UKWELI KUHUSU MAISHA
Ni siku njema tena tuliyopewa na Mungu. Tumeshajifunza kushinda kutokea nyuma/ (winning from behind).
Leo tuzungumze mambo ya kuzingatia kuhusu maisha.
Kuna vitu muhimu saba, kuviangalia hasa pale unapohisi umechelewa.
(i) Kila point ya maisha kuna watu lazima watakutangulia.
Hii ni muhimu sana, kuelewa. Huwezi kuwa wa kwanza kila wakati. Lazima kuna watu watakutangulia kifedha, kiimani, kiafya, na kila kitu.
Kuna wakati utakuwa wa pili, wa kati na hata wa mwisho. Ukielewa hii, utapata amani, maana utaelewa katika maisha kuna kuzidiana.
(ii) Unaweza kuanza wa mwisho lakini haina maana utamaliza wa mwisho.
Unaweza kuchelewa kuanza shule, kuanza biashara, kupata kazi. Kuna watu wamechelewa vitu vingi sana, lakini wamekuja kuwa wakubwa, wamekuja kuwa wa kwanza. The fact that umechelewa kuanza haina maana kuwa utakuwa wa mwisho. Elewa cha muhimu ni namna utakavyomaliza. Hata kwenye riadha siyo lazima yule aliyeanza ndio anakuwa wa kwanza.
(iii) Kila mmoja katika maisha anao uwezekano wa kushinda.
Kuna nafasi kubwa sana ya kila mtu kufanikiwa. Kadiri unavyopandisha viwango vyako kuwenda juu, ndivyo unajipa nafasi ya kushinda. Kila nyota ya angani ina nafasi ya kung’aa. Ni mara chache sana kusikia ndege zimegongana. Kule juu nafasi ni kubwa sana. Na ukiwa huko juu, mnakuwa wachache sana. Hii ni tofauti ukiwa chini, mnakuwa wengi kama magari.
(iv) Wale walioko mbele yako leo, kuna siku walikuwa na hali ya kwako.
Wala siyo cha ajabu. Tena kuna wengine walikuwa na hali mbaya sana kuliko hata ya kwako. Wala siyo kwamba wao ni maalum sana. Kama wao walipita katika hali ya kwako, mpaka leo unawakubali, na wewe pia unaweza kufanya vitu, ukafika level zao. Ina maana wana ushuhuda, ya kwamba kuna siku walikuwa kama wewe.
(v) Hauwezi ukashinda kwenye maisha kwa kuwachukia wale walioko mbele yako.
Ni muhimu tu kuwa mnyenyekevu na kujifunza. Mtu aliyefanikiwa, badala ya kumchukia, au kujiunga na wale wanaomsema vibaya.
Jaribu kufuatilia historia yake, jifunze kupitia yeye. huwa kuna pattern fulani watu waliofanikiwa huwa lazima waipitie. Si kila aliyefanikiwa amefanya mambo mabaya. Kuwa wengi tu, wamefanikiwa katika njia za halali kabisa. Jifunze.
(vi) Commitment yako ni muhimu kuliko fursa na kipawa.
Vipawa kila mtu anavyo. Talent is not enough. Kuna watu wana talents. Yaani kama ni kuimba, wanaimba. Watu wenye talent wako wengi sana, fursa pekee haitoshi. Kinachotofautisha ni commitment.
Mohamed Ali, alisema anachukia mazoezi, ila anafanya kama mtumwa ilia je aishi kama mfalme.
(vii) Hakuna mtu atayekuonea huruma.
No one will feel sorry for you. Usipopambania unachokitaka, utaishia kukipata usichokitaka. Duniani kila mtu ana matatizo yake, kila mtu anajipambania. Yaani kama una shida zako, kuna wakati anakusikiliza ila mkishaachana baada ya dakika 2 ameshasahau. Anawaza yake.
Mtawala wa Dubai, ameandika kwenye kitabu chake cha My Vision- anasema Afrika kuna mnyama anaitwa simba na Paa. Anasema kila asubuhi paa huwa anakimbia ili Simba asimle, na Simba ili aweze kuishi na kupata chakula lazima amkimbize paa amkamate. Kwa hiyo ama wewe ni simba au paa, lazima ukimbie kuiponya nafsi yako.
Kuna mambo matatu unayotakiwa kuyafanya unapoona umechelewa.
(i) Amua unataka kuwa nani, na unataka nini
Siku zote maisha huwa yanawapendelea watu ambao wanataka nini katika maisha.
Watu wengi wanakufa wakiwa na miaka 25 na wanazikwa wakiwa na miaka 75. Usije ukazikataa ndoto zako. Kumbuka ndoto zako. Ama ni ndoto ya kifedha, ndoto ya kitaalamu. Na usiruhusu mtu aseme kwamba haiwezekani. Hata kama watu milioni wakisema kwamba haiwezekani, wakati wewe unasema inawezekanA, basi itawezekana.
(ii) Jenga tabia, ya kile unachokitaka
Tengeneza tabia, zinazokupeleka kule unakotaka.
Kama unasema unataka kuwa mwanariadha mzuri, je, una tabia za wanariadha. Lazima utengeneze tabia ambazo zinakwenda kule unakotaka. We first make our habits, and then habits make us. Na hata James Clear amesema, if you want to build habits that last, join a group where your desired behavior is the normal one. Sasa huwezi kuwa unataka kuwa mwekezaji halafu unaandamana na watu wanao-spend tu fedha.
(iii) Be passionate
Hakikisha unachofanya siyo option. Siyo hiyari. Iwe ni principle. Make it necessity. Charles Duhigg anasema kwenye kitabu cha The Power of habits, make sure unaondoa analysis. Vitu vije automatic. Ukisema unataka kufanya mazoezi, ama inyeshe mvua, au liwake jua, utaamka na kufanya mazoezi. siyo option. Kama unataka kufanikiwa, hakuna kitu cha kukuzuia kama utaamua kufanya kwa lazima.
Naendelea Kujifunza: Tujifunze Pamoja.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.