Kuwa kama Nyuki:Tengeneza asali mwanangu.

Siku moja nikiwa nasema na mentor wangu Mwendazake Mama yangu mzazi Queen Elizabeth Endesha aliniambia…

“Great Things Never Come from the Comfort Zone”.

Akimaanisha, mambo makubwa kwenye maisha huwa hayaji ukiwa “umerelax”.

“Comfort zone” ni lile eneo ambalo umelizoea na hutaki mtu akutoe hapo.

Ni ile aina ya maisha ambayo umeshajisemea moyoni kuwa hapa nimefika.

Kuna watu comfort zones zao ni cheo chao cha sasa.

Yaani anaona ameshafika tayari na ameridhika…

…matokeo yake wala hafanyi cha ziada ili kukua zaidi.

Kuna wengine kila siku wanataja Kiwango chao cha Elimu.

Utawasikia, “Mimi nimesoma bwana”…

Matokeo yake, hataki kujifunza kitu cha ziada na amedumaa.

Kuna watu faida ambayo anaipata kwa sasa kwenye biashara yake…

…imempumbaza kabisa na anaona ameshafika kabisa.

Comfort zones, zimeua ndoto za watu wengi sana.

Angalia na wewe usiue ndoto zako.

Inawezekana kweli hapo ulipo hakuna matatizo yoyote yale…

…ile unaweza kuwa mkubwa zaidi ya hapo.

Unaweza kufanya makubwa zaidi ya hapo.

Ubaya ni kuwa ukiendelea kung’ang’ania comfort zone, utaondoka kwa aibu.

Chukua hatua mapema!

Umejifunza nini hasa kwenye ujumbe huu? Niandikie kwenye comments.

NB: Muda Wowote Ukihitaji Usaidizi Wangu Zaidi Fanya Yafuatayo


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment