Kwa Ambao Mwili Bado Unatembea, Ila Moyo Ulishazimia…
Siku moja, nilipigiwa simu na mtu ninayemuadmire akaniambia…
“I feel like I can’t take it anymore, I better die”
(Najihisi nimefika mwisho, siwezi kuendelea, bora nife).
Hapa ndio nilijithibitishia kuwa…
…hata wenye NGUVU huwa WANAHISI KUCHOKA.
Kuna zile nyakati ambazo unalazimika kwenda ofisini…
Kuhudhuria Vikao…
Kuzungumza na watu n.k…
Unafanya Kama WAJIBU…
…Ila ukweli usiopingika ni kuwa, NGUVU ZIMEKUISHIA.
Usisahau jambo hili, hata watu wanaoonekana kuwa ni HODARI kwa NJE…
…huwa WANAZIDIWA na kuishiwa NGUVU, wewe sio wa KWANZA.
Kuna watu bado wanafanya biashara kwa nje…
…ila kwa ndani walishakata tamaa.
Kuna wengine wako kwenye mahusiano kwa nje…
…ila kwa ndani moyo wao ulishaondoka.
Ni hali ngumu Kujikuta nayo…
…ila ikitokea lazima uamue KUTOKATA TAMAA moja kwa moja.
Ukiwa katika hali hii unahitaji kufanya mambo mawili:
Moja, ni kuzungumza na mtu unayemuamini…
…hata kama hatakusaidia Ila utatua mzigo.
Mbili, Kama inawezekana, pata muda upumzike.
Usijilazimishe zaidi ya unavyoweza…
…kila mwanadamu ana mipaka.
Kumbuka kuwa SIMBA ambaye MOYO UMEZIMIA huanguka mwenyewe…
…na kufa bila KUSHAMBULIWA.
Kama umejifunza kitu comment neno “NIMEJIFUNZA”
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.