Winning from behind.

Karibuni tena katika muendelezo wa kujifunza. Wale wote ambao mmekuwa mnawashirikisha wenzenu, katika series hizi, shukrani sana kwenu. Leo tuongee kidogo kuhusu winning from behind. Unashindaje kutokea nyuma. Watu wengi sana wanajiona wamefail, sababu wanahisi wameshachelewa.

Yaani muda umeshapita. Na hii ni kutokana na pia kujilinganisha na wengine. Inawezekana unaona umechelewa kuanza biashara, umechelewa kupoata ajira, umechelewa kupata mwenza, kupata mtoto na menhingeyo. Na akingalia katika marafiki zake, wana familia, watu mnaosali nao. Kila pande unazoangalia unaona kabisa umechelewa.

Cha kutumaini hapa, lazima uelewe kuwa unaweza kushinda kutokea nyuma. Kuna watu wengi sana, walianza kwa kchelewa lakini wamekuja kupata mafanikio.

Kuna negative impact, unapokuwa na hisia ambazo, watu waliochelewa wanakuwa nazo.

(i) Watu wengi huwa wanakata tamaa.

Wanakata tamaa kwenye maisha yao. Inawezekana hata wewe hapo, kuna sehemu unahisi umechelewa. Chochote ambacho unahisi kuwa umechelewa kukifanya, na ukakubali kuwa umechelewa, basi ni rahisi sana kukata tamaa.

(ii) Ukishakuwa na hisisa za kuchelewa, Hautaweka juhudi za kutosha.

Sababu taayari unakuwa unaamini kuwa hata ukifanya bidii, hautafanikiwa, kama kuchelewa umeshachelewa

(iii) Unaona hakuna muda wa kubadilisha maisha yako.

Yaani unaona kama muda hautoshi. Ukiangalia swala la kuweka akiba, kuanza biashara, na mengineyo, unaona kabisa muda hautoshi. Ukiwa na hisia za kuchelewa, hautachukua hatua. Na usipochukua hatua, unazidi kuchelewa.

(iv) Unaweza kufanya maamuzi magumu.

Ukishaona umeshachelewa, unajikuta unachukua maamuzi magumu na mabaya. Kama unahisi labda umekosa mwenza unaweza kuchukua mtu ypyoye au hata kujibebesha mimba, ukiamini kuwa ndio utaolewa. Au unaweza hata kuiba ofisini ili tu ukimbizane na wenye fedha.

Hizi short cut huwa mwisho wake siyo mzuri. Unaweza kufanya vitu ambavyo, ulikuwa haufanyi sababu ya hisia za kuchelewa.

(v) Unaanza kujisikia kukubali kuwa katika hali uliyopo, bila kufanya juhudi zozote.

Uwezo wako ni mkubwa, na fursa zipo. Lakini sababu umeingiwa na hali ya kukataa tamaa, basi unaamua kukubaliana na mazingira na hali iliyopo.
You settle for less. Unakuwa na cycle fulani ambayo, unaenda nayo hivyo hivyo.

(vi) Hawako tayari kujaribu vitu vipya.

Huwa hawataki kutake risk. Yaani hata wakipewa fursa, wanakuwa wanaikataa. Wanaamini wanachofanya ndio sahihi. Yaani hawataki kujiongeza kabisa.

Hizi ni hisia tu, na usipombana nazo utajikuta ni mtu wa hivyo hivyo. Hata kidogo ulichonacho, unaweza kukiona hakina maana. Lakini hata hicho ulichonacho ni cha muhimu.

Naendelea Kujifunza: Tujifunze Pamoja.

TheHeartBeatofAfrica


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment