video ya dakika tisa na sekunde 31 ya kile ilichosema ni picha zilizokusanywa kutoka kwenye ndege yake ya uchunguzi wa maeneo nchini Israel, pamoja na bahari na bandari na viwanja vya ndege vya mji wa Haifa. Haifa iko kilomita 27 kutoka mpaka wa Lebanon.Wametuma ndege za uchunguzi na ndege zisizo na rubani kwa Israel katika kipindi cha miezi minane iliyopita, huku kikirushiana risasi na jeshi la Israel sambamba na vita vya Gaza.Mjini Washington, Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) ilisema kuwa Marekani haitaki vita vipana zaidi vya kikanda katika Mashariki ya Kati.Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema, takriban wiki moja iliyopita, “Israel haitakaa kizembe wakati Hezbollah inashambulia ardhi ya kaskazini mwa nchi,” akisisitiza utayari wa Tel Aviv “kurejesha usalama” kwenye mpaka na Lebanon.Unaweza kusoma;Je Iran itajiunga na Hezbollah katika vita na Israel?Israel-Hezbollah: Kazi ya kulinda mpaka hatari zaidi Mashariki ya Kati
  10. 19 Juni 2024Kukutana kwa Putin na Kim ni ‘habari mbaya kwa ulimwengu wote’: Mchambuzi wa zamani wa CIAKim Jong Un akimkaribisha Putin mjini PyongyangCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESKama ambavyo tumekuwa tukiripoti, Marekani imeishutumu Urusi kwa kugeukia Korea Kaskazini kwa ajili ya zana za kijeshi wakati wa vita vya Moscow nchini Ukraine.Kwa mujibu wa mchambuzi mmoja wa zamani wa CIA, ziara ya Putin huko Pyongyang inaangazia jinsi “mataifa” mawili yanavyoweza kuimarisha uhusiano wao licha ya kutengwa na jumuiya ya kimataifa.”Nadhani inasikitisha sana kwamba Putin analazimika kutegemea nchi ya 198 kiuchumi duniani kusaidia juhudi zake za vita,” Sue Mi Terry aliiambia BBC News.”Ni habari mbaya kwa ulimwengu wote,” Terry aliendelea, akionesha wasiwasi kwamba ushirikiano ulikuwa unaruhusu Korea Kaskazini kujaribu silaha zake kwa ufanisi.Lakini Terry, ambaye sasa ni mkurugenzi katika kituo cha washauri, Wilson Center, alisema ushirikiano huo unaweza kudumu mradi tu Urusi imvamie jirani yake. Inaweza kuwa zaidi ya “ndoa ya urahisi kwa wakati huu”, alisema.Unaweza kusoma;Sababu 3 za Putin na Kim Jong-un za kutaka kuwa marafikiPutin aonya kuwa Urusi inaweza kutoa silaha za kuyashambulia mataifa ya Magharibi
  11. 19 Juni 2024Moto mbaya wazuka katika ghala la silaha nchini ChadMlipuko mbaya katika ghala la silaha za kijeshi nchini ChadIdadi isiyojulikana ya watu wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya moto mkubwa kuzuka katika ghala la kuhifadhia silaha nchini Chad na kusababisha milipuko mikubwa, mawaziri wakuu wa serikali wamesema.Waziri wa Mambo ya Nje Abderaman Koulamallah alisema moto huo ulitokea katika ghala la kijeshi katika eneo la Goudji mjini N’Djamena.Rais Mahamat Idriss Déby ametuma salamu za rambirambi kwa waathiriwa na familia zao, bila kutaja idadi ya majeruhi.Picha za video, ambazo hazijathibitishwa na BBC, zinaonesha milipuko angani usiku.Mashuhuda walisema walisikia milipuko kwa mbali. Ghala la silaha huko Goudji ndilo ghala kuu la silaha la nchi hiyo na liko kaskazini mwa mji karibu na makao makuu ya kijeshi, kambi ya jeshi la Ufaransa na uwanja wa ndege.Waandishi wa habari wanaofanya kazi katika shirika la habari la AFP walisema moto huo ulisababisha silaha kuruka angani.Kulikuwa na “milipuko ya risasi za kila aina”, afisa wa Ufaransa, ambaye aliomba kutotajwa jina, pia aliliambia shirika hilo.Mkazi mmoja aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba aliwaona watu watatu waliojeruhiwa barabarani, huku mwingine akisema jirani yake alipoteza maisha. “Milipuko mikubwa ilituamsha,” Moustapha Adoum Mahamat alisema. “Nyumba yetu ilikuwa ikitetemeka kana kwamba kuna mtu anatupiga risasi. Kisha tukaona moto mkubwa kwenye kambi ya kijeshi na moshi na vitu vikilipuka angani,” alisema.”Tuliweza kuona silaha zikiruka juu yetu.” Bw Koulamallah, waziri wa mambo ya nje na msemaji wa serikali, aliwataka wananchi kuwa watulivu baada ya milipuko hiyo.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, na rais ameahidi kufanyika kwa uchunguzi kuhusu tukio hilo.
  12. 19 Juni 2024Mwanajeshi wa Marekani afungwa jela kwa takribani miaka minne nchini UrusiSgt.Gordon BlackCHANZO CHA PICHA,REUTERSMahakama ya Urusi imemhukumu mwanajeshi wa Marekani kifungo cha miaka mitatu na miezi tisa jela kwa tuhuma za wizi na kutishia kumuua mpenzi wake, mashirika ya habari ya serikali yameripoti.Sajenti Gordon Black alihukumiwa na mahakama ya Vladivostok nchini Urusi na atatumikia muda wake gerezaniSgt Black, ambaye alikamatwa mwezi Mei, alikana mashtaka ya tishio la mauaji lakini alikiri kwamba alikuwa na hatia “sehemu” ya kumuibia rubles 10,000 ($116; £89) .Atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo, mashirika ya habari ya serikali yalisema.Waendesha mashtaka walikuwa wametaka afungwe jela miaka minne na miezi minane, huku utetezi wake ukitaka aachiliwe huru.Maafisa wa Marekani walisema Sgt Black mwenye miaka 34, alikutana na mpenzi wake huko Korea Kusini.Alijiandikisha kama askari mwaka wa 2008 na alitumwa Iraqi mwaka wa 2009 na Afghanistan mwaka wa 2013.Hivi karibuni alitumwa kwenye Jeshi la Nane, Jeshi la Marekani la Korea huko Camp Humphreys.Jeshi la Marekani lilisema Sgt Black hakuomba kibali rasmi na idara ya ulinzi haikuidhinisha kusafiri kwake kwenda Urusi au China, ambako alikuwa amesafiri kwanza alipokuwa akirejea kutoka Korea Kusini.Hakuna ushahidi kwamba alikusudia kubaki Urusi.Urusi inawashikilia Wamarekani wengine gerezani. Mwandishi wa Wall Street Journal Evan Gershkovich ambaye amekuwa gerezani tangu Machi 2023, wakati Mwanajeshi wa zamani wa Marekani, Paul Whelan alihukumiwa miaka 16 jela mnamo 2020.Alsu Kurmasheva, mhariri wa Urusi na Marekani wa Radio Free Europe/Radio Liberty inayofadhiliwa na Marekani, amekuwa akishikiliwa tangu Oktoba mwaka jana na anaweza kufungwa jela miaka 10 kwa tuhuma za kueneza habari za uongo kuhusu jeshi la Urusi.Mahakama siku ya Jumanne ilikataa kumwachilia Bi Kurmasheva kabla ya kesi yake kusikilizwa.Watu wote watatu wameendelea kusisitiza kuwa hawana hatia, na serikali ya Marekani inasema mashtaka dhidi yao hayana msingi.
  13. 19 Juni 2024Ramaphosa kuapishwa kuiongoza Afrika Kusini kwa muhula wa piliGetty ImagesCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESMaelezo ya picha,Cyril Ramaphosa anatarajiwa kutangaza ajenda ya kuokoa uchumi unaodororaCyril Ramaphosa anatazamiwa kuapishwa kama rais wa muhula wa pili nchini Afrika Kusini, licha ya kushindwa kupata wabunge wengi katika uchaguzi wa mwezi uliopita wa chama chake cha African National Congress (ANC).Wabunge walimchagua tena kusalia kama rais wiki iliyopita kufuatia makubaliano ya kuunda serikali ya mseto kati ya ANC, mpinzani wake wa muda mrefu wa Democratic Alliance (DA) na vyama vingine.Chama cha ANC, ambacho kimetawala tangu mwisho wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994, kilipoteza wingi wa viti kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa Mei 29 kutofanikiwa kupata ushindi wa moja kwa moja.Wakuu wengi wa nchi na watu mashuhuri kutoka kote ulimwenguni wanatarajiwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa inayofanyika katika mji mkuu, Pretoria.Ofisi ya Rais imeorodhesha baadhi ya nchi zitakazo “wakilishwa kwa kiwango cha juu” katika uzinduzi huo, zikiwemo Angola, Uganda, Msumbiji, China, Misri, Taifa la Palestina na Cuba.Sherehe hizo, katika siku ambayo ofisi ya rais inasema ni siku ya kawaida ya kazi, itajumuisha maonyesho ya muziki na kisanii, salamu ya bunduki 21, ndege za kijeshi na maandamano yaliyopita na vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo.Chama cha uMkhonto weSizwe (MK) kilichoundwa miezi sita iliyopita na Rais wa zamani Jacob Zuma kimesema maafisa wake hawatashiriki katika hafla ya “kifahari”.Chama hicho, ambacho kilipata asilimia 15 ya kura na kupata viti 58 vya ubunge, pia kilisusia kikao cha kwanza cha bunge Ijumaa iliyopita.Bw Ramaphosa amesalia na kiti cha urais ingawa ANC ilipoteza asilimia 17 ya kura na viti 70 bungeni.#Amepata kiti cha urais kupitia mpango wa kugawana madaraka na DA inayounga mkono biashara, mpinzani wa kihistoria, na vyama vingine.ANC ilipata 40% ya kura, huku DA ikishika nafasi ya pili kwa kupata 22%.Muungano huo ni kuelekea kwenye kituo cha kisiasa, kwa sababu vyama vya mrengo wa kushoto vya ANC na vyama vilivyojitenga na wafuasi wengi vilikataa mwaliko wa kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa.Bw Ramaphosa anatarajiwa kuteua baraza la mawaziri punde tu baada ya kuapishwa, ambalo litajumuisha washirika wake wapya wa muungano – DA na vyama vingine vitatu vidogo. Kwa pamoja, muungano huo unachukua asilimia 68 ya viti bungeni.Rais pia anatarajiwa kutangaza ajenda ya kuokoa uchumi unaodorora.Chini ya utawala wake, ukuaji wa kiuchumi umeendelea kudorora huku kukiwa na kukatwa kwa umeme, kuongezeka kwa uhalifu na ukosefu wa ajira.Bw Ramaphosa alikua rais kwa mara ya kwanza 2018 wakati mtangulizi wake, Bw Zuma, alipolazimika kujiuzulu kwa sababu ya madai ya ufisadi – ambayo aliyakanusha.Unaweza kusoma;Kwa nini kuporomoka kwa ANC ni ishara mbaya kwa vyama vya ukombozi Afrika?ANC chaelekea kugawana madaraka baada ya kushindwa katika uchaguzi
  14. 19 Juni 2024Kwa picha: Ziara ya Putin Korea kaskaziniGwaride kubwa la barabarani na ngoma zilizofanyika kwa viongoziTumeshuhudia picha za viongozi hao wawili wakipita mitaani kwenye gari la wazi.Hiyo ilifuatia takriban dakika 10 za vikundi tofauti vilivyopangwa kwa wingi vikicheza densi na nyimbo, pamoja na kundi la kijeshi lililotoa salamu ya bunduki 21.Putin na mwenyeji wake pia walifanya mazungumzo ya ana kwa ana: Hizi ni baadhi ya picha za matukio ya ziara ya Putin nchini Korea Kaskazini:gCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGEShCHANZO CHA PICHA,RIAhCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGEShCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESfCHANZO CHA PICHA,POOLhCHANZO CHA PICHA,RIA KREMLIN POOLMaelezo ya picha,Putin akifanya mazungumzo na mwenyeji wake Kim
  15. 19 Juni 2024Kim asema Korea Kaskazini ‘inaunga mkono kikamilifu operesheni ya Urusi nchini Ukraine’Tunapatavidokezovya mkutano kati ya Putin na Kim, ambapo Kim alikuwa amedai hapo awali kuwa nchi zote mbili zinaingia katika kipindi cha “mafanikio mapya”.Kim pia alisema Korea Kaskazini inakusudia kuimarisha “ushirikiano wake wa kimkakati na Urusi”, kulingana na ripoti ya shirika la Urusi la Interfax. Kim pia aliongeza kuwa anaunga mkono kikamilifu “operesheni ya kijeshi” ya Urusi nchini Ukraine, shirika hilo lilisema
  16. 19 Juni 2024Uvamizi wa Ukraine ulibadilisha mtazamo wa Putin kwa Korea Kaskazini – wachambuzijCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESKorea Kaskazini mara nyingi huonekana kama taifa, lililofungwa lililoko mbali na ulimwengu. Lakini kwa miongo kadhaa limekuwa na uhusiano wa kina, ingawa wa misukosuko na Urusi na Uchina.Uhusiano wa Korea Kaskazini na Urusi ulikuwa umedorora katika miaka ya tangu kuanguka kwa Muungano wa Usovieti, Jean Leeanayefuatiliwa kwa karibu masuala ya Korea Kaskazini amekiambia kipindi cha podcast cha The Global Story.Pyongyang imekuwa “karibu tegemezi kabisa” kwa Uchina kwa 90% ya biashara yake katika miongo ya hivi karibuni, anasema.Lakini uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umebadilisha mtazamo wa Putin kwa Korea Kaskazini.Mwandishi wa Seoul wa gazeti la Financial Times Christian Davies, anasema, “Korea Kaskazini haifanyi mambo mengi vizuri. Lakini inaweza kutengeneza silaha, na kuziunda kwa kiwango kikubwa na wanavichukulia vita kwa uzito mkubwa.”China itakuwa ikitazama kwa makini maendeleo kati ya Kim na Putin, Lee anaongeza.Unaweza kusoma:Sababu 3 za Putin na Kim Jong-un za kutaka kuwa marafikiKwanini kuna wasiwasi kwamba Urusi inatumia makombora ya Korea Kaskazini nchini Ukraine?
  17. 19 Juni 2024Justin Timberlake akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewagCHANZO CHA PICHA,SAG HARBOR POLICE DEPARTMENMwimbaji Justin Timberlake alikamatwa mjini New York kwa kuendesha gari akiwa amelewa, maafisa wa eneo hilo wameiambia BBC.Nyota huyo wa pop alikamatwa na kushtakiwa rasmi Jumanne asubuhi, Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ya Suffolk ilisema katika taarifa yake.Timberlake alikuwa Sag Harbour, kijiji tajiri huko Hamptons, mahali maarufu pa majira ya kiangazi kwa watu mashuhuri.Aliachiliwa bila dhamana baada ya kushtakiwa rasmi, Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ya Suffolk ilisema.BBC imewasiliana na wakili wa Timberlake kwa maoni yake.Timberlake alikamatwa baada ya saa sita usiku polisi walipomvuta kutoka kwa gari lake la kijivu aina ya BMW kwa kuendesha gari licha ya ishara ya kusimama na kushindwa kukaa upande wa kulia wa barabara, kulingana na hati ya mashtaka.Wakati maafisa walipomsimamisha, macho ya Timberlake yalikuwa “mekundu” na “harufu kali ya kinywaji chenye kileo ilikuwa ikitoka kwenye pumzi yake”, hati ya mashtaka ilisema.Alikuwa akizungumza kwa mwenendo wa pole pole na alifanya vibaya katika majaribio ya kama yuko sawa kwa matumizi ya kileo, maafisa walisema.Pia alikataa kupumua kwenye kifaa cha kuthibitisha kama amekunya kileo, kulingana na hati ya mashtaka.”Nilikuwa na Martini na niliwafuata marafiki zangu nyumbani,” inadaiwa Timberlake alimwambia afisa aliyemsimamisha, kulingana na mshirika wa BBC wa Marekani CBS News.Anatarajiwa kufika katika mahakama ya Sag Harbour tarehe 26 Julai.Wakili wake, Edward Burke Jr., aliiambia BBC mshirika wa habari wa Marekani CBS Jumanne jioni kwamba “atamtetea mteja wake kwa nguvu zote.Timberlake, 43, alitarajiwa kuanza ziara ya kimataifa ya albamu yake ya sita, Everything I Thought It Was.
  18. 19 Juni 2024TikTok yakabiliwa na madai mapya ya kukiuka faragha ya watotodCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESTume ya Biashara ya Marekani imepeleka malalamiko dhidi ya TikTok na kampuni mama ya Uchina ya ByteDance kuhusu ukiukaji unaowezekana wa faragha ya watoto kwa Wizara ya Sheria.Tume hiyo inasema uchunguzi wake “umefichua sababu ya kuamini” kwamba makampuni “yanakiuka au yanakaribia kukiuka sheria”.Katika taarifa kwa BBC News, msemaji wa TikTok alisema wamesikitishwa na uamuzi huo.Kesi hiyo haihusiani na sheria iliyopitishwa mapema mwaka huu ya kupiga marufuku TikTok nchini Marekani ikiwa ByteDance haitauza programu hiyo.Tume ya Biashara ya Marekani pia ilisema huwa haitangazi kwamba imepeleka malalamiko kwa Wizara ya Sheria lakini katika hali hii ilihisi kufanya hivyo ni kwa manufaa ya umma.Kujibu, msemaji wa TikTok alisema kampuni hiyo haikubaliani na madai hayo na kwamba “imekuwa ikifanya kazi na Tume ya Biashara ya Marekani kwa zaidi ya mwaka mmoja kushughulikia wasiwasi wake.””Tumesikitishwa na shirika hilo kuanzisha kesi badala ya kuendelea kufanya kazi nasi kupata suluhisho la kuridhisha,” waliongeza.Tangazo la tume hiyo linaongeza shinikizo linalozidi kuongezeka la TikTok nchini Marekani.Mnamo Aprili, Rais Joe Biden alitia saini kuwa sheria mswada ulioipa ByteDance muda unaozidi mwaka mmoja hivi kuuza programu au kupigwa marufuku nchini humo.Hiyo ina maana kwamba tarehe ya mwisho huenda ikafika muda fulani mwaka wa 2025, baada ya mshindi wa uchaguzi wa urais wa 2024 kuchukua madaraka.Sheria ilianzishwa ili kushughulikia wasiwasi kwamba TikTok inaweza kushirikisha data ya mtumiaji na mamlaka ya Uchina – madai ambayo kampuni imekanusha.Mnamo mwezi Mei, TikTok iliwasilisha kesi kwa lengo la kuzuia sheria hiyo, ikisema kuwa ni “uingiliaji wa ajabu wa haki za uhuru wa kujieleza” wa kampuni hiyo na watumiaji wake milioni 170 wa Marekani.
  19. 19 Juni 2024Biden ajikuta pabaya katika suala la uhamiajigCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESMaelezo ya picha,Uhamiaji na mpaka wa Marekani na Mexico unatajwa na Wamarekani wengi kuwa wasiwasi wao mkuu wa uchaguzi.Rais wa Marekani Joe Biden ameapa “kutoingiza siasa” katika suala la mpaka wa kusini na uhamiaji, jambo ambalo linaweza kuwa changamoto wakati Marekani ikikabiliana na uchaguzi wa rais wa Novemba.Maoni ya Bw Biden yanawadia kwa kile alichokiita “siku njema” ambapo alitangaza amri ya utendaji inayolenga kulinda mamia ya maelfu ya wenzi wa wale wasio na vibali vya raia wa Marekani kutokana na kurejeshwa makwao na kuwaruhusu kufanya kazi Marekani.Matendo yake, hata hivyo, yameleta ukosoaji kutoka kwa chama cha Republican na baadhi ya Democrats wenzake vile vile, na kumlazimu rais kukabiliana nayo yote ili kuwaridhisha.Kura za maoni zinaonyesha kuwa wengi wa wapiga kura wanachukulia uhamiaji kama mojawapo ya matatizo muhimu zaidi yanayoikabili nchi.hCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESMaelezo ya picha,Bw Biden amekosolewa kuhusu uhamiaji kutoka upande wa kushoto wa chama chake, ikiwa ni pamoja na mbunge wa Washington Pramila Jayapal.Hatua hiyo mpya ya kiutendaji iliyotangazwa na serikali siku ya Jumanne imesifiwa sana na wanaharakati wa uhamiaji na pia Democrats, ambao wengi wao wameisifu kama mpango muhimu zaidi kwa wahamiaji wasio na vibali ambao tayari wako nchini Marekani tangu utawala wa Obama kutangaza sheria ya kuchelewesha kwa muda kufukuzwa kwa watu wasio na vibali ambao walikuja Marekani kama watoto mwaka wa 2012.Lakini hatua ya hivi punde ni kinyume kabisa na agizo lake kubwa la uhamiaji lililotolewa mapema mwezi Juni, ambalo linawaruhusu maafisa kuwaondoa haraka wahamiaji wanaoingia Marekani kinyume cha sheria bila kushughulikia maombi yao ya hifadhi.Hatua hizo za utendaji zilizotengana kwa muda wa wiki mbili tu zimeangazia changamoto ambayo Bwana Biden anakumbana nayo katika suala la uhamiaji.”Biden daima hujikuta katika hali ngumu,” mtaalamu wa mikakati wa chama cha Republican Doug Heye aliiambia BBC. “Lolote analofanya litapata upinzani. Huu ni mfano kamili
  20. 19 Juni 2024Habari za hivi punde,Putin na Kim wanawasili katika viwanja vya Kim Il Sung kwa ajili ya sherehe za makaribishohCHANZO CHA PICHA,KREMLINRais Vladimir Putin wa Urusi na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamewasili katika uwanja wa Pyongyang – uwanja wa Kim ll Sung, uliopewa jina la kiongozi mwanzilishi wa Korea Kaskazini, linasema shirika la serikali la Urusi RIA.Shirika hilo limeongeza kuwa “sherehe kuu ya kuwakaribisha kwa heshima ya ziara ya [Putin] imeanza”.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd|2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment