Jinsi ya kuwa na furaha!!!

Karibu tena katika episode nyingine. Leo tukumbushane kuhusu kitu kimoja. Usipoteze furaha. Watu wengi sana wanaamini kuwa siku wakifika hatua fulani ya maisha, basi furaha itakuwa kubwa. Furaha si zao la vitu, furaha ni zao la moyo wako. Watu wanaishi kwenye someday mentality.

Watu huwa wanawaza furaha ni zao la kumiliki vitu, au kuwa kwenye mazingira fulani.

Kuna watu wameshawahi kujiua, ila ukiwaangalia ni watu wenye mali nyingi, na walikuwa wanapata kila kitu walichoikuwa wanahitaji. Maisha ya mwanadamu yalivyo huwa kuna gap, linaloitafuta furaha. Ila ukweli furaha huwa inapatikana ndani wala si nje. Inawezekana, hata wewe unakuwa kwenye hali hiyo.

Kwa nini ni muhimu kuitunza furaha yako. Kuna vitu vitano vya kuangalia.

(i) Furaha inavutia watu sahihi kwenye maisha yetu.
Furaha ni energy. Furaha ni kitu ambacho mtu anaweza akakihisi unapokutana naye.

Na ndiyo maana unaweza kukutana na mtu, hamfahamiani, akakuangalia akatabasamu, na wewe ukatabasamu, bila wewe kujua. Ukiwa na furaha, unavutia watu wenye furaha. Ukiwa mtu wa huzuni, utavutia watu wenye huzuni.

Yaani utakuta watu wako, ni watu wanaolalamika, kama wewe. Kwa hiyo kama unataka kuvutia watu, wenye mtizamo chanya kwenye maisha yako, inabidi uanze wewe.

(ii) Furaha inakusababisha uwaze vizuri.
Watu wengi wenye ubunifu, ni watu wenye furaha. Huwezi kuwaza vizuri, ukawa mbunifu, kama wewe ni mtu huzuni.

Yaani ni mtu wa kulalamika kila wakati. Hata wewe ni shahidi, ukiwa hauna furaha, kuna makosa mengi sana huwa unayafanya. Ukiwa hauna furaha, unaweza kuwakwaza watu bila hata wewe kujua. Na ndio maana ni muhimu sana kuitunza furaha yako, vinginevyo inaweza ikakugharimu.

(iii) Furaha inakupa nguvu.
Nguvu ya kufanya vitu kwa nje, inatokana na furaha yako ya ndani. kuna mtu mmoja ambaye ni shabiki wa simba anasema, aliwahi kutembea kifua wazi, akiwa anashangilia ushindi kutoka uwanja wa taifa, mpaka ubungo. Yaani haelewi ilikuwaje mpaka akatembea umbali mrefu akiwa na wenzake wanashangilia, tena akiwa kifua wazi. Yote hiyo ni nguvu ya furaha.

Ukweli ni kuwa kama wangekuwa wamefungwa, angeona Ubungo ni mbali sana kuliko hata uhalisia wake. Sababu angekuwa na huzuni.

Furaha ni kama fuel, inakupa uwezo wa kufanya vitu.

(iv) Furaha inakupa hisia imara.
Ukiwa na furaha inakupa stability. Ukiwa na furaha unaepuka kuchukizwa bila sababu ya msingi. Mtu asiyekuwa na furaha, hata kumsalimia tu anaweza akakasirika. Hisia imara ni muhimu sana kwa watu wanaofanikiwa. Watu wenye furaha, huwa hawaswing na mood. Ni watu ambao wako kwenye stable na hisia zao.

Hata wakisikia Habari mbaya, wanapata muda wa kutulia na kutafakari.

(v) Furaha inakupa matumaini ya kesho.
Angalia watu wenye furaha, wanaweza kuwa wanapitia kwenye changamoto kubwa za maisha, lakini bado wakatulia. Ni watu ambao hawakati tamaa kirahisi. Anaamini kesho itakuwa bora kuliko leo.

Watu wenye huzuni, ni watu wa kukata tamaa. Ukizoea kukosa furaha, ni kitu ambacho kinaendelea kujitengeza ndani yako. yanakuwa ni maisha yako ya kila siku.

Vitu ambavyo unaweza kuvifanya ili upate furaha. Kumbuka furaha haupewi na mtu. Usitegemee furaha utapewa labda nyumbani, kazini au na marafiki zako.

Fanya vitu hivi kutengeneza furaha yako.

(i) Jifunze kuwa mtu unayeyaona mambo Chanya.
Ukiwasiliana na mtu, hajapokea simu usianze kuwa hasi. Ni muhimu kutengeneza positivity kwenye maisha. Watu wengi waliofanikiwa, wanaona positivity katika negativity.

(ii) Sikiliza na angalia vitu vinavyokuongezea furaha.
Dunia imejaa habari mbaya kila sehemu. Mfano, mauaji, ajali, mafumamizi na kila swala la ubaya. Jitahidi kutafuta Habari Chanya ambazo zitafanya uone, dunia bado ni sehemu sahihi ya kuishi.

(iii) Ambatana na watu wenye furaha.
Achana na watu wanaowaza negativity. Watu wenye huzuni. Tafuta watu wenye furaha, watu wanaowaza mambo Chanya. Watu ambao wanaona bright future. Furaha ni wajibu wako, na endelea kujihusisha na watu wenye furaha.

Furaha ni energy kama tulivyoanza hapo juu.
Unatakiwa kuilinda sana furaha yako.

Mafunzo zaidi ya Empowerment Mathematics,sikiliza Radio Fortune Africa-Ukweli Na Burudani.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment