Unapotafuta kutimiza maono makubwa kwenye maisha yako itaambatana na MAUMIVU makali.
KUKUA kwenda kiwango kingine huambatana na VIKWAZO vikubwa.
Na mara nyingi itakufikisha sehemu ambayo unatakiwa kuchagua…
UENDELEE kuwa wa kawaida…
Ama UKUBALI kukabiliana na MCHAKATO…
…na udhihirishe UKUU ulioko ndani yako.
Mandy Hale aliwahi kusema kuwa…
…“ Growth is painful, Change is Painful.
But nothing is as painful as staying stuck somewhere YOU DON’T belong”.
Akimaanisha kuwa Kukua huambatana na maumivu, mabadiliko huambatana na maumivu.
Ila maumivu makali zaidi ni yale ambayo yanatokea pale…
…UNAPOKWAMA mahali fulani ambapo unajua kabisa sio SEHEMU sahihi kwako”.
Kama unajua ulipo HAUJAPACHAGUA bali UMEKWAMA…
…Ni wakati wa kufanya kitu ubadilishe hali hiyo.
Moja ya majuto ya watu wengi wanapokuwa wazee sana ni…
“Natamani nisingekubali kuwa wa kawaida wakati nilikuwa na nafasi ya kufanya mambo makubwa”.
Wengi kwa kuogopa gharama inayoambatana na MABADILIKO na KUKUA kwao…
…waliamua kukwepa wanachopaswa kufanya.
Hebu jiulize – Hivi wewe unapambana kuwa vile unavyoweza kuwa…
…ama umeshakubali maisha yakuchagulie yanavyotaka uwe.
Na umekubaliana nayo?
Usikubali kukwama mahali ambapo haupataki.
Usikwame kwenye kiwango cha elimu ambacho unaweza kuongeza…
Usikwame kwenye kazi ambayo unaweza kubadilisha…
Usikwame kwenye mahusiano ambayo unaweza kuyaboresha au kusitisha…
Usikwame kwenye kuamini ndoto yako imefika mwisho.
Weka maazimio kuwa…
“Bila kujali UKUBWA wa MAUMIVU utakayopitia hatuaacha KUTAFUTA KUKUA…
…na KUPATA MABADILIKO unayotatafuta.
Feel The Pain and Do It Any How!
Hapo ULIPO UMEKWAMA ama UMECHAGUA kuwa HIVYO?
The HeartBeat of Africa
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.