Vita vya mapenzi.

VITA VYA MAPENZI

Leo tuangalie vita vya mapenzi (The battle of love). Moyo wa binadamu huwa unawindwa. Ni target ya watu wengi sana. Moyo unawindwa, ama kwa mazuri au kwa mabaya.

Na kuna wengine watakwambia sababu ya kukuwinda na wengine hawatasema. Na hata wale waliokwambia wanaweza kuwa hawakusema ukweli.
Mapenzi yamewafanya baadhi ya watu wawe hodari.

Kuna watu ambao walipoanza tu mahusiano, mambo yao yakanyooka.

Lakini mapenzi hayo hayo, yamefanya watu wawe dhaifu sana. Yamefanya watu waanguke kabisa. Hata biashara zao zimekufa kabisa, sababu tu ya kuwa na mapenzi na mtu fulani.

Mapenzi ni upanga unaokata sehemu zote mbili.
Kuna mambo ambayo, unatakiwa uyatambue kabla hujampa mtu moyo wako. Kama unavyoona kwenye mpira wa miguu. Hasa pale, wakati kona inapigwa, kila mtu anagombania mpira. Basi ndio hivyo inavyokuwa kwenye moyo wako. Unagombaniwa.

Usipojua thamani ya moyo wako, utakuwa umepoteza thamani ya hatima ya maisha yako.

Kuna vitu vya kuchunguza kabla hujaingia kwenye mahusiano.

(i) Know your worth- usiwe cheap.

Usikubali kuwa mtu mrahisi. Si kila mtu anastahili kupewa moyo wako. Moyo una thamani kubwa. Maumivu ya moyo yanahusisha, sehemu kubwa ya maumivu ya maisha yako. Kila mtu unayempa upendo kwenye maisha yako, ukumbuke umempa moyo wako. Na ndio maana akiondoka unasikia maumivu. Na ndio maana usiwe cheap.

(ii) Usiseme ndio kwa kinywa wakati moyoni ni Hapana.

Usiruhusu kinywa chako, kiusaliti moyo wako. Wakati mwingine, mazingira yanaweza kukulazimisha kusema ndio, wakati ndani ya moyo ni hapana.

Utakapoesema hapana, leo utakuwa umejitoa kwenye kifungo kikubwa sana. Maana ukisema ndio utakuwa umempa mtu matumaini ambayo hayapo.

(iii) Usikimbizane wa watu waliokuzunguka

Sababu, kila mtu ameshaingia kwenye ndoa, basi na wewe uingie. Kama hauko tayari, usijipe presha kwa kuangalia majirani. Usikubali watu wakulazimishe kutembea njia ambayo hauko tayari kuipita. Bora uchelewe upate mtu aliye sahihi

(iv) Usikubali hisia zako ziharibu maisha yako

Kuna wakati sababu ya hisia, mtu anakubali kufanya vitu ambavyo vinakuja kumharibia maisha yake.

Anakubali kufanya vitu vinakuja kuharibu historia yake, na jina lake. Hisia zimeharibu destiny za watu wengi. Jipe muda kabla ya kufanya maumuzi. Pia, omba ushauri. Usijiamini peke yako. Moyo ni mdanganyifu, wakati mwingine moyo unaweza kukudanganya hata wewe mwenyewe. Tafuta mtu ambaye unaweza kujadiliana naye.

Kama ilivyoelezwa hapo juu. Vita ya mapenzi, imewafanya watu wafurahie maisha, na wengine imewafanya walie. Zingatie haya kama sehemu ya kuulinda moyo. Linda sana moyo wako kuliko chochote ukilindacho.

Tembea Mjini YouTube na Subscribe.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment