Wewe ni shahidi;
Kuna mahali walikukataa, leo unashukuru Mungu ulipo; sababu walikukataa
Unaweza kukataliwa kwa vitendo au kwa Maneno…. wala usiumie wanaokukataa wanafanya kazi nzuri ya kukupeleka sehemu sahihi ambayo nguvu yako itatumika vema;
Kazini kwako kuna dalili zozote zinaonesha hutakiwi?
Wapangaji wenzako na mwenye nyumba je? Kanisani kwenu? Majirani? Ndugu zako wakuzaliwa? Kwenye eneo la biashara? Shuleni? Kijiweni hapo? Darasani?
– uliomba kazi sehemu wakakukataa kumbe walikuwa wanasababisha uende sehemu husika;au ulifukuzwa kazi majira hukutarajia.Ni biashara yako uliowategemea wakupe mkono wa heri walikukataa kipindi unawahitaji.Ni Katika mahusiano.
Ile hasira ya kukataliwa unapambana na jambo kwa nguvu nyingi kumbe ndo Mungu anataka uende huko!
Yesu Bwana si waka mkataa kumbe ndo wanamsukuma kwenye kile kitu alichotakiwa kufanya!
Kukataliwa ni kanuni ya kutoboa maishani kama ukichukuliwa kukataliwa huko kwa mtazamo chanya !
Kama unahisi unakataliwa maeneo fulani
Usiwe mnyonge best ni sauti ya Mungu hiyo ili ukachanue zaidi mahali pengine au kwenye kitu chako……
Nakutakia Ijumaa Kuu.
#TheHeartBeatofAfrica
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.