Watu wengi wamekubali kuwa vile ambavyo watu wengine WALITARAJIA.
Yaani, mipaka ya mafanikio yao na WANAVYOWEZA kuwa…
…imewekwa na MAONI ya watu wengine badala ya MAONO yao.
Hivi unajua inawezekana kabisa kile ambacho wewe unakiita MAFANIKIO…
…ni asilimia ndogo sana katika kile unachoweza KUKIFANYA?
Usikubali kuwa MKUBWA katikati ya WADOGO wengi…
…tafuta nafasi yako katikati ya WAKUBWA wengine.
Leo, nataka utafakari Swali hili…
“Hivi hii level niliyopo ndio mwisho wa UWEZO wangu…
…au ni kwa sababu NIMERIDHIKA?”
Ukiona kuwa unaweza KUWA zaidi ya ulivyo…
…basi FANYA KITU leo kuelekea safari ya UKUU WAKO.
Wewe ni MKUBWA zaidi ya ULIVYO SASA.
Umejifunza kitu? Kama Umejifunza Kitu tafadhali naomba comment maneno “NITA JITAFUTA, MPAKA NIJIPATE”
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.