Epuka makosa haya unapokutana na Mtu unayetaka kujifunza kutoka kwake.


Ni jambo la kawaida kila mtu kutamani kupata dakika chache…

…na mtu unayetaka kujifunza kupitia yeye.

Ili ufanikiwe kupata unachotaka, Epuka Makosa Haya Unapokutana Na Mtu Unayetaka Kujifunza Kwake.:

1. Kutokuwa Na Agenda Maalum.

Watu wengi unaotaka kujifunza kwao wako bize…

…muda wao ni wa thamani sana.

Jiandae agenda zako na ikiwezekana ziandike…

…ili uende moja kwa moja kwenye kilichokupeleka.

Usianze kuongea hovyohovyo, mtu akigundua haujajipanga…

…anaona wewe sio mtu sahihi wa kukupa muda wake.

2. Kushindwa Kuuliza Maswali Muhimu.

Siri ya kujua iko kwenye maswali ya kimkakati.

Badala ya kutumia muda mwingi kumsifia, kumueleza unavyomkubali, ulivyomfahamu n.k.

Jikite kwenye maswali muhimu yatakayokupa unachotaka.

Ni vizuri kuyaandaa maswali haya mapema kabla haujakutana naye.

3. Kuongea Sana

Jifunze kuwa msikilizaji zaidi ya mzungumzaji.

Usitake kujionyesha unajua sana.

Usimkatishe kila anapokuwa anaongea.

Ikiwezekana uwe na notebook ya kuandika mambo muhimu anapoongea.

Mpe nafasi ya kuongea na wewe uwe msikilizaji.

4. Jali Muda Wake.

Kama alikuambia ana dakika 10 zikiisha maliza maongezi, labda kama yeye atataka kuendeleza.

Usilazimishe aendelee kuongea wakati ameshakuambia kuna kitu anataka kukiwahi.

Ukiwa king’ang’anizi sana, siku nyingine atakukimbia.

5. Usishikeshike Simu Kila Mara.

Uko hapo kwa sababu unataka kujifunza.

Attention yako iwe kwake na sio kwenye simu.

Onyesha kuwa unathamini Muda aliokupa kwa kuweka simu pembeni kwenye muda wote wa maongezi.

Weka simu yako silent ili isipige kelele wakati mnaongea.

Kosa lipi kati ya haya unaona watu wengi wanafanya?

All Rights Reserved|© Cantona Group Ltd


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment