
Baada ya kifo cha Mkenya Joshua Cheruiyot Kirui kwenye Mlima Everest mnamo Mei 22, 2024, familia imefanya uamuzi mgumu wa kuacha mwili wake ubaki kwenye Mlimani.
Mwili wa mpandaji wa mlima kutoka Kenya, Cheruiyot Kirui, aliyefariki wakati akijaribu kufikia kilele cha Mlima Everest bila oksijeni, utabaki kwenye mlima huo mrefu zaidi duniani, kulingana na familia yake. Katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumatano, familia yake ilisema walifanya uamuzi mgumu baada ya mashauriano ya kina na kuzingatia kwa makini mambo yote.


Kulingana na taarifa iliyoandikwa na rafiki yake wa karibu James Muhia, familia yake haikutaka kuhatarisha maisha ya mtu yeyote kwa kujaribu kuurudisha mwili wake kutoka kwenye ufa alioangukia, ambao ulikuwa takriban mita 48 kutoka sehemu ya juu kabisa duniani.
Familia pia ilitoa rambirambi kwa familia ya Nawang, Sherpa (mbeba mizigo na mwongoza njia) wa Cheruiyot katika safari hii, ambaye bado hajapatikana.
All Rights Reserved|© Cantona Group Ltd
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.