Anza upya!

Kuna baadhi ya changamoto ambazo utazipitia kwenye maisha yako, na zitakulazimisha KUANZA UPYA.

Yaani, kuna mambo yanaweza kukutokea yakaharibu mipango yote ambayo mwanzoni ulikuwa nayo, na ukajikuta unaanza kila kitu mwanzo.

Majira haya yanaitwa “Reinveinting Season”, yaani majira ya kujiumba upya.

Kuna watu ambao iliwahi kuwatokea katika biashara, aidha WAKAPOTEZA kila kitu au wakajikuta yule waliyedhani wataenda naye mbali, HAFAI tena inabidi wagawane na kila mtu achukue njia yake.

Wapo ambao imewatokea kwenye MAHUSIANO, yaani sio kwamba walipanga, ila kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao na ambazo HAWAKUZITARAJIA, imewabidi waanze upya.

Wengine walijua ukaribu wao na huyo mtu itakuwa “For life”, ila ndio hivyo, inabidi wafungue UKURASA MPYA.

Haujawahi kuona wale ambao walijua watakuwa kwenye hiyo OFISI kwa miaka mingi, wakaweka NGUVU ZAO zote, kuja kushtuka, inabidi WAONDOKE.

Wengi wakipitia kipindi hiki huwa wanajiona WAMEFELI na wanajaa na MAUMIVU.

Kumbuka ni MAJIRA kwenye maisha, usichelewe KUANZA UPYA.

Funika yaliyopita, Fungua Ukurasa Mpya, “Re-invent Yourself”.

All Rights Reserved|© Cantona Group Ltd


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment