Kuna siku MOYO wako utapitia hali ya KUZIMIA.
_____Yaani, kuna mambo utakuwa unayapitia…
…na NGUVU zitakuwa kama zimekuishia .
Na utaanza kuona MATUMAINI yanafifia.
Mara nyingi, siku kama hizi hautaweza kulala vizuri kabisa.
Usingizi utapaa na itakuwa kama wengi uliotamani wawe karibu nawe…
…wanakuwa MBALI nawe.
Hizi ni siku ambazo unatamani hata mtu akuulize “Unaendeleaje?”.
Bahati mbaya sana itaonekana kama kila mtu yuko bize na mambo yake.
Wengi wamepoteza NDOTO zao katika kipindi hiki.
Wengi wamekata tamaa katika kipindi hiki.
Naomba nikukumbushe, hiki ni KIPINDI CHA MPITO…
…hakitadumu milele.
Hauko mbali na KUKIVUKA, na utakuja KUSHUHUDIA baadaye…
…kuwa MUNGU alikuvusha.
Usikate Tamaa, Usiishie Njiani.
All Rights Reserved|©Cantona Group Ltd
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.