Hivi umewahi kujiuliza, kwa nini Messi anajulikana dunia nzima. Kuna wachezaji wangapi wa soka, lakini wanajulikana kwa wale tu wanaofuatilia mpira?
Kwa kawaida dunia huwa haiwashangilii watu wa chini wala watu wastani. Dunia huwa inawashangilia watu wa viwango vya juu. Watu ambao huwa wanafanya vitu vikubwa. Watu ambao ni exception. Siyo tu hata kwa watu, kitu chochote ambacho kimefanya kazi ya viwango vya juu. Hivi leo mji wa Dubai, umekuwa ukifanya mambo makubwa, kiasi ambacho ndio unawakilisha nchi ya UAE. Na ni mji mdogo tu.
Sisi huwa tunafanya nini kujitofautisha na wengine. Yaani tutoke kuwa kwenye watu wa chini, twende kwenye watu wa wastani, halafu tufike hatua za juu. Pale ambapo kazi zako zitajulikana na kuhitajika. Pale ambapo watu hata kama watakuwa hawakujui, lakini watakuwa wanakutangaza kwa mema. Watakuwa wanakutangaza kwa ushauri, na mazuri unayoyafanya.

Tafuta ujuzi, uelewa, umiliki, utaalamu ambao utakutofautisha na wengine. Wakitajwa watu kwenye eneo lako, wewe ndio unatokea pale juu. Kama ambavyo miaka ya karibuni kwenye mpira wa miguu wakitajwa wachezaji bora, Ronaldo na Messi ndio wanatokea pale juu. Yaani watu wanabishana kati ya hao wawili nani bora, ingawa kuna maelfu elfu ya wachezaji wengine.


Picha:CR7 na Messi
All Rights Reserved|©Cantona Group Ltd
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.