Ujasiri wa Kumaliza-John Stephen Akwari.

Akiwa ameshakimbia Umbali wa kilomita 30 Kati ya Kilomita 42 za mashindano, alipata changamoto ya Kuumia Mguu. Badala ya KUACHA kabisa mashindano, yeye aliamua KUJILAZIMISHA kuendelea KUKIMBIA taratibu akiwa na MAUMIVU makali.

Hata angeishia njiani, kila mtu ANGEMWELEWA. Kama ambavyo wewe unajiambia “Kila Mtu Atanielewa”.

Hii ilikuwa ni kwenye mashindano ya Olimpiki ya majira ya joto yaliyofanyika nchini Mexico mwaka 1968.

Hatimaye alifanikiwa KUMALIZA, Ila ilikuwa ni baada ya saa moja tangu mashindano yalipoisha akiwa ni mmoja wa watu 17 waliofanikiwa kumaliza mbio hizo Kati ya 79 walioanza.

Alipofika kwenye Mstari wa kumaliza alipohojiwa na Waandishi kwa nini HAKUISHIA NJIANI alijibu-“Nchi yangu haijanituma zaidi ya maili 5,000 kuja KUANZA mbio bali kuja KUMALIZA MBIO”

Huyu ni John Stephen Akwari, Mtanzania anayetufundisha UJASIRI wa kupambana na MAISHA.

Hata kama leo Moyo Umevunjika, Unatoka MACHOZI au unavuja DAMU, Dhamiria kuwa UTAMALIZA MBIO ZAKO na HAUTAISHIA NJIANI.

Nakuombea MUNGU AKUPE NGUVU UMALIZE USIISHIE NJIANI.

HakiMiliki© Cantona Group Ltd|2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment