Siku moja nilikuwa nasema na Mamangu mwendazake Queen Elizabeth Endesha (General)kabla hajatuacha 16/10/ 2021 nakumbuka nikimsimulia Mentor alikua msikivu na hakukosa wosia kuhusu CHANGAMOTO KUBWA nilizokuwa napitia,alipenda kusema najua uwezo wako,nafahamu unaweza fanya lipi,usiweze kataa tamaa.Una nguvu ndani yako ndoto zako itatimia.
Moyoni mwangu nilitarajia ANIONEE HURUMA au anipe MSAADA wa haraka niliokuwa NAHITAJI.
Nilipomaliza kuongea, alianza kuongea kwa kutumia nukuu ya Wilson Kanadi akasema, “Cantona, kumbuka hili mwanangu: To be The Best, You Must be Able to Handle The Worst”.
Yaani, ili uwe BORA lazima UJENGE UWEZO wa kukabiliana na mambo MAGUMU na NYAKATI NGUMU za maisha yako.
Nimejifunza kwa vitendo kuwa, uwezo wa kukabiliana na nyakati ambazo unadhania HAUTAVUKA ni muhimu sana katika kutengeneza UKUU wako.
Inawezekana leo kuna “Worst” moment unapitian Ofisini, Kwenye Mahusiano, Biashara, Uongozi n.k
Naomba nikukumbushe kuwa, watu IMARA na WAKUU huwa wantengenezwa nyakati za DHORUBA kama unazopitia.
Kama HAUTAZIMIA MOYO na ukaamua kuendelea kushikilia IMANI yako, UTAVUKA ukiwa MSHINDI.
Ni wakati wako wa KUTENGENEZWA Kuwa bora zaidi, USIKATE TAMAA.

Comment: Ninaandaliwa ili niwe bora zaidi.
TheHeartBeatofAfrica
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.