“Ni Nani Atalitaja Jina Lako Kwa Mfalme?”
Hivi unajua kuna watu wana VIPAJI na UWEZO wa kipekee…
…Ila changamoto ni kuwa HAKUNA ANAYEWATAJA?
Ni ukweli usiopingika kuwa, kuna wakati unachohitaji ni…
…MTU MMOJA wa kutaja jina lako MAHALI sahihi na kwa WAKATI sahihi.
Kuna MAENEO hauwezi kufika ila UNAHITAJIKA…
…kuna VIKAO unajadiliwa na hauna hadhi ya KUHUDHURIA Ila unahitaji KUTAJWA.
Ingawa YUSUFU alimsisitiza mtu aliyemtafsiria ndoto kuwa akirudishwa KAZINI ikulu asimsahau KUMTAJA…
…Ila cha Kushangaza alikaa miaka 2 akiwa AMEMSAHAU na hakumtaja.
Usisahau kuwa, kuna watu wengi sana ambao wanaujua UWEZO wako…
…wanafahamu Kipaji Chako ila HAWATAKUWA tayari KUKUSEMEA vizuri kwa MFALME (Bosi, kiongozi Mkuu n.k).
Wengine ni kwa sababu ya WIVU, wengine wanaona Kama muda wako BADO…
…wengine WAMEKUSAHAU na wengine wanaogopa UTAWAZIDI.
Leo, yangu ni maombi kwa ajili yako.
“Mungu asababishe, yeyote anayetakiwa kukutaja kwa MFALME, basi ASIKAE KIMYA”
Na iwe hivyo.
Ameen!
Kama umejifunza kitu comment neno “NIMEJIFUNZA KITU”.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.