Ni ajabu ndio Uhalisia!!!

Wanasubiri Ufike Juu Ndio Wakusapoti…

Kuna watu HAWATAKUSAPOTI hadi utakapofika JUU.

Yaani, Hawa ni wale ambao wanasubiri kila mtu akusapoti…

…ndipo na wao wakusapoti.

Kuna watu ni MARAFIKI zako, wanajua UWEZO wako na wanayajua MAONO yako.

Kuna wengine ni NDUGU zako na kila siku umekuwa ukiwaambia kuhusiana na MAONO yako…

…cha ajabu hawa wote HAWAKUSAPOTI chochote.

Kinachoweza kukushangaza ni Kuwa, anaweza kutokea mtu mwingine mwenye maono kama ya kwako…

…na WAKAMSAPOTI kwa 100% halafu wewe WANAKUCHUNIA.

Jifunze, KULIELEWA na KULIKUBALI jambo hili MAPEMA.

Kuna wengine wanasubiri HADI UTOBOE…

Wengine hadi UWE NA JINA ndio waje kusema…

…“Ni ndugu yangu au ni rafiki yangu”.

Cha muhimu ni kuwa na HEKIMA ya kujua kila mmoja…

…UTAMUWEKEA mipaka gani muda huo UTAKAPOFIKA.

Umejifunza kitu? Kama umejifunza kitu comment “NDIO, NIMEJIFUNZA KITU”


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment