Mtambue adui ili uishi naye!!!

Adui yako wa kweli siyo mtu anaekudharau kwa sababu ya umaskini wako, bali ni mtu yule anaekuchukia kwa sababu ya mafanikio yako.
Leo kuna watu watakupenda kwa sababu hali yako ya maisha iko chini, unawategemea na kuwaomba msaada, ndugu yangu usiwe mwepesi kuwaamini kama watu wema kwako kwa sababu ya msaada wanaokupa. Ishi nao kwa hekima na kwa upendo, maana rangi yao halisi itathibitika siku utakapofanikiwa katika jambo lako.
Katika ulimwengu tuliopo tumezungukwa na maadui wengi tusiowajua watu wanaoridhika wakiona maisha yetu yana changamoto za kiuchumi, hatuendelei, na tunaishi kwa kutegemea msaada wao.
Siku ukipandishwa cheo, ukijenga nyumba, ukinunua gari nakadhalika, hapo ndipo utakapoanza kuwagundua maadui zako.
Kuna kundi la watu utakaowapoteza siyo kwasababu umewakoaea ila ni kwasababu umeyapatia maisha. Hao ndiyo maadui na ndiyo watu wabaya kwako ambao usiku na mchana wanapambana ili kuona unabakia katika kiwango kile kile cha maisha.
Ashukuriwe Mungu kwa ajili ya watu wa aina hii maana ni lazima wawepo ili raha ya mafanikio yako na kuinuliwa kwako itimilike, maana imeandikwa, “Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu.” (Zaburi 23:5). Ukubwa wa meza ambayo Mungu anatuandalia inalingana na wingi wa maadui wasiotaka tufanikiwe.

Mungu akubariki sana na akuinue mbele ya macho ya watu wasiotaka ufanikiwe.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment