Leo nimejiuliza swali, hivi mimi huwa najadili nini na watu wangu wa karibu?
Mwaka 1968 Bill Gates alikutana na rafiki yake Paul Allen ambaye walikuwa wanasoma darasa moja.
Siku moja wakiwa bado shuleni walikuwa wanasoma jarida la “Fortune Magazine” ambalo lilikuwa linaelezea makampuni 500 makubwa duniani.
Bill Gates akamuuliza rafiki yake Allen “Hivi umeshawahi kufikiria jinsi ya kuendesha kampuni kubwa kama hizi zilizotajwa?”. Allen akamjibu, “Pengine siku moja tutakuwa na kampuni yetu ya Kompyuta Kubwa kama hizi”.
Hivi ndivyo safari ya kuijenga kampuni kubwa duniani ya MICROSOFT ilivyoanza.
Hivi ingekuwaje kama Allen angemcheka kuhusiana na lile swali lilikuwa limejaa maono makubwa?
Mtu mmoja alisema watu wa CHINI hujadili WATU wengine, watu wa KATI hujadili MATUKIO na watu wa JUU hujadili MAWAZO.
Je, wewe huwa unajadili mambo gani ukiwa/ukichat na rafiki zako? Hebu angalia magroup yako ya watsapp yamejaa stori za WATU, MATUKIO au MAWAZO.
Hata kama wewe ni Bill Gate ila kama hauna Allen anayeeleweka basi UTAFELI.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.