Usivunje mahusiano na mtu kwa sababu umehitaji msaada kwake na unajua…
…ana uwezo wa kukusaidia ila hajakusaidia.
Sio kila wakati mtu atakupa msaada pale unapotaka.
Kuna wakati haitawezekana kwa sababu:
1. Kuna shida kubwa zaidi itakuja mbele yako ambayo Mungu …
…anawahifadhi hao watu ili waje kukusaidia shida hiyo itakapotokea.
Wakikusaidia sasa hivi, hiyo shida kubwa itakapotokea…
…wanaweza wasiwe msaada kwa sababu wataona walishafanya.
Kiufupi ni kuwa Mungu anawahifadhi ili…
…waje kukupa Msaada Mkubwa zaidi.
Muda wao haujafika, ukifika watafanya na…
…utashukuru kwamba hawakukusaidia katika shida yako ya sasa hivi.
2 ). Kuna uvumilivu unatakiwa kujengewa…
…ili Ukomae ufikie ndoto zako.
Ni kama mtoto usipomruhusu aanguke wakati anajifunza…
…kutembelea, hataweza kutembea.
Kuna mambo yanatokea na unaachwa peke yako…
…ili ujenge misuli ya changamoto kubwa mbele yako na kujifunza kusimama peke yako.
Uko darasani, usikimbie mtihani.
3 ). Kuna watu wana kiburi na wakikusaidia itakuwa matangazo kila kona.
Wanaamini hauwezi kufanikiwa bila wao.
Unapokuwa na shida hata kama wana uwezo wa kukusaidia…
…Mungu anawazuia ili wasije kujisifu.
Mungu anataka kuonesha kuwa anaweza KUKUFANIKISHA BILA wao, atatumia watu wengine.
4 ). Kuna misaada ambayo inakuja na masharti ambayo…
…yanaweza kukudhuru na kukupotezea mwelekeo wa maisha kabisa.
Kuna watu kwa sababu ya misaada waliyopokea…
Iliwalazimu kukana imani yao au kufanya mambo ambayo…
…wameyajutia maisha yao yote na kuwakosesha imani.
Kuna misaada inaambatana na ndoano ndani yake.
Mungu anawazuia kwa sababu anakupenda na…
…hataki uingie huko usije ukaharibikiwa.
Jifunze kushukuru!
Kama mtu hajakusaidia USIMGEUZE kuwa ADUI yako.
Endelea kupambania MALENGO YAKO kuna siku utafanikiwa tu.
Kumbuka sio kila ambaye hakupi Msaada unapohitaji anakuchukia..
…wengine wanatumiwa na Mungu kukusaidia kwa kutokukupa unachotaka.
Kama umejifunza kitu comment neno “NIMEJIFUNZA”
Kwa mafunzo ziada ya Marriage Mathematics,sikiliza Radio Fortune Africa.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.